Msimamo wa Mwenye Swali la Fatwa Ju...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa Mwenye Swali la Fatwa Juu ya Watoaji wengi wa Fatwa.

Question

Watoaji wa fatwa wakiwa wengi katika nchi, Je, fatwa ya mmoja kati yao ni inatosha, au ni lazima kumtafuta mmoja mwenye swali la fatwa bora kuliko wengine? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenye swali la fatwa akitaka kujua hukumu ya suala, haijuzu kwake kumuuliza mtu asiyejulikana kuwa na elimu, bali atamuuliza yule anayeaminika kuwa ni mtu wa kutoa fatwa, na haitoshi sura yake kuwa ndio inayobainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wanachuoni, kwa sababu, si kila anayenasibishwa na elimu, au kuelimisha na kusomesha inajuzu kwake awe anatoa fatwa, bali lazima awe na ujuzi wa kutosha katika uwanja wa kutoa fatwa, na mwenye swali la fatwa ajue hivyo, kwa upande wa uzoefu wake, na si kwa upande wa umashuhuri wake. An-Nawawiy katika kitabu chake: [Adabul-Fatwa] anasema: “Inajuzu kwa yule mwenye uzoefu wa kutoa fatwa awe anatoa fatwa hizo. Na baadhi ya wanachuoni wanasema: Inategemea na kukiri kwake kuwa ana uzoefu mkubwa wa kutoa fatwa, na sio umashuhuri wake tu. Na haitoshi kwa uzoefu na ujuzi tu, kwa sababu uzoefu na umashuhuri kati ya watu wa kawaida havitegemewi. Huwenda kutokana na mchangamano, na kuhusu ujuzi lazima uambatana na elimu halisi, na rai sahihi inapewa nafasi ya kwanza”, [Uk. 72, Ch.ya Dar Al-Fikr]. Na miongoni mwa sura za Uzoefu ni amri ya Mwenye madaraka, au Makamu wake amteue Mufti, au mtu ye yote anayeruhusiwa kutoa fatwa na Mwenye madaraka.
Mwenye kuzingatia katika tafsiri ya wanachuoni wa Misingi kwa kuwepo watoaji wengi wa fatwa, anaangalia utegemezi wao kama ni sharti la uwezekano, ambapo mwenye swali la fatwa hawezi kumuuliza Mufti kwa sababu ya umbali, hofu, na vizuizi vinginevyo vinavyoweza kujitokeza, basi kuwepo kwake ni mfano wa kutokuwepo, hata akiwa katika nchi husika, au kunyume cha hivyo, na maendeleo ya vyombo vya mawasiliano yana athari kubwa ya sharti la uwezekano, hali ya kuwepo katika nchi ya mwenye swali la fatwa watoaji wengi wa fatwa wenye umahiri wa kazi hii, basi mwenye swali la fatwa ima anajua maoni yao katika suala husika au la, na kama asipojua maoni yao, wanachuoni wa Misingi wanahitilafiana kuhusu nani anayestahiki kuulizwa na mwenye swali la fatwa, nao wana kauli mbili:
Ya kwanza: nao ni ya kuchaguliwa: Mwenye swali la fatwa anamuuliza anayemtaka, na halazimiki kutafuta mwenye elimu zaidi, na hii ni kauli ya wengi wa wanachuoni wa Misingi.
Ya pili: Mwenye swali la fatwa atafute mwenye elimu zaidi, na kauli hii pia ni ya jamaa ya wanazuoni wa Misingi, miongoni mwao ni Ibn Al-Qassar, Ash-Shatibiy; wafuasi wa Madhehebu ya Malik, Ibn Suraij, Al-Qaffal Al-Muruziy, Kadhi Hussein, na AsSama’aniy; wafuasi wa madhehebu ya Shafiy, na kauli hii imechaguliwa na Ibn Aqiil, na Ibn Al-Qaiym; wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal.
Amir Badahah katika [Taisii At-Tahrir] anasema: “(Inajuzu kumfuata mwenye elimu bora pamoja na kuwepo mwenye elimu bora zaidi) katika kauli ya wengi wa wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal, kama vile: Al-Qadhiy, Abul-Khattab, na Mtungaji wa Ar-Raudhah, na wafuasi wa Madhehebu ya Hanafiy, na Malik, na wengi wa wafuasi wa Madhehebu ya Shafiy (na Ahmad, na jamhuri ya wanachuoni) wamekubali (kukataza), kama vile: Ibn Suraij, Al-Qaffal, Al-Muruziy, Ibn As-Samaniy; na tofauti hapa inahusu nchi moja, kwa sababu hakuna tofauti kuwa halazimiki kuwafuata wanachuoni bora wa dunia yote, kama alivyoitaja Az-zarkashiy katika sherehe yake, namapokezi ya Ahmad na wengi wengineo”. [4/251, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Az-Zarkashiy katika [Al-bahr Al-Muhiit] anasema: “Pakiwa na Mufti mmoja, basi lazima amuulize, lakini wakiwapo wanazuoni wengi; Je, analazimika kutafuta mwenye elimu zaidi? Kuna rai mbili: kutokana na tofauti iliyotangulia kuhusu kumfuata mwenye elimu tu; ya kwanza: ni rai ya Ibn Suraijn Al-Qaffal: analazimika kutafuta mwingine, kwa sababu anaweza kumfikia kwa kusikia kwa waadilifu, na hili si jambo gumu. Na Al-Ustadh Abu-Isihaq Al-Isfrainiy ameikubali rai hii, pamoja na Al-Kiya, kwani mwenye elimu zaidi anaweza kuongozwa na siri za Sheria. Ya pili, nayo ni ile inayochaguliwa: hailazimiki kumtafuta mwingine, bali anamchagua na kumuuliza anayemtaka miongoni mwa wanachuoni. Ar-Rafi’y anasema: hii ndio rai sahihi kwa wanachuoni. Akasema pia: rai hii ni bora zaidi, na hakuna ulazima wa kufanya bidii kwa ajili ya kupata dalili. Na Shafiy R.A, anasema kuhusu mtu aliye na upofu: na amfuate kila anaemwongoza kati ya Waislamu upande wa Qibla, na hakuamrishwa afanye bidii ya kuwa na yakini”. [8/365, Ch. ya dar Al-Kutbiy].
Al-Ghazaliy katika [Al-Mustasfa] anasema: “Suala la: nchi isipokuwa na Mufti mmoja tu, inamlazimu mtu wa kawaida kuuliza, na wanazuoni wakiwa wengi, atamuuliza anayemtaka miongoni mwao, na halazimiki kumuuliza mwenye elimu zaidi ya wengine, kama ilivyofanywa wakati wa masahaba, ambapo watu wa kawaida walikuwa wanamuuliza mwanachuoni mwenye elimu zaidi, na watu hawakukatazwa kuwauliza wasio kuwa Abu-Bakr, Umar, na Makhalifa tu. Wengine wanasema kuwa: inalazimika kumuuliza mwenye elimu zaidi, wakiwa wenye elimu ni wa ngazi moja, basi achague anayemtaka. Na hii inapingana na kauli ya pamoja ya Masahaba, ambapo mwenye elimu zaidi hakumkataza mwenye ngazi ya chini atoe fatwa, bali inatakiwa kumuuliza yule aliyemjua na elimu na uadilifu, na wote walivyo”. [Uk. 373, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na katika [Al-Wusul Ila Al-Usul] na Ibn Barhan: “Wanachuoni walihitilafiana juu ya mtu wa kawaida akiwa na tukio, je, inajuzu kwake kumfuata anayemtaka miongoni mwa wanachuoni, au analazimika kuangalia ngazi ya wanaojitahidi?, Baadhi ya wanachuoni wanasema: analazimika kutafuta masuala katika milango ya Fiqhi, akahifadhi majibu yake, akamuuliza mwanachuoni kuhsu majibu haya, akijibu, basi amfuate, wengine wanasema: amfuate yule elimu yake imedhihirika, kumejuliwa na kuenezwa, na wengine wanasema: atoe swali na mwanachuoni, je, wewe ni mwenye jitihada hata niweze kukufuata? Akijibu naam, basi amfuate, na hii ni madhehebu sahihi zaidi”. [2/363-364, Ch. ya Maktabat Al-Maarif, Riyadh].
Al-Mardawiy katika [At-Tahbiir] anasema: “Kauli yake: (Inajuzu kumfuata mwenye elimu tu kwa rai ya wengi wa wanachuoni. Na imesemwa: akidhani ni bora zaidi au mfano wa hayo, na kwa rai ya Ibn Aqiil, Ibn Suraij, Al-Qaffal, na As-Sama’aniy: analazimika kufanya bidii, akichagulia mwenye elimu zaidi, na maana hii ni ya Al-Kharqiy na wengineo. Ahmad ana mapokezi mawili). Na kauli ya kwanza ni ya wengi wa wanachuoni, miongoni mwao: Al-Qadhiy, Abul-Khattab, na mtungaji wa Ar-raudha, na waliisema pia: waffuasi wa Madhehebu ya Hanafiy, Malik, na wengi wa wafuasi wa Shafiy. Kauli ya pili: Inajuzu kumfuata anayeona kuwa ni mwenye elimu zaidi au mfano wake, na inachaguliwa na At-Taaj As-subkiy, Al-Baramawiy, na jamaa, na maelezo ya kauli hii ni: akidhani kuwa ni mwenye elimu tu, basi kauli yake ni dhaifu, kwa sababu, kutokana na kanuni, haiachi kauli nguvu kwa ajili ya kauli dhaifu. Ibn Aqiil anasema kuwa: analazimika kufanya bidii, akichagulia ya nguvu, na maana yake: kauli ya Al-Khaqiy na Al-Muwafaq katika [Al-Muqnii] na wengineo katika suala la kuelekea Qibla, na aliisema pia: Ibn Suraij, Al-Qaffal, Al-Qadhiy Hussein, Ibn As-sam’aniy, Al—Baqillaniy, na Ahmad ana mapokezi mawili; yanaohusu kauli ya kwanza na ya pili. Dalili ya kauli ya kwanza kuwa: wengi wa masahaba walio wenye elimu tu walikuwa wakitoa fatwa, wakati wa kuwepo wenye elimu zaidi, kwa wingi na umashuhuri, na hakuna anyekataa, na hii ni ijmaa kuwa: inajuzu kumuuliza mwenye elimu tu, pamoja na kuwepo mwenye elimu zaidi, na Mwenyezi Mungu alisema: {Basi waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya Mwenyezi Mungu vya kale) ikiwa nyinyi hamjui}. [AN NAHAL 43], na Mtume S.A.W., amesema: “Masahaba yangu ni kama nyota; kwa ye yote kati yao mmemfuata, mtaongoka”, na bila shaka, ni kati yao aliye bora zaidi kuliko wote. Pia mtu wa kawaida hawezi kuchagulia, kutokana na kasoro ya elimu yake, kama akiombwa hivi, basi ataombwa aina ya jitihada. Lakini Ibn Al-hajib alikosoa hivi kuwa: mwenye elimu zaidi anajuliwa na umashuhuri na awe marejeo kwa wanachuoni, kwa sababu ya wingi wa waulizaji wake na ni wa kimaumbile”. [8/4080-4084, Ch. ya Dar Ar-Rushd].Jumla ya dalili ya wenye rai ya kwanza ni zifuatazo:
1- Inajuzu kumuuliza mwenye elimu ya kawaida, pamoja na kuwepo mwenye elimu zaidi, na dalili ya hii ni Hadithi ya A’asiif, yaani (mwenye ajira) kuwa; bedui alikuja kwa Mtume S.A.W., akisema kuwa: mwanangu alikuwa mwenye ajira kwa mtu fulani, na mwanangu alimzini mke wake, na watoaji fatwa walisema: mwana wako ampigiwe mawe, na mimi nikatoa fidia ya mbuzi mia na mjakazi, kisha nkauliza wanachuoni, wakasema: apigwe mijeledi mia na muda wa mwaka mmoja ugeneni. Dalili hapa ni kuuliza wanachuoni pamoja na kuwepo Mtumw SAW, na Mtume hakukataa hivi. Vile vile, Masahaba kati yao ni mwenye elimu na mwenye elimu zaidi, lakini mwenye elimu ya kawaida alikuwa akitoa fatwa, pamoja na kuwepo mwenye elimu zaidi, bila ya kukanusha.
2- Mwenye swali la fatwa hawezi kujua aliye bora na mwenye elimu zaidi kati ya wanachuoni, na tukimlazimu hivyo, basi atapata mvurugiko mgumu, hasa kwa kuwa yeye halazimiki kufanya bidii ya kujua hukumu ya sheria, vile vile, halazimiki kufanya hivyo kwa kujua Mufti aliye mbora au amtafute alie bora, na zaidi ya hayo, mwenye swali la fatwa anatakiwa kumuuliza Mufti mwenye mbinu za kutoa fatwa, na sharti hili linapatikana kwa mwenye elimu ya kawaida. [Al-luma’, na Abi-Isihaaq , Uk. 256, Ch. ya Dar Al-kalim At-Taiyb, na Dar Ibn Kathiir].
3- Kuwepo kwa Mufti aliye bora zaidi hakuondoshi fatwa ya mwenye ngazi ya chini, basi hakuna kizuizi cha kumuuliza wa ngazi ya chini.
Wenye kauli ya pili walitoa dalili kuwa: kuombwa kauli ya mwingine hakujuzu, ila baada ya kujua kuwa yeye ni mhusika, kwa dalili ya hakimu na mchunguzi wa bidhaa, haijuzu kuombwa maamuzi yao ila baada ya kujua kuwa wao ni wahusika, vile vile, suala la kufuata, na hali ya kuwa mwenye swali la fatwa hakujua ujuzi wa Mufti wake, basi hatamtegemea, na kauli yake haitakuwa bora kuliko ya mwingine; [Al-Wadhih, 5/466, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah]. Pia Mamufti mbele ya mwenye swali la fatwa ni kama dalili zinazopingana mbele ya mwenye jitihada, na katika hali ya kupingana mwenye jitihada ataiwekea kipaumbile rai yenye nguvu. Vile vile mwenye swali la fatwa kwenye Mamuti wengi, na jambo la kuchagua linaambatana na dhana, kwa hiyo, anayeamini kuwa Shafiy, Mwenyezi Mungu amrehemu, ni mjuzi sana na kwamba Madhehebu yake ni sawa kabisa, basi haijuzu kufuata madhehebu ya mwingine kwa matamanio tu, n.k.
Inaweza kujibiwa kwa dalili za hawa wenye rai ya pili, kama ifuatavyo:
Kutoa dalili kuwa: Haijuzu kuombwa kauli ya mwingine ila baada ya kujua kuwa yeye ni mhusika, ni nje ya maudhui ya majadiliano; kwa sababu mtu asiyehusika na kutoa fatwa haijuzu kamwe kumuuliza. Na suala letu hapa ni kwa yule anayehusika pamoja na wengine.
Na ni kosa kutoa kauli ya kuwa Mamufti mbele ya mwenye swali la fatwa ni kama dalili zinazopingana kwa mwenye jitihadani, kwa sababu kuchagua dalili iliyo bora, hii kimsingi ni miongoni mwa kazi za mweye jitihada, kwa wingi wa elimu yake, na nguvu ya akili yake, kinyume na mwenye swali la fatwa ambapo hakuna maana ya kuchagua kwake mbora kati ya Mamufti. Hapo ikifikiriwa kuwa suala hili linairejea ile dhana ya mwenye swali la fatwa, na ndiyo hivyo. Kutokana na tofauti iliyopo kati ya Mamufti, basi hakuna kosa kwa aliyefuata dhana ya mufti mmoja ingawa inaipinga dhana ya Mufti mwingine.
Na haisemwi kuwa mwenye swali la fatwa akimiliki hiari ya kumuuliza Mufti anayemtaka kati ya Mamufti itakuwa ni kufuata matamanio. Hii inakuwa sawa katika wakati waliopo Mamufti hawa wasio na ujuzi wa kutoa fatwa, kama tukitumia hiari kati ya kila anayenasibishwa na elimu au kutoa fatwa bila ya ujuzi kamili, basi kufanya hivyo ni kufungua mlango wa kufuata matamanio kwa wenye fatwa.
Ama hali ya pili iliyopo ni: mtu mwenye swali la fatwa kuyajua maoni ya Mamufti katika suala hilo la fatwa, kama vile mmoja wao akiwa amesema: ni makuruhi, na mwingine akasema: ni haramu, hapo wanachuoni wa Misingi wanahitilafiana juu ya yule ambaye rai yake in inachaguliwa. Na Az-Zarkashiy alizitaja kauli kumi za suala hili. Lakini sisi tunasema hapa: mwenye swali la fatwa ana hiari ya kuchagua kauli moja anayoitaka, hata angalau mwenye kauli ni iliyo bora zaidi ataachwa, na sababu ya hayo ni kuwa: inajuzu kumuuliza mwenye elimu tu, pamoja na kuwepo Mjuzi mwingine mwenye elimu zaidi yake, kama ilivyotangulia kuelezwa.
Na inabainika kuwa: Mamufti wakiwa na ujuzi wa kutosha kutoa fatwa, mwenye swali la fatwa ana hiari isiyo na mipaka ya kumuuliza mmoja kati yao, wakati akiwa na dhana ya nguvu kuwa Mufti huyo ni mhusika wa kutoa fatwa, na ana haki pia ya kuchagua rai moja miongoni mwa rai zao wote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas