Mfumo wa Maarifa wa Kiislamu na Baadhi ya Uelewa Usiofahamika.
Question
Hivi kuna fikra na dhana zilizoenea juu ya urithi wa Kiislamu na mfumo wake wa kimaarifa, kuwa vimetuletea mifumo ya elimu za sasa?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Kuna matatizo mengi ambayo yanazigubika akili za mtafiti au mwenye kutafuta elimu ya sasa pindi anapokaribia urithi wake. Huenda tatizo la kwanza - linafungamana na mtafiti mwenyewe, linatokana na maarifa potofu kuhusu urithi katika sehemu zake na ujumla wake, na tatizo la pili - ambalo linasimama mbele yake - linafungamana na masafa kati ya urithi na elimu ya sasa, na linakuwa katika misamiati mingapi isiyofahamika kati ya lugha ya sayansi ya jamii na ubinadamu na maandiko ya urithi, bali na maandiko ya misingi mikuu miwili ya Uislamu ambayo ni “Qur`ani na Hadithi”.
Fikra na nadharia zilizoenea juu ya urithi wa Kiislamu na mfumo wake wa kimaarifa, haukuwa isipokuwa ni hali isiyofahamika imekuja katika mifumo ya sayansi za sasa, upande wa kadhia ya kuachwa bila vigezo, nakunasibishwa na vigezo. Haiwezekani kusema kuwa mfumo wa kimaarifa wa Kiislamu umeachwa moja kwa moja bila vigezo, na mfumo wa Kimagharibi ni wenye kunasibishwa kwa vigezo, nadharia hii ni batili. Na ubatilifu wake ni kule kusema “unasibishaji” ni kama msingi pia wa kuachiwa bila vigezo, ambapo inachukuwa maana ya neno kuachwa bila vigezo ni kutokuwa na mjadala wowote ndani yake, pia vyovyote watakavyo pinga hawa kuhusu kadhia ya kuachwa bila vigezo na wao pia wanaingia ndani yake, ni lazima kwetu sisi kufungua mshikano huu!
Pia kadhia ya Maadili na vitu halisi, na wito kuwa mfumo wa Kiislamu ni wa kimaadili, ama mfumo wa Kimagharibi ni vitu halisi na wala sio maadili, ni nadharia yenye makosa na kuchanganya, kwa sababu mfumo wa Kimagharibi pia ni wa kimaadili. Tofauti kati ya mifumo miwili hii ni kuwa mfumo wa Kiislamu unategemea Wahyi “ufunuo” kama chanzo cha maarifa yake, na mfumo mwengine hautegemea Wahyi au ufunuo. Au maarifa ya Uislamu yanasimama katika vyanzo viwili: Wahyi na uwepo… wakati ambapo maarifa mengine yanasimama kwenye uwepo peke yake. Hakuna tofauti katka kupata elimu kwa maadili au pasi ya maadili, maadili ni lazima, lakini tofauti ipo kuhusu: ni nani atakaye yafahamisha haya maadili? Pande za Magharibi - na wanaofanana nao - wanapingana kimfumo pale ninaposema: mimi ninategemea Wahyi “ufunuo” katika maarifa yangu. Watasema kuwa: hakuna tatizo kuamini Wahyi au ufunuo, kwa sababu mfumo wa Kimagharibi unasema: wewe upo huru katika imani yako, ima ufanye Wahyi au ufunuo ndio chanzo cha maarifa yako hakuna…. Kwani Wahyi ni chanzo chenye kufungamana na imani tu.
Kisha kadhia ya Dini au “Imani” na Elimu: wao wanatenganisha kati ya maarifa na imani, na wanafanya ni vitu viwili vyenye kupinzana, wanayafanya masuala ya imani kuwa yapo nje na masuala ya elimu, na wanaihusisha elimu na maana ya Science“Sayansi”. Na ukweli kuwa elimu ni “Sayansi” ni neno lililowekwa kuhusisha “elimu ya vitendo ambayo haithibiti isipokuwa kwa vitu vyenye kuonekana”, pindi ukifanyika uenezaji wa maana hii juu ya kila “Elimu ni Sayansi” basi maswala ya uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu yatazingatiwa si maswala ya mtazamo wa kielimu, kwa sababu sisi hatujamuona Mungu Mtukufu, na kadhia ya Uungu haingii kwenye maabara.
Ama kwetu haya hayakubaliki, kwa sababu “Elimu” kwetu sisi ni “Ufahamu unaoendana na ukweli unaotokana na ushahidi ni sawa sawa kwenye maabara au akili au kawaida…. n.k.”. Na “Elimu” kwetu sisi sio maarifa, kwa sababu elimu haipelekei kutanguliwa na ujinga tofauti na “maarifa” ambayo yanapelekea kutanguliwa na ujinga.
Tatizo ni katika hali ya sintofahamu iliyopo ya kutowezekana kufasirika neno “Elimu” la Kiarabu katika neno lisilo kuwa “Sayansi” na linalopelekea kwetu maana pana zaidi, pia tunahitaji tafasiri yake yenye maelezo katika jumla na wala si neno moja. Kwa mfano kunakuwa na hali ya kutoeleweka neno “Sayansi” linalomaanisha “Elimu ya Empirical” (Elimu ya kutegemea majaribio, na si nadharia) kufasirika kwetu “Elimu”!!
Tatizo la kufasiri na tofauti ya vitendea kazi vya lugha mbalimbali ni tatizo kubwa hakuna budi kuzinduka nalo, ni sawa sawa katika kuzungumzia urithi wa Kiislamu au kuzungumzia elimu za kisasa zenye mfungamano wa kina na elimu zengine. Uelewa wa Kiislamu haujafasiriwa kwenye lugha zengine, na wala haijatumika juhudi katika hilo kama juhudi zilizochukuliwa katika kuandaa terminology “Maneno” ya Kihindu ambayo yamehamishiwa kwenye uelewa wa watu wengine ndani ya makamusi makubwa, ambapo mwenye kusoma falsafa na elimu za Dini na jamii mbalimbali kwa lugha ya kiengereza kifaransa au lugha zengine inakuwa ni wepesi kwake kufahamu Terminology “maneno” ya Kihindu mpaka simulizi za sauti.
Pindi alipokuja “René Gino”([1]) ambaye ni Mfaransa ili kutafasiri kuhusu Uislamu hakupata ya kufasiri isipokuwa kwa kutumia terminology “maneno au misamiati” ya Kihindu. Kwa mfano neno “Sheikh wa Tariqa” hakupata neno lenye maana hiyo ndani ya lugha ya Kifaransa ndipo akachukua neno “Guru” la Kihindu. Na pindi tulipokuja sisi kuchukua toka kwa huyu mtu hatukupata ndani ya kamusi za Kifaransa neno “Guru”.
Haya ndiyo tunayojaribu kuyafanyia kazi sisi hivi sasa kiasi cha maneno kama mia tatu yameingia kwenye Kiingereza maneno kama: Haj, Jihad, Umma, Ulama….. na tafasiri za sauti kuhusu lugha ya Kiarabu iliyopo hivi sasa huko Magharibi haikuchukua kwenye lugha ya Kiarabu wala kwenye misingi au elimu za Kiislamu, lakini imechukua kupitia maisha yaliyopo ndani ya nchi za Kiislamu na kupitia pia wasomi waliopo… na hili lawezekana kabisa kuwa ni hatari inayozidi kuchukua nafasi katika ubadilishanaji wa uelewa mbaya wa lugha, wao wanawaona Waislamu wanapigana, basi wanayafasiri matendo hayo chini ya neno JIHADI nayo ni katika aina ya uzushi, wala haiwezi kuwa maana ya JIHAD ni aina ya vitendo vya ugaidi, ufisadi duniani na kupenda kumwaga damu, na linganisha hayo na maneno kama “Imani”, “Dini”, “Siyasa”, “Mtume”, “Utawala”, “Umma” na “Elimu”.
Kwa ufupi ni kuwa hakuna kamusi ya maneno “Vocabulary Glossary” ya Kiislamu… bali wao wametuletea maneno mengi hasa kupitia teknolojia iliyoingizwa toka nje mfano wa TT, Komputa, bunge take away… tunayatumia katika lugha ya Kiarabu kama yalivyo na hasa maana ambayo inakusudiwa, basi ni kwa nini hatulizungumzii neno “ELM” pindi tusipokuta ndani ya lugha ya Kiingereza linalokubaliana kwetu…?
Waislamu wa mwanzo walitengeneza daraja kati yao na wengine kwa misingi ya yale yaliyopo kwa Waislamu wenyewe, na kuwaingizia Uarabu wengine, wakati ambapo sisi hivi leo - na ndani ya kipindi hiki cha kihistoria - tunatengeneza daraja kutoka kwao, na tunadai kuwa ni mchanganyiko wa yale yaliyopo kwetu na yaliyopo kwao, sisi tunataka msaada kupitia lugha zao ili yakubalike maneno yetu na ya wekwe kwenye vyombo vyao vya kilugha! Hili ni tatizo kubwa la kutofahamu kikamilifu kadhia hii. Basi kinachohitajika hivi sasa katika wigo wa kushindwa ustaarabu, na kutegemea ustaarabu wa walioshindwa ustaarabu walioshinda kuwafahamisha wengine mshindi na lugha yake.
Na kwa upande wa misamiati isiyofahamika kati ya mwanafunzi wa sayansi za kijamii na za ubinadamu za hivi sasa na maandiko ya urithi, baadhi wanaona umuhimu wa kuwepo mtu wa kati anayesimama kati ya mwanafunzi wa masomo ya elimu za jamii na mwanafunzi wa masomo ya sheria ili kuondoa yaliyomo kwenye ufahamu huu, lakini - upande huu ambao sisi tupo - tunafanya haraka kwenye yale ya kina zaidi na mbali zaidi ya hayo, tunataka mwanafunzi kuwa mzalishaji mwenyewe wa maarifa elimu na ufahamu, na mwenye uwezo wa kuhamisha na kuyafanyia kazi, japo kuwa jambo lenyewe limekusanya vikwazo vingi na ugumu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: kitabu: “Njia ya Kufahamu Urithi” cha Mufti wa Misri. Dkt. Ali Juma.
(1) Ni mwanafikra wa Kifaransa ambaye alisilimu na kujiita yeye mwenyewe Sheikh Abdulwahid Yahiya, alizaliwa mwaka 1886 na kufariki mwaka 1951 na walisilimu watu wengu Magharibi kupitia yeye.