Kundi la Wahabeshi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kundi la Wahabeshi

Question

Limetufikia ombi linalohusiana na ufahamu kuhusu “kundi la Wahabeshi” na yanayofungamana na wao miongoni mwa maelezo yao imani zao na mfumo wao. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..

Kundi la Wahabeshi wananasibishwa na Sheikh Abdullah Ibn Muhammad Ibn Yussuf Al-Harariy, amezaliwa mwaka wa 1328 H / sawa na mwaka wa 1910, katika mji wa “Harar” unaopatikana eneo la Habasha.

Al-Habashiy alihifadhi Qur`ani akiwa na umri mdogo, alisoma elimu za sheria nchini kwake, kama vile masomo ya Tafsiri, Hadithi, Fiqhi na Lugha, alisafiri nchi mbalimbali, kama vile nchi za Hijazi na Shamu mwishowe akaishi huko Beirut.

Wafuasi wake wakati mwingine wanaitwa wahabeshi, na wakati mwingine wanaitwa Jumuiya au Mushaariiyiin, wakinasabishwa na Jumuiya yao ya Al-Mashaariy Al-Islamiya, lakini unasibishwaji wa kwanza ndio ulioenea zaidi.

Makao makuu ya kundi hili ni huko Lebanon, wamekuwa na ushiriki mkubwa katika jamii ya Lebanon kwenye maeneo mbalimbali, ya kisiasa kielimu kihabari na kijamii.

Ama kwa upande wa kisiasa: kulikuwa na wagombea wawili wa nafasi ya ubunge, mmoja alishinda ndani ya Beirut, naye ni Dkt. Adinan Al-Tarabulsiy, ushindi huo ulikuwa mwaka 1992.

Upande wa kielimu: walianzisha shule maalumu nyingi kwa hatua mbalimbali za masomo kuanzia msingi mpaka sekondari.

Kwa upande wa habari: wamekuwa na idadi kadhaa za machapisho mbalimbali katika Elimu za Tauhid, Fiqhi, Taswafu na elimu zinginezo, kama vile wana gazeti lao wao wenyewe, nalo ni: gazeti la Manaar Al-Hudaa, pia wana kituo cha kurushia matangazo “radio” jina lake: “Radio ya Ulinganiaji Iman” nayo ni radio inayorusha matangazo yake nchini Lebanon na nje ya Lebanon, kama vile wana tovuti mbalimbali za elektroniki zinazo eneza fikra na nadharia zao kwa zaidi ya lugha moja, miongoni mwa hizo ni tovuti iliyopo kwenye link hii http://alharary.com/vb: na link ifuatayo: http://www.aicp.org .

Upande wa kijamii: wana klabu yao.

Kwa upande wa kiidara: wana matawi mbalimbali ndani ya mikoa ya Lebanon.

Hizi ni juhudi na harakati zao ndani ya ardhi ya Lebanon, ama nje ya Lebanon: wamekuwa na harakati za nje na ofisi nyingi ndani ya nchi mbalimbali, miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na: Jordan, Australia, Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa, Sweden, Ujerumani, Denmark na nchi nyingi nyingine.

Ama kuhusu ufadhili wao: huwa wanasema: ufadhili wao wanajitegemea kupitia ushiriki wa uwanachama na kujitolea kwa wahisani ambao wanaongezeka siku baada ya siku, kuongezea pia miradi yao mbalimbali, kama vile miradi ya shule vyuo vikuu, kuongezea vituo vyengine vya afya. Wanasema pia: wanaendesha miradi yao inayokwenda sawa na hilo, hawachukui ruzuku kutoka nchi yoyote, mwaka 1983 walitoa orodha ya majina ya wahisani wao.

Baadhi ya wazushi wanaeneza habari kuwa wanapata ruzuku yenye shaka ndani yake, lakini madai haya hayajawa na athari yoyote, isipokuwa ni ibara ya uzushi tu uliojengwa na utangulizi wenye kuchekesha, wakati mwingine wanadai kuwa free mason ndio chanzo cha ufadhili, wakati mwingine Wayahudi, na wakati mwingine kutoka maadui wa Uislamu kwa lengo la kuimarisha kundi ndani ya jamii ya Kiislamu. Angalia sehemu ya kitabu hiki: [Kundi la Wahabeshi cha Al-Shaharaniy 1/108: 126 chapa ya Dar Aalimu Al-Fuad].

Ama kuhusu itikadi zao mitazamo yao na maelekezo yao, tumepata idadi kubwa ya vitabu vyao na machapisho yao ambayo yameandikwa na Sheikh wao Al-Habashiy, au vimeandikwa na baadhi ya wanafunzi wake na wafuasi wake, na kuchapishwa kupitia kwenye miradi yao ambayo inasimamia uchapishaji wa utunzi wao na vitabu vyao, na tumeweza kupitia vitabu na machapisho yao kufahamu imani zao madhehebu yao ya kifiqhi pamoja na mwenendo wao.

Miongoni mwa vitabu vya Sheikh Al-Habashiy tumefahamu:

1-      Idh-haarul Akiida Al-Sunniya Sharhu ya Akiidatul Twahawiya, chapa ya pili 1416H – 1996 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

2-      Bughyat Al-Twalib cha Ufahamu wa Wajibu wa Kidini, chapa ya tatu 1416H – 1996, chapa ya Dar Al-Mashaariiu.

3-      Al-Tahdhir Al-Ashar’iy al Wajib “Juzuu ya Kwanza” chapa ya pili 1425H – 2002 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

4-      Ad-Dalil Al-Ashaar’iy juu ya uthibitisho wa maasi kwa mwenye kuniulia mfuasi wangu, chapa ya kwanza 1419H – 1998 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

5-      Al-Sirat Al-Mustaqim, chapa ya tisa 1413H – 1993 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

6-      Sarih Al-Bayan katika kumjibu yule mwenye kutofautiana na Qur`ani, chapa ya kwanza 1415 – 1995 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

7-      Mukhtasar Abdallah Al-Harariy: chenye elimu muhimu ya Dini, chapa ya sita 1417H – 1996 chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

8-      Al-Matwalib Al-Wafiya, Sharhu ya Aqiidatul Al-Nasfiy, chapa ya pili, 1418H – 1998, chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

9-      Al-Maqalatul Al-Suniya katika kuonesha upotovu wa Ahmad Ibn Taimia, chapa ya tano, 1423H – 2002, chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

Miongoni mwa vitabu vya wafuasi wake na wanafunzi wake:

1-      Al-Tahdhir Al-Ashar’iy kwa mwenye kwenda kinyume na watu wa Sunna, kimeandaliwa na: kitengo cha utafiti na masomo ya kiislamu katika Jumuiyatul Mashaariiu Al-Khairiya Al-Islamia, pasi na maelezo.

2-      Amru Khaalid katika mizani ya sheria, cha Sheikh Usama Al-Sayyid, ni miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh Al- Mashaariiu.

3-      Al-Qardhawiy fi Al-Arai, cha Sheikh Usama Al-Sayyid, chapa ya kwanza 1423H – 2002, chapa ya Dar Al-Mashaariiu.

4-      Al-Qaul Al-Fasl Al-Munjii katika kumjibu Hassan Qatraji, maandalizi: Jumuiyat Al- Mashaariiu Al-Khairiya Al-Islamia, chapa ya pili 1418H-1997, chapa ya Dar Al- Mashaariiu.

5-      Al-Nahj Al-Swawiy katika kumjibu Sayyid Qutwubu na kufuatilia Faisal Maulawiy, kusambazwa: Jumuiyat Al-Mashaariiu.

Kwa ufupi tumeona kwao yafuatayo:

Kwa upande wa imani: tumeona imani ya Sheikh Al-Habashiy kupitia vitabu mbalimbali miongoni mwa hivyo: sharhu yake katika masuala ya imani ya Al-Twahawiya, na sharhu ya imani ya Al-Nasfiya, naye katika jumla ya sharhu zake hazipo mbali na vitabu vya imani ya watu wa Sunna miongoni mwa watu wa Al-Ashaaira na Al-Maturidiya, lakini ameelezea vitu tofauti na kauli zenye kutegemewa kwenye madhehebu, japo kuwa kumekuwepo baadhi wenye kusema kwa mtazamo wake, miongoni mwa kauli hizo:

1-      Kauli ya kuwa Mitume inafaa kwao kuwa na makosa madogo madogo kinyume na makosa madogo {sherehe ya Twahaawiya uk. 56, sherehe ya Al-Nasfiya uk. 137}.

Usahihi ni kuwa Mitume ni wenye kulindwa kutokana na makosa hata kufanya vitendo vyenye kuchukiza, kama ilivyoandikwa katika Hashiyat Al-Baijuriy ala Jauharat Al-Taheed. [uk. 200, 201 chapa ya Dar es Salaam]

2-      Ruhusa ya kuwakufurisha madhehebu ya Al-Muutazila kwa madai kuwa wanasema: hakika mwanadamu ni mwenye kutengeneza matendo yake, kama ilivyo katika kitabu chake cha [Al-Sirat Al-Mustaqim, uk. 65: 66 na sherehe Al-Nasfiya uk. 96].

Amesema mwanachuoni Ad-Dusoqiy katika (kitabu chake cha sherehe ya Ummu Al-Barahiinu, uk. 47 chapa ya Dar Al-Twaba): “Usahihi ni kutowakufurisha kwa sababu wanasema: hakika ya mja hufanya matendo yake yeye mwenyewe hiyari kwa nguvu Alizomwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu, nao ni uwezo uliopo ambao ameuumba kwa mwanadamu”.

Na akasema Ibn Abdeen katika kitabu chake uk. 3/46 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya: “Ipo ruhusa ya kuwakufurisha watu wa Al-Muutazila na mfano wao wakati wa kuzungumza nao katika kujibu madhehebu yao kuwa wamekufuru, kwa maana, inapelekea kutokana na kauli yao kwa jambo fulani kukufuru, na wala haipelekei hilo kuwakufurisha, pia wao hawakusema hivyo isipokuwa kwa mfanano wa dalili ya kisheria kwenye dhana yao, na ikiwa watakosea walazimishe……..” lakini baada ya hapo amefahamu kwenye (sharhu Al-Nasfia uk. 97) na akasema: “Piandi tunapo wakufurisha basi hatumaanishi kukufurisha kila mwenye kujinasibisha na Muutazila, lakini tunachomaanisha: mwenye kuthibitika kwenye haki yake kadhia maalumu inayopelekea kukufuru kwake”.

3-      Na miongoni mwa rai zake ni pamoja na kufaa kukosoa Maswahaba katika yale waliyokosea, ikiwa na kumpinga kwao Swahaba Muawiya R.A. chanzo: [sharhu Al-Twahawiya uk. 213: 215, na mfano wake katika sharhu Al-Nasfiya uk. 148:149, kama alivyotunga kitabu alichokiita: “dalili za kisheria juu ya kuthibiti uasi kwa mwenye kuniulia Sahaba zangu na wafuasi wangu]”.

Na lililopitishwa kwa watu wa haki ni kuwa Amir wa Waumini Ally R.A. alikuwa yupo sahihi ama waliomuua walikuwa kwenye makosa, lakini pamoja na hayo wametamka pia kuna ulazima wa kuyanyamazia yale yaliyokuwa yanamvutano kati ya Masahaba na kutoyaingia yale yaliyokuwa yakiendelea kati yao ambayo yanagusa haiba zao takatifu, au kuyapinga, kwa sababu wao wametanguliza mengi, na kuyaingilia yaliyo kati yao ni kama fitina ya ndani ya kuwahukumu Wafalme.

Imepokelewa na Ahmadi katika kitabu cha: [Fadhaaili Al Swahaba 2/910 chapa ya Taasisi ya Ar-Risaala] kutoka kwa Ibn Abbas R.A. kuwa Mtume amesema: “Musiwatukane Masahaba wa Muhammad, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameamrisha kuwatakia msamaha, hali ya kuwa Mwenyezi Mungu anajua kuwa watauwana”.

Imepokelewa na Khilal katika kitabu cha: [Kitabu Al-Sunna 2/461 chapa ya Dar Ar-Raaya] kutoka kwa Umar Ibn Abdulaziz kuwa: alikuwa pindi anapoulizwa kuhusu saffin na jamal alisema: ni jambo Mwenyezi Mungu Ameondoa mkono wangu katika hilo wala siingizi ulimi wangu ndani yake”.

Na akasema Imam Al-Ashaariy katika kitabu cha: [Ibana uk. 260 chapa ya Dar Al-Ansar] kuwa: yale yaliyotokea kwa Ally Zubeir na Bibi Aisha R.A. kwa hakika yalikuwa ni katika ufafanuzi wa maelezo na jitihada, Ally ni Imam na wote ni katika watu wa jitihada, Mtume S.A.W. amewabashiria Pepo na kuwa ni mashahidi, basi inaonesha kuwa wao wote walikuwa katika njia sahihi na ya haki katika jitihada zao, na vile vile yale yaliyoendelea kati ya Ally na Muawiya R.A. pia imeonesha ni ufafanuzi na jitihada. Masahaba wote ni maimamu waliosalama si wenye kutuhumiwa kwenye Dini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamewasifu Masahaba wote, na tumetakiwa kuwatukuza kuwafuata na kuwa mbali na kila mwenye kupunguza nafasi ya Sahaba yoyote yule miongoni mwao R.A.

Na pakasemwa kuambiwa Ahmad Ibn Hanbal kama ilivyo kwenye wasifu wa Ibn Al-Jauziy uk. 221 chapa ya Hajar: “Ewe Baba wa Abdillahi, unasemaje kuhusu yale yaliyotokea kati ya Imam Ally na Muawiya? Akasema: Sina ninachokisema kuhusu wao isipokuwa ni mazuri tu”

Amesema Al-Maruudhiy: nimemsikia baba wa Abdulillahi – yaani: Imam Ahmad – alitajiwa Masahaba wa Mtume S.A.W. akasema: Mwenyezi Mungu Awarehemu wote, Muawiya, Amru Ibn Al-Aas, Abu Musa Al-Ashaariy na Al-Mughira wote hao Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewasifu ndani ya Kitabu chake, na Akasema: {Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na waliopamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu Amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa} [AL FATH, 29].

Na akasema Imam Al-Nawawiy katika kitabu cha [Sharhu Muslimu 18/11 chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Araby] wakati wa kusherehesha kauli yake Mtume S.A.W. pale aliposema: “Pindi Waislamu wawili wanapoelekezea mapanga yao basi muuwaji na muuliwaji wote ni watu wa motoni”. Fahamu kuwa vitendo vya umwagaji damu vilivyo tokea kati ya Masahaba R.A. havingii katika ahadi hiyo, na madhehebu ya watu wa Sunna wanasema ni haki ya kuwadhania dhana njema pamoja na kuyanyamazia migogoro iliyokuwa inatokea kati yao, na kuleta maelezo ya mauaji yao na hali ya kuwa wao ni wenye kufanya jitihada hawakuwa wakikusudia kufanya maasi duniani, isipokuwa kila kundi lilikuwa linaamini kuwa lipo kwenye haki na kwenda kinyume na wao ni upotovu hivyo inapaswa kushambuliwa ili kurudi kwenye amri ya Mwenyezi Mungu, baadhi yao walikuwa ni tatizo na baadhi yao walikuwa ni wenye kufanya makosa ni wenye kusameheka kwenye makosa yao, kwa sababu walikuwa ni katika hali ya jitihada zao, na mwenye kufanya jitihada katika jambo pindi akikosea hana dhambi, Imam Ally R.A. alikuwa ni mwenye haki na kufanya vizuri katika vita hivyo, huu ndio mtazamo wa madhehebu ya watu wa Sunna, kadhia zilikuwa ni zenye shaka shaka mpaka kundi moja la Masahaba walishangazwa na kujitoa pasi na kupigana na kuacha kusaidia.

Ama kuhusu Sahaba Muawiya R.A. ambaye ni mwandishi wa wayhi “ufunuo” Mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haitimiy alikuwa ameandika kitabu alichokiita: “Tathir Al-Jinan wa Al-Lisan Anil-Khoodh wal tafuuhu bithalabi Muawiya Ibn Sufyaan” pia sheikh Abdulaziz Al-Farhariy alitunga kitabu alichokiita “Al-Naahiya an twaan Amir al muuminiin Muawiya”

Kwa upande wa matawi: Sheikh Abdallah Al-Habashiy ni mwenye kufuata madhehebu ya Imam Shafiyy, aliwahi kutunga kitabu jina lake “Mukhtasar Abdillahi Al-Hirariy Al-Kaafil bi elimu Dini Al-Dharuuriy” alikusanya ndani yake jumla ya masuala ya imani na masuala ya sheria “Fiqhi” ikiwa ni pamoja na mambo ya usafi “twahara” Hijja na sehemu ya hukumu za miamala “mashirikiano”, kisha akazungumzia kuhusu maasi ya moyo na viungo, nayo ni ufupisho wa kitabu kinachoitwa “Silmu Al-Taufiq” cha sheikh Abdillah Ibn Al-Husein Al-Hadhramiy.

Sheikh Al-Hirariy alisherehesha kitabu alichokiita “Bughyatu Al-Twalib ilaa Maarifat Elimu Ad-Diiniy Al-Waajib” na kuelezea kwa mapana masuala matini na kutoa dalili zake.

Kwa upande wa mwenendo: imekuja katika ufasiri wake uliosambaa mwanzoni mwa baadhi ya vitabu vyake, miongoni mwa hivyo: [Al-Matwalib Al-Wafiyya uk. 12, 14] kuwa yeye alipata Ijaza kwenye Tarika ya Ar-Rifaaiya kutoka kwa sheikh Abdurrahmaan Al-Sibsiby Al-Hamawiy, na sheikh Twaahir Al-Kayaaliy Al-Humuswiy, na alipata Ijaza kwenye Tarika ya Qadiriya kutoka kwa sheikh Ahmad Al-Arabiy na sheikh Al-Twayyib Ad-Damashqiy na wengineo – Mungu Awarehemu – pia alipata Ijaza ya Tarika ya Al-Naqshabandiy kutoka kwa sheikh Abdulghafuur Al-Afghaniy Al-Naqshabandiy, na yaliyo pokelewa ni kuwa Sheikh Al-Hirariy anawaunga mkono wafuasi wa Tarika ya Ar-Rifaaiya.

Na katika kitabu cha [Al-Tahdhir Al-Shariy Mimman Khaalafa Ahli Al-Sunna” cha Sheikh Al-Habashiy uk. 76] kuna kauli yake: ushirika wa mja kwa Mola wake ni ushirika ulio safi, hii ndiyo Al-Taswauf. Ama hawa ambao Taswaufi kwao ni ibara tu ya kuimba na kubeba tasbihi kisha kusema fulani amesema hivi na fulani amesema hivi, hawa ni watu wavivu na kudai ni watu wa Taswaufi lakini hawaifanyii kazi hiyo Taswaufi kwa njia ya watu wa Taswaufi – kwa maana ya sufi walio na msimamo thabiti – kama vile Sheikh Al-Juneid.

Imekuja katika baadhi ya vitabu vyake akikosoa yale yanayosemwa na baadhi ya watu wanaojinasibisha na Tasaufi kwa kauli vitendo na imani iliyokinyume na Sheria Takatifu, kama vile kupinga kwake imani ya madhehebu ya Muungano” ([1]) kitabu cha: [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib 1/15, 21] na kupinga kwake kauli ya kuwa Mtume S.A.W. ameumbwa kutokana na nuru ya Mwenyezi Mungu [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib uk. 28], na kupinga kwake kauli ya mwenye kusema ujinga wa watu wa Taswaufi: Mawalii na watu maalumu hakuna haja kwao ya kusoma elimu ya Dini wala sheria, isipokuwa inatosha kwao ufunuo [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib 1/170].

Na tahadhari yake kutokana na neno ujinga wa watu wa Tasaufi ambao hawatambui sheria, na pindi wanapopingwa na mpingaji katika yale yanayokwenda kinyume na sheria husema: nyinyi ni watu wa mambo ya nje na sisi ni watu wa mambo ya ndani hatuwezi kukubaliana. [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib 1/194].

Na tahadhari yake kwa yale yaliyozushwa na watu wa Tarika ya Shaadhiliya faas kuondoa herufi laam na kuhusisha herufi ya alifu na haa katika jina la Mwenyezi Mungu wakati wakulitaja. [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib 1/175, 176].

Na pia tahadhari yake kutokana na watu wa tarika ya Shaadhiliya Al-Yashratwiya kwa kile kilichothibiti kwao kuhusika na kwenda kinyume na sheria pamoja na Dini. [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib uk. 144 – 148. Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib mimman khaalafa ahlu al-sunna uk. 89, 90].

Watu wengi wamemjibu Sheikh Al-Habashiy na wafuasi wake na kuwakosoa katika masuala mengi, tumepata idadi kadhaa ya vitabu hivyo navyo ni:

1-     Al-Habashiy Shudhuudhuhu wa Akhtwaauu, cha Abdurahmaan Muhammad Said Damashqiya “kimeingizwa kwenye mtandao wa kimataifa wa Internet”.

2-     Diraasat Naqdiya fii Aqiidati Al-Ahbash Al-Harariya, mtunzi: Muhammad Hassan Bakhiit, na Muhammad Mustafa Al-Jadiy, nayo ni tafiti ya shahada ya uzamifu kitivo cha masomo ya akida na misingi ya Dini chuo kikuu cha Kiislaamu Ghaza Palestina, kimechapwa kwenye gazeti la chuo kikuu cha Kiislaamu – mfululizo wa masomo ya ubinadamu – Juzuu ya kumi na nane Toleo la Pili – June 2010.

3-     Ar-Raddu alaa Abdillah Al-Habashiy, cha Abdulillah Muhammad Al-Shamiy, chapa ya Dar Al-Itilaai.

4-     Fataawa Muaaswira, cha Dkt. Yuusuf Al-Qardhawiy 3/693 – 710 chapa ya Dar Al-Qalam ya uchapishaji na usambazaji, chapa ya pili 2002.

5-     Firqatu Al-Ahbash kuanzishwa kwake, imani zao, athari zao, cha Dkt. Saad Ibn Ally Al-Shahraniy, chapa ya Dar Aalam Al-Fawaid, Riyadh, chapa ya kwanza 1423.

6-     Al-Maqalat Al-Saniya fi Kashf Dalalat Al-Firqa Al-Habasha, cha Abi Suhaib Abdulaziz Ibn Suhaib Al-Malikiy “kimeingizwa kwenye mtandao wa kimataifa wa Internet”.

7-     Mausuat Ahl Sunna, katika kujadili misingi ya kundi la Al-Ahbash na wale wanaowakubali katika misingi yao, cha Abdirahman Demashqiy, chapa ya kwanza 1418H- 1997 chapa ya Maktaba Al-Shaqriy.

Na baada ya kuviangalia vitabu hivi tumekuta kuwa masuala yanayo kosolewa dhidi ya Ahbash vinagawanyika katika masuala ya imani na masuala ya sheria.

Ama masuala ya Imani yanayokosolewa kwa watu wa Al-Ahbash, katika kufuatilia maelezo juu yao imeonekana kwetu kuwa mwenye kukosolewa kwa ukweli sio Al-Habasha na wafuasi wake, isipokuwa anayekusudiwa kukosolewa ni madhehebu ya watu wa sunna na jamaa miongoni mwa Al-Ashaaira na Al-Matridiya kama walivyo, jina na picha ni ukosoaji wa Al-Ahbash, na mwenye kufungua kurasa za masuala haya yanayokosolewa atafahamu hilo, kutokana na hilo: ni kuwa kumfahamu Mwenyezi Mungu ni wajibu wa kwanza, na kukosolewa Al-Ahbash kutoigawa Tauhid ya pande tatu ya Uungu Majina na Sifa, na maelezo ya nje yake ni yenye kufanana na sifa, na ufahamu wa imani na kutoathiri sababu zenyewe, na masuala mengine ambayo yamefanywa na baadhi ya watu wanaojinasibisha na waja wema waliotangulia ikiwa ni uzushi wakibainisha mwenendo ambao umeridhiwa na umma.

Ama masuala ya Sheria yanayokosolewa kwa watu wa Ahbash, yametajwa katika vitabu vya kimadhehebu, lakini mkosoaji hakufahamu maneno ya Al-Habashy na kumzushia maneno, au ufahamu wake na kushangaa kwake, kwa sababu inakwenda kinyume na yale aliyoyaeleza kuyatunga na kuyapinga, katika hali hizi zote mbili haiwezekani kumpinga Al-Habashy kwa sababu tu ya kuteua rai ya kisheria iliyokwisha tangulia, au ameisema mwanachuoni mwengine katika wale waliotangulia, kwa sababu hakuna madhehebu inayopingana na madhehebu, kama vile haipingwi rai na nadharia yenye tofauti ila hupingwa ile iliyokubalika, kwa sababu masuala ya matawi lengo lake ni mtu kuwa ni mwenye kukosea.

Miongoni mwa rai na nadharia hizi ni kama:-

1-      Masuala ya kufaa Tawasuli([2]) kwa Mitume na waja wema:

Rai na mtazamo wa Al-Habashiy katika masuala haya anakubaliana na Jamhuri ya wanachuoni, amesema sheikh Al-Islam Taqiyu Din Al-Sabakiy katika kitabu [Shifaa Al-Siqam uk. 119 chapa ya Haidar Abad Ad-Dakan]: fahamu kuwa inafaa kufanya tawasuli na kutaka uombezi kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume S.A.W. Yafaa hilo kwa mambo yenye kufahamika kwa kila mwenye Dini, inafahamika matendo ya Mitume mwenendo wa waja wema wanachuoni na wasomi miongoni mwa Waislamu, wala hakuna hata mmoja aliyepinga wala kusikika ndani ya zama zozote, mpaka alipokuwa Ibn Taymia na kuzungumza hilo kwa maneno hayajawahi kuzungumzwa ndani ya zama zengine.

Na akasema mwanachuoni Al-Kauthariy katika makala yake uk. 340 chapa ya Maktabati Al-Taufiqiya: “Na Tawasuli kwa Mitume na waja wema ime wakiwa hai au wamekufa imefanyika kwenya umma tabaka kwa tabaka”.

2-      Masuala ya kufaa kutafuta baraka kwa waja wema:

Mtazamo wake katika hili pia ni ule wa Jamhuri ya wanachuoni waliopita na kuwa na dalili ya hilo kwa mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo:-

Amesema Al-Qurtubiy katika tafsiri yake [10/47 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Masirya] baada ya kutajwa kwa Hadithi hiyo: “Mtume aliwaamrisha kunywa maji ya kisima cha ngamia ni dalili ya kutafuta baraka kwa athari za Mitume na waja wema, hata kama zama zao zitakuwa zimepita kwa muda mrefu na kupotea kwa athari zao, kama ilivyo katika tamko la kwanza ni dalili kwa watu wa chuki na uharibifu wa maeneo yao na athari zao.

Na vile vile Hadithi iliyopokelewa na Al-Twabaraniy toka kwa Ibn Omar R.A. Mtume S.A.W. alikuwa akiwatuma Masahaba kuleta vyombo safi na kuweka maji kisha kuyanywa wakitegemea baraka za kunawia Waislamu, nayo ni dalili ya kufaa kupata baraka kwa aliyebora kwa kilichobora, na ya kwanza ni kufaa kupata baraka kwa aliyebora.

3-   Masuala ya kutaka msaada kwa Mitume, Mawalii na Waja wema:

Si sehemu ya kujadiliwa au upotoshaji na ukafiri katika hili, kutaka msaada kwa maana ya msaada haiwezekani kuzuiliwa, kinyume na hivyo basi ingekuwa kutaka msaada kwa mambo ya dhuluma kwa mwenye kutaka kuondoa dhulma ni jambo la kuzuiliwa, bali pia ingekuwa kutaka msaada mgonjwa kwa daktari pia ni jambo lenye kuzuiliwa, ikiwa patasemwa: kutaka msaada wa kishirika umezuiliwa nayo ni kutaka msaada kwa watu waliokufa na wasiokuwepo, Haifa, kwa sababu inalazimisha kutaka msaada wakati mwengine wa ushirika na wakati mwengine si wa ushirika, masuala haya kwa ujumla wake yanaingia katika mzunguko wa sababu, kutoka na hayo jambo lililosahihi ambalo halipaswi jingine linapokosekana katika mlango huu ni kule kuamini mwenye kutakiwa msaada katika kile anachotakiwa msaada kuwa chenyewe kinaathiri, ikiwa hivyo ni hakuna tofauti kati ya kuwa mwenye kutakiwa msaada ima ni Mtume au si Mtume yupo hai au hayupo hai, na ni imani batili ambayo tunaiepusha kwa Waislamu kuongezea pia wasomi wao na masheikh, na hili ndilo lililopitishwa na masheikh wa Kiislamu na Maimamu wa Dini.

4-      Kutomkufurisha mwenye kuacha Sala:

Kauli hii ni pamoja na madhehebu ya Jamhuri ya wanachuoni, amesema Imam Al-Nawawiy kwenye [Al-Majmui 3/18, 19, chapa ya Al-Muniiriya] ni sehemu ya madhehebu ya wanachuoni kwa mwenye kuacha kuswali kwa uvivu pamoja na kuamini kwake wajibu wa Sala, madhehebu yetu yanayofahamika ni kuwa atauwawa kwa kupigwa lakini hakufurishwi, na pia amesema Imam Maalik na wengine miongoni mwa waja wema…. Hawajaacha Waislamu wanamrithi mwenye kuacha Sala na wanarithiwa pia na wao.

5-      Kufaa muamala wa riba katika nchi za vita:

Nayo ni madhehebu ya Imam Abu Hanifa: amesema Al-Sarkhasy katika kitabu cha: [Al-Mabsut 22/131 chapa ya Dar Al-Maarifa]: Riba hufanyika kati ya Mwislamu na adui katika nchi ya vita ni maneno ya Abi Hanifana Muhammad - Mungu Awarehemu- wakitanguliwa na Abi Yusuf - Mungu Amrehemu - na mikataba haramu yote ni katika maana ya riba”.

6-   Kuchukiza kutumia manukato mwanamke na kuwa nje ya nyumba yake ikiwa hajakusudia kuwaonesha wanaume:

Al-Habashiy amechukua dalili ya hili ndani ya kitabu cha: [Swarih Al-Bayan uk. 337: 351] na ufupisho wake ni Hadithi: “Mwanamke yeyote ametumia manukato na akapita mbele za watu kisha wakanusa harufu yake basi huyo mwanamke atakuwa amezini”.

7-      Kutolazimika mwanamke na kazi za nyumbani:

Na madhehebu haya ni wafuasi wa Imam Malik miongoni mwao ni Ibn Qassim na Ibn Al-Maajishuun, nayo ni madhehebu ya Imam Shafiy na Imam Hanbal, angalia [Fatawa Aliish 2/58, chapa ya Dar Al-Maarifa, Al-Muhadhabu cha Al-Shiraziy 2/482 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya, kitabu cha Al-Sharwany alaa Tuhfat al-Muhtaj 8/304, 305 chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Araby , kitabu Kashaf Al-Iqnai 5/195 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. Amesema Ibn Qudamah katika kitabu cha: [Al-Mughny 7/225 chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy]: “na wala haitakiwa kwa mwanamke kumhudumia mume wake, kuanzia chakula kupika na vinavyofanana na hivyo.

8-      Kutoharamishwa kuchanganyika kati ya jinsia mbili:

Maelezo haya yamo kwenye kitabu “Swarih Al-Bayan uk. 329 – 336” ni maneno mazuri hayakuchukua tu kitendo cha kukutana kwa mawanamme na mwanamke kuwa ni mchanganyiko ulio haramu lakini uharamu ni kule kukutana sehemu ya faragha, au kuwa wazi mwanamke na kuondoa sitara yake, yamepokelewa maneno yanayosisitiza hilo ndani ya Sunna na maneno ya wanachuoni.

9-               Kufaa kupeana mkono na mtu wa mbali ikiwa mkono umeveshwa nguo:

Nadharia hii au rai hii ndiyo iliyotajwa katika maneno ya watu wa Shafiy ambapo wameharamisha kupeana mkono kati ya mwanamke na mwanamme wa kigeni isipokuwa kwa masharti mawili: kuzuia fitina na kuwepo cha kuzuia kutogusana ngozi mbili ikiwa itahitajika kuwa hivyo, haya yamekuja pia kwenye kitabu cha [Minhaaj na sharhu ya Ar-Ramliy 6/191, 192 chapa ya Dar Al-Fikr]: inafaa kusugua paja la mwanamme kwa sharti la kuwepo kizuizi na kuzuia fitina.

10-Kauli ya Bidaa (uzushi) njema.

          Na maelezo yake yapo ndani ya kitabu cha “Swarih Al-Bayan uk. 173” na baada ya kurasa hizo, na kunukuliwa kutoka kitabu cha “Itqan Al-Sunna” cha sheikh Sayyid Abdillah Ibn Al-Swiddiq – Mungu Amrehemu–

Uchambuzi: Bidaa (uzushi) una hukumu tano za kisheria, wanachuoni wengi wameelezea, na kushuhudiwa na yale yaliyopokelewa na Malik kutoka kauli ya Amiir Al-muuminiin Omar Ibn Khatwab R.A. aliposema mbele za watu kuhusu ibada za tarawehi mwezi wa Ramadhani: “Ni neema ya Bidaa hii” akasema Ibn Abdulbarr kwenye kitabu cha: [Istidkaar 2/67 chapa ya Dar Al-kutub Al-Ilmiya]: neno Bidaa katika kamusi ya kiarabu: ni uzushi ambao haujawahi kuzushwa, katika yale yalikuwa katika Dini tofauti na Sunna ambayo iliyofanyiwa kazi, na kilichokuwa uzushi hakipingani na msingi wa sheria na Sunna hiyo ni neema ya uzushi kama alivyosema Umar kwa sababu asili ni kile kilichofanywa kwenye Sunna”.

Na amesema Imam Ibn Abdusalaam katika kitabu cha: [Kawaid Al-Ahkam uk. 204 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elamiya]: Bidaa: ni kitendo ambacho hakijafanyika zama za Mtume S.A.W. nayo inagawanyika kwenye: Bidaa ya wajibu, Bidaa haramu, Bidaa inayopendeza, Bidaa inayochukiza, na Bidaa halali, na njia ya kufahamu hizo: ni kupingana Bidaa na misingi ya sheria, ikiwa itaingia katika misingi chanya basi hiyo itakuwa ni Bidaa ya wajibu au lazima, ikiwa itaingia katika misingi ya haramu hiyo itakuwa ni Bidaa haramu, ikiwa itaingia katika misingi inayopendeza itakuwa ni Bidaa inayopendeza, ikiwa itaingia katika misingi ya kuchukiza hiyo itakuwa ni Bidaa inayochukiza, na ikiwa itaingia katika misingi ya halali itakuwa ni Bidaa halali.

Na katika masuala yaliyo maarufu yaliyoenezwa kwa Wahabeshi: ambayo yameegemezwa kwa sheikh wao ni kuwa hakuna Zaka ya vitu vya thamani zaidi ya thahabu na fedha.

Na katika kurejea vitabu vyao, tumekuta anasema ndani ya kitabu chake: [Bughyat Al-Twalib uk. 207]: “ama isiyokuwa dhahabu na fedha katika vitu vya thamani hakuna zaka ndani yake kwa kauli ya Imam Shafiy na Malik R.A. na ni wajibu kwa Imam Abi Hanifa, sarafu inayotumika ndani ya zama hizi haina Zaka kwa kauli ya Imam Shafiy na Imam Malik, na nilazima kwa kauli ya Imam Abi Hanifa, kwani yenyewe inachukua nafasi ya dhahabu na fedha, mwenye kuchukua kauli za Maimamu hawa wawili basi hakuna Zaka kwenye sarafu hizi, na mwenye kuchukua au kufuata madhehebu ya Abi Hanifa zaka yake huchuliwa kwa akiba”.

Na akasema pia kwenye uk. 216: “Hakuna Zaka kwenye vitu vya thamani zaidi ya dhahabu na fedha, kwa sababu Mtume S.A.W. hakutana Zaka zaidi ya vitu hivyo viwili, na wala haiangaliwi badala thamani mbadala ya vitu hivyo ya miamala kati ya watu kwa kauli ya Imam Shafiy”.

Na mfano wa hili lipo kwenye kitabu cha: [Swarih Al-Bayan, uk. 259: 260] na pia kauli yake “Ama mwenye kuitumia sarafu hii katika mauzo na manunuzi kwa lengo la kupata faida basi hiyo ni biashara, hufanyiwa thamani mwishoni mwa mwaka, ikiwa itafikia kiwango chake kwa moja ya sarafu mbili hutolewa Zaka ya biashara. Madhehebu ya Abu Hanifa ni kuwa fedha ikiwa ni katika vitu vya thamani kutumika katika bidhaa ya biashara basi ndani yake kuna Zaka”.

Na kauli hii japokuwa haitumiki na jopo la wanachuoni wa zama hizi, isipokuwa imekutwa kauli ya wale waliomtangulia Alhabashy, miongoni mwa kauli hizo ni ile iliyokuja katika kitabu cha: [Fatawa Sheikh Aliish mfuasi wa Imam Malik 1/164, 165]: nini kauli yetu kuhusu sarafu ambayo ina muhuli wa Sultani na kufanyiwa kazi kama dirham? Je ina zaka ya kitu cha thamani au zaka ya biashara au hakuna kabisa ndani yake Zaka?

Basi nikajibu kwa tamko: Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Sala na Salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, hakuna Zaka ndani yake, kwa kuingia kwake kwenye neema na aina maalumu ya nafaka matunda dhahabu na fedha, hii inakuweka karibu kuwa pesa za shaba zilizopigwa muhuli wa Mfalme na kutumika hizo hazina Zaka, na mwenye pesa zake zikatimiza mwaka na thamani yake ikiwa ni kiasi cha dirhamu mia mbili basi hakuna Zaka ndani yake.

Katika Tarraaz baada ya kutaja Abi Hanifa na Imam Shafiy ulazima wa zaka na kukubaliana kutokuwepo zaka kwenye thamani yake, na kwa upande wa Imam Shafiy kuna kauli mbili kwenye kuitoa amesema: kuwa yenyewe haina zaka ambapo hakuna tofauti kuwa hazingatiwi uzito wake wala idadi yake lakini kinachozingatiwa ni thamani yake, lau itawajibishwa kwenye matirio yake basi ingezingatiwa sharti la kutimiza mwaka na wala si thamani yake, kama ilivyo kwenye dhahabu nafaka na matunda, na kama itaondoshwa kufungamanishwa kwake basi itachukuliwa kwenye hukumu ya shaba chuma na vinavyofanana na hivyo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anajua zaidi”.

          Wakasema baadhi ya wafuasi wake kwenye kitabu cha: [Haashiyatu Al-Tirmidhiy kuwa ametaja – 4/29” kuwa sheikh Al-Islam Shamsuddiin Al-Anbaabiy amesema kwenye jibu la swali lilifikishwa kwake: “Sarafu iliyotajwa inafaa kuuzia na kununulia: kwa sababu yenyewe ni yenye thamani, na chenye kumilikiwa katika hizo huchukuliwa ni katika mali ya biashara inalazimika kutolewa zaka katika thamani kwa masharti yenye kufahamika, lakini hakuna zaka kwenye sarafu yenyewe kwa sababu yenyewe si katika vitu vya Zaka. Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi.

Kusudio katika maelezo haya sio kutetea kauli hii, isipokuwa ni kuweka wazi hata kama itapingana na wasomi wa zama za sasa, ila Al-Habashy hakuzusha yeye mwenyewe au kupokelewa kuwa ni maelezo yenye kubomoa Dini, au kupuuzia nguzo ya zaka au kufanya ghushi na udanganyifu kama wanavyomtuhumu baadhi ya watu. Angali: [Mausuat Ahl Sunna 2/921 chapa ya Maktabati Ashqriy].

Tuhuma nyingi zimeelekezwa kwa Habashiy na wafuasi wake pasi na kutaja wenye kutuhumu dalili ya kuzingatiwa au kuegemezwa tuhuma hizo kwa chanzo cha mmoja mwenye kufahamika au kuzingatiwa, isipokuwa zenyewe ni kwa upande wa: wameniambia baadhi ya watu, na wakasema baadhi ya watu wenye kuaminika, kwa upande wa ulazima yasiyo lazimika miongoni mwa yale yasiyowezekana kwa Mwislamu mcha Mungu akajiingiza ndani yake na kubeba dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu, imepokelewa na Abu Dawud toka kwa Ibn Omar R.A. kuwa Mtume S.A.W. Amesema: “Mwenye kuvutana kwenye jambo la batili hali ya kuwa anajua, hatoacha kuwa kwenye hasira za Mwenyezi Mungu mpaka ajivue na kwenye mvutano huo, na mwenye kumsingizia Muumini kwa lile asilokuwa nalo Mwenyezi Mungu atamweka kuwa ni mtu wa motoni mpaka pale atakapoondoa kile alichomsingizia” na katika tuhuma hizi:-

1-     Ni kutuhumiwa Sheikh Al-Habashiy kuwa yeye ni Myahudi wa falasha – nao ni Wayahudi wenye asili ya Ethiopia – na kuja kwake nchini Lebanon kulikuwa ni kufungamana kwake na Wayahudi, japokuwa imekuja kwenye fasiri zake kuwa ni mtu aliyesafiri toka Madina kuelekea Jarusalem kisha kuelekea Damascus. 

2-     Histori ya Hirariy ndani ya nchi yake imesimama katika kukufurisha na alishirikiana na mtawala wa Hirary dhidi ya taasisi za kuhifadhi Qur`ani mwaka wa 1940 pasi na ukweli, kisha wanataja kuwa alipigana vita na taasisi hizi, kwa sababu zenyewe zilikuwa zinasambaza na kufundisha nadharia za Wahabi! Angali: [Firqat Al-Ahbasha cha Shaharani 2/1239].

3-     Wahabeshi wanatengeneza hukumu pasi na vile alivyoteremsha Mwenyezi Mungu na wao ni watetezi wakubwa wa watawala wa kanuni zilizowekwa na wanadamu badala ya kuwa watetezi wa sheria ya Mungu. Angalia: [Fatawa Lajinatu Daima huko Saudi Arabi, na hii ni tuhama mbaya kwao kwa sababu wao wanasema: hakika kuhukumu tofauti na alivyoteremsha Mwenyezi Mungu ni kufuru hakuna zaidi ya ukufuru”.

4-     Wahabeshi wanatoka kwenye nchi ya ukafiri wakiwa pamoja na wanawake makafiri.

5-     Wahabeshi wanasema: hakika ardhi ni yenye kutandikwa, wala hatujapa maelezo hayo toka kwa yeyote miongoni mwao bali ugonvi huu unawakuta kwa sababu ya kauli yao kuhusiana na upande wa Qibla nchini Marekani kuwa chenyewe ni upande wa kusini mashariki na wala sio kasikazini mashariki, haya haikuwa hoja yao, lakini hoja yao katika hili ni vitu vyingine miongoni mwa hivyo: ni kuwa makaburi ya Waislamu wa zamani ni kama mfano wa makaburi ya “sakara mento” huko Califonia ya zamani ambayo historia ya kuzikwa kwa Waislamu hao inarejea kabla ya mwaka 1937, na makaburi ya “Toro” katika jimbo la Novascotia huko Canada ambapo inarejea historia ya kuzikwa kwao ni kabla ya miaka hamsini, imeonekana Waislamu walikuwa wanaelekea wakati wa kusali upande wa kusini mashariki, na wanashikamana na fatwa zilizotolewa toka kwa Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharif wa zamani Sheikh Jaad Al-Haq Ally Jaad Al-Haq – Mungu Amrehemu – mtazamo wao unaunga mkono rai ya sheikh Jaad kuhusu kuelekea Qibla.

6-     Wahabeshi wanafanya mambo ya uchawi, aliyewatuhumu katika hili ni Abdurahman Damashqiya katika kitabu chake: [Ahbaash Shudhuudhuhu wa Akhtwaahuu uk. 51: 52] lakini hajaleta dalili juu ya kauli yake isipokuwa na simulizi ya mwanamke asiyefahamika ambaye alichukua nafaka ili zimsaidie katika kuondoa wasi wasi wa uchawi, na yeye Abdurahman Damashqiya anazo baadhi ya nyaraka zinazo tolewa na kusambazwa na Wahabeshi nazo ni nyaraka za uchawi, simulizi hizi wapokezi wake hawafahamiki na huwenda nafaka hizi ni nafaka zinazotumika na madaktari wa maradhi ya saikolojia kwa wenye matatizo ya wasi wasi, na huwenda karatasi za uchawi ambazo zinatajwa ni hirizi zilizoandikwa Qur`ani, naye hakuwa picha hata moja ndani ya kitabu chake pamoja na shime kubwa aliyokuwa nayo ya kufuatilia dogo na kubwa, jambo la kushangaza ni kuwa yeye anathibitisha kwao tuhuma hizi kwa maneno yanayopinga haya toka kwa mmoja wa sheikh wao naye ni Usama Sayyid, ambaye amesema: “lau tungekuwa tuna uchawi basi ingekuwa mwenye kutupinga sisi ni wa kwanza kuathirika na uchawi wetu”.

Ama yanayochukuliwa ambayo yawezekana kuyakusanya na kuyaelekeza kwenye kundi hili nayo ni kama yafuatayo:

Uharaka (wepesi) wao katika kuwakufurisha na kuwaona wapotoshaji na ufasiki pamoja na kushambulia kwao wale wanaopingana nao katika masuala mbalimbali:

Miongoni mwa masuala hayo ni:

1-      Yanayonasibishwa kwao ikiwa ni pamoja na kumkufurisha kwao Izz Al-Din Baliq na kusema anapaswa kutenganishwa na mke wake ([3])hilo na kwa sababu ya kupinga kwake utume wa Nabii Adam.

Utume wa Adam umethibiti kwa kutajwa ndani ya Qur`ani Sunna na kauli ya wanachuoni, amesema mwanachuoni Al-Tiftazany katika sharhe [Al-Aqaid Al-Nasfiya uk. 87]: “ama Utume wa Adam A.S. Qur`ani imeonesha kuwa aliamrishwa na kukatazwa pamoja na kuonesha wakati wa zama zake hapakuwa na Nabii mwingine, na pia katika Sunna ([4])na makubaliano ya wananchuoni, hivyo kupinga utume wake unakuwa ni ukafiri”.

Amesema Ibn Hazmu katika kitabu cha: [Maraatibu Ijmaai uk. 173 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: wamekubaliana kuwa kila Nabii aliyetajwa ndani ya Qur`ani huyo ni Nabii wa kweli, kama vile Adamu, Idriisa, Nuhu, Huud, Swaleh, Shuaibu, Yuunus, Ibrahim, Ismail, Is-haq, Yakuub, Yussuf, Harun, Dawud, Suleiman, Ilyaas, Al-Yasaa, Lut, Zakaria, Yahya, Isa, Ayub na Dhil Kifli”.

Lakini kukufurishwa tu mtu fulani, ni katika haraka juu ya jambo kubwa ambalo sheria ya Kiislamu imelitahadharisha jambo hilo, kama vile kauli ya Mtume S.A.W. pale aliposema: “Mtu anaposema kumwambia ndugu yake ewe kafiri basi umethibiti huo ukafiri kwa mmoja wao” ukafiri katika kichochoro hiki si wenye kuachwa kwa watu wa upande mmoja.

2-      Msisitizo wao wa kukufurishwa wenye kusema “upande” hata wasipoamini kuwa Mwenyezi Mungu yupo sehemu fulani ni mwenye kupatikana sehemu kama ilivyo katika kauli ya Al-Munji uk. 19 na wenginezo.

Ama lile lililopo kwa watu wa haki watu wa Sunna na Jamaa ni kuwa Mwenyezi Mungu Ameepukana na mfanano wa viumbe katika sifa zote za viumbe, na kutokana na hayo ni pamoja na kuepukana kwake na mipaka pande na maeneo, kwa sababu hizo ni sifa za viumbe, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwa mwenye kufanana na hao kwa lolote, kwa sababu Yeye Mwenyezi Mungu lau angekuwa upande fulani angekuwa ni mwenye kupahitajia hapo, na kuhitaji kwa mwengine kunapowezekana inalazimu kuwa ni lazima, na yasiyokuwa hayo katika yale ambayo hausiki nayo Mola Mtukufu. Angalia kitabu cha: [Sharhu Al-Maqaasid cha Saad Al-Tiftazaniy 4/45, 46 chapa ya Aalam Al-Kutub].

Kauli inayohusisha upande kwa Mwenyezi Mungu ni kauli ya uzushi bila shaka yoyote, na inalazimisha kauli hiyo ukafiri, lakini ukafiri kwa kila mwenye kusema upande hata kama atakuwa anakanusha kuwa Mwenyezi Mungu hana hizo pande basi anakuwa ni mwenye kuangaliwa, kwa sababu ulazima wa madhehebu si madhehebu, na kufuata hawa wasemao “upande” kwa maandiko ya wazi na baadhi ya ibara zilizo pokelewa toka baadhi ya waja waliotangulia, pamoja na kuegemea kwa ujumla kwenye mwili yote haya ni yenye kuzuiliwa kukufurishwa mtu madamu msemaji amekanusha kuwepo eneo fulani, kwa sababu hukosea na kusema: Yeye yupo mbinguni lakini bila kuegemesha upande gani. Ameashiria katika hili Sultani wa wanachuoni Al-izz Ibn Abdulsalaam katika kitabu cha: [Qawaid Al-Kubra 1/201, 202” na akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu Amelazimisha kumfahamu kwa uenzi wake umilele wake upweke wake na Yeye ni yupo hai Mwenye kujua Mwenye uwezo Mwenye kuhitaji Mwenye kuona Mwenye kuzungumza Mkweli katika habari zake, na kuamrisha watu wote kuamini hivyo kwa sababu ya ugumu kwao kupata dalili za kumfahamu kwake, akapelekea ulazima wa kuamini hivyo. Ama kuwa kwake Mwenye ujuzi na mwenye uwezo, wametofautiana watu, pia kauli ya maneno yake ya enzi, na kile alichojisifu Yeye Mwenyewe kuwa na uso mkono miwili macho mawili ni sifa za kimaana zinazojitegemea, au ni kielelezo kinachorudisha sifa, anaelezea uso kwa maana ya Yeye Mwenyewe, na kuelezea kuwa na mikono miwili ni ishara ya uwezo, macho mawili kwa maana ya elimu, lakini pia watu wametofautiana hivi kuna pande au hana upande wowote? Jambo lenye kupelekea mvutano ndani yake na ugumu wa kupata dalili zake, imeongelewa sana na watu wa Al-Ashaariy – Mungu Awarehemu – katika sifa ya ukale na kubakia milele je ni katika sifa hasi au sifa zake? Kumekuwa na makala nyingi za watu Al-ashaariy mpaka amezikusanya Ibn Fork ndani ya juzuu mbili, na yote hayo ni katika yasiyowezekana kuona hawa ndio waliosahihi kwa upande wa watu wenye kufanya jitihad, isipokuwa ukweli upo kwa mmoja wao na waliobaki ni wenye kukosea kwa kosa lenye kusameheka, kwa sababu ya uzito wa kutokosea na kuachana na makosa, hasa kauli ya mwenye kuamini suala “upande” kwani imani ya kuwepo si mwenye kuhangaika wala kutulia wala kujitenga na ulimwengu wala kuungana nao, wala hayumo ndani ya ulimwengu wala nje ya ulimwengu, kwa kawaida si yenye kufuatwa na mwenye asili ya kuumbwa, na wala pia hafuatwi yeyote isipokuwa anapokuwa ameleta dalili ngumu kueleweka na ngumu kufahamika, kutokana na ugumu huu ndipo Mwenyezi Mungu Ametoa msamaha kwa waja, kwa sababu hiyo basi Mtume S.A.W. alikuwa hamlazimishi yeyote kwa aliyekuwa Mwislamu kulitafuta hilo, asipokuwa alikuwa ni mwenye kuwakubalisha kwa kila anachokifahamu kuwa hawawezi kuepukana na makosa, bado Mkhalifa waongofu na wanachuoni wenye kujitahidi wanakiri hilo pamoja na kujua wengi hawakusimama kwenye ukweli lakini hata hivyo sheria za Kiislamu zinawatambua ikiwa ni pamoja na kufaa kurithiana na kuwaombea dua pale wanapokufa kuoshwa na kukafiniwa pamoja na kubebwa jeneza lao na kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu, lau Mwenyezi Mungu Asingetoa msamaha wake na kusamehe kutokana na ugumu wa kujitenga na makosa basi zisingepitishwa kwao hakumu za Kiislamu kwa Waislamu wote, na mwenye kuzania kuwa Mungu anachukua nafasi ya sehemu katika miili ya watu au viumbe wengine basi huyu atakuwa amekufuru.

Na imekuja katika kitabu cha: [Fatawa Ashihaabu 4/20 chapa ya Maktaba Islamiaya]: kuwa aliulizwa juu ya mwenye kusema: hakika Mwenyezi Mungu yupo upande fulani je huyo anakuwa ni Mwislamu? Akajibu msemaji aliyetajwa ni Mwislamu hata kama atakuwa anazusha.

Akatoa maelezo mwanachuoni Al-Bujairamiy katika kitabu cha: [Sharhe Al-Minhaj 1/311 chapa ya Dar Al-Fikri Al-Arabiy] juu ya maelezo ya mwanachuoni Aziyaad: “Kinachozingatiwa katika suala la mwili ni kutokufuru” kwa maana ya kutohusisha mwili moja kwa moja, kinyume na hivyo kwa kusema: hakika Mwenyezi Mungu Ana mwili kama miili mingine basi anakufuru kama ilivyopitishwa na sheikh wetu, na mwenye kusema: Hakika Mwenyezi Mungu yupo upande fulani hakufuru hata kama itahusisha mwili kwa sababu ulazima wa madhehebu sio madhehebu”.

Na amesema sheikh Al-Hamawiy mfuasi wa dhehebu la Imam Abu Hanifa katika kitabu cha: [Ghamz Al-Uyun, 2/200 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya] kuhusu upande ni uzushi na wala hakuna ukafiri.

Na kama tulivyosema hapo nyuma: kuna tofauti kati ya kusema ukafiri neno lenyewe na ukafiri kwa mwenye kulisema, kwa uwezekano wa kutokea chochote chenye kutokea katika vile vya kupelekea ukafiri kwa kujisahau.

3-      Tahadhari vitabu vya Dkt. Muhammad Said Ramadhan Al-Buty uk. 69: 70 kuhusu ukafiri na kupinga, kwa sababu amesema: pindi inapotokea kupingana andiko la Qur`ani na kauli ya kisayansi, basi mimi ninasema: haitolewi maelezo na ufafanuzi Qur`ani isipokuwa tunaacha Qur`ani na kuchukua maelezo ya kisayansi”.

Na maneno ya sheikh Al-Buty yana mwelekeo sahihi, nayo ni kuwa pindi inapotokea mgongano wa wazi wa andiko la Qur`ani na andiko la kisayansi mfano wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua} [YASIN, 38].

Uwazi wa aya ni kuwa jua ndilo ambalo linazunguka, basi ikiwa hili linatofautiana na ukweli wa kisayansi uliothibitishwa kuwa ardhi ndiyo inayozunguka, basi sisi hapo tunaijengea hoja aya na tunasema: jua linazunguka kwa maana: katika mtazamo wa mwenye kutazama hana uhakika, kwa sababu macho ufafanuzi wake kina unalizimisha kuwa aya haipo kwenye uwazi wake na hii ni mgongano katika migongano ya ufafanuzi, lakini ufafanuzi jumla ikiwa ni pamoja na maelezo ya Al-Buutwiy.

4-   Tahadhari ya kitabu cha: [Fiqhi Sunna cha sheikh Sayyid Sabiq] kilichotaja adhabu ya kifo kwa mtu aliyeritadi 2/453 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Arabiy]: Mwislamu hazingatiwi yupo nje ya Uislamu na wala haukumiwi kuwa ni mwenye kuritadi isipokuwa kinapokuwa kifua chake kimekunjuliwa kwenye ukafiri na moyo wake ukaridhika na huo ukafiri na akaingia kweli kwenye ukafiri([5]).

Na vile vile kukusudia kwake kubomoa kauli za jopo la wanachuoni na kwenda kinyume na wanachuoni katika masuala mbalimbali pasi na kuweka wazi na kubainisha hoja. Angalia: [Al-Tahdhir As-Shariy Al-Waajibu uk. 36: 37].

Na lilikuwa lenye kufaa ni kutanabahisha juu ya kosa – ikiwa lipo – na kumtaka msamaha muhusika na wala sio kumkimbia na kutahadharisha kila kitabu chake kwa sababu ya makosa yaliyomo ndani yake, wala hakuna kitabu kinachokosa makosa ukiondoa kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Na jambo la kushangaza zaidi na chungu kuwa mmoja wao – naye anaitwa Usama Al-Sayyid – ameweka wazi ukafiri wake na – Mungu Atukinge – yeye sheikh pamoja na sheikh Al-Qardhawiy, akasema ndani ya kitabu chake [Al-Qardhawiy fil araa” uk. 352] akimwambia sheikh Qardhawy:

Ukafiri umefungua milango yake iliyofungwa - Na kufungua uwezekano wa madirisha yote.

Na kuweka sharti la kufunguliwa kifua ni ujinga wa wazi - Na kumfuata Imam wako Al-Shaukaniy.

Umekutana na bwana aliyetangulia katika ukafiri wake - Na kuzama kwenye bahari ya uovu na upotovu.

5-   Mashambulizi yao dhidi ya daktari Yussuf Al-Qardhawiy na kutoa tahadhari dhidi yake na vitabu vyake na kumuelezea kuwa si katika wasomi kama ilivyoandikwa katika kitabu cha: [At-Tahdhiir As-Shariy Al- Wajibu uk. 66] isipokuwa imefikia kuonekana kafiri [chanzo killichopita uk. 68], na hilo ni kutokana na kilichopokelewa kupitia mazungumzo aliyoyafanya kwenye runingi. hakika Mtume S.A.W. alikuwa akifanya juhudi wakati mwingine katika mambo ya kisheria na akikosea katika jitihada zake.

Habashiy alisema akizungumzia: “kunasibisha makosa kwa Mtume S.A.W. katika masuala ya sheria ni ukafiri wa wazi”.

Na wala hilo si la kupelekea ukafiri moja kwa moja, huenda makusudio ya sheikh Qardhawiy katika mambo ya sheria: ni mambo ambayo hayajafikiwa na wahyi “ufunuo” ndani yake, na kuhitaji hukumu za sheria takatifu, hayo ndio yanayo nasibishwa kwa upande huo.

Watu wa misingi ya Dini kuna madhehebu kuhusu kufaa jitihada zake Mtume S.A.W. katika mambo haya, na ambayo yamekuwa na kundi kubwa la Jamhuri ya Al-Shaaira na wazungumzaji ni kufaa, miongoni mwao wapo waliosema uwezekano wa kukosea, wakinukuu hayo toka kwa Abi Yussuf na Ahmad.

Kisha wakatofautiana wanaosema kuwa yafaa jitihada kwa Mtume S.A.W. lakini je inafaa kwake kukosea katika jitihada hizo au hapana?

Wafuasi wengi wa Al-ashaaira na Muutazila wamekubaliana kuwa kukosea Mtume ni jambo lipo, na wakachukuwa dalili kuwa ikiwa haifai kukosea Mtume katika mambo ya jitihada basi asingeingia kwenya makosa, lakini ameshawahi kufanya makosa, basi imekuwa ni jambo lenye kuwezekana kukosea, na dalili ya kuingia kwenye makosa Mtume S.A.W ni kuchukuwa fidia kutoka kwa mateka wa vita vya badri, kisha Mwenyezi Mungu akamzindu katika hilo kwa kauli yake: {Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda baraabara katika nchi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima}[AL ANFAAL 67]. {Lau isingeli kuwa hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingeli kupateni adhabu kubwa kwa vile mlivyo chukua}[AL ANFAAL 68].

Na akatunga mtunzi wao – naye ni Usama Sayyid – kitabu alichokiita: [Qardhawiy fiil Araai] akifuatiliwa kile anacho kiona ni sehemu ya makosa ya Qardhawiy, miongoni mwa hayo kuna makosa yanaweza kuwa ni makubwa, na mengine yanaondoka yenyewe kwa kadiri anavyoendelea kuelezea sheikh Qardhawiy na kuongeza zaidi kupinga ya sheikh Qardhawiy na hata katika Dini yake, makosa yanayojitokeza yanaweza kuzinduliwa na kujadiliwa kwa upole kabisa na kwa hekima pasi ya kupoteza juhudi kubwa za wanachuonni au kuwashusha nafasi zao au kuwapinga wao na nia zao.

6-      Alichokifanya Habashiy katika tafsri ya sheikh Shaarawiy na fut’wa zake, ambapo ametahadharisha, na kusema: ndani yake kuna makosa makubwa mengi [Al-Tahdhir Al-Shariy Al-Wajib uk. 39: 41] na kutoa mfano wa baadhi ya ibara na makosa yaliyotokana na uchache wa uchambuzi wa kina kwa sababu sheikh Shaarawiy – Mungu Amrehemu - hakuwa mwenye kutunga hivi vitabu lakini vilikuwa vikitengenezwa kupitia mihadhara yake ya sauti, na yafahamika tofauti kwa yale anayosema mtu miongoni mwa yanayowezekana kuingizwa kwenye usamehevu na kufaa na kati ya yale anayoyaandika kuyahariri kuyapitia kwa kina na kuyarejea vizuri, hasa baadhi yanayochukuliwa ambayo ameyataja Hirariy hayapo wazi katika uchukuaji, isipokuwa yenyewe ni yale yanayokubali ufafanuzi, na kusisitiza kuomba radhi pia: kuleta yanayochukuliwa toka kwa msomi mkubwa mwenye kufahamika kwa elimu yake na uchamungu wake, anasema Dkt. Mahmuod At-Twanaahiy – Mungu Amrehemu – katika makala yake [2/565 chapa ya Dar Al-bashair Islaamiya]: “kuwa ni sheikh mkubwa amekuja wakati wa wanachuoni wenye kuhifadhi wenye vigezo, na yeye amekuwa ni sura kwa ulimwengu wa Al-Azhar, mwanzilishi wa masomo ya lugha ya kiarabu na sheria zake, akiwa na uwezo mkubwa wa lugha kwa ngazi zake nne: sauti, sarufi, kanuni na dalili, na kuonesha mashairi ya ajabu ya Kiarabu katika zama zake mbalimbali, pamoja na maelezo mengi ya Qur`ani Takatifu na masomo yake pamoja na vipaji vingine wanafahamu zaidi wafuasi wa sheikh.

Na akasema pia [2/568]: “ama sheikh Al-Shaarawy hakuacha kitu kilichoandikwa, ama hivi vitabu vinavyosambazwa masokoni ambavyo vinabeba jina la sheikh Shaarawy, havipaswi kuwa sehemu ya kuaminika na kukubalika, nayo ni kazi ya kukusanya kupitia rekodi zake za radio na runinga, nayo ni kazi inayofanywa na baadhi ya wasambazaji, ni lazima kwa Al-Azhar na familia ya sheikh kudhibiti uchapishaji huu, na kuzuia kusambaa kwake masokoni. Sheikh Mwenyewe – Mungu Amrehemu - alikataza kazi hii, na akasema mara ya mwisho ya kusaini kwake, kama maelezo yalivyokuja kupitia gazeti la [Al-Ahram 19/6]: “Maamuzi yake ya mwisho kusaini alitoa wito kwa wasambazaji kuwa pale wanapoandika vitabu kupitia maelezo ya sheikh wawe na ufahamu mzuri wa andiko na kuelewa vizuri sana, ili pasiwe na ukwepeshaji wa andiko na kufahamika vibaya na kueleweka na sisi vibaya, kwa hili nachukuwa uwamuzi wa kutosambazwa kitabu chochote kinacho nasibishwa na mimi pasi na kukipitia mimi mwenyewe au yule anaye niwakilisha mimi”.

7-      Kutuhumiwa sheikh Al-Khaznawiy Al-Naqshabandiy kuwa ameritadi, kwa sababu alisema katika yale yaliyonukuliwa toka kwake kuwa: Twarika ni jambo la lazima. Amesema Al-habashy: “Mwenye kulazimisha jambo ambalo si la lazima katika yale yanayofahamika katika Dini kuwa si ya wajibu basi atakuwa ameritadi”. “Ukurasa wa 156, 157 katika kitabu [At-Tahdhiir As-Shariy Al-Wajib”.

Na maneno ya Al-khaznawiy yana mtazamo sahihi unaochukuliwa, nayo ni usafishaji ambao unaendana na tasaufi, usafishaji wa nafsi kutokana na maradhi ya ndani na kuisafisha na uchafu, yote hayo ni yenye kuhitajika kisharia. Kutokana na hayo Abdillah Ibn As-Swiddiq Al-Ghumariy alitunga kitabu na kukuita: [Hassan At-Talat-twuf fii wujuubi suluuki At-Taswaufu] na kuelezea maana hii kwa uelewa zaidi ya huu.

Pia aliwafahamu kwa uharaka wao wa kutoa hukumu, katika hayo ni pamoja na:-

1-      Hukumu ya kufaa kumpa mkono mwanamke wa mbali katika kuzaliwa ni katika mambo ya upotoshaji, kama ilivyokuja kwenye kitabu “Bughyat Al-Twalib cha sheikh Al-Habashiy uk. 425.

Na siyo hivyo tu, ambapo masuala haya ni katika masuala yenye mvutano kati ya maimamu, nayo ni maswala ya maelezo ya kina kwao, Imam Abu Hanifa ameelezea uharamu wa mwanamme kumpa mkono mwanamke akiwa kijana hata kama hapatakuwa na fitina, ikiwa hakuna uzito na umuhimu wa kufanyika hilo, lakini wamjuzisha kumpa mkono mwanamke mzee ambaye hana matamanio, na Imam Hanbal ameliunga mkono hilo. [Tibyiin Al-Haqaiq sherehe ya Kanzu Ad-Daqaaiq 6/18, chapa ya Dar al-kitaabu al- Islaamiy, kas-Shaaf Al-Iqnaa an Matni Al-Iqnaai 2/154, 155 chapa ya Dar al-kutubu al-ilmiya]

Na ameharamisha Imam Malik moja kwa moja ni sawa sawa ikiwa itahofiwa matamanio au siyo matamanio, ni sawa sawa ukawa upeaji mkono ni kwa kijana au mtu mzima. [Haashiyatu As-Swaawiy sharhe ya As-Swaghiir cha sheikh Ad-Dardiir 4/760, chapa ya Dar Al-Maarif].

Ama maelezo ya Imam Shafiy yanaeleza kutojuzu au kufaa mwanamme kumpa mkono mwanamke wa mbali katika kuzaliwa naye isipokuwa kwa masharti mawili: usalama wa fitina, na kuwepo kizuizi ikiwa itahitajika haja hiyo. Angalia: kitabu [Nihaayatul muhtaaj sherehe ya Al-Manhaaj 6/191, 192 chapa ya Dar al-fikri, haashiyatuna As-Sharwaaniy wal ibaady alaa tuhfatil muhtaaj kitabu cha Ramly 7198, chapa ya Dar Ihyaaul turaath Al-Araby].

Na imepokelewa toka kwa Imam Ahmad juu ya kuchukiza moja kwa moja kumpa mkono mwanamke, amesema Al-Bahuutiy Al-Mambaliy katika kitabu cha [Kas-Shaafu Al- Qinaai 2/154, 155]: “Na kuelezea – yaani: Imam Ahmad – katika mapokezi ya Ibn Mansour: inachukiza kumpa mkono mwanamke”.

Na yafahamika kuwa madhehemu hayapingani na madhehebu, kuongezea pia kuto elezea anayepishana na madhehebu kuwa ni mwenye kupotea katika maswala yanayodhaniwa kuwa na tofauti, lengo lake ni kuwa rai inayohitajika, nayo ni yenye kuzunguka kati ya usahihi na makosa katika mzunguko wa jitihada, na wala sio kati ya haki na upotovu.

2-      Hukumu ya ubaya upotovu na ukafiri katika baadhi ya ibara ambazo zinachukuliwa kuwa na uzuri au maelekezo sahihi, miongoni mwa hizo: - kauli ya mwenye kusema: hakuna kadari ya Mungu wala usamehevu wa Mungu [chanzo kilichopita ukurasa wa 155] ni kuwa inadhaniwa kuwa utashi wa Mwenyezi Mungu ni wenye kuzuka. Ni kuwa makusudio ya msemaji wa haya ni duwa, na duwa hushinda kadari, imepokelewa na Ibn Maja na Ahmad toka kwa Thaubaan – radhi za Mungu ziwe kwake – kuwa Mtume S.A.W Amesema: “Haishindwi kadari isipokuwa ni kwa duwa”. Amesema mwanachuoni Al-Khaadimiy katika kitabu [Al-Bariiqa 1/188 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiya]: “fahamu kuwa duwa hurahisisha hukumu iliyopitishwa, na kuondoa hukumu iliyotundikwa ikiwa imeteremka au kuandaliwa kuteremka. Ikiwa patasemwa: kubadilika hukumu yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kitu kilichozuilika, kufanya juhudi ya kuiondoa kwa duwa pasi ya kuitambua na kuikiri hakumu yake Mola Mtukufu, Mtume S.A.W amesema: “Haijitoshelezi tahadhari kwa kadari”. Nikasema: hakika duwa pia ni katika hakumu yake Mola Mtukufu, inakuwa msababishaji pamoja na sababu yake ni katika hukumu ya Mola Mtukufu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshahukumu duwa kuwa ni sababu ya kuondoa”.

Kauli ya mwenye kusema: manii ndani yake kuna roho [chanzo ni kilichopita uk: 158], nayo ni inakusudiwa ndani ya kipindi cha baadaye.

Kauli ya mwenye kusema: kila kitu ni kwa amri yake [chanzo ni kilichopita ukurasa 158] ambapo huchukuliwa amri ya kiulimwengu na wala si amri ya kisharia.

-            Kauli ya Al-Ghazaliy: “Haiwezekani kuanzisha kile kilichokuwa” kitabu cha [At-Tahdhiir As-Shariy Al-Wajib ukurasa wa 173] wanachuoni wengi wametunga katika kusherehesha na kutoa mafundisho ya ibara hiyo, miongoni mwa wanachuoni hao ni pamoja na Al-Hafidh Jalal Ed-Dini Al-Suyutiy katika kuelezea ibara hiyo na As-Samhuudiy katika kitabu cha: [Iydhahu Al-Bayan] na katika ufasiri wa sheikh Abdulqaadir Ibn Mustafa Al-Sufuuriy mfuasi wa Imam Shafiy, amesema kwenye kitabu cha: [Al-Muhiy 2/467, chapa ya Dar Swadir]: mhakiki mkubwa ndani ya zama zake wamekubaliana watu wa zama zetu juu ya ukubwa wake alikuwa ni mwanasharia mfasiri amekuwa na fani nyingi na alikuwa ni mwenye kujitenga na watu”. Siku moja aliulizwa na baadhi ya wanafunzi kuhusu ibara ya Ghazaliy, na akasema katika maelekezo yake: “neno kutowezekana lina sehemu mbili: ya kwanza: ni kuwezekana moja kwa moja, ya pili: isiyowezekana kwa mwengine, kuwezekana huwenda ikawa kutowezekana kwa mwengine au kuwa ni lazima kwa mwengine. Mafano wake ni kama: kufufuliwa maiti toka kaburini mwao, ni jambo lenye kuwezekana, kwa sababu pindi akili inaposhsindwa na nafsi yake uhukumiwa kufaa kwake, lakini pindi Mola Mtukufu alipotoa habari yake limekuwa ni lazima kutokea kwa kuangalia habari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu haiwezi kutanguliwa na kushindikana, na kuwa ni jambo lisilowezekana kwa mwingine kwa mazingatio haya.

-            Linapothibiti hili kwako utakuwa umefahamu yale aliyoyasema hoja ya Uislamu kuwa ni kweli, na kuyaweka wazi zaidi ni baada ya kufahamu kuwa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni ya muda mrefu na Yeye ameshaelezea tokea muda mrefu kuwa chenye kuwezekana ambacho kimekutwa kipo ndani ya zama zote na sehemu yoyote na kwa sifa yoyote ile, wakati huo basi kutokea kwake kinyume na kilivyoelezewa na elimu ya Mungu haiwezekani kwa mwingine, kwa sababu lau itatokea kinyume na hivyo lazima igeuke elimu kuwa ni ujinga na hilo haliwezekani katika haki ya Mwenye Hekima Mwenye Habari Mwenye Elimu Mwenye Enzi Utashi na Uwezo, lakini linakuwa hilo sawa na elimu yake, na wakati huo jifunze kuwa kukosekana uwezekano wa kuanzisha kile kilichokwisha kuwa hakuna ndani yake kiwango cha ujinga wala kiwango cha kushindwa kwa mmiliki wa Dini zote, ni vipi anadhania hivyo hoja ya Uislamu Imam Ghazaliy ambaye elimu yake imejaa Ulimwenguni, isipokuwa kutowezekana kwa hakika ni kutokuwepo utashi na uwezo wa hilo, na kupelekea katika kushindwa kuwezekana, kuzingatia hilo kunakusumia kwenye taswira pindi wasipofahamu sehemu ya maneno na wasipoonja undani wa elimu, bali ni mitazamo yao kuwapinga wanachuoni wakubwa na kuwapinga warithi wa Mitume, wamekuwa kana kwamba wao wapo kinyume nao, Mwenyezi Mungu akaondoa uwezo wa akili kufikia maana ya undani na kushikamana na yaliyo nje ya mjengeo, na mwenye kusema kuwa herufi ya “ma” ni ya kuunganisha na wala si ya kuonesha sehemu, kwa sababu kilichonukuliwa toka kwa Imam ni kuwa amesema: hakipo kwenye uwezekano mpaka mwisho wake, basi jibu la msemaji huyu limejengeka kuwa maelezo ya hoja ya herufi “ma” kwenye uwezekano mpaka mwisho wake, hayakuwa hayo isipokuwa ni “hakuna” kama ilivyonukuliwa toka kwake na baadhi ya waliochelewa na kumzungumzia kwa maneno marefu, pia nikasimama kwake baada ya uandishi wangu uliotangulia na nikaona ninukuu maelezo ya Imam, na katika jumla ya yaliyonukuliwa toka kwake ni kuwa Al-badri Az-zarkashy amezungumza juu ya neno hili katika uandishi wake, na kunukuu maneno ya baadhi waliomtangulia, haya ndio maelezo ya mwisho aliyoyandika kwa fikra zake yakiwa na mfululizo wa kunukuu toka kwa Imam Ghazaliy, kwa hakika nimetaja uandishi huu ni kwa sababu ya kusambaa sana kwa watu ibara hii, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye mafanikio.

-            Kauli ya mwenye kusema: Pepo bila ya watu haikanyagiki [chanzo ni kilichopita uk: 173] hali ndogo ya neno hili zuri sio hivyo inasomeka, kwa sababu Pepo kama inavyoitwa kuwa ni Nyumba ya thawabu pia vile vile inaitwa kuwa ni bustani yenye miti, na pakasemwa ni yenye mitende [chanzo Miswbaahu al-muniir uk: 122 chapa ya Maktabati Al-Elmiya] kusudio la watu katika ibara hii: sehemu yoyote itakavyokuwa na utulivu pamoja na starehe hakika mwanadamu haikamiliki furaha na starehe kwake isipokuwa kwa kuwepo kitu chenye kumliwaza au rafiki atakaye kaa naye.

Miongoni mwa yale yaliyoenea kwao na kunukuliwa na watupiwa kutoka kwao – Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi – ni kuibua kwao fitina makundi na mivutano ndani ya Misikiti na Nyumba za Mwenyezi Mungu, na kuzitumia kwao kwa nguvu ili kulazimisha fikra zao, na haya yanatokea ndani ya nchi za Magharibi na kupelekea kuchafua sura ya Waislamu ndani ya nchi hizo.

Kwa ufupi: Yaonesha kwetu sawa na yale tuliyosimamia miongoni mwa vitabu vya Sheikh Al-Habashiy na wafuasi wake wanaofahamika kwa jina la Wahabeshi pamoja na kauli zao, na marejeo yao na kukosolewa kwao na kusemwa wao kuwa ni miongoni mwa watu wa Sunna na Jamaa, hawako nje ya hayo, lakini kinachochukuliwa kwao ni uharaka katika kuwaita watu mafasiki na makafiri pamoja na kushambulia wale wanaokwenda kinyume na wao, na kubeba maelezo yao ubebaji mbaya pamoja na kuwezekana kwake ufafanuzi, au yanabeba maelezo yao ubebaji mzuri.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 


([1]) Ni muungano kamili wa miili miwili ambapo unapoashiriwa mwili mmoja basi inakuwa ni ishara pia kwa mwili mwengine, kwa maana mwili mmoja huyayuka ndani ya mwili mwengine, ni sawa na kusema kuwa, Mwenyezi Mungu ni myayuko unaopatikana katika kila kitu “imani ya watu wa tasaufi”

([2]) Ni kuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina na utukufu wa Mitume na waja wema waliotangulia.

([3]) Imenukuliwa na mwandishi wa kitabu cha “Firqatu Al-Ahbaash” 2/646, na kuandikwa kwenye gazeti la (Muslimuuna) toleo la (408) la tarehe: 03/06/1413H, na kitabu cha “Nubuwati Adam” cha jaji sheikh Faisal Muuluuwy, na kutaja pia kuwa Wahabeshi wametoa habari na kuzisambaza kwa jina la: Haqaaiqu Khatwiira Haula Qadhiyat Baliiqu Al-aaliqa baina Mahaakimi wa Dar Iftaa”.

([4]) Miongoni mwake: ni Hadithi iliyopokelewa na Tirmidhy kutoka kwa Saad Al-Khudry R.A. amesema kuwa Mtume S.A.W. Amesema: “Mimi ni bwana wa watoto wa Adem siku ya kiyama na wala sijifaharishi, mkononi mwangu nina bendera ya shukrani wala sijifaharishi, hakuna Mtume siku hiyo kuanzia Adam na wengineo isipokuwa watakuwa nchini ya bendera yangu, na mimi ndiye wa kwanza kupasukiwa na ardhi na wala sijifaharishi” na Hadithi iliyopokelewa na Habbaaan toka kwa Abi Dharr R.A. alimuuliza Mtume S.A.W. na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Manabii ni wangapi? Akasema ni laki moja na elfu ishirini, akasema Abu Dharri: ewe Mtume wa Mungu ni wangapi Mitume waliotumwa kwa watu? Akasema ni mia tatu na kumi na tatu, akasema Abu Dharri: nikasema: ewe Mtume wa Mungu ni nani wa kwanza wao? Akasema: Adamu, akasema tena Abu Dharri, ewe Mtume wa Mungu ni Mtume aliyetumwa kwa watu? Mtume Akasema ndiye, Mwenyezi Mungu amemuumba kwa mkono wake na kumpulizia roho itokayo kwake”

([5]) Kwa maana: kuritad kuna wezapatikana – Mungu atulinde – pasi na sharti hii na aya inataja katika machukizo ambayo yanayofahamika kuwa anatamka neno la ukafiri lakini sehemu yake ni kwenye ulimi pasi na kuchanganyika na moyo.

Ama mwenye kutamka ukafiri au anafanya kufuru pasi na kuwepo haja ya kufanya hivyo kwa kufunguliwa kifua chake kuwa hivyo, na hiyo ni pamoja na yale aliyokuja katika Hadithi tukufu: “hakika ya mja anaweza kuzungumza neno fulani na kufahamika na kubainika ukafiri ndani kisha kuingizwa motoni”

Na akasema Imam Annawawi katika kitabu cha Arraudha 10/64 chapa ya Maktaba Islamiya”: inapatikana hali ya kuritadi kwa kusema kauli ambayo ni ukafiri ni sawa sawa limekuja kutokana na imani au kucheza shere”

Amesema Al-bahuni katika sherehe ya Muntaha Iraadaat 2/393, 394 chapa ya Aalamu kutubu”: mwenye kuritadi: ni mwenye kukufuru kwa tamko au imani au kitendo au kuwa na shaka mwenyewe hata kama alisilimu” 

Share this:

Related Fatwas