Ulinzi wa Maeneo ya Majengo ya Mabaki ya Kale – Maeneo ya Kidini.
Question
Je, Uislamu unahimiza ulinzi wa majengo na mabaki ya kale na maeneo yaliyoshuhudia matukio ya kihistoria yenye mwelekeo muhimu wa kidini, au hayo ni marufuku, kwani kuyatukuza maeneo hayo ni jambo lililo haramishwa, na zinaweza kuwa ni katika njia za ushirikina kwani huwapelekea watu kuamini kuwa maeneo hayo yana baraka kama wanavyodhani baadhi ya wanaojinasibisha na elimu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ulinzi wamaeneo na majengo ya kihistoria na magofu ya kale yenye umbo la kihistoria ni katika mambo yanayotakiwa kisheria na yapendezayo kidini na ambayo yamehimizwa na sheria; kwani ndani yake kuna utukuzo aliouweka Mwenyezi Mungu Mtukufu katika masiku, matukio, maeneo, watu, na matendo yao mema yaliyopatikana ndani yake na kufungamana nayo. Basi hayo yanawakumbushia waislamu siku zao za kale na kuiunga mioyo yao kwa uhalisia wake na siku zake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kitabu chake kitakatifu: {Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu} [IBARAHIMU 5].
Jambo hili halina mipaka katika kuyataja masiku ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; ambayo ni matukio ya Mwenyezi Mungu katika nyakati zilizopita. Kila kinachopatikana kwa utajo huu huwa ni njia ya kukifanikisha kwake na hutakiwa kisheria. Na Msingi wa Kisheria unasema: "Hakika njia huchukua hukumu ya Makusudio Makuu" na "kwamba kisicho na mipaka huendelea kuwa hivyo hadi panapo kuwepo kinachokifungamanisha".
Imamu Azarkashiy alisema katika kitabu cha: [Al Bahru Al Muheetw 8/5, Ch. Dar Al Kutubiy]; "Na habari inapokuwa bila mipaka hakuna kinachoifungamanisha huchukuliwa hivyo hivyo kama lilivyo".
Na pia miongoni mwa faida kuu kwa ukumbusho huo kwamba inatoa dalili ya kihalisi kwa usahihi wa matukio hayo ambayo yalitokea. Ama kuondosha na kuvunja ndicho kinachokuwa njia ya kupinga matukio haya kutokana na asili yake, na kudai kuwa ni mambo yaliyotengenezwa na hayana msingi wowote wa uhalisia.
Na miongoni mwa Makusudio ya Sheria ni ufungamanishaji baina ya Ibada na matendo ya kidini na maeneo ambayo kiasili hutajwa kihistoria ya Dini: kama vile Swafa na Marwa ambayo Bibi Hajar R.A. alikuwa akienda na kurejea baina yake; basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mjuzi} [AL BAQARAH 158].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na alipo kuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia} [ALBAQARAH 125], na ikaja katika tafsiri ya Makamu (pahali pa kusimama kwa Nabii Ibrahimu) kwamba hilo ni jiwe ambalo lina athari ya mguu wa Bwana wetu Ibrahimu au mahali ambapo palikuwa na jiwe ambalo Bwana wetu Ibrahimu alikuwa akisimama juu yake alipotoa adhana yake kwa watu waje kuhiji au kuliinua jengo la Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hiyo ndiyo sehemu inayojulikana hivi sasa, na ikafanywa ni pahala pa kusali: panaombwa ndani yake, na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. [Tafsiri ya Al Baidhawiy 105/1, Ch. Dar Ihyaa At Turaath Al Arabiy], kwa hiyo jambo hili la kuifanya sehemu hiyo kuwa pakuswalia ni lazima palindwe, na kuiainisha sehemu husika na kuitangaza kwa watu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni} [AN NUUR 36] Ibn Marduweh alisimuliza kutoka kwa Anas Bin Malik na Buraidah R.A. wote wawili: "Kwamba Mtume S.A.W. akaisoma aya hiyo: {Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe}, basi mtu mmoja akasimama kwa Mtume S.A.W. na akasema: "Nyumba gani hizo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtume S.A.W, akasema: Nyumba za Manabii, Basi Abu Bakr R.A. akasimamia kwa Mtume S.A.W. kisha akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Na nyumba hii ni miongoni mwake? Na akaiashiria nyumba ya Ali na Fatma R.A. wote wawili, Basi Mtume S.A.W akasema: Ndiyo; Nyumba hiyo ni miongoni mwa zilizo bora zaidi kuliko zao. [Ad Dur Al Manthur 203/6, Ch. Dar Al Fikr].
Imamu Abu Haiyaan Al Ndalusiy amesema katika kitabu cha: [Al Bahru Al Muhetw 48/8, Ch. Dar Al Fikr]: "Na kilicho wazi ni kuwa katika (nyumba) kutokuwapo mipaka; huchukuliwa pia misikiti na nyumba zilizopo karibu na hapo panapo swaliwa na kufundishiwa masomo ya Dini".
Na Miongoni mwa kuinua katika aya tukufu ni: Utukuzaji –kama ilivyoelezwa katika mahali hapo katika vitabu vya Tafsiri:- Al Hafedh Ibn Ajawziy katika kitabu cha: [Zadu Al Maseer 298/3, Ch. Dar Al Kitaab Al Arabiy]: "Na katika maana ya (ameamrisha zitukuzwe) kauli mbili; moja yake: ni inatukuzwa", Al Hasan na Al dhahak wakasema hayo.
Basi Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alitoa idhini – yaani aliagiza – kwa kutukuza mahali hapo, basi kuwa na ulinzi wake ni lazima zaidi kuliko utukuzaji wake. Kwa kuwa kuondosha kunapingana na utukuzaji unaotakiwa pia na usio na mipaka usiozuiliwa isipokuwa kwa kile kilichozuiliwa na Sheria kwa sifa maalumu.
Na Al Baraaz alisimulia katika kitabu chake: [Al Musnad 230/12], kutoka kwa Omar R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W amekataza kubomoa kingo za Madina.
Na Atwahawiy alisimuliza katika kitabu chake: [Sharhu maaniy Al Athaar 194/4]; kutoka kwa Ibn Omar R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Msizivunje zio za mji kwani zio hizo hupendezesha mji. Na kingo ni kuta za mji".
Na juu ya Hadithi hii Imamu Al Haithamiy aliweka mlango katika kitabu chake cha: [Majma' Az zawaid 301/3, Ch. Al Qudsiy]; Basi akasema: "Mlango wa ukatazo wa kubomoa majengo yake – yaani Madina"
Na maswahaba wema R.A. wote walikubaliana kuombea Baraka katika mahali pa swala ya Mtume S.A.W. na jamaa zake, na hayo kwa kukubali kwa Mtume S.A.W. na tendo lake; basi walikuwa wakimwomba Mtume S.A.W. kuswali katika nyumba zao, ili wafanye mahali pa kuswali kwake kama mahali pa kuswali kwao, basi Al Bukhariy, Muslim na wengine wameitoa Hadithi (kutoka kwa Mhamoud Bin Ar Rabie' Al Answariy R.A. amesema: Nimemsikia Utbaan Bin Malik Al Answari, kisha Ahad Banu Salim R.A. alisema: Nilikuwa nikiswali na jamaa zangu Banu Salim basi nikaenda kwa Mtume S.A.W. basi nikasema: Hakika mimi nimeyazuia macho yangu na hakika mafuriko yamekuwa kizuizi baina yangu na msikiti wa watu wangu na ningependelea wewe uje na uswali nyumbani kwangu katika sehemu na niifanye sehemu hiyo kuwa ya Kuswalia. Akasema: Nitafanya hivyo akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi kesho iko juu yangu Mtume S.A.W. na alikuwa pamoja naye Abu Bakr R.A. baada ya mchana, kwa hivyo Mtume S.A.W. akatoa idhini, na mimi nikamwidhinisha: Basi hakukaa hadi akasema: Ni sehemu gani ya nyumbani kwako wewe unapendelea mimi niswali? Basi akamwashiria sehemu ambayo alipendelea aswalie hapo, akasimama nasi tukajipanga mistari nyuma yake kisha akatoa salamu na tukatoa salamu baada yake.
Na maswahaba R.A. wao wote walikuwa wakizichunguza sehemu alizoswalia Mtume S.A.W. na sehemu alizopata kuzitembelea au kuketi kwake, safari zake na athari yake na wakawa wanajipatia baraka kwazo na kuzitukuza pamoja na kuzuia zisidharauliwe. Na Imamu Al Bukhariy ameweka milango katika maudhui hii katika kitabu chake cha: [Sahihi] kwa kauli yake: "Mlango wa misikiti ambayo katika njia ya Madina na Mahali paliposwaliwa na Mtume S.A.W, na jamaa zake". Kisha akasimulia kutoka kwa Musa Bin Oqbah akasema: Nilimuona Salim Bin Abdillah akiyachungua maeneo ya njia na kuyaswalia. Na anasimulia kwamba baba yake alikuwa akiyaswalia maeneo hayo. "Na kwamba alimwona Mtume S.A.W. anaswalia katika mahali hapo". Na akasema: Nafia alinihadithia kutoka kwa Ibn Omar R.A. wote wawili, kwamba alikuwa akiswalia katika mahali hapo. Na nikamuuliza Salim sijui chochote kwake isipokuwa alikubaliana na Nafia katika sehemu zote, isipokuwa wao wawili walitofautiana katika Msikiti ndani ya eneo la Sharafu Ar Rawhaa.
Na Miongoni mwa hayo alighadhibika Bibi Aisha Mama wa waumini R.A. na wengineo miongoni mwa wafuasi kutokana na yaliyotendwa na Marwaan Bin Al Hakam alipomsulubisha mtu mmoja aitwaye Dhubaba katika eneo la Dhubaba, nalo ni eneo aliposwalia Mtume S.A.W na palikuwa sehemu na Quba lake, kama ni alama ya kutukuza maeneo alimoswalia Mtume S.A.W, kwa yale yasiyoendana napo.
Na Ibn Shaibah akasimulia katika kitabu chake cha: [Tariekh (Historia ya) Al Madinah 62/1, Ch. Jedah] kutoka kwa Al Harith Bin Abdulrahmaan Bin Abi Dhubab akasema: Bibi Aisha R.A. alimtumia ujumbe Marawaan Bin Al Hakam alipomwua Dhubaba na akamsulubisha juu ya Dhab: "Umechoshwa; Mtume S.A.W, alipaswalia, nawe ukapafanya kuwa ni eneo la kusulubia!". Na akasema: Dhubab ni mtu miongoni mwa watu wa Yemen alipitia mtu mmoja miongoni mwa Al Nswaar… Abu Ghassan akasema: Na baadhi ya Masheikh wetu wameniambia kwamba masultani walikuwa wakiwasulubia watu juu ya Dhubab, Basi Hishaam Bin Urwah akasema kwa Ziaad Bin Abdullahi Al Harithiy: Ajabu iliyoje! Mnawasulubia watu katika eneo lenye Quba la Mtume S.A.W,? Basi Ziaad aliacha jambo hilo na viongozi wengine waliokuja baadaye yake nao wakaliacha jambo hilo.
Ama madai ya kuwa utukuzaji wa mahali ni haramu, na zinaweza kuwa ni katika njia za ushirikina kwani huwapelekea watu kuamini kuwa maeneo hayo yana baraka basi madai hayo hayakubaliki, Kwani Sheria haizuii Uwazi wa kumtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa kinachozuiwa ni kile kinachokuwa katika hali ya kukiabudu kinachotukuzwa kama walivyokuwa wakifanya watu wa enzi za Ujahilia kwa vile wanavyoviabudu vilivyo batili na wakawa wanaamini kuwa hivyo vitu ni miungu, na kwamba inadhuru na kunufaisha kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na ama visiyokuwa hivyo katika vinavyoonesha heshima na unyenyekevu na utukuzaji inajuzu iwapo anaepewa cheo hicho anastahiki hata kama ni kitu kilicho mfano wa nyumba au kingine chochote; Na Al Bihaiqiy akasimuliza katika Sanadi yake kwamba Mtume S.A.W. alikuwa kama akiona nyumba anainua mkono wake na kusema: "Ewe Mola izidishie nyumba hii ubora, utukufu, na ukarimu pamoja na kipawa".
Adarmiy amepokea kutoka kwa Ekrimah Ibn Abi Jahl R.A. kwamba alikuwa akiweka Msahafu juu ya uso wake na akisema: "Kitabu cha Mola wangu, Kitabu cha Mola wangu".
Basi, kwa hiyo kukipa cheo kile kilichopewa cheo na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumtukuza Mwemyezi Mungu. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo}. [AL HAJ 32]. Na pia utiifu kwa Mtume S.A.W. ni utiifu kwa Mwnyezi Mungu Mtukufu ambaye alimtuma: {Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao.} [AN NISAA 80]. Na ufungamao wake ni ufungamano wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakikawanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao} [AL FATH 10]
Ama zinaweza kuwa ni katika njia za ushirikina kwani huwapelekea watu kuamini kuwa maeneo hayo yana Baraka, Kwani hiyo imejengeka kwa kasoro katika mweleweko wa shirki; kwa hivyo Shirki ni Kumtukuza mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, au kumtukuza asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwa ajili hiyo, sijida ya Malaika kwa Adamu A.S., ilikuwa kwa ajili ya Imani na Upwekeshaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Washirikina kuyasujudia Masanamu ni ukafiri ingawa katika hali zote mbili kinachosujudiwa kimeumbwa.
Lakini Malaika kumsujudia Adamu A.S, ni kukipa cheo kile alichokipa cheo Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyoamrisha yeye, basi hiyo ni njia ya inayokubalika ambayo Mtendaji anastahiki thawabu, na kwa kuwa makafiri kuyasujudia masanamu ni kuyatukuza kama anavyotukuzwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hii ni shirki mbaya ichukizayo na mwenye kuifanya anastahiki adhabu.
Na kuamini uwepo wa baraka au kupatikana kwake kupitia kiumbe fulani hakuna uhusiano wowote na ushirikina kwa karibu au kwa mbali sembuse kukawa ndio njia yake. Isipokuwa ikiaminika kuwa kiumbe huyo anaathiri yeye kama alivyo, katika kuleta baraka kwa upekee wake, ama mtu anapoamini kuwa baraka hutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na kwamba yeye ndiye mwenye kuifanya iwe kwa mtu maalumu au kitu maalamu, au eneo maalumu, na kwamba baraka ipo kwenye vitu hivyo na sio kwa ajili ya vitu hivyo; kwani hakuna mwenye kuuathiri Uwepo huu wa Ulimwenguni isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huu ndio Upwekeshaji wenyewe haswa; kwani katika Upwekeshaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna vitendo.
Na zimekusanywa dalili nyingi zinazothibitisha Uwepo wa baraka katika viumbe kwa kupewa viumbe hivyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Alitusimulia kisa cha kuteremka sanduku ambalo lilikuwa limejaa athari za Manabii – ambalo lilikuwa likiombwa Baraka – juu ya Waisrail, Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza cha nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Mussa na kina Haruna,wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini.} [AL BAQARAH 248].
Akasema katika kitabu cha: [Tafsiri ya Jalaleen] {Alama ya ufalme wake nikukuleteeni lile sanduku}; Kisha lilikuwa na picha za Mitume, akaliteremsha kwa Adamu A.S, na likaendelea kuwafikia, wenye mabavu wakawashinda na wakalichukua na wakawa wakilifungua fungua kwa maadui zao na kwenda nalo vitani na kutulizana kwa sanduku hilo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mna ndani yake kituliza nyoyo zenu}, utulizo kwa mioyo, {kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, namna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Haruna} Na vitu hivyo vilikuwa ni viatu vya Musa na fimbo yake, Kilemba cha Haruna, kibuyu ya asali ambayo ilikuwa ikiteremka juu yao, na kisehemu cha mbao.
Na Maswahaba kuomba Baraka kutoka kwa Mtume S.A.W. katika maisha yake na athari zake baada ya kifo chake, na hata kutoka mahali ambapo alikuwa akienda, kunajulikana katika vitabu vya Sira na Hadithi.
Na miongoni mwa yaliyopokelewa na Al Bukhariy; "Kutoka kwa Ishaq Bin Abdullah Bin Twalha kutoka kwa Anas R.A. Hakika mama Sulaim alikuwa akimtandikia Mtume S.A.W, jamvi na Mtume S.A.W akawa analala kwenye jamvi hilo kwa mama huyo. Akasema: Na Mtume S.A.W, alipolala mimi nilikuwa nachukua jasho lake na kulikusanya kwenye chombo, kisha hulikusanya kwenye kichupa. Akasema: Na Anas Bin Malik alipojiwa na umauti aliniamrisha mimi nikiweke kwenye kichupa hicho kwenye sanda yake. Na akasema: Nikaweka kwenye sanda yake.
Na Imamu Bukhari alipokea kutoka kwa Ibnu Siriin akasema: nikamwambia Ubaidah: "Tuna baadhi ya nyewele za Mtume S.A.W., tumezipata kutoka kwa Anas, au kutoka kwa jamaa wa Anas". Basi akasema: "Nikiwa na unyewele wake ni bora zaidi kwangu mimi kuliko Dunia nzima na vilivyomo".
Na Ibn Asukan alipokea kutoka kwa Thaabit Al Bananiy kwamba alisema: Anas Bin Malik R.A. akaniambia: "Huu ni unyewele kutoka katika nyewele za Mtume S.A.W., basi uweke chini ya ulimi wangu". Akasema: "Basi akauweka chini ya ulimi wake na alizikwa nao chini ya ulimi wake". [Al Eswabah Fii Tmeez Aswahabah, Lil Hafedh Ibn Hajr 276/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na Ibn Abi Shaibah alipokea katika kitabu chake cha: [Al Mswanaf 557/4, Ch. Dar Al Fekr], kutoka kwa Yazid Bin Abdulmalik Bin Qusaitw alisema: "Niliwaona baadhi ya Maswahaba wa Mtume S.A.W, pale anapowaacha msikitini walaikuwa wakilielekea eneo la Membari na hulipangusa pangusa na kuomba dua, akasema: Nilimuona Yazid akifanya hivyo".
Na jambo hili halikuishia tu katika kujipatia baraka kunakopendelewa zaidi kwa kinachopendezesha, bali yamepokelewa maelezo yanayoashiria uhalali wa kuomba baraka unaopendelewa zaidi kwa kinachopendezesha. Basi Atwabaraniy alipokea katika kitabu cha; [Al Awswat] "kutoka kwa Ibn Omar R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W, alikuwa akimtuma aende kwenye maeneo ya kujisafishia, alete maji naye akayanywa huku akitarajia baraka kutoka katika mikono ya Waislamu".
Bali imekuja katika kitabu cha; [Aswahihi], kwamba Mtume S.A.W., alikuwa akiomba baraka kutoka katika mvua; na Imamu Muslim Akapokea: kutoka kwa "Anas R.A. akasema: Anas Amesema: Tulinyeeshewa na mvua tukiwa na Mtume S.A.W. Akasema: Mtume S.A.W. akamkinga kwa nguo yake mpaka ikajaa maji ya mvua nasi tukasema: Kwa nini umefanya hivyo? Akasema: Kwa sababu Mvua hiyo ni mgeni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Na ni kawaida ya wenye akili katika kila Umma kuyaheshimu mabaki ya kale ya waliokuja baada yao na waliowatangulia, na ilikuwa kawaida kwa Maswahaba, na Taabiina, Wanazuoni wa Umma, Maimamu wa Fiqhi na wa Hadithi, na waandishi wa historia, kuyaheshimu maeneo haya pamoja na Mabaki ya kale ya Kidini, na wakachukulia kuwa kufanya hivyo ni kuitukuza Sheria, na kazi hii ilizoeleka kwa Salafu na Khalafu (wa zamani na waliowafuatia) na hakuna yeyote katika wanaozingatiwa aliyewahi kutoa tamko la kuzuia jambo hili kwamba eti jambo hili ni ushirikina au linapelekea kwenye ushirikina.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.