Mfumo wa Maarifa wa Kiislamu na Tof...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mfumo wa Maarifa wa Kiislamu na Tofauti Iliyopo Kati yake na Mfumo wa Kimagharibi

Question

Ni upi mfumo wa kimaarifa wa Uislamu? Na kunatofauti ipi kati yake na mfumo wa Kimagharibi? Vipi utatusaidia mfumo wa maarifa wa Uislamu katika kufahamu vizuri zaidi urithi wa Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mfumo wa maarifa ni ule unaoelezea Akida “Imani”, nao unakusanya majibu ya yale tunayoyafahamu kuwa ni maswali makubwa au maswali ya jumla kuhusu Mungu, juu ya kuwepo, mwanadamu, ulimwengu na maisha: ninatoka wapi? Nini ninafanya? Nini kitakuwa hapo kesho?

Katika mfumo wa maarifa wa Uislamu unaobeba maswali haya yote ni maswali ya “Awali” mwanzo, haiwezekani kuendelea isipokuwa ni kabla “au baada” ya kuyajibu, wakati ambapo maswali hayo katika mfumo wa maarifa wa Kimagharibi - ikiwa wanayoona kuwa ni muhimu - basi hayo ni maswali ya “Mwisho” haiwezekani kuanza nayo, lakini inapaswa mwanadamu kuchukua hatua za haraka za - kielimu na utafiti wa kielimu - ili mwishowe kuweza kuyajibu. Mwislamu anasema kuwa yeye anajua - mwanzo - ni nini, na umekuja kutoka wapi, na kwa nini yeye mwenyewe yupo hapa, au nini lengo la kuwepo kwake…..n.k., wakati ambapo mtu wa Magharibi anazungumzia kuwa hayo siyo muhimu kuanzia.

Hakuna shaka kuwa tofauti hizi zina athari zake na mwendelezo wake kwa upande wa fikra na maadili, kwani Imani kwetu ni masuala muhimu hubadilika yenyewe tu na kuwa “fanya na usifanye” kwa maana ya utekelezaji wa amri, wakati ambapo huko Magharibi kunabakia ni masuala ya mtu binafsi hayana nafasi yeyote katika maisha ya umma.

Katika mfumo wa Kiislamu kuna kitu “Maumbile” wakati ambapo watu wa Magharibi wanazungumzia “Kuchuma”.

Kwangu kuna kilicho kitakatifu, na utakatifu ni sehemu na eneo la ngazi ya juu (Qur`ani, Mtume na Kaaba… vyote hivyo ni vitakatifu na vikubwa kwa upande wangu) wakati ambapo upande mwengine wanaona ni aina katika aina za kipagani.

Watu wa Magharibi wanaona - na wale waliopo kwenye mfumo wao - ni katika upande wa utashi, hata “Mwanadamu” (!) mfumo wa Kimagharibi unaona kuwa mwanadamu anaweza kufanyia kazi kwenye mfumo wa EmpiricalElimu ya kutegemea jaribio, na si nadharia” pasi na shaka yeyote, wakati ambapo ninamwona mwanadamu kwenye mfumo wa Kiislamu ni kiumbe wa aina yake ameumbwa na mwenye kutukuzwa na kukirimiwa {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba}[AL-ISRAA, 70].

Pamoja na mwishowe kutambua kwao kutotosheleza mifumo hii lakini wao hawaoni kabisa mfumo mwingine wowote zaidi ya mfumo wa falsafa za vitendo na majaribio.

Hili linaakisi juu ya mtazamo wa mtu binafsi na kwa wengine, sisi hatuna tatizo na wengine kutokana na umuhimu. Katika mtazamo wa Sartar “Adhabu ndiyo kwa mwingine” kitendo cha kuwepo mwingine kwake kumekuwa ni tatizo kero na maumivu, wakati huyo mwingine - katika mtazamo wa Uislamu - ni sehemu ya ulinganiaji na wala sio chanzo cha adhabu.

Watu - kwa mtazamo wa Mwislamu - ni umma wa kulinganiwa na umma wa kuitikia. Sisi ni umma wa kuitikia ambao wamemuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume S.A.W., na hao wengine ni sehemu ya kulinganiwa, ambapo ujumbe wangu hauhusishi watu hawa pasi na watu wengine, wito wetu unasema: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi}[AL-A’RAAF, 158]. {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote}[AL-AMBIYAA, 107]. Na walimwengu ni viumbe wote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu.

Katika mfumo wa maarifa wa Uislamu msingi wa maadili na imani ni maagizo na amri za Mungu (halali na haramu), wakati ambapo mfumo wa Magharibi unasimama kwenye msingi wa masilahi, sambamba na anavyomaanisha mwanadamu, kwa kiwango ambacho ulimwengu wa Magharibi unaweza kutoa na kumgharamia mbwa au paka na kutoona haja ya kuwapa maelfu wa Afrika au wa Asia wenye matatizo.

Na katika yale yanayopaswa kuzingatiwa ni kuwa mfumo huu wa maarifa wa Magharibi - kama tunavyozungumzia hivi sasa - si sehemu ya kufahamika kwa mtu wa mtaani wa kawaida wa Magharibi, lakini unaweza kufahamika kutokana na maadili yao na vitendo vyao vyenye kuhuhisha kama vile filamu, na kuwezekana kuzungumziwa na baadhi ya wasomi wao katika vitabu vya falsafa vya fikra na katika mikutano mbalimbali.

Kitu ambacho leo kinapunguza mtazamo wa Kiislamu ni utengenezaji mfumo wenye kubadilika kwa kuongeza… na katika upande huo - sisi tunazungumzia na kutengeneza mfumo wetu wa Kimaarifa - kuna tofauti kati ya fikra kwa upande mmoja na Imani kwa upande mwingine, kwa maana ya kati ya ufahamu wa akili wa kadhia na kulazimika akili na kadhia hii.

Ufahamu wa akili ni kujua, kufahamu, na kufikiria kitu, ama kulazimika akili ina maana ni umuhimu wa kuamini akili hiki kitu([1]). Basi kile tunachohitaji ni kutengeneza upya mfumo ambao utafahamiana na yatokanayo na yanayoelezwa na mfumo wake, hata kama haitalazimu.

Na kazi ya kutengeneza tena mfumo ni kazi ya kuuelezea mfumo wa maarifa wa Kiislamu, na wala siyo kazi ya kuuanzisha, faida zake haziji au kuwa wazi isipokuwa pale wakati wa kulinganishwa mfumo huu na mfumo mwingine.

Na kabla ya tatizo la “Namna ya kutengeneza tena mfumo” baadhi wanajiuliza: kwa nini tunatengeneza tena mfumo wa mtazamo wa Uislamu?

Jibu ni kuwa, hilo ni kwa ajili ya ulinganiaji… lengo ni ubadilishanaji wa ufahamu wa kina… kwa ajili ya ulinganishaji kati ya urithi wenyewe na unaolingana nao… kwa lengo pia la kufanya mazungumzo yenye kujenga pamoja na wengine!

Kwani mfumo wa maarifa wa Magharibi umeua Uungu mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini (Hegel kisha Nietzsche) ndani ya mwaka wa 1970 “Foucaul” alitangaza kifo cha mwanadamu, ili mwisho tufike kuwa hakua cha kubakia isipokuwa “kitu”. Mfumo huu wa maarifa wa Magharibi umemalizikia kwa kutengeneza uelewa kwa upande wa: utanda wazi, jinsia, afya ya uzazi, haki za mwanamke, uhalali wa kijinsia….. n.k., vitu hivi visivyokuwa wazi, ambavyo vinakusudiwa visivyowezekana kupingwa na mtu mwengine, na kuwepo katika hali ya kupingana, haiwezekani kukataliwa moja kwa moja wala kukubaliwa moja kwa moja… basi ni nani anayepinga juu ya afya na ufahamu wake?

Kisha pindi ninapotengeneza mfumo wangu maalumu wa maarifa, na kufahamu undani wa mfumo wa maarifa wa mwengine, wakati huo utaniwezesha mimi kuanza mazungumzo kuhoji na kujibu, na kutokuwa katika mgongano huu, ninakubali ninakataa kwa vigezo. 

Kwa mfano - Fukuyama - anatangaza “Mwisho wa historia” kwa maana tumefikia kwenye ukweli wa mwisho, na mfumo umeshatulia, ustaarabu ulioshinda umepiga pigo lake kali la mwisho… adui mpya ambaye anaeonekana kwenye mwisho huu - kama wanavyofikiria - ni “Waislamu” walinganiaji wa kubakia kwenye mfumo wa kiustaarabu mbalimbali, basi ikawa ni lazima kujibu changamoto hii, ndipo akaja Huntington na nadharia ya “Mgongano wa Staarabu” kisha ikaja “Gari aina ya Lexus na mzaituni” gari hii ya kijapani isipokuwa fikra ya gari na utengenezaji wake ni wa Kimagharibi, ilianza huko magharibi mwa Ulaya na ustaarabu wake wa utengenezaji, kisha ukahama na kuelekea Marekani ndani ya miaka mia na hamsini ya mwisho… na mzaituni ni Mashariki iliyoshiriki katika wigo huo, ima kuchukuwa utamaduni wa gari ya Lexus, au kuelekea kwenye wigo huo

Wamarekani wanauliza (Waandishi sitini wa vitabu) tunaingia vitani kwa ajili ya nini? .... ili wajijibu wenyewe: ni kwa lengo la kulinda maadili ya Magharibi ambayo Waislamu wanayachukia!

Kuelewa mfumo wako wa maarifa na mfumo wa maarifa wa mwengine kunanifundisha kuogelea katika mawimbi ya mkondo wa utandawazi na mfumo wa kidunia “secular” unaotuzunguka kila upande, katika sura ya teknolojia ya kisasa uelewa pamoja na nadharia za Kimagharibi, kwa upande mwingine, mfumo huu wa maarifa wa Kiislamu unahitaji tuufanyie kazi na kuutekeleza kwanza ndani ya umma wa kuitikia na kujibu kabla ya kuwafikishia umma wa kulinganiwa, mfumo wa Kimagharibi umejenga jamii zenye utendaji zaidi kuliko jamii za Kiislamu za hivi sasa. Huwenda hili ndio kitu kinachozungumziwa leo kwa jina la: “Uboreshaji wa nadharia ya Kidini na uboreshaji wa ujumbe wa Kidini”.

Na hili linaibua maswali kuhusu kuujenga mfumo wa kimaarifa na kiustaarabu wa Kiislamu katika wigo wa kuangalia mwingine au mfumo wake. La kuzingatia katika mfumo wa Qur`ani ni kuwa, ujumbe unakuja toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala si kutoka umma mmoja kwenda umma mwingine, na kisha inapaswa kuwekwa wazi ujenzi mpya wenyewe sio kama ulinganiaji wa kujiunga watu uliotawala hii leo, wakati upande mwingine wa kulingania unaendelea na kusonga mbele wenyewe. Sisi hatulinganii wenyewe umma wa kulinganiwa kuwa pamoja na sisi “Sisi” kama Waarabu kwa mfano au watu wa Mashariki, hatuhiyarishi ima kuwa na sisi au dhidi yetu, mfano wa sura iliyopo Magharibi, lakini tunawalingania na kujilingania wenyewe kuwa pamoja chini ya bendera ya haki moja kwa moja….

Kadhia inapaswa kutoifikiria kama umbile la uhusiano kati ya vyama viwili, yenyewe ni kadhia ya Mungu mwenye kutofautiana na ulimwengu, wanalinganiwa watu na viumbe vyote kwenye hilo… basi wala haipaswi kujishuhurisha na mandhari tofauti na madhumuni wakati wa kutengeneza mfumo wa maarifa wa Kiislamu.

Hili ni kwa upande mmoja, lakini pia ni lazima kutojishuhurisha na madhumuni pasi na mandhari, kinyume na hivyo tutageuka na kuwa watu wa mwisho wenye fikra zisizofanya kazi na kutokuwa na tija. Basi ni lazima madhumuni haya tuyathibitishe kwa usawa kwenye nafsi zetu: sisi Waislamu na wao si Waislamu: “Sema Enyi makafiri - mpaka kauli yake Mola Mtukufu – {Nyinyi muna Dini yenu na mimi nina Dini yangu} [AL-KAFROON. 1: 6], yenyewe ni yenye kutenganisha, kuna makundi mawili: {Hao ni kundi la sheitani} [AL-MUJADALAH, 18], {Hao ni kundi la Mwenyezi Mungu} [AL-MUJADALAH, 22}, {Kundi moja la Peponi na kundi lingine la Motoni} [ASH-SHURA, 7].

Kwa maana Qur`ani imeonesha umbo kama vile ilivyoonesha madhumuni, na ikatenganisha kati ya makundi mawili kundi la haki na kundi la batili, hilo ni kwa sababu binadamu sio Malaika. Na upumbavu wa kimadhumuni dhidi ya mandhari au umbo inaweza kutufikia sisi katika yale wanayosema watu wa Batiniya kuyapa umuhimu mambo ya mandhari pasi na malengo, wanasema hakika mandhari ya sala - kwa mfano - ni kufanya mawasiliano kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha hakuna sababu ya hatua za sala kama vile kisimamo rukuu sujudu…. n.k. Na tukifikia kwenye kiwango hiki cha kutotii basi kitaharibika kila kitu, na tutatumia wakati wetu katika mambo ya kijinga. Ufupi ni kuwa, hakuna budi - katika kutengeneza mfumo wetu wa maarifa - ya kuwepo mandhari na madhumuni pamoja, na kwa kiwango kimoja cha umuhimu.

Lakini nini uhusiano wa mfumo huu wa maarifa na kutambua kwake elimu za urithi jamii na elimu za ubinadamu?

Uchambuzi wa nukta ya kwanza: lengo la kuangalia mambo ya wakati wa nyuma na yanayorithiwa, ni kujaribu kusoma yale yaliyokuwemo ndani ya wakati huo yanayowezekana kuangaliwa tena kwa madhumuni na mandhari muhimu na kuyaelekeza kwa walimwengu, na yawezekana kupitia hilo kufika ujumbe wetu, na kuweka wazi kuwa maadamu Waislamu walikuwa wanazalisha elimu mbalimbali kwa ajili ya kuhudumia andiko basi walikuwa na ustaarabu safi wenye maendeleo, na Waislamu pindi waliposimama kugundua elimu mbalimbali ustaarabu ulianza kuporomoka, na kubadilika ibada kuwa desturi, limetusukuma hili kusema kuwa watu wenyewe wa kujibu na kuitikia wanahitaji kulinganiwa, bali wao ni wenye kuhitaji zaidi kuliko waliopo nje, umma japo kuwa idadi yake ni kubwa lakini unakumbwa na udhaifu “Kupenda dunia na kuchukia kifo” kitendo cha kuendelea kugundua elimu ndiyo ambacho kitamaanisha kuwa sisi bado tupo hai.

Imekuja hali kubwa ya kukatika hatua hii ya kuzalisha ustaarabu wa elimu ndani ya nchi za Waislamu tokea mwaka wa 1830 A.D., ambapo ndio wakati hasa imeanza historia ya maendeleo yote ya teknolojia mpya, mfano Uingereza iliingiza chuma kwenye utengenezaji wa meli kwa mara ya kwanza duniani, na hatua hii ilibadilisha kabisa sura ya maisha, maendeleo yaliyoibuka kwenye kazi za usafirishaji yalibadilisha kabisa programu ya kila siku ya mwanadamu, na wala hakuwa mwanadamu wa jana anayaishi ya leo au ya kesho kama alivyokuwa jana, bali kila siku ilikuwa imejaa matukio na harakati zinazo mtosheleza.

      Katikati ya hili, kulidhihirika elimu ya kijamii na kibinadamu iliyotokana na mfumo wa maarifa na ustaarabu wa Kimagharibi, kutokana na kulala kwa ustaarabu wa Kiislamu na mwamko wa Uislamu, pasi na kufikiria kuboresha juhudi za kuzalisha elimu ya mfumo wa maarifa ya Uislamu, (ijapokuwa kumekuwa na majaribio ya kufahamu, mfano wa shule ya maarifa ya Kiislamu ambayo ilikuwa maarufu tokea mwanzo mwa miaka ya themanini).

Sisi tunamaanisha katika elimu hizi za kijamii na kibanadamu “maudhui yake” na wala si “masuala yake” basi tofauti ni ipi? Kila elimu ina masuala yake au jumla zake kuu zenye kuelewaka, na kwa kuyaweka masuala hayo yenyewe kwa yenyewe inatubainikia kuwa jambo ambalo tunalimaanisha ni moja, nalo ni “maudhui ya elimu hii” na maudhui hii inawezekana kujiponya nayo katika kila elimu, kwa mfano elimu ya siasa bila shaka ina maudhui iliyothabiti, huwenda ikawa ni mamlaka au usimamizi wa mambo ya umma, sawa na uelewa wa Uislamu, ama kwa upande wa eneo na njia ya ufanyaji wa vitendo yote si katika mambo ya kiini cha maudhui yenyewe. Na katika hali ya kukosekana maudhui basi hiyo haiwi elimu, lakini tunasema kuwa kuna sura ya maudhui hii.

Na vivo hivyo kwani elimu zinasifa ya pekee kwa upekee wa maudhui zake na wala si kwa masuala yake… na maudhui hazina tofauti wala upendeleo ndani yake, isipokuwa kuitolea habari maudhui ya elimu - kupitia masuala yake - ili kutengeneza jumla yenye kueleweka, linatimia hilo kupitia mfumo maalumu wa maarifa kwa wazalishaji wa elimu (wanachuoni na watafiti), nao katika elimu ya kijamii - yenye asili ya Magharibi - wamejibu kuhusu masuala yake kwa mtazamo wa maarifa wa Kimagharibi, na mimi kwa nafasi yangu inapaswa kujibu hayo kwa mtazamo wangu.

Na inazingatiwa kuwa elimu zote za kijamii na kibinadamu zilikuwa ni sehemu ya shamba la “falsafa” kisha zikajitenga na falsafa kwa maudhui zenye kujitegemea, na falsafa hii ikabadilika na kuwa falsafa za elimu, kwa maana fikra zenye kusimamia namna ya kufikiri kielimu katokana na mtazamo maalumu wa wanachuoni wa ustaarabu husika.

Kwa mfano elimu ya sasa ya jamii kwa mtazamo wake wa Kimagharibi, unasemaje juu ya wahalifu na wenye kufanya dhambi? Na sisi tunasema nini pindi tunapoufanyia kazi mtazamo wa Uislamu?

Mtazamo wa Magharibi unagawa haki kwa upande wa haki ya jamii (haki ya umma) na haki ya mtu (haki ya mtu binafsi), wakati ambapo haki katika mtazamo wa Uislamu inapatikana kati ya haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja, tunakaribia kukubaliana katika kugawa, lakini tunatofautiana katika kuainisha ipi haki ya umma na ile ya mtu binafsi? Nayo - kwenye mtazamo wa Magharibi - unaona kuwa kufungwa jela mwenye kufanya dhambi inapaswa kutogusa kabisa mwili, na uzinifu ni jambo la mtu mwenyewe haifai kuingiliwa - moja kwa moja na mamlaka - na kuuwa ni jambo la umma ni katika haki za jamii, mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ndiye mwenye kusimamia mashitaka. Lakini kwangu kutekelezwa adhabu kwenye mwili wa mkosefu ni jambo lisilopingana na ubinadamu wa mtu na kuwa sawa na mtazamo wa maarifa, vile vile kitendo cha uzinifu na uchafu ni katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu haviwezi kuachwa kwa utashi na matamanio ya mtu - ambaye kiasili anaelekea kwenye ukiukaji - kama vile kulipiza kisasi kwangu mimi ni haki ya mlezi msimamizi au mzazi wa aliyeuwawa, kisha yawezekana kwa ndugu na jamaa wa marehemu kufikisha mashtaka ya kudai ulipizaji kisasi au kuridhia kulipwa dia “ni fidia inayotokana na kitendo cha uuaji” au kusamehe na kupewa sadaka tu.

Magharibi wanaona kuwa “Ngono, ufuasi wa chama na Dini” - vitu hivi vitatu - ni mambo ya mtu binafsi na siyo sehemu ya kuzungumziwa ndani ya jamii, wakati ambapo ufuasi wa kisiasa au chama kwa upande wangu ni lazima kutopingana na desturi na maadili ya jamii, pia na mambo mawili mengine, mambo haya katika mtazamo wa Uislamu yana uzio, wakati watu wa Magharibi wao hayana uzio.

Yanaongezwa katika hayo maudhui zinazo ibua hisia kwetu kwa kuporomosha mitazamo mingine, mfano “Kufanya kazi mwanamke” jambo hili halikuwa tatizo kwetu tokea hapo nyuma, mwanamke moja kwa moja anafanya kazi pindi akihitaji kufanya kazi, na wala hafanyi kazi ikiwa hakuna haja ya hilo, naye anafanya kazi ndani ya nyumba yake zaidi na kuzalisha zaidi, na hili ndio lililokuwa likifahamika kwa “Uchumi wa kivuli”.

Hivyo ni lazima kutengenisha - katika elimu za zamani na za sasa - kati ya maudhui ya elimu na masuala yake, sisi tunakubali maudhui yeyote yenye kuibua hisia, lakini tunatibia kwa mfumo wetu sisi, pia kutokana na utamaduni wetu - ikiwa tutataka - katika mipaka ya mfumo wa maarifa wa Uislamu, ili tusiangukie katika kujiletea matatizo toka kwa wenzetu, katika kutoa habari juu ya kitu fulani, jibu lolote la kuhusu masuala huwenda likakubaliana na kinachopokelewa toka kwa mwingine sawa na mtazamo wa Uislamu, na huwenda ukatofautiana. Kisha mimi ninatanguliza kwenye elimu zote za dunia akili iliyofunguka, ninakubali maudhui zake, kisha ninazijibu kwa mfumo wa maarifa na kwa asili yangu pamoja na mahitaji yangu pia, ninatengeneza na kuzalisha jumla yenye kueleweka inatofautiana na jumla zenye kueleweka kwa wengine.

Uzalishaji huu unakuwa kwa njia ya uasili, kisha lazima niwe na mbinu na mifumo. Mbinu “Methodology” ni elimu inayozalisha mfumo na mifumo “Methods” na kuweka masharti yake mjengo wake na muundo wake, nayo inamaanisha uwaji wa kitu na kunasibishwa kwenye mfumo. 

Wala haihusishwi na elimu ya jamii peke yake, elimu asili - kwa nafasi yake - inakusanya misingi miwili mikuu: malezo na falsafa inayotawala, maelezo hayana tofauti, wakati ambapo tatizo ni katika falsafa inayoendesha elimu, ambayo inaundika kwa nafasi yake kutokana na: lengo kwenye utafiti, njia za utafiti na matumizi na utendaji wa vitendo baada ya kufikia matokeo, navyo ni vipengele ambavyo vinaingilia kati mfumo wa maarifa kwa kuboresha kuongeza marekebisho kukataa na kufanya vizuri.

Na hivyo hivyo sisi - pindi tunapofikiri kwenye elimu ya sasa ya jamii na ubinadamu baada ya kuangalia mfumo wa maarifa wa Uislamu - tunafikiria kwa njia iliyopita kwa muda mrefu sana, na hili kwa sababu sisi tunafikiri tukiwa na urithi wa miaka elfu moja na mia nne, ndani yake ukiwa na kila aina ya maarifa, lakini tunachokikosa ni mfumo, kulazimika, kufanya haraka kuufanyisha kazi na vyombo vya kufanyizia kazi.

Chanzo: Njia ya Kufahamu urithi, kitabu cha Mufti wa Misri. Dkt. Ali Juma.

 


([1]) Kuna kile kinachoitwa hukumu za akili nazo ni kati ya aina tatu: ulazima, kuwezekana, kutowezekana, - wajibu wa kiakili: haiwezekani akili isipokuwa lazima iwepo, kwa sababu haiwezekani kukamilika kitu kilichopo pasi na mwezeshaji wake, yeye pekee ndio mwenye wajibu wa kuwepo pasi na kuwepo sababu ya kutangulia kuwepo kwake.

Unagawika matawi wajibu huu wa kiakili na kuwa yale yaliyo wajibu usioepukika, na yaliyo wajibu wa lazima: wajibu usioepukika: nao ni katika ulazima wa akili ambapo elimu inakuwa ni jambo la lazima, kama kauli ya Decurt: “mimi ninafikiria kwa vile nipo” hisia zangu za uwepo wangu haziepukiki. Na wajibu wa lazima: nao ni wenye kufahamika kwa “hukumu za kawaida” ambazo tunazifahamu kwa vitendo na mazoea, mfano moto unasababisha kuunguza, na mfano vitu ni vyenye kuvutwa kuja chini… japokuwa upo uwezekano wakati mwengine kutokuwa hivyo isipokuwa hali hiyo inabakia katika hali si ya kawaida au muujiza.

Yasiyowezekana kiakili: kukutana vinyume viwili, akili haikubali kitu kipo wakati huo huo ukweli hakipo, kama mfano wa kutokuwepo Mungu Muumba pamoja na kukubali uwepo wa viumbe: sawa na kusema: kuna uwepo na muwekaji wake kisha si muwekaji….!

Lenye kuwezekana kiakili: (ni kila chenye kuwezekana kukifikiria hata ikiwa hakipo kwenye ukweli isipokuwa kwa sura ya muujiza) mfano kusalia Nabii Yunus ndani ya tumbo la samaki pasi na kupata kero na adha yoyote, na mfano pia wa kutoka Nabii Ibrahim kwenye moto akiwa salama, mifano hii miwili kiakili inawezekana kwa hali ya kawaida.        

         

Share this:

Related Fatwas