Hukumu ya Kauli ya "Mwenyezi Mungu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kauli ya "Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema Kweli" Baada ya Kumaliza Kusoma Qur`ani Tukufu.

Question

Nini Hukumu ya kauli ya "Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli" baada ya kumaliza kusoma Qur`ani tukufu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake na Masahaba zake, na waliomfuata, na baada ya hayo:
Hakika kauli ya "Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli" baada ya kusoma Qur`ani tukufu, inajuzu na hakuna ubaya, bali ni miongoni mwa mambo mema.
Na dalili ya kauli ya "Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli" ni kumtaja kwa uwazi Mwenyezi Mungu; na sisi tumeamriwa kumtaja Mwenyezi Mungu kwa amri ya kiujumla, katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi}. [AL AHZAB: 41], na kwa amri maalumu katika kauli ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Mtukufu S.A.W: {Sema: “Mwenyezi Mungu amesema kweli.”} [AALI IMRAN: 95].
Na kuunga kati ya kusoma Qur`ani tukufu na utajo huu mwishoni mwake hakukatazwi kisheria; bali ni ibada iliyoongezwa kwa nyingine.
Na haisemwi kuwa ni kuingiza kitu kipya ambacho hakikuwepo katika dini, bali ni kuingiza kilicho ndani yake, na hili linafahamika katika matendo ya Masahaba watukufu, Radhi ya Allah iwashukie wote; katika Hadithi sahihi ya Rifaa Ibn Rafii’ alisema; “Siku moja, tulikuwa tukisali nyuma ya Mtume S.A.W, na aliposimama katika rakaa, akasema: Allah anamsikia kila anayemsifu, na mtu mmoja akiwa nyuma yake akasema: Ewe Mola wetu, sifa njema nyingi, na ya baraka ni kwako, na alipomaliza akasema: Nani msemaji?, mtu huyo akasema: mimi, akasema Mtume: nimeona Malaika zaidi ya thelathini wanayapokea uliyoyasema, kwa ajili ya kuyaandika mwanzo”.
Huyu ni sahaba anayeomba dua ambayo halikuwepo agizo kutoka kwa Mtume S.A.W, na hata hivyo Mtume ameikubali bila ya kukanusha, bali alimbashiria kuwa ameona Malaika wanashindana juu ya kuandika kwake. Pia haisemwi kuwa: wakati huu ulikuwa wa kutunga sheria, na Mtume S.A.W, alikuwa nao, akiwaongoza, lakini sasa hapana; kwa sababu hakuna ishara katika Hadithi inayoweza kuashiri hivyo; ama ishara ya kimatendo kama kwamba Mtume S.A.W, amepatwa na hasira kutokana na ujasiri wa sahaba huyu kuleta jambo ambalo hakufunzwa na Mtume S.A.W, au ishara ya kikauli, kwa mfano: kauli yake Mtume S.A.W,: vyema kakini usifanye tena.
Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Fath Al-Bariy: 2/287, Ch. ya Dar Al-maarifah] anasema: “Imechukuliwa kama dalili ya kuwa: inajuzu katika sala kuingiza utajo usiopokelewa, ikiwa si kinyume cha uliopokelewa”. [Mwisho].
Kauli za Wanachuoni:
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy na Shafiy walielekea kuwa: aliyesema katika sala yake: “Mwenyezi Mungu amesema kweli” baada ya kumaliza kusoma, basi sala yake haivunjiki, akikusudia utajo.
Kuhusu Madhehebu ya Hanafiy, katika kitabu cha: [Ad-Dur Al-Mukhtar, Bihashiyat Ibn Abidiin: 1/621, Ch. ya Dar Al-Fikr, Bayruit]: “(masuala): akisikia Jina la Allah Mtukufu, akisema; Mwenye utukufu, au Jina la Mtume akimsalia, au kusoma kwa Imamu, akisema Allah na Mtume wake wamesema kweli, basi sala yake imeharibika, akikusudia jibu”.
Ibn Abdiin alieleza katika Hashiyah akisema: “(kauli yake: imeharibika, akikusudia jibu) alitaja katika Al-Bahr kuwa akiema mfano wa aliyosema Muadhini, wakati akitaka kumjibu, basi sala imevunjika, hata asipokusudia, kwa sababu ni dhahiri kuwa yeye alitaka kujibu, kadhalika, akisikia Jina la Mtume, akamsalia, basi hili ni jibu. Na inafahamika kuwa asipokusudia kujibu, bali akakusudia kusifu na utukufu, basi haivunjiki; kwani kumtukuza Allah na kumsalia Mtume S.A.W, hakupingani na kazi za sala, kama ilivyo katika Sharh Al-Muniyah”. [Mwisho kwa mabadiliko].
Kuhusu madhehebu ya Shafi: katika [Hashiyat Ash-Shihaab Ar-Ramliy Ala Asna Al-Matalib: 1/179, Ch. ya Dar Al-Kitaab Al-Islamiy]: “Ibn Al-Iraaqiy aliulizwa kuhusu mwenye kusali aliyesema baada ya kusoma kwa Imamu wake; (Allah Mtukufu amesema kweli), je, inajuzu hivi, na sala haivunjiki? Akajibu; hii inajuzu na sala haivunjiki; kwa sababu ni utajo pasipo na maneno ya kibinadamu”. [Mwisho].
Na katika [hashiyat Ash-Shubramalisiy Ala Nihayat Al-Muhtaj: 2/44, Ch. ya Dar Al-Fikr, Bayruit; na Hashiyat Al-Jamal Ala Sharh Al-Manhaj: 1/431, Ch. ya Dar Al-Fikr]; “(masuala) akiesema: (Allah Mtukufu amesema kweli) kwenye kusoma kitu cha Qur`ani, Ash-shams Ar-Ramliy anasema: haidhuru”. [Mwisho].
Na katika kitabu cha: [Hashiyat Al-Qaliyubiy Ala Sharh Al-Mahaliy Lil-Minhaj: 1/215, Ch. ya Dar Al-Fikr, Bayruit]: “(haivunjiki kwa utajo) hata asipokusudia kwa kutowepo sababu au kusudio, hata ikiwa sababu, kama ilivyopita katika Qur`ani, na miongoni mwake (Subhanallahi) ya kuonya, kama itakuja, na takbiri za matendo ya sala zikiwa za mwenye kufikisha au Imamu kwa sauti. Na pia miongoni mwake (Istaantu Billahi) au (Tawakaltu Alallahi) kwenye kusikia Aya zake, na kwa rai ya Sheikh yetu Ar-Ramliy na Sheikh yetu Az-zayadiy: kila lafudhi kama (Allah Mtukufu amesema kweli) au (Amantu billahi) kwenye kusikia kusoma, kadhalika sheikh wetu Az-Zayadiy anasema: haidhuru kwa jumla, kama vile (sajatu lillahi Fi Taatillahi), na miongoni mwake akisema; (Al-Ghafir) au (As-Salaam), akikusudi Jina la Allah au Utajo, basi sala haivunjiki, na kinyume cha hii inavunjika”.
Inafahamika kutoka kila lililotangulia kuwa hakuna katazo ndani ya sala au nje yake, kwa sababu inavyojuzu ndani ya sala, bila shaka kujuzu nje yake, lakini linalofaa kwa sala kuainisha utajo uliopokelewa tu, lakini ikiwa ni kujuzu ndani ya sala kwa kusudio la utajo, basi kujuzu nje yake hivyo hivyo.
Na miongoni mwa ushahidi wa maneno ya wanachuoni katika suala hili: ilivyotajwa na Imamu Al-Qurtwubiy katika utangulizi wa Tafsiri yake kuwa : Al-Hakiim At-tirmidhiy akizungumzia Adabu za kusoma Qur`ani tukufu, aliihesabia kauli ya mtu kwenye kumaliza kusoma:"Allah Mtukufu amesema kweli" au kauli yo yote inayomaanisha hii. Na ibara yake katika kitabu cha: [Al-Jamii’ Li-Ahkaam Al-Quran: 1/27-28, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Masriyah, Kairo] ni: “miongoni mwa heshima ya Qur`ani akimaliza kusoma, amsadikishe Mola wake, na kushuhudia Mtume S.A.W, Utume, na akashuhudia kuwa ni haki, akisema: Ewe Mola umesema kweli, na Mitume wako wamefikisha, na sisi ni mashahidi wa hivi, Ewe Mola: Tujaalie mashahidi wa haki, tutekeleze uadilifu, kisha anaomba dua nyingi”.
Na haisemwi kuwa Mtume S.A.W, hakufanya hivi, nayo ni kauli ya : (Allah Mtukufu amesema kweli); kwa sababu kuacha peke yake hakupelekei uharamu, bali lazima kuwepo dalili nyingine zaidi, na kuamuliwa kuwa: Mtume akiacha jambo, hili halioneshi kuwa ni haramu, kwa sababu huenda analiacha ama liwe haramu, makuru, lisilo na nguvu zaidi, au yeye mwenyewe halipendi, kwa mfano: ameacha kula mnyama wa jangwa na hali ya kuwa halali. Kwa hiyo kuacha tu si hoja ya kukataza.
Pia haisemwi kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Sema: “Mwenyezi Mungu amesema kweli”}. [AALI IMRAN: 95], haiambatani na suala hili, hakika Mwenyezi Mungu alimwamuru Mtume wake Mtukufu S.A.W, abainishe ukweli wa Allah katika ilivyohadithiwa katika vitabu alivyoviteremsha kama vile: Taurati n.k., na kuwa Yeye ni mkweli katika alivyobainishia waja wake katika kitabu chake kitukufu.
Kwa sababu hii ni miongoni mwa kufahamu jumla ya Qur`ani kwa mujibu wa maana yake iliyopo, bila ya kujali muktadha wake, isipokuwa ufahamu huu haupingani na muktadha au ulikuwa kinyume chake, na baadhi ya wanachuoni waliona hivi wakati wa kutoa dalili; ambapo Imamu Shafi R.A, alitoa dalili ya kuleta hoja ya Ijmaa na kuharamisha kuivunja, kwa kauli yake Mwenyezi Munmgu: {Na atakayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam, napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia}. [AN NISAA: 115], kwa vile, muktadha wa Aya ni katika hali za washirikina, na muradi wa Aya ni maana mahususi, lakini Imamu Shafi ameona kuwa kuleta hoja ya Ijmaa ni miongoni mwa maana ya Aya kwa jumla. [Taz.: At-Tahriir wat-Tanwiir, na At-Tahir Bin Ashuur, Utangulizi wa tisa ya kuwa: maana yanayochukuliwa kwa jumla za Qur`ani ni miongoni mwa muradi wake: 1/96, , Ch. ya Ad-Dar At-Tunisiyah lin-Nashr, Tunisia].
Na miongoni mwa kutoa dalili ya wanachuoni kuhusu Qiyasi, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {basi enyi wenye macho, (maoni)! Zingatieni}. [AL HASHR: 2]. Kwa vile, Aya hii tukufu inazungumzia kimsingi kwa jambo lingine, huzungumzia kuwaondoa Bani An-Nadhiir nje ya nyumba zao wakiwa na nguvu, ngome, na silaha. Na hii ni ishara miongoni mwa ishara zote kwa kumtegemeza Mtume S.A.W, na ushindi wake dhidi ya maadui. Na mwisho wa Aya tukufu kwa jumla hii ya kuzingatia kwa ilivyotokea kwa Bani An-Nadhiir, na kuwa Allah Mtukufu aliwajia kwa mahali wasipopatazamia, na akatia woga katika nyoyo zao, na akawajaalia wanazivunja nyumba zao kwa mikono yao na kwa mikono ya Waislamu.
Mtaalamu Al-Alusiy katika Tifsiri yake [Rohol-Maaniyy: 28/41, Ch. ya Al-Muniriyah] anasema: “Ni wazi kutoa dalili ya Aya hii kuwa kutekeleza Qiyasi ni hukumu ya kisheria, wanasema kuwa: Mwenyezi Mungu aliamuru kwa kuzingatia yaani kuvuka kutoka kwa kitu hadi kingine, na hichi ni kipengele cha Qiyasi, kwa kuwa inachukua hukumu ya msingi iwe ya tawi”. [Mwisho].
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia kuwa kauli ya: "Mwenyezi Mungu amesema kweli" baada ya kusoma Qur`ani, inajuzu, na haina ubaya, bali ni miongoni mwa mambo yanayo pendeza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas