1- Kugusa Jiwe Jeusi au Kaaba kwa M...

Egypt's Dar Al-Ifta

1- Kugusa Jiwe Jeusi au Kaaba kwa Mwenye Kuhirimia Atakapoona Juu yake Kuna Athari ya Manukato.

Question

 Je, inajuzu kwa mwemye kuhirimia kugusa Jiwe Jeusi au Kaaba atakapoona juu yake kuna athari ya manukato?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Hakika kugusa Jiwe Jeusi katika kila mzunguko wa kutufu ni Sunna kwa mwenye kuhirimia; na Imamu Bukhari na Muslim wamepokea kutoka katika Hadithi ya Abdullahi Ibn Umar kuwa: “Mtume S.A.W, alikuwa hagusi kitu isipokuwa Jiwe Jeusi na Nguzo ya Yemeni”.
Na Imamu Muslim amepokea kutoka kwa Nafii’ na Ibn Umar kuwa yeye alisema: “Sikuacha kugusa Nguzo hizi Mbili: Nguzo ya Yemeni na Jiwe, katika nyakati zote, tangu nilipomuona Mtume S.A.W, akizigusa”.
Na wakati wa kushindwa kugusa kwa mkono, anaweza kugusa kwa kitu kilichopo mkononi mwake, na kama hataweza kugusa kwa vyovyote basi ataashiria juu yake pamoja na kusema takbiri; kwa Hadithi ya Ibn Abbas akisema: “Mtume S.A.W, alitufu akiwa amepanda ngamia, na kila alipoifikia Nguzo ya Yemeni aliiashiria na kusema takbiri”. [Ameipokea Bukhari].
Abul Hasan katika Sharhu Ar-Risalah anasema: “miongoni mwa Sunna za tawafu ni kuligusa Jiwe Jeusi, mwanzoni mwa tawafu, kama tulivyotaja, na inatakiwa kuligusa Jiwe jeusi kwenye kila mzunguko isipokuwa wa kwanza, nayo ni Sunna. Na ataligusa Jiwe kila atakapo lipitia, kama tulivyotaja hapo awali, na ataligusa kwa mdomo wake iwezekanavyo, au ataweka mkono juu yake kisha kuuwekea mdomo wake bila ya kubusu”. [Hashiyat Al-A’dawiy Ala Kifayat At-Talib Ar-Rabaniy; 1/532, Ch. Dar Al-Fikr].
Sheikh wa Uislamu Zakariya Al-Ansariy mfuasi wa madhehebu ya Shafiy anasema: “Miongoni mwa Sunna kuligusa Jiwe Jeusi kwa mkono wake mwanzoni mwa tawafu yake, kisha atalibusu, [wameipokea Maimamu wawili], na kutokana na msongamano unaozuia kulibusu na kusujudu kwake, ataligusa kwa mkono wake, akishindwa ataligusa kwa kitu kama fimbo, kisha atakibusu kitu hicho. Yaani atabusu kilichogusa, kwa Hadithi iliyopokelewa katika Vitabu Viwili Sahihi: “Kama nitakuamuruni kitu, basi itekelezeni iwezekanavyo”, na kwa Hadithi ya Muslim kuwa: Ibn Umar aliligusa, kisha akabusu mkono wake, na akasema; sikuacha hivyo tangu nilipomwoma Mtume S.A.W, akiifanya. Na kama atashindwa kuligusa, ataashiria juu yake kwa mkono. Na katika kitabu cha: [Al-Majmuu] na mengineyo anasema: au kwa kitu kilichopo mkononi mwake, kisha atabusu kitu hicho alichokiashiria, kwa Hadithi ya Bukhari kuwa: “Mtume S.A.W, alitufu akipanda ngamia, na kila alipokuja Nguzo akiashiria juu yake kwa kitu alichokuwa nacho na kusema takbiri”. [Asna Al-Matalib Sharh Rawdh At-Talib; 1/480, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Islamiy].
Hivyo kuigusa Kaaba huenda kwa ajili ya kupata baraka, kushikilia nguo za Kaaba kwa ajili ya dua, au kushikilia Al-Multazam: (ni mahali kati ya Jiwe Jeusi na mlango wa Kaaba), ambapo Sunna inahimiza kuambatana nayo, na mambo kama hayo ni fadhila inayotakiwa; kwa ilivyopokelewa na Amr Ibn Shua’ib, kutoka kwa babake, alisema: Nilitufu pamoja na Abdullahi, tulipokuwa nyuma ya Kaaba, nikamwambia kwa kusema: Je, ujikinge? Akasema: Najikinga kwa Mola na moto, kisha akaenda kugusa Jiwe, akasimama kati ya Nguzo na Mlango, akaziwekea kifua, uso, mikono na vitanga hivyo hivyo, akazitandaza sana, kisha akasema: hivyo hivyo nilimwona Mtume S.A.W, akizifanya. [Ameipokea Abu Dawud].
Na Abdur-Razaaq amepokea kutoka kwa Maa’mar, akisema: nilimwona Ayuub akiambatisha kifua chake na mikono yake kwa Nyumba. Na kutoka kwake, na Hisham Ibn Urwah, na babake kuwa: alikuwa akiambatisha kifua chake na mkono wake na tumbo lake kwa Kaaba.
Na mtu kati ya Waarabu kabla ya Uislamu alikuwa akitaka kujikinga, huingia kwenye Kaaba, na kushikilia nguo zake, na kutoka kwa Musa’ab Ibn saad, na babake akisema; katika siku ya kufungua Makkah, Mtume S.A.W, alitoa ahadi ya amani kwa watu wote isipokuwa wanaume wanne na wanawake wawili, akisema: “Wauweni hata mtawakuta wakishikilia nguo za Kaaba, na hawa ni: Ikrima Ibn Abi Jahl, Abdullahi Ibn Khatal, Maqiis Ibn Sababah, na Abdullahi Ibn Saad Ibn Abi Sarh”. [Ameipokea An-Nasaiy na Abu Dawud]. Na hii ni dalili kuwa kuzishikilia nguo za Kaaba ni jambo linalojulikana wakati wa Ujahili na wakati wa Uislamu.
Na kujitia manukato kwa shabaha ya kujipodoa kwa mwenye kuhirimia ni haramu, kwa sababu mwenye kuhirimia anakatazwa kutumia manukato katika mwili, nguo, kitanda, na kiatu chake, hata kama tayabandika manukato hayo katika kiatu chake analazimika kuiepusha; hivyo hafunikwi kwa nguo yenye manukato au mafuta yenye harufu; vile vile hachukui manukato yanayonukia. Maimamu Bukhari na Muslim wamepokea kutoka kwa Abdullahi Ibn Umar R.A, akisema: mtu alisimama akisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini amri yako kuhusu mavazi yetu hali ya kuhirimia? Na Mtume SAW, alisema: “Msivae kanzu wala suruali wala kofia wala joho, na kama mtu asipokuwa na viatu basi achukue Hofu (viatu vya ngozi tu kwa ajili ya baridi) na avikate chini ya vifundo viwili, na msivae kitu chenye manukato”.
Mtungaji wa Al-Mughniy anasema” (hatumii mafuta ya kujipaka yenye manukato au yasiyokuwa na manukato). [Al-Mughniy 3/300, Ch. Al-Kitaab Al-Arabiy].
Ar-Ruhaibaniy mfuasi wa madhehebu ya Hanbali anasema: “Ni haaramu kutumia kwa makusudi manukato, kuyagusa au kuyanusa, kwa kauli ya pamoja ya Wanachuoni; kwa Hadithi ya Mtume: “wala nguo yenye manukato”, na Ya’la Ibn Umaiyah alimuamuru kuondosha manukato; na kauli yake kuhusu mwenye kuhirimia ambaye ameangushwa chini na ngamia wake” “msimpulizie manukato”. [muttafaq], na tamko la Muslim: “msigusishe manukato”, kwa hiyo mwenye kuhirimia atakapojipulizia manukato katika nguo yake au mwili wake au kitu kati ya viwili hivyo basi ni haramu na atalazimika kutoa fidia”. [Matalib Ulin-Nuhaa Fi Sharh Ghayat Al-Muntahaa: 2/332, Ch. Ya Beirut].
Kuhusu manukato ya Kaaba, mwenye kuhirimia akitaka kupata baraka, basi inajuzu, hata akinusa manukato au kupata harufu yake; kwa sababu harufu inatokana kwa ujirani. Na kama akiweka mkono wake juu ya Kaaba na anadhani kuwa hakuna manukato au anadhani kuwa manukato makavu, kisha ikabainika kuwa majimaji na kuambatisha mkono wake basi hakuna kitu juu yake, na aiondoshe, lakini atakapokusudia hivyo atalazimika kutoa fidia, na hii ni katika madhehebu ya Shafi, katika madhehebu mpya, kama ilivyotajwa katika [Al-hawiy na Al-Mawardiy; 4/113, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Katika hali ya ugumu wa kuiondosha kutokana na msongomano na mengineyo, basi anaweza kuifuata madhehebu ya Malik yenye rai ya kutolazimika kuiondosha hali ya kuwa si nyingi; na hii ni dharura, ambapo tunatakiwa kukaribiana na Kaaba, wakati haiepushwi na manukato siku zote, kama ilivyotajwa katika [Ash-Sharh As-Swaghiir na Hashiyat As-Sawiy; 2/87, Ch. Dar Al-Maa’arif].
Kama inavyojuzu, kwa vyovyote, kugusa vilivyowekwa juu ya Kaaba miongoni mwa visafishiaji vinavyoua vjidudu, ambavyo haikusudiwi harufu yake kwa jumla.
Na kwa mujibu wa yaliyotangulia jibu la swali lililoulizwa limefahamika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

Share this:

Related Fatwas