Mwanzo wa Safu ni Nyuma ya Imamu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwanzo wa Safu ni Nyuma ya Imamu.

Question

Safu huanzia upande gani wa nyuma ya Imamu? Je, huanzia upande wa kulia au huanzia nyuma ya Imamu moja kwa moja? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu.
Imamu husimama mbele ya safu ya kwanza na Maamuma hujipanga safu yao nyuma yake, na kwa hivyo Imam huwa karibu na kati ya safu, ambapo hali hii inajulikana kiasi kwa watu wa kawaida wanaoswali, safu isiyokamilika na hasa kama ikianza baada ya kuanza Imamu Sala yake, safu huanzia upande wa kulia katika baadhi ya nyakati, kwa ajili ya fadhila za upande huo kama ilivyotajwa katika Sunna.
Suala hili limezungumzwa na wanavyuoni wa Hadithi na Fiqhi katika sura zinazohusu kupanga safu, na walijaribu kupatanisha kati ya Hadithi zilizotajwa kuhusu suala hili. Hukumu ya suala hili ni kwamba safu zote nyuma ya Imam zina hukumu moja, lakini kama kuna safu ambayo haikukamilika basi iwe ya mwisho.
Inapendekezwa kuwa Safu zote zianzie nyuma ya imamu na imamu awe katikati yake. hakuna tofauti kati ya safu ya mbele na safu ya mwisho, na kama kuna tofauti yoyote, basi sala ni sahihi na mwenye kusababisha tofauti hii atakosa fadhila za Sunna.
Dalili ya hayo ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik kwamba: “Bibi yake Mulaika R.A, alimwalika Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. chakula alichokuwa ameandaa kwa ajili yake, akala, kisha akasema: “Simameni nikusalisheni”, Anas Ibn Malik amesema: Nilisimama kwenda kuchukua mkeka wetu uliokuwa umegeuka mweusi kwa ukuukuu wake, na kwa kutumika kwake muda mrefu nikaurashia maji, akasimama Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. juu yake, na mimi na yatima mmoja tukasimama safu nyuma yake, na nyuma yetu Bi mkubwa, akatusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. rakaa mbili kisha akaondoka”. [Hadithi hii Ina hukumu ya Maqbul (Imekubaliwa)].
Ushahidi katika Hadithi hii ni kwamba Mtume, S.A.W, aliwasimamisha Anas na yatima mmoja safu moja nyuma yake, na wala hakuwasimamisha upande wake wa kulia. Na hali hii inaonesha kupendeza angalau kidogo; kwani asili ni kufanya kilicho bora, hasa kama akiendelea hivyo. Miongoni mwa dalili pia ni Hadithi hii iliyopokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. anasema: «Mwekeni Imamu kati yenu na timizeni safu yenu ». [Imesimuliwa na Abu Dawud pamoja na wengine].
Al-Badr Al-Ainiy amesema: “Kauli yake: (Mwekeni Imamu kati yenu) maana yake ni: kwamba watu wanaosali wawe makundi mawili, kundi linalosimama upande wa Imam wa kulia na lingine linalosimama upande wake wa kushoto, na Imam awe kati yao, na siyo maana ya kuwa anasimama pamoja nao bega kwa bega; kwa sababu kazi ya Imam ni kutangulia watu. Na Hadithi ya Abu Hurayrah inafahamika kwa fadhila zake na siyo kwa Wajibu, hata kama watu wote wanaosali watakuwa wamesimama upande wa Imamu wa kulia au upande wake wa kushoto sala zao zitasihi, lakini wao watakuwa wameiacha Sunna ya Mtume S.A.W na fadhila zake pia”. [Sharhu Abu Dawud kwa Al-Ainiy 3/235, Maktabat Al-Rushd].
Al-Minyaawiy amesema: “(Mwekeni Imamu kati yenu) yaani : Imamu awe kati ya safu yenu ili kila mmoja wenu kati ya waliosimama upande wake wa kulia au upande wake wa kushoto apate bahati yake ya kusikia na kuwa karibu, kama kwamba Kaaba iko katikati ya dunia ili kila mmoja apate fungu lake la baraka”. [Faidhu Al-Qadeer 6/362, Al-Maktaba Al-Tujariyah Al-Kubrah]. Ama kuhusu safu ya mwisho, hakuna Hadithi iliyotajwa isipokuwa inayoeleza kuwa kama kuna safu haikutimizwa basi iwe safu ya mwisho tu. Imepokelewa na Anas Ibn Malik, R.A. kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amesema: “Timizeni safu ya mbele kisha ifuatayo. kama kuna safu haikutimizwa basi iwe safu ya mwisho”. [Imesimuliwa na Abu Daud.]
Shams Al-Haq Al-Adhim Abadi amesema: “(Timizeni safu ya mbele) yaani safu ya kwanza, (kisha ifuatayo), yaani kisha kamilisheni safu inayofuata safu ya kwanza na auendelea. (kama kuna safu haikutimizwa). kauli hii ni dalili ya kuwa safu ambayo haikutimizwa iwe safu ya mwisho. Na katika Hadithi ya Abu Hurayrah kauli yake: (Mwekeni Imamu kati yenu) yaani wale wanaosali katika safu ya mwisho isiyokamikishwa wasimame upande wa Imamu wa kulia na upande wake wa kushoto. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi”. [Awn El-Mabod 2/260, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]. Ama yaliyotajwa kuhusu hali ya kuupendekezwa upande wa kulia, ni baada ya Imamu kusimama kati ya safu; kwani hali hii ni pamoja na dalili hizi mbili, na matini iliyotajwa siyo kinyume na hali hii, imepokelewa kutoka kwa Aisha R.A amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: «Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanasali upande wa kulia wa safu ». [Imesimuliwa na Abu Dawud].
Ibn Illan amesema: “Imepokelewa kutoka kwa Aisha, R.A, kuwa Mtume wa Mwenyezi S.A.W. amesema: «Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanasali upande wa kulia wa safu » yaani safu yoyote iliyoko kwenye upande wa kulia wa Imamu, kutoka katika Hadithi hii, maimamu wetu walifahamu kuwa kusimama upande wa kulia wa Imamu kunapendekezwa hata kama hali hii ikipingana na kusimama karibu na Imamu, maana ya hayo ni kwamba maamuma anaposwasili msikitini na akamwona Imamu anasimama mbele lakini kati ya safu na akaiona nafasi upande wa kulia na nafasi nyingine upande wa kushoto basi inapendekezwa kusimama upande wa kulia, si lazima kuwa hali ya kupendekeza upande wa kulia ipingane na kuacha Sunna ya kusimama Imamu kati ya safu inayohitajika pia, na inatakiwa kusimama upande wa kulia kama kuna nafasi inayotosha, au inapendekezwa kushindana ili kusimama upande wa kulia na watu wengine wanaosali na ambao wamebaki wanaweza kusimama upande wa kushoto, kama kwamba Sunna ya Mtume S.W.A. ni kutimiza safu ya kwanza halafu safu inayoifuata n.k.” [Dalilu Al-Falihiin Litariq Riyadh Al-Salihin 6/575, Dar El Maarefa lel Tibaa wal Nashr wal Tawzii].
Kundi la Wanavyuoni limesema kama tulivyosema :
Al-Khatwib Al-Shirbiniy alisema: Sunna ni kwamba Imamu anasimama mbele ya safu lakini kati yake na maamumu huanza kusimama ubavuni mwake, na inapendekezwa kusimama upande wake wa kulia. Ni Sunna kujaza nafasi zilizopo kwenye safu, na kwamba wasianze kusimama katika safu mpya isipokuwa baada ya kukamilisha safu ya mbele, na kuweka nafasi kwa anayetaka, na mambo yote haya yanapendekezwa siyo lazima, kama kuna aliyeenda kinyume na hayo basi sala ni sahihi pamoja na kuchukiza.” [Mughni Al-Muhtaj Ila Marefatu Al-Fadhu Al-Mihaj 1/493, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Al-Nawawiy amesema: “Kama Imamu na maamumu watakuwepo, Imamu atasimama mbele na maamumu watasimama nyuma yake, kama walikuwa wanaume wawili au wavulana wawili au mwanaume na mvulana. Hii ni kwa mujibu wa madhehebu yetu ambayo ni madhehebu ya Wanavyuoni wote, isipokuwa Abdullah Ibn Masuod na wenzake wawili Al-Qamah na Al-Aswad, wao walisema: Imamu na maamuma watasimama katika safu moja”. [Al-Majmuu Sharhu Al-Muhadhab 4/292, Daru Al-Fikr].
Al-Kasaani Alisema: Mahali (bora) kwa maamuma akiwa mwanamume ni mahali ambako ni karibu na Imamu, kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume, S.A.W: «Safu ya wanaume iliyo bora ni safu ya mbele na safu iliyo daraja la chini zaidi ni safu ya mwisho ». Na kama nafasi zote ni sawa katika ukaribu na Imamu basi inapendekezwa kusimama upande wake wa kulia, kwani Mtume S.A.W alikuwa akipendelea kuanza upande wa kulia katika mambo yote. [Badai'i Al-Sana'a fi Tartiib Al-Sharai 1/159, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ibn Qudaamah amesema: “Inapendeza kwa Imamu kusimama mbele, nyuma yake ni kati ya safu, kufuatana na Hadithi ya Mtume S.A.W: « Mwekeni Imamu kati yenu na timizeni safu yenu ». Imesimuliwa na Abu Dawud. [Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 2 161, Maktabat Al-Qahira].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu inaonesha kuwa Sunna ya Mtume S.A.W. inayopendekezwa kuifuata kuhusu kuanza safu nyuma ya Imamu ni kusimama nyuma ya Imamu moja kwa moja, na kisha Imamu kuwa kati ya safu, na kuanzia mahali pa kati sambamba na Imamu, safu zote huanza, kutimiza nafasi zilizoko upande wa kulia wa safu ni bora zaidi kuliko upande wa kushoto, na katika hali ya kutokamilika kwa safu ya mbele basi ni lazima kukamilisha safu hiyo na kisha upungufu huo uwe kwenye safu ya mwisho.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas