Ujenzi na Makazi Juu na Chini ya Ms...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ujenzi na Makazi Juu na Chini ya Msikiti.

Question

 Je, inafaa kujenga na kufanya makazi juu ya jengo la msikiti na chini ya msikiti?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Wamekubaliana wanachuoni juu ya ulazima wa kutukuzwa misikiti na kufanyiwa matengenezo, wakaelezea nidhamu ya kuingia misikitini na kukaa humo pamoja na kuhusisha sifa mbalimbali tofauti na majumba mengine ya makazi ya wanadamu kwa kuzingatia kuwa misikiti ni alama ya Mwenyezi Mungu, na kuitukuza ni katika kumtukuza Mwenyezi Mungu, hata hivyo wanachuoni wetu Mwenyezi Mungu Awarehemu wametenga eneo la juu ya jengo la msikiti na sahani ya msikiti hukumu ya msikiti kwa upande wa ulazima wa kuzifanyia matengenezo na kuheshimu utakatifu wake.
Amesema An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmu]: “Kuta za msikiti kwa ndani na nje zinachukuliwa kuwa ni sehemu ya msikiti katika ulazima wa kuzifanyia matengenezo na kuutukuza utakatifu wake, na vile vile sehemu za juu ya msikiti na kisima cha maji kilichomo ndani yake, na pia sahani yake” [2/178 chapa ya Dar Al-Fikr].
Na amesema Ibn Qudama katika kitabu cha Al-Mughniy: “Inafaa kwa mwenye kukaa itikafu kupanda eneo la juu ya msikiti, kwa sababu ni katika jumla ya msikiti, na kwa sababu hii anazuiliwa mwenye janaba kuchafua maeneo hayo, na hii pia ni kauli ya Abi Hanifa, Malik na Shafiy, wala hatufahamu tofauti” [3/196 chapa ya Maktabat Al-Kahera].
Masuala ya kujenga juu ya msikiti au kujenga chini ya msikiti ni katika masuala yenye mitazamo tofauti, ambapo baadhi ya wafuasi wa Imamu Abu Hanifa wao wanaona kuwa inafaa kujenga juu ya msikiti ikiwa ujenzi huo ni kwa masilahi ya msikiti kama vile nyumba ya Imamu kwa mfano, katika kitabu cha Hidaya: “Na mwenye kujenga kijumba chini ya msikiti, au juu ya msikiti akajenga nyumba na kuuweka mlango wa misikiti upande wa barabarani, na akajitenga na haki miliki ya msikiti, basi anaweza kuuza hiyo nyumba, na ikiwa atafariki, basi anarithiwa, kwa sababu hakuhusisha nia yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kubakia haki ya mja ifungamane na Mwenyezi Mungu, na lau itakuwa ujenzi huo kwa masilahi ya msikiti basi inafaa kama vile ilivyo kwenye msikiti wa Baytul Maqdis. Na imepokelewa na Al-Hassan amesema: “Ikiwa sehemu ya chini ya msikiti na ile ya kawaida itafanywa kuwa makazi, basi makazi hayo ni msikiti, kwa sababu msikiti ni wenye kudumu hivyo na kwa hivyo basi hufikiwa lengo la msikiti kwa sehemu ya chini tofauti na ile ya juu. Na kutoka kwa Muhammad Mwenyezi Mungu Amrehemu amesema kinyume na hivvyo, kwa sababu msikiti ni sehemu yenye kutukuzwa. Ikiwa sehemu ya juu ya msikiti ina makazi au inatumika, basi kuna ugumu wa kutukuzwa kwake.
Na kutoka kwa Abi Yusuf Mungu Amrehemu yeye ameruhusu kwa sura mbili pindi alipofika Baghdad na kukuta kuna tabu ya makazi, akazingatia kama ni jambo la dharura. Kutoka kwa Muhammad Mungu Amrehemu pindi alipoingia Rai alipitisha hayo yote tuliyoyasema, na vile vile pindi anapoamua kuifanya sehemu ya kati ya nyumba yake kuwa ni msikiti na watu wakalinganiwa kuingia eneo hilo kwa ajili ya ibada, basi ana haki ya kupauza na kurithiwa, kwa sababu msikiti ni ule usiomilikiwa na mtu yeyote. Ikiwa eneo lake limezungukwa pembezoni mwake na msikiti atakuwa na haki ya kuzuia na wala huo hautokuwa msikiti, ni kwa vile umebakia kuwa ni wa kwake na wala hajatakasa nia yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kutoka kwa Muhammad anasema kuwa hapawezi kuuzwa, kurithiwa wala kutolewa zawadi, na hivyo hivyo amesema Abi Yussuf Mungu Amrehemu kuwa patakuwa ni msikiti” [6/234 maneno ya pembeni ya ufafanuzi wake ndani ya kitabu cha: Fat’hul Qadir, chapa ya Dar Al-Fikr].
Na kwa hivyo basi, mtu yeyote mwenye nyumba na akaifanya sehemu ya juu ya nyumba yake kuwa msikiti au chini ya nyumba yake au akafanya kati kati ya nyumba yake au akawa amejenga kijumba kidogo - nayo ni sehemu ya kukusanya maji - na akajenga juu yake msikiti, basi kufaa kwake kumekuwa na kauli nyingi katika madhehebu ya Abu Hanifa:
Kauli ya Kwanza: kuwa huo sio msikiti, na kwa sababu hiyo inafaa kwake kuuza, kurithiwa isipokuwa itakapokuwa ujenzi huo ambao upo chini ya msikiti ni kwa masilahi ya msikiti.
Kauli ya Pili: ni kuwa itakapokuwa sehemu ya chini ni msikiti tofauti na sehemu ya juu, basi huo ni msikiti na ni wa kudumishwa, na kinyume na hivyo basi sio msikiti, kwa maana kutofanyiwa kazi hukumu za msikiti kwa upande wa sharti za kuingia na kukaa itikafu ndani yake na yasiyokuwa hayo katika hukumu za msikiti, nayo hayo yameelezwa na Abu Hanifa.
Kauli ya Tatu: ni kuwa ikiwa msikiti upo juu ya nyumba ya makazi na kutumika kama nyumba ya ibada huo utakuwa ni msikiti na tofauti na hivyo basi hapana, na maelezo haya yamepokelewa na Muhammad Ibn Al-Hassan.
Kauli ya Nne: ni utakuwa ni msikiti ni sawa sawa pawepo na nyumba au kutumika kama nyumba ya ibada juu ya msikiti au chini yake, na haya yamepokelewa na Abu Yussuf, na mapokezi ya Muhammad kutokana na umuhimu wake, na hilo pia ni kutokana na uhaba wa makazi.
Lakini wafuasi wa Imamu Abu Hanifa hawakuuzingatia kuwa ni msikiti, ule uliojengwa chini ya nyumba au juu ya nyumba, kwa sababu sharti za kuutoa wakfu kwao ni kuondoa umiliki wake kwa mwenye kuweka wakfu, na sharti hili halikamiliki ikiwa kutajengwa msikiti chini ya nyumba yake au juu ya nyumba yake, isipokuwa Abu Yussuf amepitisha hili kutokana na uhaba wa sehemu, kama kwamba amezingatia ni hali ya dharura.
Anasema Ibn Abdeen katika kitabu cha Rad Al-Muhtar: “Sharti la kuwa msikiti ni kuwa chini yake na juu yake ni msikiti, ili kuondoa haki ya mja ya umiliki, kwa kauli yake Mola Mtukufu {Na hakika Misikiti ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu}[AL JINN: 18]” [4/358 chapa ya Dar Al-Fikr].
Inazingatiwa kuwa wafuasi wa Imamu Abu Hanifa wanaruhusu kufanya msikiti chini ya nyumba au juu ya nyumba, lakini ni sehemu yenye mvutano wa mtazamo katika kuthibiti wakfu wake, kwa maana je itazingatiwa ni nyumba ya Mwenyezi Mungu ambayo haiuzwi, haitolewi zawadi, kurithiwa wala kuingia mwanamke mwenye hedhi na mtu mwenye janaba, au miliki yake haihusishi Mwenyezi Mungu na anaweza kuuza, kutoa zawadi na kurithiwa?
Kama vile Abu Hanifa amepitisha kujenga juu ya msikiti usiotimia ujenzi wake na kujenga chini yake, ikiwa ujenzi huo ni kwa masilahi ya msikiti, na wakazingatia nyumba ya Imamu ni katika masilahi ya msikiti, kwa sharti ya kujengwa nyumba ya Imamu kabla ya kutimia msikiti.
Na katika kitabu cha: [Ad-Dur Al-Mukhtar]: “Lau kutajengwa juu yake nyumba ya Imamu hakuna madhara, kwa sababu ni katika masilahi ya msikiti, lakini ikiwa umetimia ujenzi wa msikiti kisha ikjengwa nyumba hiyo itazuiwa, hata kama atasema: nilimaanisha kujenga nyumba ya Imamu hakubaliwi” [4/358].
Na wanaona wafuasi wa Imamu Malik uharamu wa kujenga juu ya msikiti uliokamilika, isipokuwa wametofautiana katika ujenzi wa nyumba chini ya msikiti au kuufanya msikiti chini ya nyumba au kujenga nyumba juu ya msikiti unaotakiwa kuanzishwa.
Imekuja katika kitabu cha: [Mawahib Al-Jalil cha Al-Hatwab 5/420, chapa ya Dar Al-Fikr]: “Na ukweli wa masuala ni kuwa msikiti ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ikiwa mtu ataujenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuumilikisha kwake, basi hakuna haja ya kutofautiana kuwa haifai kujenga nyumba juu yake.
Na imekuja katika kitabu cha Manh Al-Jalil cha Sheikh Eleesh: “Inafaa kupokea mgeni na kumpa chakula ndani ya msikiti wa kijijini, Imamu Malik amepunguza maelezo ya Ibn Qassim juu ya kulala wageni na kula ndani ya msikiti wa kijijini, kwa sababu mjenzi aliyeujenga kwa ajili ya Swala amefahamu kuwa wageni watalala humo kwa dharura zao, na ukawa kama kwamba ameujenga kwa ajili hiyo, hata kama ikiwa asili ya kujengwa kwake ni kwa ajili ya Sala lakini inafaa kwa yule asiye na makazi kulala msikitini, na inafaa kuchukua chombo cha kujisaidia haja ndogo usiku ndani ya msikiti ikiwa ataogopa huyu mwenye kulala kutokwa na mikojo kabla ya kutoka ndani ya msikiti. Fatwa ya Ibn Rushd inaruhusu kulala msikitini kwa kazi za ulinzi, na mwenye kulazimika kulala kutokana na utu, uzima, unyonge, ugonjwa na asiyeweza kutoka usiku kwa sababu ya mvua, upepo mkali, kiza kikubwa, matatizo ya sehemu ya kukojolea, kuna mtazamo kidogo, kwa sababu huyu mwenye kulinda kulala humo si jambo la lazima, kuulinda kutokana na matatizo ya mkojo ni jambo la lazima, wala si jambo la kawaida kwenye maasi. Na akasema: kufanya makazi chini ya msikiti inafaa, kuzuiliwa ni kuyafanya makazi juu ya msikiti”. [8/87, 88, chapa ya Dar Al-Fikr]
Tamko hili ni la wazi zuio la watu wa Malik kujenga nyumba juu ya msikiti kwa ajili ya makazi ya Imamu na asiye kuwa Imamu, isipokuwa Imamu Dardir na Dusuqiy pamoja na Hatwab wamepitisha suala la makazi juu ya msikiti ikiwa makazi hayo ni kabla ya kukamilika msikiti na wala siyo baada ya ukamilifu wake. [Hashiyat Ad-Dusuqiy, 4/19, chapa ya Dar Al-Fikr, na kitabu Mawahib Al-Jalil 5/421].
Na amekwenda kinyume katika hilo Ibn Al-Hajib ambapo amesema katika kitabu cha: [Jaami’ Al-Ummahat Uk. 446, chapa ya Al-Yamama - Damascus): “Inafaa kwa mtu kufanya sehemu ya juu ya makazi yake msikiti na wala haifai kufanya sehemu ya chini msikiti”.
Na imepokelewa na Ibn Qassim kutoka kwa Malik katika kitabu kuchukiza kufanya makazi juu ya msikiti, isipokuwa wanachuoni wa Imamu Malik wametofautiana katika maelekezo ya Imamu Malik, baadhi yao wamechukulia ni jambo lenye kuchukiza linalokaribiana na uharamu, na baadhi yao wamechukulia kuwa inachukiza ikiwa nyumba hiyo ipo kabla ya msikiti na kinyume na hivyo ni haramu kabisa [kitabu cha: Mawahib Al-Jalil 7/542, 543].
Wafuasi wa Imamu Shafiy wamezuia moja kwa moja kujenga juu ya msikiti hata kama msikiti huo utakuwa karibu zaidi kujengwa kuliko hiyo nyumba:
Katika kitabu cha: [I’anat Al-Talibeen cha Al-Bakriy Al-Demyatwiy]: “Inafaa kutoa wakfu sehemu ya juu tu ikiwa ni nyumba hiyo na mfano wake, bile sehemu ya chini ya msikiti” [3/189, chapa ya Dar Al-Fikr].
Ikiwa hawajaruhusu kufanya msikiti katika sehemu ya chini ya nyumba hata kama nyumba hiyo itakuwa ni mpya kuliko msikiti lakini lililo bora ni kuwa haifai kujenga nyumba mpya juu ya msikiti ni sawa sawa msikiti utakuwa tayari umeshajengwa au unataka kujengwa.
Kauli yenye kutegemewa kwa upande wa watu wa Abu Hanifa, ni kuwa inafaa mtu kujenga chini ya nyumba yake na juu ya nyumba yake msikiti, kama ambavyo wamepitisha kwa kauli ya wazi kuwa, inafaa kujenga chini ya msikiti sehemu ya kunyweshea maji au maduka ya biashara ikiwa wakazi wake wengi wataona hivyo, lakini hata hivyo wamezuia kujenga juu yake.
Amesema Ibn Mufleh katika kitabu cha: [Furuu]: “Mwenye kujenga msikiti chini ya nyumba yake atanufaika na sehemu ya juu. Naye Imamu Hanbal akasema hapana, isipokuwa mwenye kujenga msikiti juu ya nyumba yake atanufaika na sehemu ya chini, kwa sababu sehemu ya juu haiihitaji sehemu ya chini” [7/404, chapa ya Muasasat Al-Risala].
Na imekuja katika kitabu Kashaf Al-Qinana’ cha Bahutiy: “Kama mtu ataamua kujenga msikiti chini ya nyumba yake na kunufaika na sehemu ya juu ya nyumba yake hiyo ni sahihi na kinyume chake pia ni sahihi, kwa kuifanya sehemu ya juu ya nyumba yake kuwa msikiti na kunufaika na sehemu ya chini ni sahihi, au kuifanya sehemu ya kati ya nyumba yake kuwa msikiti na kunufaika na sehemu ya juu pamoja na ya chini” [4/241, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Na amesema Al-Mardawiy katika kitabu cha Insaf: “inafaa kuinua msikiti ikiwa wakazi wake wengi watataka hivyo, na kuifanya sehemu ya chini ni kwa ajili ya kunywesheleza maji na kuweka milango ya maduka, katika uwazi wa maneno ya Imamu Ahmad na kuchukuliwa na Kadhiy, amesema Zarkashiy katika kitabu cha Jihad: na ikasemwa kuwa: haifai, na akasema katika kitabu cha: [Al-Ria’aya Al-Kubra]: Ikiwa watataka watu wa eneo hilo la msikiti kuuinua na kujenga sehemu ya chini eneo la kunyweshelezea maji, hili likifanyika msikitini na watu wake wakataka waujenge kwa mfumo huo, ni bora zaidi” [7/111, chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Fatwa ilikwishatolewa na Mufti wa Misri kuhusu jambo hili mwaka 1369H. sawa na 1949, ambapo Sheikh Hasanein Muhammad Makhluuf alijibu swali aliloulizwa kutoka kwa mkaguzi wa mipango miji ndani ya wizara ya kazi, akisema: tumeangalia swali lenu, na jibu lake tunapenda kutoa faida kuwa msikiti unapaswa kuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hili ni kutokana na kauli yake Mola Mtukufu pale Aliposema: {Na hakika misikiti ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu}[AL-JINN, 18]. Mwenyezi Mungu Akaegemeza kwake umiliki wa msikiti pamoja na kwamba kila kitu kipo chini ya miliki yake, lengo ni kujulisha ulazima wa msikiti kuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Na kutokana na hili kumekuwa na mtazamo wa wazi kwa wafuasi wa Imamu Abu Hanifa kuwa lau kutajengwa juu ya msikiti au chini yake jengo kwa lengo la kunufaika nalo, basi jengo hilo halitakuwa msikiti, na mwenye kuujenga ana haki ya kuliuza pamoja na kurithiwa, ama likiwa jengo hilo ni kwa masilahi ya msikiti, basi hilo linafaa na linakuwa ni sehemu ya msikiti kama ilivyoelezwa kwenye kitabu cha Ad-Dar Al-Mukhtar na Fatwa za India na vyenginevyo, hili ni kabla ya kuwa msikiti, ama baada ya kuwa msikiti haiwezekani kwa yeyote kujenga moja kwa moja. Na akanukuliwa Ibn Abdiin tamko lake: “Sharti la kuwa msikiti ima ukiwa chini au juu ni kuondoka kwa haki ya kumiliki mtu, kwa kauli yake Mola Mtukufu {Na hakika misikiti ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu} tofauti na linapokuwa jengo dogo sehemu ya juu kikawekwa wakfu kwa masilahi ya msikiti, kama kilivyo kile cha msikiti wa Baytul Maqdis, haya ni wazi kwenye mapokezi.
Na imenukuliwa kutoka kwa Sahibeen kuwa inafaa kuwepo jengo la mtu chini ya msikiti au juu yake kwa hali ya kunufaika nalo au kuhusishwa na masilahi ya msikiti ikiwa kuna dharura ya kufanya hivyo, dharura hiyo ni kama vile kwenye miji ambayo ina uhaba wa majengo kwa wakazi wake. Na kutokana na hili ikiwa kuna dharura inayopelekea uwepo wa ujenzi huo, basi hakuna tatizo kuchukua kauli ya Sahibeen katika mapokezi yaliyotajwa, kwa sababu hilo linakubaliana na kanuni za madhehebu kama vile kanuni inayosema “Dharura inahalalisha yaliyokatazwa” na kanuni nyengine inasema “Matatizo huleta wepesi” na kanuni zengine nyingi, na haya yanathibitishwa kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pale Aliposema: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini}[AL-HAJJ, 78].
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia ni kuwa: inazuiliwa kujenga nyumba juu ya msikiti ambao umekamilika kazi zake kwa makubaliano ya wanachuoni, lakini ikiwa mwenye kutoa wakfu amenuia hivyo, basi inafaa - kwa kauli ya baadhi ya watu wa elimu - hata kama ni kunufaika mtu. Na pia inafaa kujenga kila chenye masilahi na msikiti kama vile nyumba ya Imamu, na hakuna kizuizi chochote katika kujenga msikiti chini ya nyumba ambayo imetangulia msikiti, na pia hata kujenga juu yake.
Na hakuna ubaya kuujenga msikiti na kujenga nyumba na milango ya maduka au vitu vyengine ikiwa watu wa msikiti huo wataona uwepo wa haja ya kufanya hivyo, ni sawa sawa ukiwa msikiti huo umeshajengwa au unatakiwa kujengwa - kwa kauli ya baadhi ya wanachuoni - na kauli zao zimetangulia kuelezwa.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas