Maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua).
Question
Nini makusudio ya kauli ya Mwenyezi Mungu : (Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua).
Answer
Mwenyezi Mungu Anasema: (Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua) Na wenye mamlaka: ni wanazuoni na viongozi.
Ama wanazuoni: Wao ndio marejeo katika kujua hukumu za kisheria na kuziweka katika kauli na vitendo.
Ama viongozi: wao wamepewa jukumu la kulazimisha kutekeleza hukumu ili kufikia maslahi ya wanadamu na wenye kuweka sera za Sharia ili kuwaweka sawa raia, Qadhi Aboubakar Bin Araby amesema katika “ Ahkam Al-Qur’aan” (472/1): [Sahihi kwa upande wangu: kwamba hao ni viongozi na wanazuoni wote; Ama viongozi: kwa sababu asili ya amri ni kutoka kwao na utawala ni wao. Ama wanazuoni: Kwa sababu kuwauliza ni wajibu unaopasa kwa watu na jibu lao ni lenye kulazimu, na kufuata fatwa zao ni wajibu] mwisho.