Ufafanuziwa wa Ibara ya (Swala kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ufafanuziwa wa Ibara ya (Swala kwa Kutumia Hekima za Ibn Atwaaillahi.

Question

 Nilisoma ibara inayosema: Kama Swala ingejuzu kwa kutumia kitu kingine kisichokuwa Qurani, basi ingejuzu kwa kutumia Hekima za Ibn Ataillahi As-sakandariy. Je, inajuzu kuikariri ibara kama hii?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Maana ya ibara iliyotajwa kuwa: Sharia sharifu ingejuzisha kuiswali swala kwa kusoma maneno isipokuwa maneno ya Qurani tukufu, miongoni mwa maneno ya kawaida ya binadamu, yanayolingana na umuhimu wa ibada ya swala, na yanayoihusu ibada hiyo katika unyenyekevu, kujitupa na kuutafakari utukufu wa Mwenyezi Mungu, hapo ingejuzu bila shaka kuifanya kwa kusoma Hikima za Ibn Ataillahi As-Sakandariy R.A. Naye ni Imamu, mwanachuoni, mfuasi wa Madhehebu ya Malik, na walii mufasi wa usufi, mwenye kuupa nyongo Ulimwengu, na miongoni mwa nguzo za Twariqa ya Shadhuli, iliyoasisiwa na Sheikh Abul-Hassan Ashadhuliy, Mwenyezi Mungu amrehemu. Na yeye ni Taju-Diin Abul-Fadhl Ahmad Ibn Muhammad Ibn Abdul-kariim Ibn Abdur-Rahmaan Ibn Abdullahi Ibn Ahmad ibn Issa Ibn Al-Hussein Ibn Ataillahi Al-Judhamiy kinasaba.
Hekima za Ibn Ataillahi ni mkusanyiko wa kanuni na misingi inayomwongoza Mwislamu kwa kumwelekeza adabu za mwenendo wa imani na ihsani, na zilizoandikwa na Ibn Ataillahi As-Sakandariy, akaweka ndani yake matokeo ya majaribio yake ya kisufi na njia za maarifa ya kiroho za ngazi ya juu, na zilibahatika kuwa umaarufu, na kupata baraka, na kukubaliwa na watu wote, na zilikuwa na msingi wa ulezi na mwenendo wa makundi mengi ya Masufi mpaka wakati huu, na zilikuwa na uangalizi wa wanachuoni ngazi iliyowapeleka kuandika maelezo mengi, miongoni mwayo ni Maelezo ya mtaalamu Ibn Ajibah yaitwayo: (Iqaadhul-Himam Fi Sharhil-Hikam), na Maelezo ya Mtaalamu wa Madhehebu ya Shafiy Al-Khatib Ashirbiniy katika kitabu chake: (Sawatiu’l-Hikam), na Maelezo ya Mwanachuoni wa Fiqhi ya Madhehebu ya Malik, Ahmad Razuq, yaitwayo: (Quratul-Ain), na Maelezo ya Mtaalamu Ibn Abbad katika kitabu chake: (Ghaithul-Mawahib Al-Aliyyah Fi Sharhil-Hikam Al-Ataiyyah).
Maana inayoonesha ibara ilyotajwa haina utata wala aibu kwa sababu mbili:
Sababu ya kwanza: ibara hii ni muundo wa kisharti, na haiwajibiki iwe sahihi na kweli itekelezeke kimatendo, bali inatosha kuwa na mfungamano kati ya sehemu yake mbili, kitenzi cha kwanza na kitenzi cha pili, ni sahihi; au kwa maneno ya mantiki: inatosha kuwepo usahihi kati ya mwanzo na mwisho wake, kama ilivyotajwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lau kama wangalikuwako humo (mbinguni na ardhini waungu (wengine) isipokuwa Mwenyezi Mungu: bila shaka zingeharibika (hizo mbingu na ardhi)}. [AL ANBIYAA: 22], na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kama tungalitaka kufanya mchezo, tungejifanyia sisi wenyewe, (tusingekutieni kati), kama tungekuwa wafanyao mchezo}. [AL ANBIYAA; 17], Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: “(Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema angalikuwa na mtoto ningekuwa wa kwanza wa kumuabudu (mtoto huyo kwa kuwa ni mtoto wa Mungu wangu”). [AZ ZUKHRUF: 81]. Mafungamano haya ya kisharti ni kweli na sahihi kwa kuwa ni maneno ya Mola wa walimwengu, ingawa hayawezekani kuyatekeleza kimatendo, kwa sababu waungu wengi na kuwepo mtoto, kwa Mwenyezi Mungu au kuwa na mchezo ni muhali kwake kiakili na kisheria, lakini usahihi wa sala kwa kutumia maneno ya kawaida ni hukumu ya kisheria inayoweza kuitekeleza kifikiria, na kama inapojuzu kufungamana jambo moja na jambo la muhali kimatendo, basi inajuzu kulifungamana na jambo la uwezekano kufikiria, na matokeo ya hayo ni usahihi wa kufungamana na kufanya sala kwa kutumia Hekima ya Ibn Ataillahi ikifikiriwa kuwepo usahihi wa sala kwa kutumia maneno yasiyotokana na Qurani tukufu, na mfano huu wa kufungamana hukumu za kisheria ulitajwa katika Hadithi ya Mtume SAW. Na Imamu Ahmad ameipokea Hadithi hiyo katika kitabu chake, kutoka kwa Anas Ibn Malik kuwa Mtume SAW, alisema: “Haijuzu kwa binadamu amsujudie binadamu mwingine, na lau ingelijuzu binadamu amsujudie mwingine, ningemwamuru mke amsujudie mumewe, kutokana na haki kubwa ya mume kwa mkewe”.
Muundo wa kimantiki wa ibara iliyopo katika swali na maana zake zinazopatikana ni zifuatazo:
Kama ikifikiriwa kuwa sala inasihi kwa kitu kisicho cha Qurani, miongoni mwa maneno sharifu na ya fasaha, basi inafikiriwa kuisihi kwa kusoma Hikima ya Ibn Ataillahi; kwa kuwa ni maneno yenye balagha na maana yake ni shrifu sana, hukaribia yawe wahyi, isipokuwa msemaji ni walii mtawa na siye Nabii masum, na haya ni ilhamu kwa Mwenyezi Mungu yanayostahiki kuwa utii wa Allah kwa njia ya kuyasoma, kuyazingatia, na kuyatafakari katika maana yake ndani na nje ya sala.
Jambo la pili: maana inayovuta bongo wakati wa kusikia ibara hii au kusoma kwake ni ngazi ya juu ya Hikima za Ibn Ataillahina maana yanayokuwepo ndani yake na kunga sharifu zinazokaribia nafsi na Mwenyezi Mungu na kuiongoza njia ya ridhaa yake na kupamba tabia na kuangaza moyo, na kwa hakika Hikima hizi za Ibn Ataillahi zinang’ara kwa nuru na upole wa kunga ambazo hazizingatiwi ila na nyoyo za waja waaminifu wa Mwenyezi Mungu na vifua vya walii wake wanaokaribishwa, na Mwenyezi Mungu ameweka ndani yake heri na baraka zinazoonesha kuwa ni ilhamu halisi ambazo Mwenyezi Mungu amezifunulia moyo wa walii mtawa Ibn Ataillahi, kama karama kwake hasa na upole kwa waja wake kwa jumla, kama vile Mwenyezi Mungu amemfunulia Mtume SAW, Qurani tukufu na ameiteremsha moyoni mwake ili iwe rehema kwa walimwengu, kwahiyo, sala ingesihi kwa kutumia maneno yasiyo ya Mwenyezi Mungu, na Manabii wake, ingesihi kwa kutumia maneno ya ilhamu yake na walii wake; kwa kuwa yote ni kutoka kwa Allah, na yote ni kwa ajili ya kuongoza viumbe na kuwaelekeza njia ya haki,
Na Maimamu walisema kuwa: yanayojuzu yawe miujiza kwa Nabii, yanajuzu kuwa karama kwa walii. [Fatawa AlAllamah Shihabud-Din Ar-Ramliy: 4/337, Ch. ya Al-Maktabah Al-Islamiyah; Tafsiir Al-imam Ar-Raziy; Mafatiihul-Ghaib: 6/497, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy; Sharhul-Maqasid, na Assa’d At-taftazaniy: 2/203, Ch. ya Dar Al-maarif An-Nu’maniyah].
Imamu An-Nawawiy katika [Sharh Shihi Muslim: 16/108, Ch. ya Dar Ihiyaa At-turaath Al-Arabiy] anasema: “Karama zinaweza kutokea kwa mambo yasiyo ya kawaida katika aina yo yote iwayo, na baadhi ya wanachuoni wamezikataza, wakadai kuwa zinahusu mambo maalum kama vile kuitikia dua n.k., na hili ni kosa la aliyesema hivi na kukana kwa hisi, bali ukweli ni kuzitokea kwa kubadilika hakika ya mambo na kuleta vitu na hali ya kutokuwa”. [Mwisho].
Wahyi wa Mwenyezi Mungu ni muujiza unaohusu Manabii, na inawezekana kutokea mafano wake unaohusu mawalii, nao ni ilhamu ya Mwenyezi Mungu, na Mtume SAW, alisema: “Hakika ilikuwa katika hao waliotangulia watu wenye busara, na miongoni mwao katika umma wangu ni Umar Ibn Al-Khattab”. [Ameipokea Hadithi hii Bukhariy katika kitabu chake, kutoka kwa Abuu-Huraira R.A, na ameipokea Muslim kutoka kwa Aisha RA].
Imamu Nawawiy katika kitabu chake: Sharh Muslim: [15/166, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] anasema: “Wanachuoni wanahitilafiana katika kufafanua maana ya (wenye busara): Ibn Wahb anasema; wenye ilhamu, na imesemekana: wenye usahihi, na wakidhani, basi wao kama kwamba wakizungumziw na kitu, na imesemekana; wanazungumziwa na Malaika, na katika mapokezi: wanasemwa, na Bukhariy anasema: ndimi zao hutamka usahihi, na hizi ni dalili za karama za mawalii”. [Mwisho].
Na ilhamu ya kweli ilikuwa miongoni mwa sifa kuu za Amiri wa waumini Umar Ibn Al-Khattab RA, kwa sababu baadhi ya ilhamu zake zimelingana na hukumu za Wahyi, na pengine na lafudhi zake pia hata kabla ya kuziteremshwa, na imepokelewa na Anas Ibn Malik RA, akisema kuwa Umar Ibn Al-Khattab RA, amesema: “Nililiwafikishwa na Mola wangu mara tatu: Niliposema Ewe Mtume wa Allah: Tuchukue usimamizi wa Ibrahimu mahali pa kusalia, basi Aya ikateremshwa: {Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahimu pafanyeni pawe pa kusalia}. [AL BAQARAH: 125]; Na Aya ya Hijabu, niliposema Ewe Mtume wa Allah waamrishe wake zako kuvaa Hijabu, kwa sababu wanakutana na watu, na miongoni mwa watu hawa ni wema, na wengine ni wabaya. Basi Aya ya Hijabu ikateremshwa; na wake za Mtume S.A.W, walikuwa na wivu wenyewe kwa wenyewe kwa Mtume, niliwasema: {(Mtume) akikupeni talaka, Mola wake atampa, badala yenu, wake wengine walio bora kuliko nyinyi}, basi Aya hii ikateremshwa”. [Wameipokea Bukhariy, na hii ni lafudhi yake; Muslim kutoka kwa Ibn Umar].
Na kutoka kwa Abi-Huraira Ra, alisema: Nilimsikia Mtume S.A.W, akisema: “Hakikubaki katika utume ila bishara njema, wakasema: ni nini bishara njema? Akajibu: ni ndoto nzuri”. [Ameipokea Bukhariy].
Na kutoka kwa Abi-huraira R.A, na Mtume S.A.W., amesema: “Itakapokaribia mwisho, huenda ndoto ya mwislamu haikaribia uongo, na mwenye ukweli wa ndoto kati yenu ni mwenye ukweli wa mazungumzo, na ndoto ya mwislamu ni sehemu moja ya sehemu arobaini na tano za Unabii, na ndoto ni aina tatu: ndoto nzuri, nayo ni bishara ya Allah; nandoto inayohuzunisha na shetani; na ndoto ya kujizungumzia mmoja nafsi yake, na mmoja kati yenu akiota ndoto ya kuchukiza au kutisha, basi asimame na kusali, na wala asiwasimulie watu kitu cho chote kuhusu ndoto hiyo”. [Ameipokea Muslim].
Matini hizi sharifu huonyesha kuwa ndoto nzuri, na ilhamu za kweli ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na miongoni mwa aina za Wahyi wa manabii, ili mawalii waliojongelewa na waja wake Mwenyezi Mungu wapate bishara na waongozwe kwa uongofu.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: inabainika kuwa ibara iliyotajwa katika swali iwe ni kwa upande wa kimuundo au kimaana, na kwa kuikariri sana, hakuwajibishi dhambi wala kosa lolote la kisheria.


Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas