Haiba ya Uislamu – Miongoni mwa Uka...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haiba ya Uislamu – Miongoni mwa Ukawaida wake

Question

Ni zipi sifa kuu za ukawaida wa Haiba ya Uislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
1- Haiba ya Uislamu imekusanya kila kitu kwa sababu ni ibara ya chimbuko la kiitikadi za kiibada kwa ujumla wake mwono wa dini ya Uislamu ambao unajiimarisha katika mwono wenye kutoa mbinyo unaotoa nusu ya ukweli na kuizinga nusu nyingine.
Mifano ya haiba ya Kiislamu, uzio wake unaanza kutoka duniani na kumalizikia mbinguni. Haiba ya Kiislamu haipambani kwa ajili ya kuiongoza tabia ya kiutu katika harakati za msuguano wake wa kila siku kwenye dunia hii. Lakini, inapaa na tabia hii ili ifungamane na ishikamane na mbingu. Hivyo, mtu wa kiungu si chochote isipokuwa ni mfano wa haiba ya Kiislamu, na anakosea vibaya mno yule ambae anadhania kwamba mtu huyu wa kiungu ni yule aliye katika kuelekea kwenye kibla cha msikiti au kilele cha mlima.
2- Kufunguka kinadharia ni moja ya ukawaida wa haiba ya Uislamu. Qur`ani Tukufu haikuvizamisha vichwa vya wafuasi wake katika usasa uliopo uliochimbuka kutokana na yaliyopita, wala katika ya kale yaliyokatika (yaliyoachana) na mustakbali wake ujao; Qur`ani Tukufu imeweka misingi ya mazingira ya binaadamu katika mahusiano yake yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Na inaonekanwa kwamba kufunguka kinadharia katika nadharia ya Kiislamu ni suala kuu la kimsingi. Kwa ajili hiyo, ndio unamkuta Mwislamu amefunguka kuendana na muda katika nyanja zote na katika kila eneo na peo zake zote. Ameshafunguka kwenye kila tamaduni za kale na za sasa. Na kupitia majadiliano haya ya kinadharia na kitamaduni, Mwislamu anaupangilia mwono wake wa Kiislamu katika kivuli cha mtindo na njia ya Uislamu.
Hii haina maana kwamba kufunguka kinadharia kunaleta utayari wa kubadili imani kama ambavyo unabadilisha rai na maoni, kwa sababu shina la nadharia ya Kiislamu haligeuki wala kubadilika, na wala haliegemei wala kumili kwa jambo lenye kulitengua shina hilo. Lakini shina hili lipo tayari kuendelea kwa lengo la kukaguliwa na kuboreshwa katika ngazi mbali mbali. Shina hilo linaweza kuchukua umbo la kisayansi na kiakedemia, au umbo la kifalsafa, au umbo la kimjadala, au namna nyingine yeyote. Ufanyikaji huu wa maumbo tofauti haumaanishi kutowezekana kwa namna yeyote ile ya nadharia ya Kiislamu kutokana na umbo jingine, lakini ina maanisha uwezo wa kuzitii namna zote za maumbo. Hivyo, katika zama za mantiki ya kisayansi ambazo zinahitaji misemo ya kisayansi, na katika zama za kifalsafa ambazo zinahitaji misemo ya kifalsafa; tunaikuta nadharia ya Kiislamu ina uwezo wa kujifungua kwenye mwito wa mahitaji ya kila zama na utamaduni wa kila zama ambazo zitamlazimisha Mwislamu kujiwekea kinga kwa silaha na kwa mantiki ya utamaduni huu. Hayo yanarejea katika ukweli wa tabia ya Uislamu kama ni imani yenye uwezo wa kukusanya zama hizo kwa pande tatu: Wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Na uwezo wa Uislamu kama ni imani ya kutendeana na tamaduni za aina zote bila ya woga au kufadhaika kwa yale yanayopambanuka na imani hii kutokana na vipengele vya mrundikano, umilele kudumu, na kujifungua.
Hivyo, kufunguka kinadharia kwa haiba ya Uislamu ni mjengeko wa mwanzo katika mijengeko au ukawaida wa haiba ya Kiislamu, na sio mabishano kwamba je mfunguko huu upo au haupo, lakini inatosha tu ni kutoka wapi na unaelekea wapi?
3- Miongoni mwa maumbo (mijengeko) ya haiba ya Kiislamu ni: Utiifu wa kiuongozi ambao tunaukuta kwa Mwislamu katika ile misuguano yake mikubwa pamoja na uhalisia wa kiutu, akijaribu kuubadilisha kuelekea kuwa bora zaidi. Hivyo, haiba ya kweli ya Kiislamu muda wote inashughulikia kwa jaribio la kishujaa na kwa ajili ya kuzibadilisha sura za vitu, kama kuubadilisha uhalisia wa kiimani, uhalisia wa kijamii, na uhalisia wa kinadharia; ili iwe karibu kwa kadri iwezekanavyo kuelekea kwenye maadili ya Uislamu, roho yake na njia yake. Hayo yanarejea katika ukweli kwamba mwono wa Kiislamu unasisitiza juu ya ulazima wa kuchanganya kati ya dini na dunia, na ulazima wa kuzigandanisha kati ya itikadi na sharia, na kati ya imani na uhalisia. Hivyo, utiifu wa kiuongozi ni ukinaifu unaochimbuka kutokana na mwendo wa msuguano wa mtu Mwislamu na uhalisia wake. Utiifu huo unatengeneza mwendo au mtikisiko wa kitendo chake kwa njia ya kuvuta picha kikamilifu kwa suala la imani, na kwa njia ya kusifika kwake kwa uwazi kwa kufunguka kinadharia.
4- Katika maumbo (sura) ya haiba ya Kiislamu ni: Kumudu kikamilifu juu ya kutengeneza misemo (makala) katika mtazamo unaosimama juu ya msingi wa Kiislamu. Hivyo, kumudu kujenga mtazamo maana yake ni kuizungumzisha akili ya Kiislamu na isiyokuwa ya Kiislamu kwa lugha ya zama yake inayoishi kwa njia ya kuvutia kiujumla ambayo itazuia misamiati yote ya kitendo cha kinadharia katika Uislamu wetu mtukufu. Hivyo katika uchumi inapasa tutumie mtazamo wa uchumi wa Kiislamu ambao utaipinga mitazamo yote ya kiuchumi, na katika elimujamii inapasa tutumie elimujamii ya Kiislamu ambayo inaipinga mitazamo yote ya elimujamii, na katika nadharia ya kiimani inapasa kwa kutumia mtazamo wa Kiislamu tuipinge mitazamo yote ya kiimani, na namna kama hii.
Inawezekana kusema kwamba ubaya wa nadhari ya Kiislamu katika zama zake za mwisho unarejea kwa yale yanayorejea kwenye kupoteza uwezo wa kujenga mtazamo (kuyachunguza mambo). Na hii inamaanisha kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na mambo yanayozuka katika zama husika kutokana na utofauti wa madhehebu na mitazamo. Na miongoni mwa sifa za msingi za haiba ya Kiislamu ni kuweza yeye – haiba - pekee kuunda misemo au makala za kiimani na kisharia katika mitazamo tofauti. Hivyo, Uislamu – kwa mfano– una falsafa ya kiuchumi iliyoshikamana ambayo inawezekana kunyofolewa kutoka kwenye misingi mikuu, na kuteremka nayo kwenye misamiati ya uhalisia wa maisha, na kuiweka katika fremu yenye kukubalika kufanyiwa kazi na kutumiwa. Hivi ndivyo tunavyoukuta Uislamu ukiwa na falsafa jumuishi ya kimamboleo ambayo inawezekana kupelelezwa katika uhalisia wa misingi mikuu na kuiwekea utaratibu wake katika mtazamo wa kimamboleo uliorekebishwa katika fremu yake ya kinadharia kwa ajili ya uhalisia wa akili ya mtu wa kileo. Na ndio namna kama hii kwa nyanja mbali mbali. Haliwezi kutimia jambo hili isipokuwa kwa kumudu kikamilifu kujenga mtazamo. Wala haimaanishi kuweka utaratibu wa misemo au makala za Kiislamu katika mtazamo wowote kama vile mtazamo wa kiuchumi wa Kiislamu au mtazamo wa kimamboleo wa Kiislamu…. Hayo hayamaanishi kuwa ni kuuvunja Uislamu wote vipande vipande na kuwa ni baadhi tu ya mitazamo, bali hili linamaanisha ulazima wa uwezo wa nadharia ya Kiislamu juu ya kusema tamko lake katika nyanja za mjadala wa uwepo na metafizikia (falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa) vyote kwa pamoja. Na hapana budi upatikane na haiba ya Kiislamu ili itekeleze jukumu lake kwa vitendo katika kusudio hili, ikivutia misingi yake ya Kiislamu ambayo itakuwa na uwezo wa kuingia na makala au misemo yake na mitazamo yake kwenye ulimwengu wa akili na dhamira ya wanamamboleo. Hapa pekee inawezekana kuwa mchango wa haiba ya Kiislamu mamboleo ni tendaji na ni wenye uwezo na ni chanya. Hivyo kumudu kwa haiba ya Kiislamu kwa kujenga mtazamo sio anasa ya kinadharia ya kileo, bali ni ulazima wenye masharti ya kuuamini ujumbe na risala ya Uislamu na ulazima wa kuinyanyua bendera yake.
5- Miongoni mwa ukawaida wa haiba ya Kiislamu ni: Imani chanya. Imani ya Kiislamu ni imani inayovuka kukinai kinafsi kwa imani kuwa ni mwingiliano wa kudumu pamoja na uhalisia wa kimaisha na kukabiliana na yale yenye kumkana Mwenyezi Mungu. Bali na kukabiliana na imani hasi iliyojificha katika ufujaji ulioshindwa wenyewe kufanya upekuzi na kujadili pamoja na kuulinda mnasibiko wa kiimani. Dalili ya wazi juu ya umbo la msingi linalotokana na ukawaida wa haiba ya Kiislamu ni wingi wa mataifa ambayo Uislamu umeyaingia sio kwa njia ya ukombozi na vita, lakini kwa njia ya msuguano wa wafanyabiashara Waislamu na Wakisufi waliokuwa wakisafiri sana na ambao wamebeba ulinganiaji (daa’wah) wa Uislamu kuupeleka maeneo ya mbali ya bara la Asia na Afrika. Wakanufaika na haiba ya kweli ya Kiislamu ambayo kwa kutumia ukawaida wake wa Kiislamu imeweza kung’arisha vitongoji hivyo kwa nuru ya Uislamu. Hivyo basi, tunakosea ikiwa tunavuta taswira kwamba imani ni mti wenye kivuli ambao tunatua mizigo yetu chini yake kisha tunalala. Kwa hakika kiwango cha mivutano, mapigano, majadiliano ya kinadharia na kiimani ndio majaaliwa yetu yaliyokwishaamuliwa, na wala haiwezekani kabisa kukabiliana navyo au kupambana navyo kwa imani isiyokuwa na vitendo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: Kuhusu nadharia ya Kiislamu kwa namna ya kifasihi (Fil Fikril Islaamiy minal Wajhatil Adabiyya), kilichoandikwa na Dk. Muhammad Ahmad Al-Azb. Kairo: Baraza la Juu la Utamaduni, 1983 A.D. (uk. 47 – 70).
 

Share this:

Related Fatwas