Kuosha Najisi ya Mbwa Mara Saba kwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuosha Najisi ya Mbwa Mara Saba kwa Mchanga.

Question

Je, inatosha kuosha najisi ya mbwa kwa kusafisha mara saba kwa mchanga badala ya kuosha kwa maji au ikawa kwa kuosha mara saba kwa maji na moja yake kwa mchanga? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Abu-Hanifa na Imamu Shafi na Imamu Malik waliafikiana juu ya kuwa mabaki ya chakula cha mbwa na mate yake mdomoni ni najisi, na pia chombo cha maji cha mbwa ni najisi, na dalili yao katika swala hilo ni Hadithi iliyosimuliwa na Al-Shaykhan -na tamko hapa kwa Muslim- kutoka katika Hadithi ya Abu-Hurairah alisema: “Twahara ya chombo cha mmoja wenu atakapokiramba mbwa ni kukiosha mara saba, na moja yake (hizo mara saba) iwe ni kwa mchanga”. Na alisema vilevile: Mtume S.A.W., alisema: “Mbwa Mbwa akiramba maji katika chombo cha mmoja wenu lazima akisugue kwa mchanga kisha akioshe mara saba kwa maji”.
Neno (Twohara) haliwi ila kutoka katika hadathi nyepesi na nzito au kwa sababu ya najisi, wala haisawiriki uwepo wa hadathi nzito au nyepesi juu ya chombo na hii ni dalili juu ya kwamba mabaki ya chakula na mate ya mbwa ni najisi [Tazama: Al-Majmuo’ 2\585, Ch. Maktabet Al-Irshad, Jedah], kama kuagiza kukiosha chombo na kukojolea maji ni dalili juu ya najisi; na lau pangeaizwa kuogea bila maana itakuwa ni kupoteza mali pure, na jambo hili ni haramu.
Na kwa upande mwengine Wafuasi wa Madhehebu ya Kimalik walisema kwa kauli tofauti na rai zilizotangulia, pale waliposema kuwa mabaki ya chakula na mate ya mbwa ni safi, kwani wanaona kwamba kila kiumbe hai ni safi hata kama kiumbe hicho ni mbwa au nguruwe, kadhalika wanasema kuwa jasho lake kiumbe hicho, machozi yake na mate yake ni vyote ni visafi, na wao wana dalili zao juu ya jambo hili [Hashiyat Al-Desoqiy 1\50, Ch. Dar Ihyaa At-Tutath Al-Arabiy].
Na kwa hakika imepokewa katika usafishaji wa najisi ya mbwa, Hadithi ya Abu Hutairah na wote wameafikiana naye. alisema: Mtume S.A.W., alisema: “Twahara ya chombo cha mmoja wenu atakapokiramba mbwa ni kukiosha mara saba, moja yake kati ya hizo mara saba iwe kwa mchanga)) .
Na Abu Dawud alisimulia kutoka kwa Abu Hutairah kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alisema: “Mbwa akiramba katika chombo chenu, basi mkioshe mara saba; ya mwisho kati yake iwe ni kwa mchanga”.
Wafuasi wa Kishafiy na wa Kihanbaliy waliafiki kwamba utohara wa najisi ya mbwa unakuwa wajibu kwa kuosha mara saba na moja yake ni kwa mchanga, na ni bora zaidi kuosha kwa mchanga kuwe mwanzo, na maana ya wazi ya kuosha sio kwa sababu ya najisi tu, kwani ikiwa najisi ni sababu ya kuosha tu, basi yatosha kuosha mara tatu, au asihitajike kuosha kwa mchanga katika mmoja ya majosho saba bali maana ya kuosha ni ibada. [Tazama: Asna Al-Matwaleb 1\21, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy.na Al-Inswaf 1\310, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy, na Kashaaf Al-Qinaa’ 1\182, CH. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na Wafuasi Madhehebu ya Kishafiy wanaona kuwa ni wajibu kuosha kwa mchanga mara moja miongoni mwa mara saba za kuosha najisi, na haifai kuosha kwa sabuni au kitu chochote cha kisasa badala ya mchanga, na kwa upande mwengine Wafuasi wa Madhehebu ya Hambal wanaona kuwa sabuni yaweza kutumika badala ya mchanga.
Na Wafuasi wa Madhehebu ya Kimalik wanaona ni kuosha najisi ya mate ya mbwa mara saba kwa maji tu bila ya kutumia mchanga, na kuosha mara saba sio kwa ajili ya najisi bali kuosha hapa ni ibada ya kutii amri ya sheria. Naye Ad-Dosoqiy anasema hivyo kwa dalili ya kwamba: “kutumia mchanga hakukuthibiti katika Mapokezi yote ya Hadithi, bali kumethibiti katika baadhi yake tu, na hata zile baadhi ya Hadithi zenye dalili hazina uzito”. [1\84].
Na Wafuasi wa Madhehebu ya Kihanafi wanajuzisha kuosha mara tatu bila mchanga, na dalili yao juu ya hayo ni kwamba kuosha najisi ya mkojo wa mbwa ni mara tatu, na jambo hilo ni sawa ya najisi ya mabaki ya chakula cha mbwa, na wanasema kwamba Hadithi ya Abu Hurairah ya kuosha mara saba ilisimuliwa katika zamm za Mwanzo za Uislamu. [Al-Enayah 1\109, CH Dar Al-Fikr].
Ni wazi kwamba sharti ya kutumia mchanga au chochote mahala pake ili kupatwaharisha ni kwa mujibu ya madhehebu ya Shafi na Hambali, lakini wao wanaafikiana na Madhehebu ya Hanafi kwa kuosha kwa maji ingawa wanahitalifiana juu ya idadi ya kuosha, na haitoshi kutumia mchanga peke yake hata kama sehemu iliyonajisika ni katika mchanga, kama vile mbwa kupakojolea mahaka hapo au akapalamba lamba, na katika hali hii hakuna haja kutumia mchanga katika kutwahirisha kwa mchanga kwani sehemu hiyo inakuwa safi, na haiwu sehemu ya ibada kwani mambo ya ibada ni yale yanayopokelewa kwa maandiko tu.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia, mbwa akiichafua sehemu yoyote kwa mkojo au kwa mate yake, sehemu hiyo itatwahirishwa kwa kuosha na mchanga, na haitoshi kutumia mchanga peke yake tu hata kama mchanga huo utatumika mara saba. Na kuna uwezekano wa kuyatumia maji yaliyochafuliwa kwa mchanga kama yatatosha kuoshea mara saba, na katika wakati huo yatatosheleza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas