Tafasiri ya Ibara: "Hakuna Bora Zaidi Kuliko Kilichokuwepo" Imam Al-Ghazaliy.
Question
Baadhi ya wanachuoni wamempinga Imam Al-Ghazaliy katika kauli yake: “Hakuna bora zaidi kuliko kilichokuwepo” wakidhania kuwa ndani ya maneno haya kuna hali ya kushindwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ni upi ukweli wa jambo hili? Na ni nini maana sahihi ya kauli hii ya Imam Al-Ghazaliy?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuwezekana: kunako kusudiwa ni uwezo, kunatokana na kauli yao: amemuwezesha kufanya kitu, kwa maana: amemfanya kuwa na mamlaka na uwezo, na kumuwezesha jambo mtu fulani: maana yake amemrahisishia na kumfanyia wepesi, na inasemwa: Fulani hawezi kuinuka, kwa maana: hana uwezo [Angalia: kamusi ya Al-Wasit, mada ya mkn]
Uwezo kilugha: ni nguvu na kuweza. Na istilahi kwa upande wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: ni sifa ya enzi inayojitegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu inayopelekea kupatikana uwezekano na kukosekana sawa na matakwa. [Angalia Kitabu cha Al-Baijury juu ya maana ya Tauhid uk. 120, chapa ya Dar es salaam – Kairo]
Uwezo unafungamana na jambo lenye kuwezekana, nao ni wenye kukubali kuwepo na kukosekana, wala uwezo haufungamani na jambo la lazima, kwa sababu wenyewe kama utafungamana na ulazima basi uwepo wake unakuwa ni wa lazima, na kama utafungamana na sifa hiyo kukosekana kwake kuna kuwa ni kinyume na ukweli, kwa sababu wenyewe haukubali kukosekana, na vile vile uwezo hauwezi kufungamana na jambo lisilowezekana, kwa sababu kama utafungamana nalo uwepo wake unakuwa ni kinyume na ukweli kwa sababu wenyewe haukubali kuwepo, na kama utafungamana na hilo basi kukosekana kwake kunakuwa ni jambo la lazima, na kwa hili kusudio la kauli yake Mola Mtukufu pale aliposema {Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu}[AL-BAQARA, 284]. Kwa maana: kila kitu kinaweza kuwepo au kutowepo. [Angalia kitabu cha: Al-Baijury juu ya maana ya Tauhid uk. 121].
Neno kuanzisha: chanzo chake ni ameanzisha: kwa maana amekuja na kitu kizuri. Amesema Al-Juhary katika: [Juzuu (3/1183) chapa ya Dar Al elim lil Malaayeen]: “Nimeanzisha kitu: “Nimekigundua si kwa kuiga, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwanzilishi wa mbingu na ardhi, uanzishi: muanzishi. Na uanzishi: pia muanzishi”.
Amesema Ibn Mandhwur katika kamusi ya: [Lisan Al-Arab 8/6 -7 chapa ya Dar Swaadir]: “Uanzishi: ni kitu ambacho kinakuwa mwanzo, na katika Qur’ani {Sema: Mimi si kiroja (mpya) miongoni mwa Mitume}[AL-AHQAF: 9], kwa maana: sikuwa Mtume wa kwanza kuletwa walishaletwa kabla yangu Mitume wengi… mwanamume mwanzilishi na mwanamke mwanzilishi ni pale anapokuwa lengo katika kila kitu, anapokuwa msomi, mtukufu au shujaa”.
Na akasema Al-Fayruz katika kamusi ya: [Al-Muhit 1/702, chapa ya Taasisi ya Risala[: “Neno uanzishi: ni jambo ambalo linakuwa mwanzo …. Na lengo katika kila kitu”.
Na maana inayofahamika kutokana na ibara: “Hakuna ubora zaidi kuliko kilichokuwepo” ni kuwa mfumo wa kuumba na mambo ya ulimwengu pamoja na hukumu ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake na mfumo wake ambao unapitia mambo yote ya dunia na Akhera, ameufanya Mwenyezi Mungu kwa umakini na ubora zaidi, Mola Mtukufu Amesema: {Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu}[AR-ROOM: 8].
Na Akasema tena: {Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?} [YUNUS: 32].
Makadirio ya kuwepo mfumo wa kuumba je ni kweli au upo makini zaidi ya alivyokadiria Mwenyezi Mugnu Mtukufu ni jambo lenye kuhesabika katika jumla ya mambo yasiyowezekana ambayo hayafungamani na uwezo wa Uungu, na wala sio maana ya hili ni kutowezekana kuweka mfumo usio kuwa mfumo huu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka atakuondoeni na alete viumbe wapya! Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu} [IBRAHIM: 19, 20}.
Kitendo cha kuleta waja wapya huenda hili likafungamana na utashi wa Mwenyezi Mungu, lakini makusudio ni kusema haiwezekani kuweka mfumo ulio bora zaidi kuliko mfumo huu, kwa elimu yake Mola Mtukufu kuwa hakuna ubora wala umakini zaidi ya wa kwake, na kufungamana utashi wake Mtukufu kwa kuufanya mfumo wa ulimwengu ni bora zaidi, kwa hili akili wala haijengi taswira ya mfumo wa ulimwengu uliokuwa nzuri zaidi ya mfumo aliyoufanya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na madamu mfumo ni nzuri zaidi basi unafungamana na elimu na utashi wa Mungu kwa makadirio yake na kuuweka kwake na kuwepo kwake, hakijabakia kilicho kizuri zaidi kinachofungamana na elimu pamoja na utashi, kwani kuwepo kitu kisichofungamana na elimu ya Mwenyezi Mungu na kutaka kwake ni jambo lisilowezekana, na kwa hili basi haufungamani uwezo kwa sababu uwezo unafungamana na vitu vyenye kuwezekana na wala sio mambo ya wajibu au yasiyowezekana.
Hii ndiyo maana ya kina iliyosahihi ya jumla ya maneno yaliyomo kwenye hiyo ibara iliyopokelewa kutoka kwa hoja ya Uislamu Ibn Hamid Al-Ghazaliy Mwenyezi Mungu Aitakase roho yake, lakini unabaki usahihi wa maana hii ukiwa umesimama kwa kuthibiti tangulizi mbili:
Utangulizi wa Kwanza: ni kuwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Amefungamanisha matakwa yake kwenye kukadiria mfumo ulio nzuri zaidi ukiwa ni sawa sawa kabisa.
Utangulizi wa Pili: ni kuwa mfumo ambao ameuweka Mwenyezi Mungu Mtukufu – kwa nguzo zake zote za kidunia na kiakhera juu na chini – ni wenye kufungamana na utashi huo unaoendana na makadirio ya mfumo ulionzuri zaidi na kuuweka, pindi tangulizi hizi mbili zinapothibiti ibara inakuwa ni sahihi kuwa: “Hakuna ubora zaidi kuliko kilichokuwepo”.
Na katika yanayofahamika ni kuwa pindi inapothibiti kuumbwa kitu fulani na kusifika kuwa ni miongoni mwa vitu vizuri basi inalazimika kuthibiti kuwa utashi wa Mungu umefungamana na uumbaji bora, na kuwa uumbaji mwengine ulio nzuri zaidi ya huu ni jambo lisilowezekana na lipo kinyume na uwezekano, kwa kulazimika kwake kuwa kinyume na ukweli.
Imechukuliwa kama dalili kauli yake Mola Mtukufu pale aliposema: {Hakika tumemuumba mwanadamu kwenye umbile zuri}[AT-TIN: 4].
Kuumbwa mwanadamu kwenye umbile zuri zaidi ya umbile hili ni jambo lisilowezekana, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameelezea kuwa hili ndio umbile zuri, amesema Imam Ibn Jariir At-Twabriy katika tafasiri yake ya: [Jaamii Al-Bayaan 24\506-508, chapa ya Taasisi ya Risala]: wametofautiana watu wa maelezo katika kuelezea kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu inayosema: {Hakika tumemuumba mwanadamu katika umbile zuri...} na kauli ya kwanza sahihi katika hilo ni kusema: hakika maana ya: tumemuumba mwanadamu katika sura nzuri na iliyosawa, kwa sababu kauli yake Mola: {umbile zuri} ni sifa ya aliyeondolewa, nayo katika neno umbile umbile zuri, kana kwamba pamesemwa: hakika tumemuumba katika umbile umbile lililozuri zaidi” na akasema Ibn Atiya katika kitabu cha: [Muhariri Al-Wajiz 5\499, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: na wamesema baadhi ya wanachuoni kwa ujumla, kwa maana: mwanadamu ni kiumbe aliye nzuri umbile, watu hawajaona msisitizo kwa mwenye kuapa juu ya kutoa talaka kuwa mke wake ni nzuri zaidi kuliko jua na kupinga aya hii”
Na akasema Al-Qurtwubiy katika tafasiri yake: [Al-Jamii li Ahkam Al Qur’ani 20\114, chapa ya Dar Al Kutub Al Masriya]: “Hili linaonesha kuwa mwanadamu ni kiumbe wa Mwenyezi Mungu nzuri ndani na nje, mwenye umbile zuri, mpangilio nzuri wa mwili wake: kuanzia kichwa chake na vilivyopo kichwani, kifua na vinavyokusanywa na kifua, tumbo na vilivyomo tumboni, tupu na vinavyopatikana kwenye tupu, mikono miwili na vinavyokunjuka kupitia mikono, miguu miwili na vinavyobebwa na miguu, na kwa sababu hiyo wanafalsafa wamesema kuwa: mwanadamu na ulimwengu mdogo, ambapo kila kilichopo kwa viumbe vipo kwake”
Na anasema Imam aS-Suyutwiy katika kitabu chake: [Tashyeen Al-Arkaan, 5\475, chapa ya Dar Al-Wa’i Al-Arabi – Halab] baada ya kuchukuwa ushahidi kupitia aya iliyotangulia: “Na hili ni andiko la moja kwa moja kuwa sura ambayo aliyoumbiwa mwanadamu hakuna uzuri zaidi yake, na vile vile tunasema kwa wanyama wengine waliobaki kuwa na wenyewe wapo katika sura ambayo hakuna uzuri zaidi sura hiyo iliyopo, na ushahidi ni kauli yake Mola Mtukufu: {Yeye ndiye Mola ambaye amekifanya kizuri kila kitu alichoumba}[AS-SAJDA, 7].
Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Mwenyezi Mungu Ameteremsha hadithi bora: Kitabu chenye maneno yanayopatana (na) yanayokaririwa, husisimka kwayo ngozi za wale wanaomwogopa Mola wao; kisha ngozi zao na mioyo yao huwa laini kwa kumkumbuka Mola wao. Huo ndiwo mwongozo wa Mwenyezi Mungu, kwa huo Humwongoza Amtakaye, na anayehukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hakuna wa kumwongoza}[AZ-ZUMAR: 23].
Kuteremka hadithi au kitabu cha uongofu kilicho bora zaidi ya Qur’ani ni jambo lisilowezekana kama ilivyokuwa wazi kwenye maelezo ya hii aya, kwa sababu Qur’ani ndio kitabu kilicho bora zaidi, na hii ni kutokana na mfumo wa kisheria wa Qur’ani kwani baadhi ya aya zilizofutwa kisomo japo kuwa zilikuwa ni Qur’ani kabla ya kuondolewa kwake lakini baada ya kuondolewa haziitwi Qur’ani japo kuwa ukweli ni katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu Qur’ani ni mfumo maalumu wa maneno ya Mungu yaliyo fadhilishwa kuliko mengine, na aya zake zinafadhilishwa kati ya zenyewe kwa zenyewe kwa mujibu wa mtazamo wa japo la wanachuoni.
Anasema Sheikh Ibn Taimiya katika kitabu cha: [Majmuui Al-fatawa 17\11, 13 chapa ya Majmaa Al-Malik Fahd]:
“.... na Amesema Mola Mtukufu: {Mwenyezi Mungu Ameteremsha hadithi bora: Kitabu chenye maneno yanayopatana (na) yanayokaririwa, husisimka kwayo ngozi za wale wanaomwogopa Mola wao} imeelezewa kuwa ni hadithi bora na kujulisha kuwa Qur’ani ni katika hadithi au kitabu kilichobora zaidi ya vitabu vyengine vilivyoteremshwa toka kwa Mwenyezi Mungu na visivyoteremshwa kutoka kwake... na kauli kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa bora baadhi ya yenyewe kwa wenyewe ni kauli iliyopokilewa toka wa waja wema waliotangulia ni kauli ambayo inaungwa mkono na Maimamu wanachuoni wa fiqihi toka makundi manne na wengineo, na maneno ya wasemaji wa hilo ni wengi na kuenea kwenye vitabu vingi”
Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kusifia mfumo wa kuumba na kina cha makadirio yake: {Na akakiumba kila kitu na akakikadiria kipimo}[AL-FURQAN, 2]. Inaonesha juu ukamilifu wa uangalizi wa viumbe na makadirio kwa ujumla wake na kwa kina zaidi.
Amesema Ibn Aashuur katika kitabu cha: [At Tahriir wa at Tanweer 18\318- 319, chapa ya Dar at Tuunisia cha Usambazaji – Nchini Tunisia]: “Kuumba: kuweka, kwa maana ameweka kila kilichopo kuanzia vile vitu vikubwa mpaka kidogo chake. {Ameumba kila kitu} {Na akakikadiria kipimo} ni dalili juu ya umakini wa kuumba umakini unaojulisha kuwa Muumba ni mwenye kusifika na sifa za ukamilifu” na maana ya neno {Basi Akakikadiria} akavifanya kwenye viwango vimoja maalumu na wala sio kujitokeza tu, kwa maana ameviumba vikiwa amevikadiria, kwa maana pia vimewekwa kwa hekima na kudhibitiwa vinafaa kwa kile kilichoumbwa kwa ajili yake hakuna tofauti ndani yake wala kasoro, na hili linahukumika kuwa Yeye ameumba kwa utashi wake na kufahamu namna alivyotaka na aina yake kama ilivyo kwenye kauli Yake: {Hakika yetu sisi tumeumba kila kitu kwa kipimo} [AL-QAMAR, 49], imetangulia katika kauli yake Mola Mtukufu: {Ameteremsha maji kutoka mawinguni, na mbuga zikapita maji kwa kadiri yao}[AR-RA’AD], na msisitizo wa kitenzi na mtendewa kwa kauli yake: Kipimo ikiwa ni dalili ya kuwa ni makadario kamili katika aina ya makadirio”
Imekuwa ngumu kwa baadhi ya wanachuoni kufahamu kusudio la Imam Al-Ghazaliy katika ibara hiyo, na wakadhania kuwa ndani ya ibara hiyo kuna kiwango cha kushindwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini kwa upande mwengine kumekuwa na wanachuoni wengi waliotoa juhudi kubwa katika kuibeba ibara juu ya maana inayokubaliana na sehemu ya hoja ya Uislamu Abi Hamid Al-Ghazaliy.
As Suyutwiy amesema ndani ya kitabu cha: [Tashyeed Al-Arkaan 5/475]: “Kitendo cha kukanusha katika maneno ya hoja ya Uislamu hakinasibishwi na uwezekano wa kuwepo kitu kisicho kuwepo, lakini kinanasibishwa kuwa kwake kizuri zaidi katika vilivyopo, katika hoja ya Uislamu ya kuwepo kitu ambacho kinawezekana kuwepo kwake kikawa ni kizuri zaidi kuliko kilivyokutwa, pamoja na kukatika kwake na uhalali wa uwezo wa kupatikana kwake, mkanushaji wakati huo atakuwa amesifika sifa zenye kuwezekana na siyo sifa ya uwezo kabisa”
Amesema Sheikh wa Uislamu Ibrahimu Al-Baijury katika kitabu chake cha: [ukurasa ya 87): imetokea katika maneno ya Al-Ghazaliy: Hakuna ubora zaidi kuliko kilichokuwepo, kuna makundi wakayatia ubaya kuwa ndani yake kuna maana ya kushindwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujibiwa kwa majibu yaliyokuwa mazuri zaidi kuwa kusudio la maana ya: Hakuna ubora zaidi kuliko kilichokuwepo, ni kutokana na kutofungamana na elimu ya Mwenyezi Mungu na utashi wake kwa kitu kisichokuwepo, ambacho ndio huu ulimwengu, ambapo haiwezekani kutofungamana elimu ya Mwenyezi Mungu na utashi wake na hilo, basi amesema kweli kuwa hakuna uwezekano kwa mazingatio haya hata kama inawezekana kwake mwenyewe”
Na anasema Ibn Hajar Al Haitamy katika: [Fatwa Al Hadithiya uk. 40 chapa ya Dar Al Fikr]: “jibu la maneno ya Al-Ghazali yaliyotajwa: hakika utashi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu pindi ulipofungamana na kupatikana kwa huu ulimwengu na akauweka pamoja na kuhukumu sehemu ya ulimwengu kubakia mpaka mwisho na sehemu nyengine kubakia muda wote nayo ni Pepo na Moto, hilo lilikuwa ni kizuizi cha kufungamana uwezo wa Kiungu kwa kukosekana ulimwengu wote, kwa sababu uwezo hauwendani isipokuwa kwa kitu chenye kuwezekana na kukosekana kwake haiwezekani si katika dhati yake, isipokuwa yale yanayoendana naye katika yale tuliyoyataja, na inapokuwa kukosekana kwake haiwezekani vile tulivyosema imekuwa kupatikana kwake mara ya kwanza ni kwenye hekima ya hali ya juu na umakini na inakuwa ni nzuri zaidi kiasi kinachowezekana kupatikana.
Amesema katika kitabu cha: [Tuhfat Al Muhtaj 1/23 – 24, chapa ya Dar Ihyau Al-Turath Al-Arabi]: na pindi alipoangali ukweli wake – kwa maana ya ukweli wa upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika matendo yake ambayo hayana mfano – na yale yanayofungamana na hoja ya Uislamu Al-Ghazaliy – Mwenyezi Mungu Amrehemu – Amesema: hakuna uwezekano kuanzisha kile kilichokuwepo. Kwa maana kila kiumbe siku zote wakati wowote anapoingia katika hatua ya kuumbwa inakuwa hakuna aliyenzuri kuliko yeye kwa upande kwamba elimu imefanya vizuri utashi umehusisha na uwezo umedhihirisha wala hakuna upungufu katika mambo haya matatu, basi ikawa kudhihiri kwake kwa sura nzuri na yenye ukamilifu pasi na kutafautiana kwa upande wa …….. {Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema} [AL-MULK, 3], bali kwa dhati zake kwa kuzingatia hukumu, kupingana kwake hilo lina lazimika kushindwa kwa muumba wa huu ulimwengu kuleta kilicho kizuri zaidi au kuwajibika kufanya kitendo kinachofaa zaidi au kuwa yeye mwenye kujiumba ni kiini cha ujinga, ikiwa itawezekana kuumba kizuri zaidi kwa kufungamana kuwepo uwezo na kukosekana kwake katika hali ya kuwepo kwake kuna lazimisha kukutana kwa vinyume viwili nalo ni jambo lisilowezekana halifungamani na sifa ya uwezo na wala halikanushi hilo kufaa uwezo pande mbili sehemu ya mbadala kwa kufungamana kila moja kati ya hizo mbili badala ya mwengine, kisha upingaji unakuwa ni wenye kudhaniwa”.
Sawa na maneno ya Ibn Hajar katika kitabu cha: [Tuhfat Al Muhtaji 1/23 – 24] anasema Ibn Kassim Al Ibadiy kauli yake: “Hakuna ubora zaidi kuliko kilichokuwepo”, ni wazi katika uwezekano tofauti na kilichokuwepo, kinyume na hivyo pangesemwa: haiwezekani isipokuwa kwa kile kilichopo, na kuwezekana ni tofauti na kile kilichopo pamoja na kulazimika kuwa kile kilichopo ni kizuri zaidi kinalazimisha uwezekano wa kisicho kizuri, na ikiwa inawezekana kwa kisicho kizuri basi ni kutoka wapi kuwa kile kilichopo kuwa ndio kizuri zaidi, isipokuwa imefaa kutokuwa hicho ni kizuri zaidi, kwa sababu upo uwezekano wa kisicho kizuri kuzingatiwa, na jawabu ni kuwa kisicho kizuri ikiwa kinawezekana inafaa kuwa ndio uhalisia kinyume na hivyo kisiwezekane basi ni kutoka kuwa uhalisia ndio nzuri zaidi, na ikiwa si chenye kuwezekana basi hapasemwi si katika uwezekano kuanzisha kilichopo isipokuwa ni kusema si katika uwezekano isipokuwa kwa kile kilichopo”.
Kisha Al-Ibadiy anajibu kuhusu mgongano huo kwa kusema: “Inawezekana kujibu kwa kuteua maelezo ya kwanza – nayo ni kuwa kisicho kuwa kizuri zaidi kinawezekana kwa upande wa dhati yake – lakini kuwezekana huenda kukazuia chengine basi inafaa kuzuia kutokea kisicho kizuri zaidi ili kuipa nguvu ya kutokea kilicho kizuri kwa kufungamana na elimu pamoja na utashi, kwa sababu hekima imo ndani yake”.
Hivyo basi hekima ya Mungu ndiyo ambayo imehukumu kuumba ulimwengu katika nidhamu iliyo nzuri ambapo imekuwa si katika uwezekano kuwepo nidhamu iliyo nzuri zaidi kuliko hii, na haya ndiyo yaliyopitishwa na Sheikh Ibn Taymia katika maelekezo yake ya ibara ya Imam Al-Ghazaliy.
Anasema Ibn Taimiya: “Yanyaokusudiwa ni kuwa Mola Mtukufu anaumba kwa kutaka kwake na kuteua kwake, na Yeye huwa anachagua kilicho kizuri zaidi, na kutaka kwake kunakupa nguvu zaidi kilicho kizuri zaidi, na huu ni ukweli wa utashi wala haingii akilini kutaka kuupa nguvu mfano juu ya mfano, lau ungekadiriwa kuwepo kwa mfano wa utashi huu basi huo ni ukamilifu na ubora zaidi, viumbe ni wenye kusifika hivyo na inazuilika kuwa kiumbe ni mkamilifu zaidi kuliko muumba mwenye kuweza kuumba ni mkamilifu zaidi kuliko kilichoumbwa, basi imelazimika kuwa kile kinachosifiwa na utashi wake ni kikamilifu zaidi kuliko kinachosifiwa na utashi wa mwengine, ni lazima kipatikane kile cha kwanza zaidi na kilicho kizuri na bora, naye Mola Mtukufu anafanya kwa kutaka kwake na kwa uwezo wake, basi mwenye kushindwa hawi na uwezo, na mwenye kuweza ambaye anaweza kufanya na anakuwa ni mwenye uwezo hupewa nguvu zaidi utashi, na kile anachokielezea Al-Ghazaliy kuwa amesema: si katika uwezokano kuanzisha kizuri kuliko huu ulimwengu, hilo lau lingekuwa hivyo na kisha asinge umba basi ungekuwa ni ubahili unaopingana na moyo wa kutoa, au kushindwa kunakopingana na uwezo, maneno haya yamepingwana na kundi kubwa, na maelezo yake ya kina ni kuwa chenye kuwezekana kinakusudiwa hapa chenye kuweza, hakuna shaka kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza tofauti na huu ulimwengu na kufanya uzuri zaidi kwa kitu chengine, na anaweza tofauti na alivyofanya kama tulivyobainisha hayo sehemu nyengine isiyokuwa hii na kubainika hayo sehemu nyengine isiyokuwa ndani ya Qur’ani, huenda ikakusudiwa kuwa haiwezi kuwa kizuri zaidi wala kikamilifu zaidi, hili halina ubishi kwenye uwezo, bali umethibiti uwezo wake kwa asiyoyafanya lakini amesema: aliyoyafanya ni bora zaidi na yenye ukamilifu kuliko yale asiyoyafanya, na hii ni sifa yake Mola Mtukufu ya ukarib utoaji na kufanya wema, naye Mola Mtukufu ni mkarimu zaidi wala hafikiriwi kuwepo aliye mkarimu zaidi yake Mola Mtukufu tofauti na wanayosema watu madhalimu ni ujitukuzaji mkubwa” [Jaamii Rasaail 1/141 – 142, chapa ya Dar Al Atwaa – Riyadh].
Na anasisitiza Ibn Taimiya mzunguko wa masuala kuhusu maana ya utoaji wema na hekima anasema: “Makusudio hapa ni kuwa kila akifanyacho Mola na kukiumba kitu basi kuwepo kwake ni bora zaidi kuliko kukosekana kwake naye pia ni mmbora kuliko vilivyopo vyengine vinavyo kadiriwa ni viumbe mbadala, kama tulivyotaja katika yale anayo yaamuru kuwa kutenda kwake ni bora kuliko kuacha kwake, na Yeye ni mbora wa utendaji kuliko vitendo vinavyofanywa na wengine, kama ilivyo katika kauli yake Mola Mtukufu: {Pindi inapoadhiniwa sala ya Ijumaa basi fanyeni haraka kwenda kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni kuuza kufanya hivyo ni bora kwenu ikiwa munafahamu} [AL-JUMAA, 9].
Na kauli yetu: kitendo chake ni bora kuliko kuacha kwake ni sawa sawa kuacha kuwepo au kukosekana kuwepo na Mola Mtukufu ni mwenye kupigiwa mfano bora naye ni mbora kuliko yeyote na mwenye kustahidi sifa kuliko yeyote na ni mbora wa sifa kamilifu na yupo mbali na sifa za mapungufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi