Kuupangusa Uso kwa Mikono Miwili Ba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuupangusa Uso kwa Mikono Miwili Baada ya Dua katika Swala na Katika Ibada Nyingine

Question

 Ni ipi hukumu ya mwanadamu huupangusa uso wake kwa mikono miwili Baada ya dua?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Maana ya kupungusa (kufuta) katika lugha ni: kufuta au kupaka na pia ni kupitisha mkono katika kitu au juu yake. [Kamusi ya Maqayeyes Al Lughah kwa Ibn Fafes 32/5 kidahizo cha Ma-sa-ha, Ch. Dar Al Fikr]. Ikisemwa kwamba mtu amepaka kitu kwa maji au mafuta, maana yake amepitisha mkono wake katika kitu ukiwa umekunjuliwa. Na dua ni njia nzuri zaidi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huonesha ukweli wa kumwelekea na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na katika dua kuna kuuelezea ufukara na unyonge wa mja, pamoja na kuzitambua nguvu na uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya kila kitu.
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, aliita Ibada. Basi Abu Dawud ametoa katika Sunna yake, na At Termizi na akaisahahisha, Na Ahmad, Abu Hayaan na Al Hakem na wakaisahahisha kutoka kwa An Nu'maan Bin Basher R.A. anasema: Mtume S.A.W. amesema: "Dua ni Ibada", kisha akaisoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike}[GHAFIR 60].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamurisha dua na akaisisitizia, kama ilivyotajwa katika Qur'ani tukufu: {Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.} [AN NISAA 32], na Anasema: {Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangechukia makafiri.} [GHAFIR 14], na Akasema: {.Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka (55). Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema}. [AL- AARAF 55-56]
Na Mtume S.A.W., akatutahadharishia kutokana na kutoomba na kumtaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, Basi Al Bukhari ametoa katika kitabu cha: [Al Adab Al Mufrad] na At Termidhi na wengineo katika kitabu cha: [Ak Mustadrak] kwa Al Hakim na akasahihisha isnadi yake kutoka kwa Abi Hurairah akasema: Mtume S.A.W, amesema: "Mtu yeyote asiyemwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Basi atamghadhibikia"
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hamrejeshi mja wake anaponyanyua mikono yake kwa upole, kutaka kujibiwa na unyenyekevu isipokuwa humkidhia haja yake hiyo. Na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amembariki mja wake mwenye haja pale anapozidisha maombi katika haja hiyo. Humpa au humnyima. Basi Ahmad na Al Hakim wakatoa na wakaisahihisha kutoka kwa Abu Said kutoka kwa Mtume S.A.W, Hakuna Muislamu yeyote atakayemwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua ambayo haina ndani yake kosa lolote au uvunjaji wa undugu isipokuwa humpa kwa dua hiyo moja kati ya mambo matatu: anaweza kumharakishia maombi yake, au akamcheleweshea hadi Siku ya Malipo, au akamwepushia mbali ubaya Mfano wake.
Maimamu na wanazuoni wa fiqhi wameeleza kuwa kupangusa uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza dua ni Sunna; ikasemwa: na ni kama vile mnasaba uliopo hapo kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa hairejeshi mikono hiyo mitupu, kwa hiyo ni kama vile rehema zake zimeishukia kwa wingi na jambo hili likanasibiana na kuzipeleka rehema hizo usoni, ambapo hicho ni kiungo kitukufu kuliko vyote na chenye haki zaidi ya ya kutukuzwa. [Subul AS Salam kwa AS Swana'aniy 707/2 , Ch. Dar Al Hadeeth]
Imetajwa katika kitabu cha: [Hashiyat As Sarnibaliy Ala Duwar Al Hukaam] miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Imamu Hanafi; mlango wa (sifa za Swala), katika kutaja dua zilizotaja katika Sunna baada ya Swala kwa kila anayeswalia, na inapendezwa kwa anayeswali kuzitaja kisha anahitimu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Subhaana Rabbika}, kwa kauli ya Aliy R.A: Na atakayetaka kupima kwa kutumia vipimo bora zaidi cha malipo ya Siku ya Malipo basi maneno yake ya mwisho pale anaposimama alipokaa yawe (Subhaana Rabbika) na kisha apanguse uso wake kwa mikono yake miwili mwishoni. Kwa kauli ya Ibn Abbas R.A., kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Pindi unapomwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mwombe kwa matumbo ya mikono yako na wala usiombe kwa migongo ya mikono, na utakapomaliza basi ipangusie usoni mwako". Ilitolewa na Ibn Majah kama katika kitabu cha: Al Burhaan". [Hashiyat As Sarnibaliy Ala Duwar Al Hukaam 80/1, Ch. Dar Ihiyaa At Turaath Al Arabiy]
Na An Nafrawiy anasema katika kitabu cha: [Al Fawakeh Ad Dawaiy] miongoni vitabu vya Madhehebu ya Imamu Maliki: "Na inapendeza kuupangusa uso wake mtu kwa mikono yake mwishoni mwa Dua, kama alivyofanya Mtume S.A.W." [Al Fawakeh Ad Dawaiy kwa An Nafrawiy 335/2, Ch. Dar Al Fikr]
Imamu An Nawawiy kutoka wanazuoni wa Kishafi ametaja miongoni mwa jumla ya adabu za dua ni kuupangusa uso baada ya dua katika mlango wa matajo ya kupendeza katika kitabu cha: [Al Majmuo'], basi akasema: "Na miongoni mwa adabu za kuomba dua ni katika nyakati na sehemu na mazingira masafi na mazuri na kuelekea Kibla na kunyanyua mikono na moja kuupangusa uso wake baada ya kumaliza kuomba dua na kushusha sauti iwe kati ya sauti ya juu na ya, chini." [Al Majmuo' kwa An Nawawiy 487/4, Ch. Dar Al Fikr].
Imamu An Nawawiy alisema kitamko cha mwisho katika kitabu cha: [At Tahqiq] kwamba kuupangusa uso baada ya dua ni Sunna (Mandubu) na pia Sheikh wa Uislamu Zakariya Al Answariy alinukuu kutoka katika kitabu cha: [Isniy Al Matwaleb 160/1, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]. Na Al Khatwiib As Sherbiniy katika kitabu cha: [Mughniy Al Muhtaaj 370/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Al Bahutiy; Mwanazuoni Mkuu wa Kihanbali alisema: "(Kisha anaupangusa uso wake kwa mikono yake hapa), yaani: baada ya kunuti, na (nje ya Swala) akiomba dua". [Sharhu Muntaha Al Iradat 241/1, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah, na tazama pamoja nacho: kitabu cha Al Iswaf 173/2, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy, na kitabu cha: Kashaaf Al Qinaa' 420/1, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]
Na dalili ya hayo yaliyotajwa kutoka kwa Mtume S.A.W, kwamba alikuwa akiupangusa uso wake kwa mikono yake baada ya dua. Basi Imamu Tirmidhi na Al Hakim wakaitoa Hadithi hii kutoka kwa Omar R.A. akasema: "Mtume S.A.W alikuwa anapoikunjua mikono yake kwa ajili ya dua alikuwa hairejeshi isipokuwa baada ya kuipangusa usoni mwake".
Hafidh Ibn Hajar akasema katika kitabu cha: [Bulughul-Maraami Uk. 464, Ch. Dar Al Falaq-Ar Reyaadh]: "Imetolewa na Tirmidhi, na yana dalili, na miongoni mwake ni Hadithi ya Ibn Abbas kwa Abu Dawud na wengineo, na jumla yake yanahukumu kwamba ni Hadithi hassan". As Swana'niy alisema katika kitabu cha; [Subel As Salaam709/2, Ch. Dar Al Hadith], "Ina dalili juu ya usheria wa kupangusa uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza dua".
Na pia inaombwa dalili kwa Hadithi iliyotolewa na Abu Dawud, Ibn Majah, Al Hakim na Al Baihaqiy katika kitabu cha: [Al Fatawa Al Kubra], kutoka kwa Ibn Abbas R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W., alisema: "Mwombeni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa matumbo ya mikono yenu na wala msimwombe kwa migongo yake, na mtakapomaliza kuomba basi panguseni nyuso zenu".
Na As Suyutwiy amenukulu kutoka kwa Sheikh wa Uislamu Abi Al Fadhl Bin Hajar katika kitabu cha [Al Amaal] kitamko chake katika Hadithi: "Hadithi hiyo ni Hadithi hassan". [Tazama: Fadhu Al Wa'aa kwa As Siyuti, Uk. 74, Ch. Maktabat Al Manaar- Jurdian] Na inatajwa katika kitabu cha: [Sunan Abu Dawud na Musnad Ahmad] kutoka kwa Yaziid Bin Said Bin Thumamah kwamba Mtume S.A.W., alikuwa akiomba dua akainua mikono yake kisha akaupungusa uso wake kwa mikono yake.
Na miongoni mwa yaliyopokelewa kutoka kwa Maswahaba Mwenyezi Mungu Mtukufu awe radhi juu yao wote, katika kuupungusa uso kwa mikono yake miwili, baada ya kuiinua kwake kwa kuomba dua, iliyotolewa na Al Bukhariy katika kitabu cha: [Al Adab Al Mufrad] mlango wa "Kuinua mikono katika kuomba dua", katika tendo la Ibn Omar na Ibn Az Zubeir katika kuupungusa uso kwa mikono miwili baada ya kuomba dua, basi akasema: "Ibrahim Bin Al Mundhir alituzungumzia na akasema: Muhammad Bin Feleh akatuzungumzia: akasema: Baba yangu aliniambia kutoka kwa Nu'ayen na yeye ni Wahb akasema: "Nimewaona Omar na Bin Zubeir wakiomba dua huku wakivipaka viganja vyao kwa kuvizungusha usoni". [Imepokelewa na Al Bukhari katika kitabu cha Al Adab Al Mufrad 214/1]
Na As Suyutwiy akanukulu katika kitabu cha: [Fadhu Al Wa'aa Uk. 101], kutoka kwa Al Hassan Al Basweriy kitendo chake kwa kuupungusa uso wake kwa mikono yake baada ya kuomba dua: "Al Firiyaniy akasema: Ishaq Bin Rahawiyh akatuzungumzia, akasema: Al Mu'tamer Bin Sulaiman alituambia: akasema: nilimwona Abuu Ka'ab Bin –Swaheb Al Harer- anaomba dua akiinua mikono yake, na anapomaliza hupangusa uso wake kwa mikono yake, basi nilimwambia ulimwona nani anafanya hivyo? Akasema: Al Hassan Bin Abi Al Hassan. Isnaadi hassan".
Ama kwa upande wa kupakaa mikono miwili usoni baada ya dua baada ya kumaliza Dua ya kunuti katika swala ya Faradhi huu ni mtazamo wa Madhehebu ya Shafi, ameusema Kadhi Abi At Tweyib, na sheikh Abu Muhammad Aj Juweniy, na Ibn As Swabaagh, Al Metwaliy, Ghazali, na Al Emraniy mtunzi wa kitabu cha: [Al Bayaan], [Tazama kitabu cha Al Majmua. Kutoka Kwa An Nawawiy 500-501/3]. Nayo ndio inayotegemewa katika madhehebu ya Imamu Ahmad kama ilivyonukuliwa hapo mwanzo kutoka kwa mwanachuoni mkubwa Al Bahuutiy kama ilivyotangulia kuelezwa.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia: iwapo mtu atafuta uso wake kwa mikono yake miwili baada ya dua itajuzu, bali hiyo ni miongoni mwa jumla ya adabu ya kuomba dua ambayo wanazuoni walizitaja katika vitabu vyao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas