Mfano wa Kimaarifa wa Kiislamu na Baadhi ya Dhana Zenye Utata
Question
Je, kuna fikra na dhana zieneazo juu ya turathi ya Kiislamu na mfano wake wa kimaarifa dhana ambazo zinapatikana kwetu kutokana na mifumo ya elimu za kisasa?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuna matatizo mengi yanayoikabili akili ya mtafiti au mtafutaji wa elimu ya kisasa wakati wa kugusa mambo ya turathi. Miongoni mwazo;
Ya kwanza: Yahusianayo na mtafiti mwenyewe; nayo ni uchache wa maarifa kuhusu mambo ya turathi katika Misingi yake na Matawi yake.
Ya pili: Ni suala tunalolichunguza hapa, nalo linaambatana na masafa yaliyo baina ya turathi na elimu ya kisasa; linaambatana na idadi ya istilahi zenye utata zinazopatikana katika elimu za kijamii na sayansi ya kibinadamu pamoja na matini za kiturathi, bali zinaambatana na matini za vyanzo viwili vikuu vyenyewe; Qur`ani Tukufu na Sunna yenye kutakaswa.
Kuna fikra na dhana zilizoenea kuhusu turathi ya Kiislamu na mfano wake wa kimaarifa; ni mambo yenye utata yaliyotokana na mifumo ya elimu za kisasa, k.v. suala la kutokuwa na kikomo na lenye kikomo, basi hatuwezi kusema kwamba mfano wa kimaarifa wa Kiislamu hauna kikomo na wa kimagharibi ni mfano wenye kikomo; kwani kauli hii ni batili. Na ubatili wake unakuja katika kauli kuwa: "Ni wenye kikomo" Kitendo cha kuainisha jambo kuwa ni lenye kikomo wakati ambapo si lenye kikomo, na kutokana na hayo, kila wakitaka kukanusha kutokuwepo katika suala lisilo na kikomo wanajikuta wapo ndani ya suala hilo. Na sisi tunalazimika hapa kutatua utata huu!
Kadhalika suala la kimaadili na la kimaada na kudai kuwa mfano wa Kiislamu ni wa kimaadili na kwamba mfano wa kimagharibi ni wa kimaada sio wa kimaadili ni kauli isiyo sahihi yenye utata; kwani mfano wa kimagharibi unaweza kuwa wa kimaadili, na tofauti iliyo baina ya mifano miwili ni kwamba mfano wa Kiislamu unategemea wahyi kama chimuko la maarifa mbali na mfano wa kimagharibi ambao hautegemei wahyi. Kadhalika dali la kuwa maarifa ya Kiislamu yana vyanzo viwili; wahyi na Uwepo.. wakati ambapo maarifa ya kimagharibi yana chanzo kimoja nacho ni Uwepo. Hapa tofauti haihusiani na kitendo cha kuikagua elimu kwa mujibu wa mtazamo wa maadili au kutofanya hivyo; maana maadili ni jambo la wajibu na kugeuka kuungana nayo ni lazima, lakini tofauti inaambatana na yule atakayeainisha maadili hayo? Mfano wa kimagharibi na mifano inayofanana nao hugongana na mfano wa Kiislamu nikisema: nategemea Wahyi kupata maarifa yangu, ambapo wenye mshikamano wa mfano wa kimagharibi watasema: Hakuna kizuizi cha uamini wa wahyi; kwani mfano wangu (wa kimagharibi) unasema: wewe una uhuru wa kuamini lakini hauruhusiwi ufanye wahyi ni chanzo cha maarifa kwani wahyi ni chanzo cha imani tu.
Kisha suala la dini (au imani) na elimu: Wanatofautisha baina ya maarifa na imani, wakaifanya jozi ya mawazo mawili ambayo hayaendi pamoja, wakaweka suala la imani mbali na wigo wa elimu pamoja na kulinyima neno la elimu katika dhana ya “sayansi” ilhali elimu (sayansi) ni neno lililoundwa hasa kwa ajili ya elimu ya kimajaribio ambayo “Haithibitiki kielimu ila baada ya utazamaji” na tukisema kwamba dhana hiyo haina mpaka na inaambatana na kila inayokuwa ni “elimu na ya kielimu”, basi suala la kuwepo kwa Mwenyezi Mungu litakuwa silo la kielimu; kwani hatukumtazama Mwenyezi Mungu na suala la Uungu hauwezi kuingia maabara.
Jambo hili kwetu halikubaliki; kwani “elimu” kwetu ni “utambuzi usio legalega inayooana na hali halisi ilivyo itegemeayo dalili ipatikanayo katika maabara, akili au ada … n.k.”; kwani kwetu maarifa yanapatikana baada ya kuwepo hali ya kutokufahamu jambo ambalo halipatikani katika elimu ambayo haitanguliwi na ujahili.
Tatizo linalotokana na kutoweza kufasiri neno la Kiarabu (elimu) kwa neno lingine lisilokuwa la (sayansi), linaongoza maana kunjufu kwa mtazamo, kwa hiyo tunahitaji kulifasiri kwa njia ya maelezo ambapo haiwezekani kulifasiri kwa neno moja. Hali kadhalika, utata unatokea wakati neno (Sayansi) ambalo linamanisha (elimu ya kimajaribio / Empiricism) linafasiriwa kwetu kwa (elimu).
Kitendo cha kufasiri na tofauti za mifumo ya lugha mbalimbali ni tatizo kubwa ambalo lazima lizingatiwe wakati wa kuchunguza turathi ya Kiislamu au elimu za kisasa zenye nyanja ambazo zinaungana. Dhana za Kiislamu hazikufasiriwa kwa lugha za kigeni, wala hazikutolewa juhudi kama zile zilizotolewa kwa kutayarisha istilahia ya Kihinduki (ya Kisanskiti) ambayo ilifasiriwa kwa lugha za kigeni kwa kuiweka katika kamusi kubwa; ambapo mtafutaji elimu ya falsafa na dini na jamii kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa pamoja na lugha nyingine, anaweza kufahamu kirahisi istilahia ya Kihinduki hata ikiwa ikiandikwa kwa mbinu ya nukuu za kimatamshi (transcription). Kwa mfano, René Guénon (mwana fikra wa Kifaransa aliyesilimu na akajiita Sheikh Abdul Wahid Yahiya, alizaliwa mwaka wa 1886 na kafa mwaka wa 1951, na kwa sababu yake watu wengi kutoka nchi za kimagharibi waliingia katika Uislamu) alipotaka kufasiri mambo yanayohusiana na Uislamu alitegemea istilahia ya Kihinduki ambapo neno “Skheikh Tariqa” hakukipata kisawe chake katika lugha ya Kifaransa isipokuwa kutoka neno “Joro” la Kihinduki. Wakati ambapo tulipotaka kutafutia maana ya neno “Joro” hatukulipata katika kamusi za Kifaransa.
Hilo ni jambo ambalo tunajaribu kulitenda kuhusu istilahi mia tatu zilizoingia katika Kiingereza k.v. Haj, Jihadi, Umma, Ulama … ambapo nukuu za kimatamshi zilizopo katika nchi za kimagharibi hazikuchukuliwa na Kiarabu wala misingi yake au elimu za Kiislamu, bali zilichukuliwa kutoka maisha yaliyo katika nchi za Kiislamu na akili za watu wake. Suala ambalo linakuwa kiini cha hatari inayosaidia kupanua pengo lililopo linaloleta hali ya kutofahamiana. Wale wakiona Waislamu wanapigana, basi wanaiainisha hali yao kwa Jihadi, jambo ambalo linakuwa ni mojawapo wa aina ya kugeuza maana ya maneno; kwani neno la Jihadi kwa mujibu wa dhana hii linamaanisha ugaidi, uharibifu katika nchi na upendo wa mauaji (kumwaga damu). Kwa mtazamo huu wale wanakagua misamiati mingi k.v. “Imani” , “Dini” , “Siasa” , “Nabii” , “Ukhalifa” , “Umma” , na “Elimu”.
Tatizo linatokana na kutokuwepo kamusi ya maneno na misamiati ya Kiislamu, wakati ambapo walituletea misamiati mingi inayoambatana na vifaa vya kisasa k.v. Tv. kompyuta, bunge, take away … na sisi tunaitumia katika lugha yetu misamiati ile kama ilivyo na kwa maana waliyoitaka, basi kwa nini hatusemi kwamba neno la “elimu” kwa maana yake iliyopo katika Kiingereza halilopo katika lugha yetu ya Kiarabu. Waislamu wa mwanzo walianzisha njia pamoja na wengine juu ya msingi wa maarifa waliyokuwa nayo Waislamu wa mwanzo, na sisi katika kipindi hiki cha kihistoria tunaanzisha njia tena kwa kufaidika na maarifa kutoka kwa wengine kumbe tunadai kwamba ni mseto wa tuliyonayo na waliyonayo. Sisi tunaomba lugha zao zikubali maneno yetu ndani yake! Tatizo kubwa hapa linatokana na hali ya kutofahamu kikamilifu suala hili, ilhali inatakiwa katika hali hii ya kushindwa kistaarabu, tufuate upande wenye kushinda kistaarabu pamoja na kutambua hali na lugha yake.
Kuhusu istilahi zenye utata zilizo baina ya mwenye kutafuta elimu za kijamii na za kibinadamu za kisasa kwa upande, na matini za kisheria kwa upande mwingine, basi baadhi wanakuwa na mtazamo wa ulazima wa kuwepo hali ya kati na kati baina ya mwenye kutafuta elimu za kijamii na mwenye kutafuta elimu za kisheria ili tufikie madhumuni ya dhana hizo. Lakini sisi – katika mtiririko huu wa maneno – tunajitahidi tufikie mbali ya hayo ambapo tunataka mtafutaji elimu mwenyewe awe mzalishiji wa maarifa hata ikiwa kazi hii ina mgogoro na ugumu.
Rejeo: Sheikh Ali Juma’ Mufti wa Misri: Njia ya kufahamu Turathi.