Kumwingilia Kimwili Mke Maiti.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwingilia Kimwili Mke Maiti.

Question

 Imekuwa ikisemwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari Fatwa inayohalalisha kwa mwanaume anapofiwa na mke wake kumwingilia kimwili kabla ya kuoshwa kwake na kuzikwa, na kuzingatia kuwa huu ni mwisho ulio alama ya uhusiano wao, katika upande wa kumpenda na kumuaga. Je. Hukumu hiyo ni sahihi ya kisheria?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Basi kustarehe kwa kumwingilia mke ni haki ya mwanaume kwa kuwa tu wanaendelea kuwa katika uhusiano wa ndoa, na huondoka haki hii kwa kila kinachokata uhusiano wa ndoa na humalizikia kwa kufungwa kwa ndoa. Na umauti ni sababu tosha na ya kimaumbile inayoyakata mahusiano ya ndoa kwa kuwepo kwake hudhihirika haki mpya au huharakishwa haki za muda, kama vile kiwango cha mahari kilichobaki, mirathi, kuhalalika kwa mwanaume kuoa mwanamke wa tano ikiwa mke wake aliyefariki ni wa nne, na uhalali wa kumwoa dada wa marehemu baada ya kuwa haramu katika maisha yake kwa uharamu wa kuwakusanya wote wawili kwa wakati mmoja.
Akasema katika kitabu cha: [Ad-Dur Al-Mukhtaar] Na yeyote atakaemtuhumu mke wake aliye hai tuhuma kubwa ya zina katika nchi ya kiislamu…” Ibn Abdiin anasema katika kitabu chake: [Radu Al-Mehtaar] “Kauli yake: (Mke aliye hai) kwani maiti haiwezi kuuendelea kuwa mke. [484/3, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Na kwa hili, wakati wowote atakapofariki mke huondoka mfungamano na panakawa hakuna tena haki ya mume kujistarehesha na mwili wa mke wake, na kuuzuia mwili wa mke wake kwa wakati mfupi ili aweze kukidhi haja yake kwa mke wake huyo na kumchezea na matamanio yake, haya yote yanaenda kinyume na mila na desturi na maadili mema na yanakatalika kimaadili yaliyo sawa. Kama ambavyo inapingana na Makusudio Makuu ya Sheria ya Kiislamu katika mazingira ya tukio baada ya mauti na yale yanayoambatana nayo miongoni mwa hatua za kumhifadhi maiti na uharakishaji wa kumwandaa kwa kumwosha na kumvika sanda na kumswalia na kumzika na kumhuzunikia kwa kutengana naye na yale yaliyomtokea katika msiba wa kifo, na kupata mawaidha na kuzingatia na kuonyeka kutokana na kujigamba kwa dunia na kutumbukia katika matamanio yake.
Ibn Hajar Al-Haitamiy; mwanazuoni mkuu akataja kuwa: “Mtu kumwingilia mke wake aliyekufa ni haramu, bali ni katika madhambi makubwa”. Akasema katika kitabu cha: [Az-Zawajer 236/2, Ch. Dar Al-Fikr], “Dhambi kubwa ya tatu, ya nne, ya tano, ya sita, ya saba, ya nane, na ya sitini baada ya mia tatu, ni kumwingilia mshirika kwa mtumwa mshirika, na mume kumwingilia mke wake aliyekufa...”
Na katika kitabu cha: [Manhu Aj-Jaliil 246/9, Ch. Dar Al-Fikr], Haadhibiwi adhabu maalumu mtu atakayemwingilia mke wake au kijakazi wake baada ya kufa kwake hata kama ni haramu kufanya hivyo, ndio atashikishwa adabu”.
Na kutokana na yaliyotanguliza: inabainika kutojuzu kuwa mume amwingilie mke wake baada ya umauti wake. Na kwamba kitendo hiki ni haramu na kinastahiki adhabu na mtu kutiwa adamu kwa kwenda kinyume na sheria na kwenda kinyume na maumbile na kupingana na mila na desturi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas