Kuhiji kwa Niaba ya Maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhiji kwa Niaba ya Maiti

Question

Mimi ni Mmisri, ninaishi katika nchi ya Umoja wa Falme za Imarate, na mmoja miongoni mwa jamaa zangu alifariki kabla hajaenda kuhiji, na alikuwa na uwezo wa hali na mali wa kuitekeleza ibada hii ya Hija. Je, ninalazimika kumfanyia ibada hii ya Hija? Na kama ninalazimika kufanya hivyo, Je ni kwa mahali gani pa kuhirimia?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Swali hilo limegawanyika katika sehemu mbili; ya kwanza: kuhiji kwa niaba ya maiti mwenye uwezo wa hali na mali, ya pili: mahali pa Ihramu (Miqati) kwa mtu anayetaka kuhiji badala ya maiti.
Ama sehemu ya kwanza; ni kwamba Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri imetoa Fatwa nyingi katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita. Maana ya fatwa hizo ni: Kwamba anayeweza kuhiji kabla ya umauti wake na akawa hakufanya hivyo, basi lazima ahijiwe kwa mali yake ya mirathi, kwani imepokelewa kwamba mtu mmoja alisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika baba yangu alifariki dunia na hakuhiji, je, mimi ninalazimika kuhiji kwa niaba yake? Mtume S.A.W., akasema: Unaonaje kama baba yako angefariki akiwa anadaiwa, je, wewe utalilipa deni hilo? Mtu huyo akasema: Ndiyo, Mtume S.A.W., akasema: basi deni la Mwenyezi Mungu lina haki zaidi ya kulilipa”. [Hadithi hii imepokelewa na An-Nasaaiy]
Basi Mtume S.A.W, alisema kuwa Hija ni deni lisilofutika kwa mauti, na hukumu yake ni wajibu, na inashurutishwa mtu atakayehiji kwa niaba ya marehemu awe amekwishahiji Hija yake katika Uislamu, kwa Hadithi iliyopokelewa kwamba; “Mtume S.A.W., alimsikia mtu mmoja anasema: (ninaitikia) Labaika kwa niaba ya Shabramah, Mtume S.A.W., akasema: Ni nani Shabramah? Mtu huyo akasema huyo ni kaka yangu -au ndugu yangu- Mtume S.A.W., akasema: je, ulihiji hija yako ya Uislamu? Mtu huyo akasema: Hapana. Mtume S.A.W., akasema: basi hiji Hija yako ya Uislamu halafu hiji kwa niaba ya Shabramah! [Hadithi hii napokelewa na Abu Dawud na Ibn Majah, na ikasahihishwa na Ibn Habaan].
Na kuhusu sehemu ya pili; ni kwamba wanazuoni wa Fiqhi walihitalafiana kuhusu mahali pa kuhirimia (Miqati) kwa mtu ambaye atahiji kwa niaba ya mwingine, je, mahali hapo ni pa marehemu au pa huyo anayehiji badala yake? Basi wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi na Hanmbali wanaona kwamba mahali pa kuhirimia (Miqati) kwa mtu anayehiji kwa niaba ya mtu mwingine ni mahali hapohapo pa mtu anayehiji kwa ajili yake yeye mwenyewe. Basi akitokea Al-Kuufa na akawa anahiji kwa niaba ya mmisri, basi mahali pa kuhirimia (Miqati) yake ni mahali pa watu wa Misri siyo watu wa Iraq. Na wanazuoni wameweka dalili ya hayo kwamba kuhiji ni wajibu juu ya maiti kutoka nchini mwake, basi inawajibika kuhiji kwa niaba yake kutoka katika nchi yake ya asili, kwani kukidhi Hija kunafanywa kama vile kukidhi kwa Swala na Saumu.
Na wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki wanaona kuwa ni vyema wakachunguza mambo hayo; na ikiainishwa kwa mtu anayemuhijia mtu mwingine mahali pa kuhirimia – kama lazima ahiji kutoka nchi maalum - basi analazimika kuhirimia pahali pa kuhirimia pa nchi hiyo husika, hata kama nchi hiyo si nchi yake au nchi ya marehemu, na kama hakuainishiwa mahali maalum, basi lazima afanye kuhirimia kutoka katika nchi ya marehemu kama walivyosema wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi na Hanmbali.
Ama kwa upande wa wanazuoni wa Madhehebu ya Shafi wanatofautisha baina ya Hija ya Uislamu na Hija ya kukariri; na kwa ajili hiyo wakasema kama walivyosema wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi na Hanmbali katika Hija ya Uislamu, na kama wanavyosema wanazuoni wa Maliki katika Hija ya kukariri. Na maelezo yafuatayo kutoka kwa wanazuoni yanalibainisha jambo hilo:
As-Sarkhasiy Al-Hanafiy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Mabsuotw]; “Na kama mtu alikuwa anawajibika kuhiji na akaanza na Umra katika miezi ya kuhiji, kisha akahiji kutoka Makkah basi atazingatiwa kuwa ni mkosa kwa tamko lao wote; kwani analazimika kuhiji kwa niaba ya maiti kutoka mahali pa kuhirimia (Miqati). Na mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha akahiji, basi atahiji kutoka katikati ya Makkah, na hilo litakuwa kinyume cha alivyoamrishwa kutekeleza ibada hiyo. Kwani yeye aliwajibika kutumia fedha za marehemu kwa ajili ya matumizi ya safari ya Hija, lakini akatumia katika safari yake binafisi. Kwani safari yake ilikuwa kwa ajili ya Umra na yeye katika Umra alikuwa akijifanyia mwenyewe ibada hiyo. [156/4, Ch. Dar Al-Fikr]
Ibn Najiim Al Hanafiy amesema katika kitabu cha [Al-Kinz] kwenye tamko la Azulai’iy; “Na ama masharti ya kujuzu kumfanyia mtu ibada ya hija, miongoni mwayo ni kwamba anayefanyiwa ibada hiyo ya Hija lazima awe na upungufu maalumu”. Akasema: “mwanazuoni Mkuu; Sheikh As-Sandiy rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwe juu yake, katika kitabu chake cha: [Al-Mansak Al-Kabiir] “Kwamba miongoni mwa masharti ya kusihi kwa Hija kwa niaba ya mtu mwingine, ni kwamba mtekelezaji wa ibada hiyo afanye kuhirimia mahali pa Miqati, na ikiwa atafanya Umra na alikuwa anatakiwa kufanya ibada ya Hija, kisha akahiji kutoka Makka basi inasihi kutokana na tamko lao wote.” [66/3, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Islamiy]
Na katika sharhul-Kharashiy Al-Malikiy juu ya [Muhtasri wa Kalili]; pamesemwa kwamba: “Kama Miqati ya marehemu, yaani marehemu akiainisha Miqati kwa mtu anayehiji kwa niaba yake, basi hamna neno, na kama marehemu hakuainisha Miqati na akampa uhuru wa kuchagua Miqati basi mtu huyo lazima achague Miqati ya asili ya maiti, yaani Miqati ya maiti aliyokuwa anafanya kuhirimia kwake. Kama vile, mahali pa AJ-Juhfah kwa watu wa Misri, watu wa Magharibi, na watu wa Shamu na mahali pa Yalmam kwa watu wa Yemeni. [90/2, Ch. Dar Al-Fikr]
Na As-Shamsiy Ar-Ramliy wa Madhehebu ya Shafi amesema katika kitabu chake cha: [Nihayatu Al-Muhtaaj]; “Na wasia (unasihi) (kwa kufanya Hija ya kujitolea (kukariri) katika uwazi wake), kutokana na kujuzu hija kwa niaba ya mtu mwingine, na hayo ni maelezo ya uwazi zaidi, (na anahiji akitokea nchi au Miqati yake), au kwa kutokea mahali pengine akiwa mbali zaidi ya Miqati, (kama atafungamanishiwa) na kuufanyia kazi wasia wake, (na kama atauweka wasia katika hali ya kutokuwa na mipaka) (basi iwe kutoka katika Miqati yake) anamhijia mtu (kwa usahihi zaidi) kwa kutegemea kiwango cha chini zaidi cha daraja (na Hoja ya Uislamu) na hata kama hakuiusia basi itazingatiwa kufanyika kama inavyojulikana (ni kutoka katika rasilimali) kama yalivyo madeni yote. (Na akiweka wasia kwake basi iwe kutokana na rasilimali na pamesemwa kutokana na theluthi ya mirathi) na anahiji badala yake (kutoka Miqati) na hiyo ni sahihi zaidi”
Na katika kitabu cha: [Al-Inswaf] kwa Al-Mardaawiy Al-Hanbaliy; “(Na anayewajibika kuhiji na hakuhiji kabla ya kifo chake basi kitatolewa kiasi ya matumizi ya Hija na Umra kutokana na mali yake yote) bila ya upingano na wala hitilafu, hata akiwa aliacha Hija kwa hiari yake au hapana, na ilikuwa kutoka ambapo ilimwajibikia kutokana na usahihi kutoka madhehebu, iliyotajwa kwayo, na jamhuri ya maswahibu wanayokubaliana. [409/3, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy]
Na kutokana na yaliyosemwa hapo juu;, jamaa wa maiti atamfanyia Ibada ya Hija marehemu kwa mali ya urithi aliyoiacha, ni sawa yeye mwenyewe au atampa mtu mwingine jukumu hilo. Na kuhusu sehemu ya kuhirimia mtu anayemfanyia ibada ya hija marehemu, atalazimika kuhirimia katika Miqati ya watu wa Misri, na tunaiona hali ya muulizaji kwamba iwapo hali itakuwa ngumu basi jambo hili ndani yake lina nafasi, atahirimia katika Miqati yake yeye na wala sio Miqati ya marehemu ndugu yake, na Miqati yake ni ile ya watu wa Najdi ambako kwa sasa panaitwa “As-Sail Al-Kabiir”, na katika hali hiyo atalazimika kuchinja kondoo, kwa kutohirimia katika Miqati yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas