Usahihi wa Hadithi ya "Maji ya Zamz...

Egypt's Dar Al-Ifta

Usahihi wa Hadithi ya "Maji ya Zamzam Hunywewa kwa Kile Kilichonuiwa Kwayo"

Question

Ni upi Usahihi wa Hadithi ya: "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo"? Na ni ipi hukumu ya kuyatumia maji hayo?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Ibn Majah, Ahmad, Adarqatwniy, Al Haakem, Ibnu Abi Shaibah, na Al Baihaqiy walipokea katika [Asunnan], na Al Manqariy katika kitabu cha: [Fawaid Al Manqariy], kutoka kwa Hadithi ya Jaber R.A., alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo". Na Al Baihaqiy akaipokea Hadithi katika kitabu cha: [Shua'bul Emaan], kutoka kwa Ibn Amru, na kuna dalili kwenye Adarqatwniy, na Al Haakem kutoka kwa Ibn Abaas, kwa nyongeza ya: "Na unapoyanywa maji ya Zamzam kwa ajili ya kuomba ponyo kwayo, basi Mola atakuponya, na Ukiyanywa kwa ajili ya kuondosha kiu basi Mwenyezi Mungu Mtukufu hukikata kiu hicho, na Ukiyanywa kwa ajili ya kukushibisha, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu hukushibisha kwayo. Nayo ni… ya Jiburilu – alikanyaga sehemu hiyo kwa mguu wake na maji yakabubujika - na akayanywa Ismail (na mama yake).
Na Adelaimiy alipokea kutoka kwa Ibn Abaas kwa shabaha yake, bila ya nyongeza, "Ukiyanywa kwa ajili ya kuomba ulinzi basi Mwenyezi Mungu atakulinda", Na Al Haakem, Al Baihaqiy, Al Mundhiriy, Ibn Auyayenah na Ademiyatwiy wakaisahihisha. Na Al Hafedh Bin Hajar aliipa hukumu ya Hasan.
Muhammad Bin Idrisa Al Qadiriy akasema katika kitabu cha: [Izalet Adahsh wa Al Walah Ann Al Mutahair; Katika Usahihi wa Hadithi ya: "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo" [Uk. 130, Ch. Al Maktab Al Islamiy]: "Na kwa ujumla, basi umethibitika Usahihi wa Hadithi hiyo".
Na Assyutwiy akasema katika kitabu cha: [Hashiyat Assyutwiy juu ya Sunnan Ibn Majah, 49/3, Ch. Dar Al Maarifah]: "Hadithi hii ni mashuhuri kwenye ndimi za wengi na wajuzu waliohifadhi Hadithi wametofautiana ndani yake, wamo miongoni mwao walioisahihisha, na, miongoni mwao walioipa hukumu ya Hasan, na pia wamo miongoni mwao walioidhoofisha, na hukumu inayotegemewa ni ile ya kwanza".
Na Assyutwiy akasema katika kitabu cha: [Adurur Al Muntatherah, Uk. 173, Ch. Chuo Kikuu cha Mfalme wa Su'ud]: "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo". Az Zarkashiy akasema: Hadithi hiyo ilipokelewa na Ibn Majah kutoka kwa Hadithi ya Jabe kwa Sanad nzuri. Na Al Khatweb akapokelea katika kitabu chake cha: [At Tareekh], kwa Sanad imesahihishwa na Ad-Demiytwiy, nikasema: Na pia imesahihishwa na Al Minqeriy, na Ibn Hajar akaipa hukumu ya Hasan, kwani ilikuja kwa njia ya Jaber.
Al Munziriy akasema katika kitabu cha: [Atargheeb wa Atarheeb 136/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: Imepokelewa na Ahmad kwa Isnadi sahihi, na Al Baihaqiy, na akasema: ni hadithi ngenikutoka hadithi ya Ibn Abi Al Mawaliy kutoka kwa Ibn Al Munkader, Suwaid peke yake akaipokelea kutoka kwa Ibn Al Mubarak kutoka kwa mfumo huo kutoka kwake.
Na imepokewa na Ahmad pamoja na Ibn Majah Hadithi ikiwa na hukumu ya Marfuu kutoka kwake na kupokelewa na Abdullahi Bin Al Mua'mal kwamba akamsikia Abu Azubair anasema: mimi nimesika Jaber Bin Abdullahi anasema: (akaitaja Hadithi hiyo), na hiyo ni Isnadi nzuri.
Al Hafidh Bin Hajar akasema katika kitabu cha: [Juzu' Fih Ajawab kwa Hadithi hiyo, Uk. 270 na baadaye, Ch. Dar Al Basha'er]: "Na iwapo itaamuliwa hivyo, basi ngazi ya Hadithi hii kwa wajuzi waliohifadhi Hadithi, kwa kukusanyika njia hizi ni kwamba inasihi kuitumia kama hoja kwa misingi ya wanazuoni wa Hadithi, inayotambulika. Halafu akataja kutoka kwa Al Haafedh Ademiatwiy kwamba aliisahihisha, … Kisha akasema: Tulipokea katika kitabu cha: [Al Mujalasah] kwa Abi Bakr Adainuriy kwamba Sufiyan Bin Auiyayinah alizungumzia Hadithi ya: "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo". Basi mtu mmoja akajitokeza na kusimama barazani kisha akasema: Ewe Baba wa Muhammad! Je, Hadithi ya maji Zamzam uliyotuhadithia ni sahihi? Akasema: Ndiyo, yule mtu akasema: "Hakika mimi hivi sasa nimekunywa ndoo moja ya maji ya Zamzam kwa kuwa ninataka wewe unihadithie Hadithi mia moja". Basi Sufiyan akamwambia: Keti! Basi yule mtu akaketi, na Sufiyaan akamhadithia Hadithi mia moja … Na imekuwa ikijulikana kuwa Imamu Shafi, yeye alikunywa maji hayo kwa ajili ya kuwinda kwa shabaha, na akawa anafanikiwa katika kila viwindo kumi anapata viwindo tisa.
Na Abu Abdullahi Al Haakim, aliyanywa maji ya Zamzam kwa ajili ya kupangilia vyema Elimu mbalimbali na kwa ajili ya mambo mengine mengi, akaja kuwa Mpangiliaji bora kabisa wa zama zake, na wala haujulikani wingi wa idadi ya wanazuoni waliyoyanywa maji ya Zamzam kwa ajili ya mambo ambayo waliyafanikisha. Na akatutajia Al Haafidh Zein Ediin Al Iraqiy kwamba aliyanywa maji ya Zamzam kwa ajili ya kitu fulani na akakifanikisha. Na mimi niliyanywa mwanzoni nilipoanza kutafuta Hadithi, na nikamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anipe uwezo mkubwa wa kuzihifadhi Hadithi kisha nikazunguka kwa muda unaokaribia miaka ishirini nami nikajikuta ni mtu ninaetaka nipate cheo zaidi ya hicho nilichokipata na nikamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu cheo cha juu zaidi ya hicho na ninatumaini kwa Mola kuwa nitakipata.
Na Al Hakim Atarmiziy katika kitabu cha: [Nawader Al Usul] kutoka kwa baba yake kuwa yeye alikuwa akitufu usiku na akazidiwa na haja ndogo na akachelea iwapo angetoka msikitini kwa ajili ya kwenda sehemu ya kukidhi haja yake miguu yake ingechafuka kwa uchafu wa watu, na huo ulikuwa ni msimu wake, basi akaelekea yalipo maji ya Zamzam na akayanywa kwa ajili ya jambo hilo, na akarejea kwenye ibada ya kutufu, akasema: sikuhisi kuwa na mkojo hadi Asubuhi.
Al Hatwab akasema katika kitabu cha: [Mawahebul Jalil 116/3, Ch. Dar Al Fekr]: Na ama Hadithi ya "Maji ya Zamzam hunywewa kwa kile kilichonuiwa kwayo" basi Al Hafedh Asakhawiy akaizungumzia akisema: inapokelewa na Al Haakim na akasema kwamba Hadithi hiyo ina Isnadi sahihi, na ilisahihishwa na Ibn Auiyina kutoka kwa waliomtangulia, na kutoka waliokuja baada yake ni Al Hafedh Ademiyatwiy.
Na asili ya Hadithi hiyo ni ile iliyotajwa katika kitabu cha: [Sahihi Muslim], "kutoka kwa Abu Dhar Al Ghefariy R.A. kwamba Mtume S.A.W, aliyazungumzia Maji ya Zamzam akasema: "Hayo ni Maji yaliyobarikiwa na ni chakula kinachoshibisha". Na Atwayalsiy akaongeza: "Na ni dawa inayoponya magonjwa".
Kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia: Ni halali kuyanywa Maji ya Zamzam ili kupata kheri ya Dunia na Akhera.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas