Toba ya Kweli.

Egypt's Dar Al-Ifta

Toba ya Kweli.

Question

Nini makusudio ya "Toba ya kweli"? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Neno "Toba" ama “msamaha” kilugha lina maana ya “kurejea”. mfano, kutokana na makosa yake, mtu amerejea na kuachana nayo” na iwapo mtu atarejea kwa Mwenyezi Mungu, ina maana kuwa, huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake upo juu ya mja kwa kurejea kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema {na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu} [AT TAWBAH 118]
Ama katika istilahi ni: Kujutia na kujivua na maasi, kwa kuwa ni maasi na si kwa ajili ya kuwa na madhara ya kimwili au katika mali, na kuwa na nia ya kutorudia tena kadiri awezavyo. Na wengine wakasema, ni kurudi kutoka katika njia iliyopinda na kwenda katika njia iliyo sahihi. Imam Ghazali amesema; kujua ukubwa wa kosa, na majuto, na kuwa na nia ya kuacha pale ujuapo kosa hilo na kwa baadae na kutorudia tena.
Kupitia istilahi hizo pamoja na kutafautiana kimaelezo lakini lengo lake ni moja, pia kuomba msamaha inasemwa ni ile hali ya kujutia pekee kwani kufanya hivyo utakuwa kama vile umeshajua kosa lako na hutafanya tena. Kwa ajili hiyo, Mtume ( rehema na amani zimshukie) anasema: “Kujuta ni kuomba msamaha (toba)” [Hadithi hii imetolewa na Ahmad katika kitabu chake na Ibn Majah]. Na kujutia ni kule kuuhuzunisha moyo kwa kujutia kuwa usingelifanya kosa hilo.
Kuomba msamaha kutokana na makosa ni wajibu kisheria tena kwa haraka sana, hii ni kwa makubaliano ya wanachuoni. Kwani ni katika misingi muhimu ya Uislamu na nguzo ya dini na ni njia ya mwanzo ya wachamungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Natubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} [AN NUUR 31].
Uombaji wa msamaha ni hali ya kuihakiki nafsi na ni uchunguzi wa ndani na kuirudi nafsi, maneno kama haya ya uhakiki wa nafsi na kuirudi nafsi na uchunguzi wa ndani wa nafsi itaonekana kama kwamba hayana uhusiano na uombaji msamaha, kwa kuwa ufahamu wa wengi ni kuwa neno “Kuomba msamaha (toba)” Ni ile hali ya kuacha maasi tu pekee na si vyinginevyo, lakini ukweli ni kuwa kuomba msamaha ni sifa ya kiroho na kimoyo iliyomo ndani ya Mwislamu mwenye kuchunga mambo ya dini yake na dunia yake.
Nakutubia kwa Mwenyezi Mungu ni ahadi kati ya mja na Mwenyezi Mungu Mola wake mja analazimika kutorudia kosa kwa mara nyingine, kwani kutofanyakosa haiwezekani kwa yeyote, kwani hilo ni jambo pekee ambalo Mwenyezi Mungu huwahusisha awatakao, kwa ajili hiyo kaweka uombaji wa msamaha, katika uombaji wa msamaha kuna msaada, nao ni kumtaka Mwenyezi Mungu akusaidie kukusamehe kisha uweze kurudi katika njia iliyo sahihi na kuchunga mwenendo wako ili usije kuivunja ahadi, na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu akusaidie ili uweze kufanikisha jambo hilo.
Na mwanadamu anahitaji kuomba msamaha kila siku, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha kuomba msamaha maalumu nao ni msamaha wa kweli akasema; {Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu} [AT TAHRIM; 8]
Na wanazuoni wametofautiana juu ya uombaji wa msamaha wa kweli, na kauli iliyo maarufu ni ile iliyopokelewa na Omar na Ibn Masuud na Abi Kaabna Muadh BinJabal – Mwenyezi Mungu awawie radhi – na imepokelewa kutoka kwa Muadh kuwa Mtume (rehema na amani zimshukie) amesema: “Toba ya kweli ni pale mkosaji anapojutia dhambi ambayo ameitenda, anaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kisha kutorudia tena kama yasivyorudi tena maziwa katika chuchu.” [Ameitaja Twabary na Al Aswbahaniy].
Kwa kuwa toba ya kweli ni kutorejea makosa baada yake kama ambavyo maziwa hayarudi tena katika chuchu ya (mnyama). Pia imesemwa: Ni majuto ya moyoni, na uombaji msamaha kwa ulimi, na kujivua makosa na kuwa na matumaini kuwa hutayarudia.
Hivyo, hapana budi kuomba msamaha kila siku kwani kufanya hivyo kuna manufaa mengi ya kumyanyua mwanadamu na kumtakasa kutokana na udhalilifu, na Mtume wetu ametupigia mfano mzuri katika kudumu na hali ya kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu ingawa hakuwa amefanya kosa kwani yeye amelindwa, amesema Mtume (rehema na amani zimshukie) “Enyi watu, tubuni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwake kwa siku moja mara mia.” (Muslim).
Pia maumbile ambayo Mwenyezi Mungu aliyomuumbia mwanadamu katika ulimwengu yanapelekea kumtaka aombe msamaha kila siku (kwa kudumu), na wala hatakiwi kuhisi uzito kwa sababu ya kuomba msamaha, na wala pasipatikane kuionea aibu nafsi na pia pasiwe na uzito wa kujivua na makosa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuwezeshe sisi tumuombe yeye msamaha wa kweli na wa kudumu, na atusamehe, na azikubali toba zetu, kwani yeye ni mweza wa hilo. Na mwisho wa maombi yetu ni Alhamdulillah.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: kitabu Simaatu Al asri, cha Mufti wa Misri, Profesa Ali Juma.

 

 

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas