Kufanya Kazi Kwenye Mashirika ya Ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufanya Kazi Kwenye Mashirika ya Kimataifa

Question

Hukumu ni nini ya kisheria kwa kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa (Malty National) na ambayo Rasimali yake au sehemu iliyo kubwa inamilikiwa na wasio waislamu na hasa inamilikiwa na mayahudi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Mashirika makubwa ya kimataifa, ambayo pengine yanaitwa mashirika yenye uraia mbalimbali, watu wengi kutoka kila dini na raia wote wanafanya kazi katika mashirika hayo, na kadhalika watu wengi kutoka dini na raia mbalimbali nyingi na wanashirikia rasilimali ya mashirika hayo. Na kitu ambacho kinawakosesha usingizi baadhi ya waislamu na waarabu ni kwamba - baadhi yao kama sio wengi wao - katika wachangiaji kwa fedha zao katika mashirika haya, ni mayahudi. Je inajuzu kushirikiana nao kama dini maalumu katika wakati huu ambapo mayahudi wanayashikilia kwa nguvu baadhi ya maeneo matakatifu ya Waislamu na kuna uwezekano wakawasaidia waporaji wa mali hizi wanazozipata kutokana na faida ya mashirika hayo.
Na anayetazama kiuhalisi, anaona kwamba mayahudi sio wote wanayashilia kwa nguvu baadhi ya maeneo matakatifu, na baadhi yao wanakaa katika nchi nyingine nje ya ardhi zinazoshikiliwa kwa nguvu, bali baadhi yao wanaharamisha kwenda Palestina na wanaona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatoa mayahudi kutoka Palestina, na hawajuzu kwao kurudi tena. na baadhi yao wanaona kuwa Mayahudi hata wakirejea huko haijuzu kwao wao kuwa ndio viongozi wa nchi hiyo kisha Israel ina baadhi ya mikataba na mataifa ya kiarabu na Waislamu, na wangelikuwa hawa ni wapiganaji vita basi wangelikuwa na hukumu yao pia kisheria.
Na muhtasari wa kauli hapa kwamba Mayahudi sio wote maadui, nao pengine wenye dhima au wenye ahadi, na penginie wapiganaji.
Na hukumu katika suala hilo ni yenye mifumo kadhaa; basi tukizingatia kuwa ipo namna maalumu ya ushiriki, basi utakuwa baina ya muislamu na wasio waislamu, na la asili katika hilo ni kujuzu, na hilo tulibainisha katika Fatwa nyingine.
Na pengine mfanyakazi kule ni muajiriwa wao, na hayo pia, asili yake ni uhalali, na maswahaba wa Mtume S.A.W. walifanya hayo Madina, na Mtume S.A.W. alikubali katika kazi hiyo.
Ama dalili ya kujuzu kutoka mwenye ahadi; basi ni iliyotolewa na Ibn Asaker kutoka kwa Ibn Abbas R.A., alisema: “Mtume S.A.W alipatwa na ukata (shida katika chakula), na habari hii ikamfikia Ali R.A, akatoka kutafuta kazi itakayomwingizia kitu ili kwa kazi hiyo akamwombe Mtume S.A.W, akaenda kwenye bustani ya mtu mmoja ambaye ni myahudi akamchotea ndoo kumi na saba za maji kwa kulipwa kila ndoo moja tende moja, na myahudi huyo akampa chaguo la tende, naye akachagua tende mbivu kumi na saba, na Ali akaja nazo kwa Mtume S.A.W na Mtume akamuuliza: umezipata wapi tende hizi ewe baba Hassan? Nilifikiwa na habari za ukata wako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nikaamua kutoka kwa ajili ya kutafuta kazi ili nikutafutie chakula. Akasema Mtume: umeyafanya hayo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake? Akajibu Ali na kusema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu”.
Na At-Twabarniy akatoa katika kitabu cha: [Al-Awsatw] kutoka kwa Kaab Bin Ujraha R.A., akasema: “Nilimjia Mtume S.A.W, nikamkuta akiwa amebadikika, nikamwambia: Ewe kwa baba yangu wewe, mbona ninakuona ukiwa umebadilika hivyo? Akasema: Hakuna kitu chochote kilichoingia tumboni mwangu katika vinavyoingia tumboni mwa mtu mwenye ini (aliye hai) kwa muda wa siku tatu. Akasema: nikaenda hadi nikamkuta myahudi akizinywesha maji ngamia zake nikamsaidia kuzinywesha ngamia hizo, kwa malipo ya kila ndoo moja tende moja, kisha nikamletea Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, S.A.W. Akasema Mtume: Ewe Kaab, umezitoa wapi hizi tende? Nikamwambia nilikozitoa. Akaniambia: Hivi kweli unanipenda ewe Kaab? Akasema Kaab: Ninaapa kwa kweli, ndio ninakupenda sana”. Na Isnadi yake ni nzuri kama ilivyokuwa katika katibu cha: [At-Targhiib], na kitabu cha: [Majma’ Al-Fawa’ed] Na kama tulivyosema wanazuoni wengi walitaja.
Ibn Qodamah akasema: “Na hakuna ubaya wowote wa yeye kujipatia ajira kwa mtu wa Dhimiy (myahudi au Mkristo aliye chini ya himaya ya dola la Kiisamu) maandiko yameelezea; kwani Ali R.A., aliajiriwa na yahudi, amnyweshe kila ndoo kwa tende moja, na alimwambia Mtume S.A.W., na Mtume S.A.W., hakuikana na akala kutokana na ujira wake. Na wala hajitafutii ajira kwa Mkristo au myahudi, kwani kufanya hivyo kuna ndani yake kujidhalilisha kwa Muislamu na kuwa chini ya kafiri na kwa ajili hiyo haijuzu kama vile kumuuzia, na panatokea kujuzu kwani yeye amempa kitu mbadala kwa huduma aliyoitoa na kwa ajili hiyo ikajuzu, kama vile kumkodisha kwa ajili ya kumfanyia kazi maalumu. [Al-Kaafiy 172/2, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Ama kwa upande wa kauli yake kuwa wao wanajipatia faida nyingi kutokana na hali hiyo, Jawabu ni kuwa Waislamu pia wanajipatia mali kwa ajili ya kazi waifanyayo, kama ambavyo wanaweza kujipatia manufaa kama vile petroli inayochimbwa na baadhi ya mashirika hayo. Kwa hiyo, biashara pamoja na watu wa wapiganaji inajuzu kwani ina manufaa kwa sisi Waislamu, na manufaa hayo ni mengi na mbalimbali, pamoja na wao walikuwa wakipata manufaa pia. Na miongoni mwa dalili ya kujuzu hayo ni kuwa ilitajwa katika vitabu viwili sahihi, katika kisa cha Uislamu wa Thumamah Bin Athaal, mkuu wa watu wa Yamamah aliposilimu, na katika kisa hicho: “Basi Mtume S.A.W., alimbashiria, na akamwamrisha kufanya Umra, basi alipofika Makka; mtu mmoja akamwambia: je, umeacha dini yako? Basi, akasema: Hapana. Lakini nimesilimu pamoja na Mtume S.A.W.. Na hapana Wallahi! Haitawapateni chembe moja ya nafaka kutoka Yamamah isipokuwa Mtume Wa Mwenyezi Mungu atoe idhini.
Na Ibn Hayaan ametoa pia, na alisema: “Katika habari hiyo ni dalili ya kuhalalisha biashara kwa nyumba za vita kwa watu bora”. Na iliyoelezea ilitajwa na Ibn Hayaan usimulizi wa Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Ad-Dalail] na katika usimulizi huo: “Basi wakamkasirisha na akasema: Hakika mimi, na Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika mimi sikuacha dini, Bali nilisilimu, na nimemwamini Mtume Muhammad na nimeyaamini aliyokuja nayo, na Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Thumama iko mikononi mwake haikujieni chembe moja ya nafaka kutoka Al-Yamamah -na wakati huo Al-Yamamah ilikuwa ni maeneo ya mashambani mwa Makkah- sikubakia hapo mpaka Mtume Muhammad S.A.W alipotoa ruhusa, akaondoka na kuelekea nchini mwake. Na akazuia shehena za chakula kuelekea Makkah mpaka makuraishi walipohangaika wakamwandikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wakimwomba kuhusu koo zao, ili Mtume amwandikie Thumamah ili airuhusu mizigo ya chakula, naye akafanya hivyo”.
Na dalili iliyopo hapa ni amri ya Mtume S.A.W kwa Thumamah ikimtaka apeleke chakula Makkah, nao wakiwa ni wagomvi wake kwa wakati huo. Na tulivyosema wakasema wanazuoni wengi kama yafuatayo:
Al-Kassaiy akasema: “Na ama kubainika yalio yaliyo karaha kuchukua kwenda nchi ya uadui, na yasiyo yenye karaha, basi tunasema: “Mfanyabiashara hatakiwi kupeleka msaada kwenye nchi ya adui watakaoutumia maadui hao kivita, kama vile silaha, farasi, watumwa ambao ni katika watu wa dhima (walio chini ya ulinzi wa Waislamu) na kila kinachoweza kutumiwa kivita; kwani kufanya hivyo ni kuwapelekea na kuwasaidia kupigana vita dhidi ya Waislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema: {Wala msisaidiane katika dhambi nauadui} [AL MAIDAH 2].
Haiwezekani kwa shehena, na vilevile adui anapoingia nchi ya Kiislamu hawezi kamwe kununua silaha na kama atanunua silaha basi hawezi kuziingiza katika nchi ya adui wa Waislamu kwa sababu tulizozisema: na hakuna ubaya wowote wa kubeba shehena za nguo, mizigo ya kawaida na chakula na mfano wa vitu hivyo na kuwapelekea; kwa kutobeba maana ya kusaidia kivita na kuwaokoa.
Na kwa utaratibu huu, imezoeleka kwa wafanyabiashara wa migogoro kwamba wao wanaingia katika nchi ya adui kibiashara bila ya kudhihirika kuwarudi au kuwakana; isipokuwa kuacha ni bora zaidi; kwani wao wanawadharau waislamu na kuwalingania wayafuate waliyonayo kwa hiyo kuzuia na kutoruhusu kuingia ni bora zaidi kwa ajili ya kuzilinda nafsi zao na kuziweka mbali na uzembe, na kuilinda dini isitoweke, kwa hiyo hivyo imekuwa bora zaidi. [Bada’I Aswana’i fi Tartib Ashara’i 102/7, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
As-Sarkhasiy akasema: “Naye anaweza kutoa atakacho, isipokuwa shehena, kama tulivyotaja, kama ambavyo mfanyabiashara wa Kiislamu anaweza kuwapelekea bidhaa zozote atakazo kwa ajili ya biashara yake”. Na Ashafiy –rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake- ana kauli: “Kwamba yeye anazuia kufanya hivyo pia kwa kuwa wao wanaendelea kuongeza nguvu zao kwa kubeba chakula au nguo au silaha, lakini sisi tunatoa dalili kwa yaliyopokelewa”.
Lakini tunaweka kutoa dalili kwa ilipokelewa; kwamba Mtume S.A.W., alitoa zawadi kwa Ibi Sufian R.A., tende mbivu alipokuwa Makkah kama adui, na akampa kitoweo, na akawapelekea watu wa Makkah dinari mia tano pindi walipokumbwa na janga la ukame na hivyo kutofautisha baina ya wenye kuhitaji miongoni mwao na kwa kuwa baadhi ya wanavyovihitaji Waislamu ni katika madawa na vinginevyo vinaletwa kutoka katika nchi za adui tukiwazuia wafanyabiashara wa Kiislamu wasiwapelekee bidhaa zisizokuwa silaha na wao pia watazuia hivyo na katika hili kuna madhara yasiyojificha. [Al-Mabsuot kwa As-Sarkhasiy 91/10, Ch. Dar Al-Maarifa]
Na kiakili tu, ni kwamba yaliyotangulia yanafungamana na kutokuwepo madhara kwa Waislamu yanayotokana na kazi hiyo, na kama si hivyo basi hukumu yake itakuwa tofauti.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia: basi hakika kufanya kazi katika mashirika kama hayo ya kimataifa yenye raia mbalimbali ni jambo linajuzu kisheria, ikiwa kazi hiyo haifungamani na kuwepo madhara kwa Waislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
 

Share this:

Related Fatwas