Kusoma Qur`ani Katika Kurukuu na Ku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Qur`ani Katika Kurukuu na Kusujudu.

Question

Ni upi mwongozo wa Hadithi ya kusoma Qur'ani katika kurukuu na kusujudu na kupingana kwake na katazo la kufanya hivyo? Na je kuna ubaya wowote kwa Wanavyuoni kuifuata Hadithi hii? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Hadithi iliyoulizwa imepokewa kutoka kwa Al-Baihaqi: Tumeambiwa na Abu Taher Al-Ziadi, tumeambiwa na Abu Othman Al-Basri, kwamba Abu Ahmed Mohammed Ibn Abdul Wahab alituambia, kutoka kwa Amer Ibn Khaddash, kutoka kwa Ibn Harun, akasema: Nimemsikia Ibn Juraij, kutoka kwa Dawud Ibn Abu Asim, kutoka kwa Ibn Masoud, kutoka kwa Mtume, S.A.W. alisema: "Swali rakaa kumi na mbili katika nyakati za mchana au usiku utasoma Tashahhud kati ya kila rakaa mbili, na utakapoketi katika swala ya mwisho umsifu Mwenyezi Mungu na umswalie Mtume, S.A.W. kisha utoe takbir na usujudu, usome wakati unaposujudu sura ya mwanzo wa Qur`ani (Suratul Fatiha) mara saba, na Ayatul Kursi mara saba, na useme: “La ilaha illa Allah wahdahu la sharika lahu, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ‘ala kulli shai’in qadir” mara kumi, kisha useme: Ewe Mola, ninakuomba kwa utukufu wa kiti chako, kwa mwisho wa rehema ya kitabu chako, kwa jina lako kuu, kwa utukufu wako, na kwa maneno yako yaliyotimia, kisha unaomba haja yako baada ya hayo, kisha unainua kichwa chako na unatoa salamu upande wa kulia na kushoto, na usiwafundishe wajinga dua hii ili wasije wakamwomba Mola wao dua hii naye akawajibu". [Ad-Dawaat Al-Kabiir 2/18, Ghiras kwa Uchapishaji na Usambazaji - Kuwaiti].
Imepokewa kutoka kwa Abu Al-Qasim Ismail Ibn Muhammad, anayejulikana kwa jina la Qiwam Al-Sunna (Nguzo ya Sunna): Tuliambiwa na Ahmed Ibn Ali Ibn Khalaf, Al-Hakim Abu Abdullah alisema kuwa: Muhammad Ibn Al-Qasim Ibn Abdul Rahman Alatki alisema kutoka kwa Mohammed Ibn Ashras Al-Salmi, kutoka kwa Amer Ibn Khaddash Al-Naisaburi, kutoka kwa Omar Ibn Harun Al-Balkhi kutoka kwa Ibn Juraij, kutoka kwa Dawud Ibn Abu Asim, kutoka kwa Ibn Masoud R.A. kutoka kwa Mtume, S.A.W. alisema: “Uswali rakaa kumi na mbili katika nyakati za mchana au za usiku, utasoma Tashahhud kati ya kila rakaa mbili, kama ukiketi katika swala ya mwisho umsifu Mwenyezi Mungu na msalie Mtume, S.A.W, kisha utoe takbira na usujudu, usome wakati unaposujudu Sura ya kwanza ya Qur`ani (Suratul Fatiha) mara saba, na ayatul Kursi mara saba, na kisha useme: “La ilaha illa Allah wahdahu la sharika lahu, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ‘ala kulli shai’in qadir” mara kumi, kisha useme: Ewe Mola, ninakuomba kwa utukufu wa kiti chako, kwa mwisho wa rehema ya kitabu chako, kwa jina lako kuu, kwa utukufu wako, na kwa maneno yako yaliyotimia, kisha unaomba haja yako baada ya hayo, kisha unainua kichwa chako na utoe Salaamu upande wa kulia na wa kushoto, na usiwafundishe wajinga dua hii ili wasije wakamwombe dua Mola wao naye akawajibu”.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim kutoka kwa Abu Zakaria Yahya Ibn Mohammed Al-Anbari kutoka kwa Ibrahim Ibn Ali Al-dhahli alisema: Nimeambiwa na Ahmad Ibn Harb na aliniandikia kwa mkono wake, kutoka kwa Amer Ibn Khaddash kutoka kwa Ahmed Ibn Harb alisema: Nimeijaribu dua hii na kuikuta ni ya kweli. Ibrahim Ibn Ali Al-Mahli alisema: Nimeijaribu dua hii na kuikuta ni ya kweli. Al-Hakim alisema: Abu Zakaria alituambia: Nimeijaribu dua hii na kuiona kuwa ni ya kweli. Al-Hakim alisema: Nimeijaribu dua hii na kuiona kuwa ni ya kweli. Al-Hakim alisema: Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Amer Ibn Khaddash peke yake naye ni mtu mwenye imani na ni msema kweli. [Al-Targhiib waltarhiib kwa Abu Al-Qasim Ismail Ibn Muhammad, anayejulikana kwa jina la Qiwam Al-Sunna (Nguzo ya Sunna) 3/34, Dar El Hadith - Kairo].
Hadithi hii imepokelewa kutoka mapokezi yale yale ya Al-Bayhaqi, lakini uzoefu wa kuitekeleza Hadithi hii umeongezeka, na kwa sababu hii kupelekea kukumbukwa kwa mapokezi haya katika vitabu vya kutohoa Hadithi. Hadithi hii haipatikani katika Mustadrak Al-Hakim, na sikupata mtu yeyote miongoni mwa wenye kuhifadhi aliyeeitoa Hadithi hii na kuhusishwa kwake.
Baadhi ya Wanavyuoni wa Hadithi wamekosoa matini ya Hadithi hii na mapokezi yake, imepokewa kutoka kwa Ibn Al-Jawzi miongoni mwa Hadithi Maudhui (Ni Hadithi aliyosingiziwa Mtume) (Hadithi ya uongo)) kutoka kwa Al-Hakim, na alisema: “Hadithi hii bila shaka ni Maudhui (uongo) na mapokezi yake kama unavyoona kuna Omar Ibn Harun, Yahya alisema kuwa: Mtu huyu ni mwongo, Ibn Hibbaan alisema kuwa: Omar Ibn Harun anasimulia uwongo na anadai kuwa anasimulia kwa Masheikh ambao hakuwaona, licha ya hivyo, imepokewa kutoka kwa Mtume, S.A.W. kuwa amekataza kusoma katika kusujudu”. [Al-Maudhuaat kwa Ibn Al-Jawziy 2/142, Al-Maktaba Al-Salafiah – Al-Madina Al-Munauwara].
As-Suyuti amejaribu kupunguza hukumu ya kuwa ni Hadithi Maudhu, aliposema: “Nilisema: At-Tirmidhiy alimsimulia Omar na Ibn Majah na alisema katika kitabu cha Al-Mizan: Omar alikuwa miongoni mwa wenye elimu ingawa udhaifu wake na idadi kubwa ya Hadithi dhaifu zilizopokelewa kutoka kwake na sidhani kuwa anasema uwongo kwa makusudi. Maneno ya Al-Suyuti yamemalizikia hapa
Na nilipata mapokezi mengine ya Hadithi hii, Ibn Asakir alisema: niliyasoma maandishi ya Abul Fitian Omar Ibn Abdul Karim Al-Dahstaniy, tuliambiwa na Abu Ar-Rida Hassan Ibn Hussein Ibn Jaafar Ibn Ahmed Ibn Dawud Ibn Al-Mutahhar At-Tanokhi, tuliambiwa na Aminah binti Al-Hasan Ibn Ishaq Ibn Bulbul, tuliambiwa na Abu Al-Qadhiy Abu Said Al-Hasan, tuliambiwa na Abu Obeid-Allah Mohammed Ibn Shaybah Al-Walid Ibn Said Ibn Khalid Ibn Yazid Ibn Tamim Ibn Malik, tuliambiwa na Ahmed Ibn Abi Al-Hawari, tuliambiwa na Abdul Karim Ibn Yazid Al-Ghassani kutoka kwa Abu Harith Al-Hussein, kutoka kwa baba yake Al-Hasan Ibn Yahya Al-Khashani, kutoka kwa Ibn Juraij Ibn Rabah kutoka kwa Abu Hurayrah akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mwenye kuswali rakaa kumi na mbili baada ya swala ya magharibi na kusoma katika rakaa mbili ufunguzi wa Qur`ani (Suratul Fatiha) mara saba, na Ayatul Kursi mara saba, na kusema: “La ilaha illa Allah wahdahu la sharika Lahu, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ‘ala kulli shai’in qadir” mara kumi, kisha useme: Ewe Mola, ninakuomba kwa utukufu wa kiti chako, kwa mwisho wa rehema ya kitabu chako, kwa jina lako kuu, kwa utukufu wako, na kwa maneno yako yaliyotimia, kisha unaomba haja yako baada ya hayo, kama umefanya madhambi mengi kama idadi ya mchanga na kama idadi ya siku za dunia, Mwenyezi Mungu atakusamehe, na msiwafundishe wajinga dua hii ili wasimwombe dua Mola wao naye awajibu”, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi. [Al-Laali Al-Masnuah Fil- Ahadith Al-Maudhuah 2/57, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]
Al-Suyuti hakuzungumza juu ya mapokezi ya Hadithi hii - nayo katika kitabu cha Tatikh Dameski 36/471, Dar Al-Fikr-, lakini yule Ibn Iraq alizungumza juu yake na kuongeza faida, Ibn Iraq alisema: Al-Hassan Ibn Yahya Khushani yuko katika mapokezi haya, Al-Dhahabi alisema katika kitabu cha Al-Mughni: wakamwacha jina lake, na Al-Hafiz Shams Al-Din Ibn Al-Jazari alimtaja katika kitabu cha Al-Hisn Al-Hasiin kutoka mapokezi ya Al-Baihaqiy kisha akasema: Al-Baihaqiy alisema kuwa alijaribu na aliipata Hadithi hii ni sababu ya kukidhi haja, alisema: tuliisimulia Hadithi hii katika kitabu cha [Al-Dua kwa Wahidi], na katika mapokezi yake zaidi ya mmoja miongoni mwa Wanavyuoni, na alisema kwamba aliijaribu akaikuta hivyo, alisema: “Nimeijaribu Hadithi hii na nikaiona hivyo, ingawa kuna katika mapokezi yake ambaye simjui, maneno yake yamekwisha hapa. Imepokewa kutoka kwa Ad-Daylamiy katika mapokezi ya Al-Firdaws, akisema: Nimejaribu waliosimulia Hadithi hii nikawaona wote ni wakweli mpaka Ibn Masoud. Al-Iraqi alisema katika kueleza maneno ya At-Tirmidhiy kuhusu mapokezi ya Hadithi hii na kuonesha udhaifu wake: Dawud Ibn Abi Asim hakuwahi kumwona Ibn Masoud na hakusikia kutoka kwake Hadihi hii, inaonekana Ibn Masoud ni miongoni mwa baadhi ya wapokezi, lakini Hadithi hii imepokewa kutoka kwa Dawud Ibn Abi Asim kutoka kwa Urwah Ibn Masoud Mursala, baadhi ya wapokezi wamewekwa badala ya Urwah Abdullah ikatokea wasiwasi, hata hivyo, Hadithi hii ni kinyume na Hadithi ambazo ni sahihi juu ya kusoma Qur`ani katika kurukuu na kusujudu, maneno yake yamemalizika hapa. [Tanzih Al-Sharia Al-Marfuah An Al-Akhbar Al-Shaniah Al-Maudhuah 2/112, Dar Al-Kutub Al-Ilmiayah].
Hitimisho Katika Hadithi hii ni kwamba Hadithi hii siyo sahihi kwa upande wa mapokezi yake, vile vile kwa upande wa matini yake kuna wasiwasi kwa sababu ni kinyume na kukatazwa kwa kusoma Qur`ani katika kurukuu na kusujudu kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Sahih Imam Muslim kutoka kwa Ibn Abbas, alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alifichua pazia wakati watu waliposwali nyuma ya Abu Bakr R.A., alisema: Enyi watu, haikuwa miongoni mwa bishara za unabii isipokuwa ndoto njema, ambayo Muislamu anaiona, au inaonwa kwake, tanabahini hakika nimekatazwa kusoma Qur`ani katika kurukuu au kusujudu, lakini wakati wa kurukuu mtukuzeni Mwenyezi Mungu, na jitahidini katika dua wakati wa kusujudu, ili kujibiwa kwenu”, na kutoka kwa Hadithi ya Ali Ibn Abi Talib R.A., alisema: “Nimekatazwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. kusoma Qur`ani katika kurukuu au wakati wa kusujudu".
An-Nawawiy alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W alisema: “Nimekatazwa kusoma Qur`ani katika kurukuu au wakati wa kusujudu, lakini wakati wa kurukuu mtukuzeni Mwenyezi Mungu, na jitahidini katika dua wakati wa kusujudu, ili kujibiwa kwenu”. Na katika Hadithi ya Ali R.A: “Nimekatazwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. kusoma Qura`ni katika kurukuu au wakati wa kusujudu”. Hadithi hii inakataza kusoma Qur`ani katika kurukuu au wakati wa kusujudu, lakini kazi iliyofanywa katika kurukuu ni kumtukuza Mwenyezi Mungu, na kazi iliyofanywa katika kusujudu ni kumtukuza Mwenyezi Mungu pia na kuomba dua. Kama mtu akisoma Qur`ani katika kurukuu au katika kusujudu Sura nyingine isipokuwa Al-Fatiha, basi swala yake inachukiza lakini haikubatilishwa, na kama akisoma Surat Al-Fatiha, basi kuna mitazamo miwili kwa wenzetu, rai iliyochaguliwa ni kwamba swala yake inachukiza lakini haikubatilishwa, mtazamo wa pili ni kwamba inaharimishwa na swala yake inabatilishwa, hali hiyo kama akifanya hivyo kwa makusudi, lakini kama akisoma Qur`ani na hali yake akisahau, swala yake haikuchukiza, na kama akisoma kwa makusudi au akisahau anatakiwa kusujudu kwa kusahau kwa mujibu wa madhehebu ya Imam AShafiy Mwenyezi Mungu amrehemu, na kauli yake Mtume S.A.W.: “Lakini wakati wa kurukuu mtukuzeni Mwenyezi Mungu” yaani mtakaseni na mwadhimisheni, Imam Muslim ametaja baada ya hivyo dhikr hizi zinazosemwa katika kurukuu na kusujudu”. [Sharh Al-Nawawi juu ya Sahih Muslim 4/197, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi]
Al-Mullah Ali Al-Qari alisema: “Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: (tanabahini) neno la kutahadhari (hakika nimekatazwa) yaani jambo hili limechukiza tu lakini halikuharimishwakwa mujibu wa Ibn Al-Malik, na Ibn Hajar akasema: Kwa rai hiyo zaidi ya wanavyuoni waliafikiana, na ilisemekana kuwa: ni haramu, nayo ndiyo ni kipimo, (Kusoma Qur'an) yaani: nimekatazwa kuisoma (Katika kurukuu au kusujudu) yaani: katika hali hizi mbili, Al-Khatibi alisema: wakati hali ya kurukuu na kusujudu ilipokuwa kwa ajili ya kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumtukuza, Mtume wa Mwenyezi Mungu alikataza kusoma katika hali hizi mbili, kana kwamba inachukiza kusema maneno ya Mwenyezi Mungu pamoja na maneno ya watu katika wakati mmoja. Al-Taibi alisema: hali kadhalika hairuhusiwi kutaja maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya watu katika hali ya kusimama. Ibn Al-Malik alisema: kana kwamba hekima yake kuwa nguzo bora katika swala ni kusimama, na dhikr bora ni Qur`ani, kana kwamba Mwenyezi Mungu akafanya dhikr bora kwa nguzo bora, na amekataza kufanya kitu kingine katika hali hizo, ili isidhaniwe kuwa dhikr hizi ni sawa na dhikr nyingine, na imesemekana kuwa: kusoma Qur`ani kuliainishwa katika hali ya kusimama au kukaa wakati wa kutoweza kusimama, kwani hali hizi ni za kawaida kinyume na hali ya kurukuu na kusujudu ambazo ni dalili ya unyenyekevu na ibada. Vile vile inawezekana kusema kuwa: hali ya kurukuu na kusujudu ni dalili ya unyenyekevu na ibada na zinafaa na kuomba dua na kufanya tasbihi, basi akakataza kusoma Qur`ani katika hali hizi mbili kwa ajili ya kuheshimu Qur'ani na kwa heshima ya msomaji wake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Al-Qadhiy alisema: hali ya kupiga marufuku ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, inaonesha kuwa hairuhusiwi kusoma Qur`ani katika hali ya kurukuu na kusujudu, lakini kama mtu akisoma Qurani katika hali hizi mbili, basi swala yake haikubatilishwa ila akisoma Suratul Fatiha, katika hali hii Wanavyuoni hawakubaliani, kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Shafiy: kwani ameongezeka nguzo moja, lakini mfumo wa sala haukubadilika”. [Mirqatul Mafatiih Sharhu Mishkatul Masabiih 2/711, Dar Al-Fikr].
Ibn Taimiah alisema: “Katika katazo la Mtume S.A.W. kusoma Qur'ani wakati wa kurukuu na kusujudu ni dalili kuwa Qur'ani ni maneno matukufu, nayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na kusujudu ni udhalili na unyenyekevu kutoka kwa mja, kutokana na adabu ni kukataza kusomwa Qur’ani wakati wa kurukuu au kusujudu na bora kusubiri.” [Al-Fatwa Al-Kubra kwa Ibn Taymiyah 5/338, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu inaonyesha kwamba hakuna makubaliano juu ya ubatili wa sala katika hali iliyotajwa, na kwamba umma wa Wanavyuoni wanachukiza kusoma Qur’ani wakti wa kurukuu na kusujudu, lakini kuna baadhi ya Maulamaa waliotangulia walioruhusu kusoma Qur’ani wakati wa kurukuu na kusujudu, hasa katika swala iliyofaridhishwa. Al-Haafiz Ibn Rajab Al-Hanbali akasema: Kundi la Wanavyuoni waliruhusu kusoma Qur’ani na kusujudu. Imepokelewa kutoka kwa Abu Ad-Dardaa kwamba alikuwa akisoma Suratul Baqarah wakati wa kusujudu. Na Sulaiman Ibn Rabia, Ubaid Ibn Umair, na Al-Mughirah, Na imepokewa kutoka kwa Al-Nakhii kwamba kuhusu aliyesahau kusoma Aya au aliiacha kuisoma, akakumbuka wakati wa kurukuu, akasema: anaruhusiwa kuisoma wakati wa kurukuu.
Na imepokewa kutoka kwa Al-Mughirah kuwa alisema: Wao walikuwa wanafanya hivyo. Ata'a aliulizwa juu ya kusoma wakati wa kurukuu na kusujudu akasema: Niliona Ubaid Ibn Omair akisoma Qur’ani wakati wa kurukuu katika swala iliyofaridhishwa. Na baadhi yao wameruhusu kufanya hivyo katika swala ya Sunna isipokuwa swala iliyofaridhishwa. Imepokelewa kutoka kwa Sulaiman Ibn Musa kutoka kwa Nafi kutoka kwa Ali, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, alikataza kusomwa Qur`ani wakati wa kurukuu na kusujudu katika swala iliyofaridhishwa, lakini katika swala ya Sunna, basi hakuna ubaya. Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Ismaili na sanad yake imekatika, kwani Nafii anaisimulia kutoka kwa Ibn Hanin, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ali, kama hapo awali. Mwisho wa Hadithi labda ni pamoja na baadhi ya walioisimulia. na kuna tofauti katika Sulemani Ibn Musa. [Fath Al-Bari Ibn Rajab 7 / 186- 189, Maktabat Al-Ghurabaa Al-Athariyah - mji wa Mtume].
Hoja ya kuzuia, ambapo baadhi ya wanavyuoni walioisema kuwa Qur'ani hairuhusiwi kusomwa katika hali ya udhalili na unyenyekevu wakati wa kusujudu na kurukuu, rai hii haithibitishwi, lakini inawezekana kuwa ni sahihi, inaweza kuchukuliwa kama hekima si sababu, vile vile kuna hekima nyingine zaidi ya hapo juu. Al-Sha'rani alisema: “(Tuliahidi Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. kuswali swala ya haja kwa ajili ya kuonesha ufukara na haja kama zawadi iliyopelekwa na mtu kwa mwingine ambaye ana haja kwake kabla ya kukutana naye, nilisikia Bwana wangu Ali Al-Khawas R.A. anasema: inapaswa kusimamisha swala ya Tasabiih (Swala ya kumsifu Mungu) kabla ya kuswali swala ya haja kufuatana na iliyopokewa kuwa swala hii inasababisha kusamehewa madhambi yote, na kwamba swala hii ni moja ya sababu kubwa kukidhi haja, na kwamba kuchelewa kwa kukidhi mahitaji kwa sababu ya madhambi mara kwa mara. Pia nimesikia akisema kuwa: ni lazima kufikiri katika dhikiri (Dua) za kusujudu katika mwisho wa swala ya haja ambayo baada yake anamaliza swala, na ishara ya kufikiri kwa umakini ni kuhisi kwamba viungo vyake vianakaribia kukatika na mifupa yake inakaribia kusagikasagika kutokana na heshima ya Mwenyezi Mungu, na katika wakati huu inatarajiwa kujibika dua, na kuelezea hali hii ni kwamba hakuna yeyote anayeweza kusoma Qur'an katika kusujudu kwani mja anakuwa karibu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa iliyopokelewa” [Al-Uhuud Al-Muhamadiyah uk. 55, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Vile vile katika jibu inawezekana kusema kuwa aliyoisoma anayeswali si kwa nia ya kusoma bali kwa nia ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kama katika ibada nyingine, na wanavyuoni walizungumza juu ya suala hili kama katika hukumu yao kwa anayesoma Qur'ani wakati ambapo ana janaba.
Al-Khatwib Al-Sherbiniy alisema: “(na inaruhusiwa) kwa mwenye janaba (dhikiri yake) na dua nyingine kama waadhi habari zake na hukumu zake (si nia ya kusoma Qur'ani) kama kauli yake wakati wa kusafari: {Ametukuka Mwenyezi Mungu aliyetutiisha haya, na tusingaliweza kutenda haya wenyewe} [AZ ZUKHURUF: 13], na wakati wa kupata msiba tunasema: {Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye tutarejea} [AL BAQARAH: 156] wala aliyetamka pasipo na makusudi, kama akikusudia kusoma Qur'ani peke yake au pamoja na dua hairuhusiwi hivyo, na kama hakuainisha nia yake hairuhusiwi pia, kama alivyosema, kwani kusoma Qur'ani hakuzingatiwi isipokuwa kwa makusudi tu, rai hii ilichaguliwa na mwandishi na wengine. Inaonekana kwamba hali hii inapatikana katika hali isiyo ya Qur'an kama katika Aya mbili zilizopita hapo juu, ingawa Az-Zarkhasiy alisema: Hakuna shaka katika kukataza yasiyopatikana utaratibu wake katika Qur'ani, na baadhi ya waliochelewa wamemfuatilia katika rai hii. hii pia ni pamoja maoni ya Ar-Rawdhah, lakini kama mtu akisoma kitu kutoka Qur’ani bila ya kukusudia kusoma Qur’ani basi inaruhusiwa” [Mughni Al-Muhtaj Ila Maarifat Maani Alfaadh Al-Minhaj 1/217, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ibn Hajar aliasema: inaonekana kutoka matini ya Hadithi ile kuwa mtu anasujudu kati ya Tashahhud na kusema taslim akisema hivyo. [Rejea: Al-Dirayah Fi Takhrij Ahadith Al-Hidayah 2/239].
Hatukupata jibu kwa tuhuma hii, lakini inaweza kusemwa kuwa hii ni kama kusujudu kwa wakati wa kuisoma Qur’ani, na kama kwamba kuacha umbo la kawaida katika swala ya Sunna imekubaliwa katika swala ya Tasabiih, hali hii inakubaliwa hapa, au hali hii hubeba juu ya sijida ya mwisho. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.
Al-Shawkaaniy amesema kuwa Hadithi hii ni Munkar kwa kukiuka sahihi, lakini ameongezeka akisema: “Al-Sunna haithibitishwi kwa majaribio, na mtendaji wa kitu hakuwa mzushi kwa kuamini kwamba kitu hiki ni Sunna, na hali ya kujibu dua haimaanishi kwamba sababu ya kujibu ni thabiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, inawezekana Mwenyezi Mungu anajibu dua pasipo na kuomba dua kwa Sunna naye ni Mwenye huruma nyingi, inawezekana kujibu dua ni kuvuta kwao kidogo kidogo, hata hivyo, imethibitika katika Sunna bila shaka kwamba imekatazwa kusoma Qur'ani wakati wa kurukuu na kusujudu, na hiyo ni mojawapo ya ishara kubwa zaidi kwamba Hadithi hii ni ya uongo, hasa katika isnad yake Omar Ibn Harun Ibn Yazid Al-Thaqafiy Al-Balkhiy aliyetajwa, naye ni miongoni mwa wenye kutuhumiwa, na pengine kusifu kwa Ibn Mahdi juu ya Omar Ibn Harun kutoka upande wa kuwa ni mwenye kuhifadhi, vile vile mwanafunzi wake Amir Ibn Khaddash, labda Hadithi hii ni miongoni mwa Hadithi za uongo anazozisimulia, na ajabu kama vile kupitishwa kwa Al-Bayhaqi, Alhakim, na Al-Wahidi na waliokuja baada yao na majaribio katika jambo wanalojua kwamba linapingana na Sunna iliyotukuka”. [Tuhfatul Dhakiriin Biidat Al-Hisn Al-Hasiin uk. 214, Dar Al-Qalam - Beirut]
Al-Mundhiriy alisema: “Amer Ibn Khaddash huyo ni Al-Naysaburi, Sheikh Al-Hafidh Abu Hassan alisema: alikuwa na Hadithi nyingi za uongo, naye ni mtuhumiwa ingawa alisifiwa na Ibn Mahdi peke kufuatana na ujuzi wangu, na kutegemea katika majaribio haya siyo juu ya Isnaad tu, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi. [Al-Targhiib wal Tarhiib kwa Al-Mndhiri 1/274, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na kujibu suala la kutothibitika kwa Sunna kwa majaribio, inajibiwa kuwa suala hili linazingatiwa kuwa ni kufuata Hadithi dhaifu, na kuna Fatwa katika hukumu hii kwetu.
Pia kuna Hadithi nyingi wapokezi waliziangalia matini zao na walihukumiwa kwake kwa usahihi, kwani si lazima ya udhaifu wa Sanaad unasababisha udhaifu matini, na mfano wake ni maneno ya Ibn Al-Qayyim: ama Hadithi ya Abi Raziin, ambayo inaashiriwa na Al-Bukhaari, ni Hadithi ndefu, na tunaitaja kwa urefu wake ili kutimiza kitabu chetu, nayo Hadithi hii ina utukufu na nuru ya unabii unaolazimisha usahihiwake. [Rejea: Hadi Al-Arwah Ila Bilad Al-Afrah, uk. 243, Matba’t Al-Madani - Kairo].
Kuna masuala mengine ambayo wanavyuoni waliruhusu suala la jaribio, ambalo linasaidia kile kilichosemwa na makundi mbalimbali ya wapokezi wa zamani.
Ibn Al-Qayyim alisema: “Imepokewa kutoka kwake kuwa alisema: “Sageni vyakula vyenu kwa ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na swala, wala msisahau ukumbusho wa Mwenyezi Mungu ili nyoyo zenu zisiwe ngumu”, inawezekana Hadithi hii ni sahihi, na kwa kweli jaribio linathibitisha hivyo”. [Zad Al-Maad Fi Hadi Khair Al-Ibaad 2/370, Mu’asast Al-Resallah]
Al-Baihaqiy alisema: “Tuliambiwa na Abu Abdullah Al-Hafidh, tuliambiwa na Abu Al-Abbas Al-Asam, tuliambiwa na Abdul Malik Ibn Abdul Hamid, tuliambiwa na Roh, tuliambiwa na Usama Ibn Zaid, kutoka kwa Aban Ibn Saleh, kutoka kwa Mujahid, kutoka kwa Ibn Abbas alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika katika ardhi wanaandika majani ya mti yaliyoanguka ardhini, basi kama mmoja wenu amepatwa na shida au alihitajia msaada wowote aseme: nisaidieni waja wa Mwenyezi Mungu, atasaidiwa Mungu akipenda”. Hadithi hii inasimamishwa kwa Ibn Abbas, ingawa inatumika kwa wema miongoni mwa Wanavyuoni kwa sababu ya ukweli wake kwao walipoijaribu, na Mwenyezi Mungu akubariki”. [Al-Adab kwa Al-Baihaqiyuk. 269, Mu’asast Al-Kutub Al-Thaqafiyah - Beirut].
Al-Sakhaawiy alisema katika mapokezi ya Hadithi ya “Maji ya Zamzam ni kwa ajili ya mnywaji wake”: “Sheikh wetu -yaani Ibn Hajar- alisema: Hadithi hii ni hasana ingawa inasimamishwa, na inathibitishwa kwa Hadithi ya Abu Dhar: “Ni chakula kwa mwenye njaa na uponyaji kwa mwenye ugonjwa”, na asili yake katika Muslim, na Al-Tayaalisi alisema, na daraja la Hadithi hii kwa makubaliano ya Wanavyuoni ni sahihi, kundi la Wanavyuoni wameijaribu wakasema kuwa ni sahihi, vile vile imesahihishwa na Ibn Uyaynah mmoja wa Wanavyuoni waliotangulia, na baadaye Al-Domiaty, Na Al-Mundhari, lakini Al-Nawawi ameidhoofisha.” [Al-Maqasid Al-Hasanah. 568, Dar Al-Kitab Al-Arabi - Beirut]
Ibn Abdin alisema: “Faida: Ibn Hajar katika kitabu cha Al-Idhaah kutoka kwa baadhi ya Sufi Mwenyezi Mungu awarehemu alitaja kuwa: Kama ukipoteza kitu, useme: Ewe Mkusanyaji wa watu katika siku isiyo na shaka ndani yake Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi, nikusanye na kitu hiki, na anataja jina lake, Dua hii imejaribiwa. Al-Nawawi amesema: niliijaribu na niliona kuwa ni muhimu kwa ajili ya kupata unavyopoteza mara kwa mara. Imepokewa Hadithi hii kutoka kwa baadhi ya Masheikh, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi. [Hashiyat Ibn Abidin 4/286, Dar Al-Fikr]. Hili ni kundi la Wanavyuoni waliosema kuwa inaruhusiwa kuifuata Hadithi iliyojaribiwa na isiyo sahihi kwa mujibu wa Sanad yake.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu inaoneshwa udhaifu wa njia za Mapokezi ya Hadithi inayothibitisha uhalali wa kusoma Qur'ani wakati wa kurukuu na kusujudu na kupingana kwa matini yake na maana yake na ile iliyo na nguvu zaidi na iliyothibitika zaidi kutoka Hadithi zinazokataza hilo. Hata hivyo, kundi la Wanavyuoni wanaona kuwa inaruhusiwa kufuata Hadithi hii katika swala iliyofaridhishwa na katika swala ya Sunna, lakini rai iliyo sahihi zaidi katika suala hili ni kutoruhusiwa kwa kufuata Hadithi hii, na si lazima kubatilika kwa swala hii kwa kufanya hivyo kama walivyosema umma wa Wanavyuoni kwamba swala hii inachukiza, wala hakatazwi mwenye kuswali swala hii akifuata Wanavyuoni walioruhusu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas