Dalili ya Kuzuia Kisingizio (Sad Al...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dalili ya Kuzuia Kisingizio (Sad Al-Dharia)

Question

Tunasikia kutoka kwa baadhi ya watu kuwa dalili ya kuharimisha kwa suala moja ni kuzuia visingizio. Hivyo, ni nini maana ya kuzuia visingizio? Je, ni miongoni mwa dalili za kisheria? 

Answer

Sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Kuzuia kisingizio ni maneno mawili: moja wapo liliongezwa kwa lingine, kuhusu neno la kwanza -nalo ni kuzuia- maana yake ni pinga. Na neno la pili ni kisingizio na maana yake ni udhuru au hoja.
Ni wazi kwamba kuzuia kisingizio katika lugha maana yake ni kufunga vizuri kwa barabara zinazopelekea kitu fulani.
Kuhusu maana ya istilahi kwa kuzuia kisingizio Al-Baji anasema: Ni suala ambalo linaonesha kuruhusiwa na linasababisha tendo linalozuiliwa. [Ihkaam Al-Fusuul kwa Al-Baji 2 / 695-696, Dar Al-Gharb].
Ibn Al-Arabi alisema: “Kila mkataba unaoruhusiwa na unaoweza kupelekea tendo lililokatazwa.” [Ahkaam Al-Quran 2/265, Darul Kutub Al-Elmiyah].
Hukumu katika suala hili ni kwamba asili ya mambo ni uhalali, na kwamba kuzuia kisingizio katika jambo ambalo udhuru wake ni nadra, jambo ambalo Wanavyuoni wa umma walikubaliana -kama Al-qrafiy alivyosema- jambo hili ni tahadhari yenye kulaumiwa; kwa sababu ya uhaba wa uharibifu uliotokana nao, na jambo la nadra halina hukumu, kwa mujibu wa Fiqhi, na kwa sababu tendo hili halina ufisadi, na Mwenye Sheria alizingatia maslahi ya umma na hakuzingatia jambo la nadra, basi jambo ambalo udhuru wake ni nadra kutokana na kisingizio litabaki kwenye asili yake ambayo ni uhalali na wala usijaliwe mtazamo wa wanaopinga, kama vile; maji yaliyopatwa na jua katika sufuria ya chuma katika nchi za joto, maji haya yanachukiza matumizi yake kama kuna maji mengine; kwa hofu ya kutokea kwa madhara ya nadra, lakini kama hakuna maji mengine inapaswa kuyatumia; kwa kutokwepo madhara kwa ujumla, na hairuhusiwi kuzuia maslahi ambayo ni zaidi ya madhara, na kama vile kutolima zabibu kwa hofu ya kutengenezwa pombe, vile vile kuzuia kukaa karibu na nyumba jirani kwa hofu ya kutokea kwa uzinzi, hii yote ni kisingizio hakizuii na matatizo hayatatuliwi. [Rejea: Qawaid Al-Ahkaam fi Masalih Al-Anaam kwa El-Ezz Ibn Abdul Salam 1/100, Darul Kutub Al-Ilmiyah, na Al-Fruuq kwa Al-qrafi 2/32, Alamul Kutub].
Hairuhusiwi kutahadhari katika kuzuia kisingizio kinacho pelekea madhara mengi tu, kama katika madhehebu ya Imamu Al-Shafi na madhehebu mengine, na kwani hakuna uwezekano wa kutokea madhara. [Al-Muwafaqat kwa Al-Shatbi 2/361, Darul Maarifa].
Dalili ya hivyo ni kwamba asili ya mambo ni uhalali, basi hakuna jambo lolote linaharimishwa isipokuwa kwa dalili yenye nguvu, imepokelewa kutoka kwa Abu Thalabah Al-Khushni -R.A- kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu amefaridhisha mambo ya dini kwa hivyo usiyapuuze. Vile vile kaweka mipaka usiikiuke. Amekataza baadhi ya mambo kwa hivyo usifanye. Yale aliyoyanyamazia ni kwa ajili ya huruma zake kwako wala hakusahau kwa hivyo usiyadadisi”. Al-Nawawi alisema: Hadhidi hii ni nzuri, imesimuliwa na Al-Daraqutni na wengine.
Ibn Rajab alisema: “na kauli yake kuhusu mambo aliyoyanyamazia: (kwa ajili ya huruma zake kwako wala hakusahau) ina maana kwamba, Mwenyezi Mungu alinyamazia baadhi ya mambo kwa ajili ya huruma zake kwa waja wake, ambapo hakuyaharimisha mambo hayo kwao ili kuwaadhibu kwa kuyatenda, wala hakuwalazimisha kuyatenda ili kuwaadhibu kwa kuyaacha, lakini aliwasamehe tu, kama wakiyafanya mambo haya basi hakuna aibu yoyote, na kama wakiyaacha hali ni ile ile, na katika Hadithi ya Abu Ad-Dardaa: kisha akasema kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau} [MARYAM: 64]. Kama kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: {Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau} [TAHA: 52]. Na kauli yake S.A.W: “kwa hivyo usiyadadisi”, inawezekana marufuku haya yanahusiana na zama za Mtume S.A.W, kwa sababu ya idadi kubwa ya utafiti na swali kuhusu mambo ambayo hayakutajwa labda ni sababu ya kuyalazimisha au ya kuyaharimisha, na Hadithi ya Saad Ibn Abi Waqas ina dalili ya hivyo, inawezekana kukataza ni kwa jumla, na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Salman kutoka kwa maneno yake yana dalili ya hivyo, ambapo idadi kubwa ya utafiti na swali kuhusu mambo ambayo hayakutajwa labda ni sababu ya kuyalazimisha au ya kuyaharimisha, basi kukubali kwa msamaha katika mambo haya, na kuacha kuyatafutia na kuyaulizia ni bora, inawezekana hali hii inahusiana na kauli ya Mtume S.A.W: “Wameangamia wapindukiaji mipaka. Amesema hivi mara tatu” Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim kutoka kwa Hadithi ya Ibn Masoud, na wapindukiaji mipaka: ni wanaodadisi mambo ambayo hayana umuhimu kwao, na hali hii inawezekana kushikwa na wanaozingatia maana ya kauli ambayo ni dhahiri, na wanaokana maana ya kweli, na kipimo kama vile kundi la Dhahiriah.
Na uchunguzi katika hali hii – na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi - kwamba kutafutia mambo ambayo yana matini ya kibinafsi au ya matini jumla katika sehemu mbili:
Ya kwanza: Kutafutia kuhusiana na maana za matini sahihi kutokana na maana na kipimo wazi na sahihi, hii ni haki, nayo ni miongoni mwa yanayolazimishwa kutendwa na wenye jitihada kuhusu kujua kwa hukumu za kisheria.
Ya pili: ni kuangalia kwa makini katika mawazo na tofauti inayotengwa, kutofautiana kati ya mambo yanayofanana ambayo haionekani athari yake katika Sheria, pamoja na kuwepo kwa sifa zinazosababisha kuchanganya kati ya mambo haya, au inachanganywa kati ya mambo yanayotofautiana kwa sifa zisizofaa, na hakuna dalili inayothibitisha athari yake katika Sheria, kuzingatia na utafiti huu haufai wala haukubaliki, ingawa umetokana na makundi ya Wanavyuoni wa Fiqhi, lakini mtazamo unaokubalika ni mtazamo unaokubaliwa na Masahaba na waliokuja baada yao kama vile; Ibn Abbas na kadhalika, na labda haya ni makusudi ya Ibn Masoud aliposema: “Jihadharini na kupita mipaka, jihadharini na kuulizauliza, na fuateni walivyofuata Masahaba”. [Jami Al-Uluum Walhikam 2/170, Muasastu Resalah].
Ibn Hazm alisema: “Masuala yanayofanana siyo haramu kwa yakini, na kama siyo haramu basi ni halali kufuatana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Na kwa nini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipokuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka} na mambo yasiyo haramu basi ni halali, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.} na kauli yake Mtume S.A.W: “Wenye makosa zaidi katika Uislamu ni walioulizia kitu ambacho hakukikatazwa lakini alikikatazwa kwa ajili ya swali yake”. [Al-Ihkam fi Ussul Al-Ahkam 6/3, Darul A-Faaq Al-Jadiidah].
Madhehebu ya Imam Malik na Ahmad Ibn Hanbal ni miongoni mwa madhehebu maarufu zaidi zinazosema kwa kuzuia kisingizio: Imepokelewa kutoka kwa madhehebu ya Imamu Malik kwamba Al-Hatwab alisema: “Madhehebu yake R.A, inategemea kuzuia kisingizio na kujiepusha mambo yenye shaka, madhehebu hii ni mbali na mambo yenye shaka zaidi kuliko madhehebu nyingine”. [Mawahib Al-Jalil kwa Al-Hatwab 1/26, Darul Fikr].
Kuhusu madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbali, Ibn Al-Najjar anasema: “(kisingizio kinazuie nayo ni mambo yanayoonekana kuwa yanaruhusiwa na yanayopelekea mambo yasiyoruhusiwa) na maana ya kuiziba ni kutoitenda kwani ni haramu”. [Al-Kawkab Al-Muniir 4/434, Maktabat Al-Obeikan.
Al-Zarkashi anasema: “Al-Qurtubiy alisema: Imam Malik na wenzake walipendelea kuzuia kisingizio, wengi wa watu wamempinga Imam Malik”.
Kisha aliainisha masuala yenye hitilafu akisema: “Fahamu kuwa mambo yanayopelekea haramu yanaweza kupelekea haramu pasipo na shaka yoyote au la, kama yakipelekea haramu pasipo na shaka yoyote ni lazima kuyajiepuka, ama mambo yanayopelekea haramu kwa shaka, yanaitwa kisingizio, nayo ni lazima kuyazingatiwa” [Al-Bahr Al-Muhiit kwa Az-Zarkashi 8/90, Darul Kutubi].
Wanavyuoni wasemao kwa kukizuia kisingizio walitaja dalili kutoka Qur`ani na Sunnah, kuhusu Qur`ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Wala msiwatukane hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda} [Al-ANAAM: 108].
Ibn Al-Arabiy anasema: “Wanavyuoni walikubaliana kuwa maana ya aya hii ni: Msitukane miungu ya wapagani ili wasitukane Mungu wenu, matusi pasipo na hoja ni tendo la mwenye duni. Mtume S.A.W. Alisema: “Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kuwatusi wazazi wake, (maswahaba) wakasema: ewe Mtume wa Allah! Na je mtu anawatusi wazazi wake? Akasema: “ndio, anamtusi mtu baba wa mwenzie naye anamtusi babaye, na anamtusi mtu mama wa mwenzie naye anamtusi mamaye”. Mwenyezi Mungu amekataza katika Qur`ani kutenda mtu fulani tendo linalopelekea haramu, kwa hivyo Wanavyuoni wetu wameshikilia aya hii katika suala la kuzuia kisingizio, nayo ni ya kila mkataba unaoruhusiwa na unaopelekea jambo lililopigwa marufuku ... Imesemekana kuwa: Washirikina walisema kuwa: kama hukuacha kutukana miungu wetu tutamtukana Mungu wenu, basi Mwenyezi Mungu akashusha aya hii”. [Ahkam Al-Qur’an kwa Ibn Arabiy 2/265].
Katika Sunna ilielezwa kuhimiza kumcha Mungu na kujiepusha mambo yenye shaka, kama alivyosema Mtume S.A.W: “Lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu). Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allah alie tukuka ni makatazo Yake”. Na kauli yake: “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka”. Imepokelewa kutoka kwa At-Tirmidhiy na An-Nasaiy. Na akauli yake: “Udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka) katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua”. Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim. Al-Shawkaniy amefanya Hadithi hizi miongoni mwa Hadithi bora zinazothibitisha sura hii. [Rejea: Irshaad Al-Fohul kwa Al-Shaukani 2/196, Darul Kitab Al-Arabi].
Hata hivyo, Wanavyuoni wanaokataza kuzuia kisingizio wanamini kwamba dalili zilizotajwa katika suala hili ni dalili za jumla tu, hazigusia masuala yote, kwa sababu ya chombo kinachotumika katika masula haya ni aina nyingi wala si aina moja tu. Ni ajabu kuwa mmoja wa wanavyuoni wa Maliki ni yule anaelezea hii, ambapo Al-Qarafiy Al-Malikiy anasema: “Fahamu kuwa kisingizio ni sababu ya jambo fulani, nao ni sehemu tatu, miongoni mwa visingizio hivi ni vilivyokubaliwa na watu kuwa ni lazima kuvizuia visingizio hivi, na miongoni mwa ni waliotofautiana kuhusu jambo hili, ambapo walisema inakatazwa kulimwa zabibu kwa hofu ya kutengenezwa pombe, vile vile kukaa jirani na nyumba kwa hofu ya kufanya uzinzi, basi hakuna kitu chochote kutokana na vitu hivi kimekatazwa, hata kama kikiwa chombo cha haramu, na masuala ambayo Wanavyuoni wamekubaliana kuyaziba kama vile; kukataza kwa matusi ya sanamu kwa mtu anayeweza kulaani Mungu S.W, na kama vile kuchimba visima katika njia za Waislamu kama akijua kuwa wanaweza kuanguka katika visima hivi au alidhani hivyo, pia kutia sumu katika chakula chao kama akijua kuwa wanaweza kula na wanakufa, na Wanavyuoni wametofautiana kuhusu masuala kama vile; kumtazama mwanamke kwa sababu ni kisingizio cha uzinzi na pia kuzungumza pamoja naye, vilevile miongoni mwa masuala yaliyokatazwa ni biashara ya muda kwenye madhehebu ya Imam Malik, na inasemuliwa kuhusu madhehebu hii kusema kwa kuzuia visingizio, na sivyo hivyo, lakini miongoni mwao ni masuala yaliyokubaliwa na Wanavyuoni kama ilivyotangulia, wakati huu inaonekana kutokwepo kwa maslahi ya kutoa dalili ya Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Al-Shafiy katika suala la kuzuia kisingizio kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua.} [AL-ANAAM: 108], na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pia: {Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walioivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Jumaamosi} basi Mwenyezi Mungu amewapuuza kwa sababu walifunga samaki siku ya Jumamosi, na walisingizia kuvua siku ya ijumaa, na kwa kauli yake Mtume S.A.W: “Mwenyezi Mungu amewalaani Wayahudi, mafuta (shahamu) imeharimishwa kwao, basi waliiuza na wakala bei zao”.
Hiyo alisema: “Hizi ni dalili nyingi wamezitaja ili kuthibitisha sula la kuzuia visingizio, na hazina faida, kwa sababu dalili hizi zinathibitisha kuwa Sheria imezuia visingizio kwa ujumla, na jambo hili limekubaliwa na Wanavyuoni wote, lakini hitilafu hasa katika visingizio venyewe, kama vile biashara ya muda na kadhalika, ni lazima kutajwa dalili zinazohusiana na suala la hitilafu lenyewe, au dalili hizi hazina faida hata kama wakikusudia kupima juu ya visingizio hivi vilivyokubaliwa na Wanavyuoni, basi inapaswa hoja yao kuwa ni kipimo tu” [Al- Fruuq3/266].
Zaidi ya hayo, Hadithi zilizotajwa katika suala hili zinathibitisha kuchamungu, na hakuna kutokubaliana kuhusu suala hili, kwa sababu kumcha Mungu ni suala pana na linapedekezwa, lakini kulifanya linapendekezwa si wajibu, na miongoi mwa inayothibitisha hivyo Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Oqbah Ibn Al-Harith ambapo alisema: “Nimemwoa mwanamke, mwanamke mweusi amekuja kwetu, akisema: nimewanyonyesheni, nikaenda kwa Mtume S.A.W, nilimwambia kuwa: nimemwoa msichana fulani binti fulani, akaja kwetu mwanamke mweusi akasema: nimewanyonyesheni, naye mwongo, akasema, Mtume ameniacha. alisema: nimekuja mbele yake, nikasema yeye ni mwongo, akasema: ni namna gani naye alisema kuwa amewanyonyesheni, achana naye”. [Imepokelewa kutoka kwa Imam Al-Bukhaariy].
Al-Aini anasema katika kitabu chake: [Al-Umdah]: “Mwandishi alisema: idadi kubwa ya wanavyuoni walisema kuwa: Mtume S.A.W. alimshauri swahaba huyo kujiepusha suala lenye shaka kwa hofu ya kupata faraja ambayo labda inasababisha jambo la haramu, kwa sababu imethibitisha uharamu wa hivyo kwa mujibu wa kauli ya mwanamke yule, lakini haikuwa yenye nguvu wala thabiti... lakini Mtume S.A.W alimshauri swahaba yule kujitahadhari tu, dalili ya hivyo ni kwamba Mtume S.A.W. alipoambiwa kwa hali ya swahaba yule akageuza uso wake kwa upande mwingine, basi kama suala hili ni haramu Mtume S.A.W. hakugeuza uso wake mbali naye, bali atamjibu kwa uharamu moja kwa moja, lakini aliporudia suala hili kwa mara nyingine tena akajibu kwa kumcha Mungu”. [Umdatul Qarii 11/167, Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].
Miongoni mwa majibu ya wahusika pia ni: chombo ni aina mbalimbali na sio aina moja tu, nacho kinafuta hukumu tano za kalifisho.
Hitimisho: Hakuna kutokubaliana kwamba matini za Sheria zilizohusiana na kuzuia kisingizio inapaswa kuzifuata, na rai hii iliyochaguliwa na Wanavyuoni wote, na mfano wake ni kukataza kutukana kwa miungu ya washirikina ili hali hii isisababishe matusi kwa Mwenyezi Mungu, na kukataza kusali katika wakati maalumu. Na maoni sahihi iliyochaguliwa ni kutozingatia suala la kuzuia kisingizio ni dalili inayotegemewa na mwenye jitihada katika hukumu yake juu ya masuala madogo, na kama suala hilo halikuzingatiwa dalili basi halitegemewi katika mchakato wa kuamua rai bora, hivyo, mchakato huu ni sehemu ya fatwa hii inayoweza kuwekwa chini ya kichwa cha “kuamua rai bora kufuatana na maslahi”.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu, kuzuia kisingizio ni miongoni mwa dalili zisizokubaliwa na Wanavyuoni, na inafuatiwa suala hili kwa mujibu wa yaliyokubaliwa na Wanavyuoni kuwa ni haramu, si kwa mujibu wa mambo yenye madhara nadra.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas