Fikra ya Kiislamu: Tamko kuhusu (Ka...

Egypt's Dar Al-Ifta

Fikra ya Kiislamu: Tamko kuhusu (Kanuni zake – Mifumo yake ya Kimaadili – Misingi yake).

Question

 Je, yawezekana kuleta mtazamo kuhusu kanuni za fikra za Kiislamu mifumo yake ya kimaadili na kanuni zake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Fikra ya Kiislamu ni mfumo asili usiohitaji kuiga, isipokuwa unahitaji hoja na dalili, na unahitaji pia kuleta mtazamo sahihi kuhusu Uislamu katika alama zake kuu, ili mtu yeyote aweze kupima kati ya Uislamu na Dini zengine, madhehebu yanayoingina ndani ya Uislamu kutoka nje, pamoja na kuhifadhi pande zote za Uislamu pasi na kuingia katika mivutano ya kimadhehebu pamoja na tofauti za kifiqihi.
Fikra ya Kiislamu ni yenye kukusanya maudhui ambazo zinazungumzisha akili ya mwanadamu katika yale yanayogusa uhalisia wa ulimwengu wetu na ulimwengu wa kuona, na kutoa msukumo wa kuzingatia na kuangalia yale yanayofungamana na kadhia ya Imani Ibada Misingi Mivutano na Maadili katika Uislamu.
Fikra ya Kiislamu sio fikra ya nadharia katika siasa tu au vita, na wala sio nadharia ya kukutana tu wala sio nadharia ya masuala haya au yale, lakini yenyewe ni mjengo wa kiimani unaopanuka zaidi kwenye uhusiano wa mtu na mtu hapa ardhini mpaka uhusiano wa mtu na ulimwengu pamoja na sayari ya ardhi, kisha uhusiano wa mtu na ulimwengu ardhi na Muumba Mtakatifu.
Kazi ya kufikiri inatanzuka kwa vipengele vyepesi kama wanavyosema wanachuoni wa elimu ya saikolojia, kunakipengele kinafanya kazi ya kuuliza swali linalochomoza akilini au tatizo linamtokea mwanadamu na kutumia hisia zake, na kushikamana na njia ya muongozo kuelekea kwenye jibu lenye kukinaisha na analoridhia.
Kisha kawaida akili inafuata aina ya tabia na kutekeleza mfumo uliopo ambao akili inaufuata, au mfumo wa Kiungu ambao umeletwa na Mitume amani iwe juu yao.
Fikra ya Uislamu kwa ujumla wake inajikita juu ya: Kanuni za Kiimani – mifumo yake ya Kimaadili – Misingi yake ya Kiroho na Mivutano yake ya Kimaadili.
a- Kanuni za Kiimani kwenye fikra za Kiislamu:
Akida katika uelewa wake inamaanisha ni imani ambayo imejikita moyoni kwa misingi inayozingatiwa ni muhimili wa muungano na mapenzi kati ya wenye kujivisha Imani, na inakusanya kanuni na misingi ya Imani Kiislamu kama ifuatavyo:
Uhuru wa Kuamini: ambapo Sharia ya Kiislamu inazingatiwa kuwa ni Sharia pekee ya mbinguni ambayo imelingania uhuru wa Imani, na kuacha uhuru kamili kwa kila mwanadamu katika kuamini kile atakacho, Mola Mtukufu Amesema {Hakuna kutenzana nguvu kwenye Dini} [AL BAQARAH, 256].
Na Akasema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu {Hivi wewe unalamizimisha na kutenza nguvu watu ili wapate kuwa waumini}[YUNUS, 99].
Usafi wa Kuamini: kusudio kuu ambalo limesisitizwa na Qur`ani Tukufu kwa daraja la kwanza ni kutakasa Imani na Ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mfunguzi wa mbingu na ardhi, Mitume wote walilingania hilo {Enyi watu, mwabuni Mwenyezi Mungu hamna nyinyi Mola mwengine asiyekuwa Yeye} [AL A’RAAF, 59].
Misingi ya Imani: kumuamini Mwenyezi Mungu peke yake –kuamini uwepo wa Malaika– kuamini vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii wake na Mitume yake – kuamini Mitume – kuamini kukufauliwa na siku ya mwisho, misingi hii imeelezewa na Qur`ani Takatifu pale Mola Aliposema {Mtume ameamini yale yaliyoteremshwa kwake toka kwa Mola wake na Waumini wote ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake hatutenganisha kati ya yeyote katika Mitume yake na wakasema tumesikia na tumetii usamehevu ni wako Mola wetu na kwako ndio mafikio}[AL BAQARAH, 285].
Na Akasema tena Mwenyezi Muhgu Mtukufu {Na yeyote mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake na Siku ya mwisho basi hakika huyo amepotea upotevu wa mbali kabisa}[AN NISAA, 136].
Kuthibiti kwa Imani: nako ni katika misingi mikubwa ya Imani ya Kiislamu, na ambayo inawezekana kupitia hiyo kupambana na matukio yenye kuleta hali ya wasi wasi ambayo inayowakuta watu wengi, hakika Mola Mtukufu ametuongoza kwenye umuhimu wa kuthibiti katika Imani, na kuacha hali ya wasi wasi na shaka Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu {Kuna miongoni mwa watu wanamuabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni ikiwa atapatwa na jambo la kheiri anatulia nalo na ikiwa atapatwa na fitina hugeuza uso wake, amepata hasara duniani na siku ya mwisho na huko ndiko kupata hasara kukubwa}[AL HAJJ, 11].
Uwazi wa Imani: imani ya Uislamu inasifika na sifa ya uwazi kushikamana na kupanuka yale huwenda yametangulia akilini Na imani ya Uislamu inasimama katika kumkiri Mwenyezi Mungu peke yake kuwa ndio Mola Mlezi Muumba na Mwenye kuabudiwa, na kwa upweke wake katika Dhati yake Sifa zake na Matendo yake.
b- Mifumo ya Kimaadili kwenye fikra ya Kiislamu:
Mifumo ya kimaadili katika fikra ya Uislamu inajikita katika uelewa wa Ibada, ambayo kwa ibada hiyo mwanadamu hufikia furaha ya dunia na akhera, na ibada katika Uislamu ina ufahamu wake mpana ambao unakunjuka mpaka kwenye matendo ya maisha mbali mbali ya wanadamu wote {Sema, hakika sala yangu na ibada zangu na uhai wangu na kifo changu ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote} [AL ANAAM, 162].
Na Ibada katika Uislamu inazingatiwa ni sehemu muhimu katika sehemu za kimalezi ambazo Uislamu umezikunjua ili mwanadamu apate kujifunika kwenye kivuli chake, nayo ibada na mafunzo ya maadili, na malezi ya nafsi ili iweze kupambana na matatizo ya maisha, na kumfungulia milango ya akhera, na Ibada kwa upande mwengine na mtihani na majaribu Mola Mtukufu Amesema {Na tunakujaribuni kwa mambo ya shari na kheir. Na kwetu sisi mutarejeshwa}[AL ANBIYAA’, 36].
Na katika upande wa tatu wa haki ya Mungu, Amesema Mola Mtukufu {Sikuumba majini wala watu isipokuwa waniabudu}[ADH DHARIYAAT, 56].
Upande wa nne, Ibada katika Uislamu hutengeneza maana ya maisha ya mwanadamu mwenyewe, na husaidia mwanadamu kwenye kufikia ukamilifu pasi na kusubiri mpaka wakati wa kufa matamanio ya mwili kama vile ilivyokuwa katika baadhi ya Dini, au kupitia mfululizo unaofuatana katika upandikizaji wa roho kama vile ilivyo kwenye imani ya Wabanyani, au baada ya kufa sehemu ya mwili kama ilivyo kwenye imani ya Budha. Uislamu unatoa nafasi ya juu suala la nia ambayo kwa hiyo nia inapatikana ibada, na hubadilika desturi na kuwa utiifu, kama vile Uislamu umeweka sharia za ibada ambazo ndani yake kuna malezi ya roho na mwili, malezi ya Dini na dunia, malezi ya kujiandaa kinafsi na kimaadili, malezi ya umoja na kundi, malezi ya mambo bora na nidhamu usawa na undugu kama vile kwenye sala, malezi ya matumizi ya kati na kati na pasi na kufanya matumizi hovyo na kuchunga hali ya watu mafakiri kama vile mfumo wa zaka, malezi ya huruma subira na kuimarisha utashi na kuhuhisha dhamira kama ilivyo kwenye ibada ya funga, na malezi juu ya misingi ya mashariano undugu usawa usalama toba na kuomba msamaha. Uislamu unatoa umuhimu mkubwa katika mfumo wake wa kitabia kwenye sala ya kidunia kati ya mtu mmoja na wanaomzunguka, wala haitoshi uhusiano kati ya mtu na Muumba wake tu.
c- Misingi wa kiroho wa fikra ya Kiislamu:
Hakuna shaka kuwa upo mfumo timilifu mkubwa ambao unwakilisha msingi wa kiroho wa fikra ya Kiislamu, ukiongozwa na: uhuru – uadilifu – amani – uchamungu – utekelezaji – usawa na msingi wa kiroho unaotokana na Dini sahihi wenyewe peke yake ni wenye uwezo wa kumuongoza mwanadamu, kwa sababu misingi huu ni {utengenezaji wa Mwenyezi Mungu ambaye amtengeneza vilivyo kila hakika Yake ni mwenye habari kwa yale muyafanyayo}[AN NAML, 88.
Hakuna shaka kuwa kila msingi miongoni mwa misingi ya Uislamu unastahiki kusimama hapo kwa maudhui au zaidi ya maudhui.
Na pindi ulipokuja Uislamu na misingi yake wenyewe ulifuata katika kazi ya kujilingania njia ya hekima na maneno mazuri, Amesema Mola Mtukufu {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walio ongoka}[AN NAHAL, 125].
Na misingi ya Kidini pamoja na ya kiroho ni yenye kuathiri kwenye akili za watu, na katika mwenendo wao na kutengeneza sehemu kubwa ya maadili yao, Uislamu umesimamisha sheria zake zote katika upande wa ibada na mambo ya matendeano kwenye msingi wa kimaadili, Mola Amesema {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu,na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, nauovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka} [AN NAHAL, 90].
Hakika msingi wa kimaadili ndani ya Uislamu unasimama kuzuia dhidi ya kudondoka kwetu kwenye misingi isiyosahihi ambayo inafanya kazi kwenye ustaarabu wa kisasa kama vile kuwa lengo lina halalisha njia ya kulifikia, tafsiri ya historia uhalisia bali tafasiri ya mambo yote, tafasiri ya maadili ya kibanadamu na zenginezo miongoni mwa ukiukaji wa kifikra ambao Uislamu umetuzuilia kwa lengo la kusimamisha maisha yote juu ya msingi kuamini Mwenyezi Mungu peke yake, na kuchukuwa kwa Mwenyezi Mungu mfumo wa kimada mfumo wa kiroho mfumo wa maisha na mfumo wa kimaadili.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Vyanzo:
- Fikra ya Kiislamu (misingi yake – mifumo yake – maadili yake) kitabu cha Dkt. Muhammad Al-Sadiq Afifiy, chapa ya Kairo maktaba ya Al-khanjii 1977.
- Katika fikra ya Kiislamu kwa upande wa kiadabu, kitabu cha Dk. Muhammad Ahmad Al Azb, chapa ya Kairo: Baraza kuu la utamaduni, toleo la mwaka 1983 uk. 55.

 

Share this:

Related Fatwas