Itikafu Isiyokuwa Katika Misikiti M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Itikafu Isiyokuwa Katika Misikiti Mitatu Mitakatifu.

Question

Je, inajuzu kukaa Itikafu katika misikiti isiyo kuwa misikiti mitatu mitakatifu? Na ni jibu gani linalokutokana na Hadithi ya Hudhaifah (Mwenyezi Mungu amwie radhi) iliyosimulia juu ya jambo hili? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kwa hakika, wengi wa waislamu wanafanya Itikafu misikitini katika siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhani, kwa kufuata Sunna ya Mtume S.A.W., katika jambo hili, lakini kuna baadhi ya watu wanaoeneza habari za kuzizuia itikafu katika misikiti isipokuwa misikiti mitatu mitakatifu.
Na mara nyingi wanazuoni wa Fiqhi wanalitaja swala la Itikafu mwishoni mwa mlango wa Saumu, na wanafasiri aya za Qur`ani wanahimiza maudhui ya itikafu wanapofasiri Aya ya Suratul BAQARAH iliyohadithia juu ya itikafu, na wakielezea juu ya hukumu yake ya kisharia na sharti zake.
Na hukumu ya itikafu isiyo kuwa misikiti mitatu mitakatifu-Msikiti wa Makka, Msikiti wa Madina na Msikiti wa Baytul Maqdisi-inajuzu, na katika msikiti wowote unachukuwa hukumu ya msikiti, inajuzu kufanya itikafu ndani yake.
Na dalili yake juu ya hivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu alitaja jina la misikiti kwa ujumla siyo mahala maalumu penye mipaka, kama katika aya ifuatayo Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini}. [AL-BAQARA:187], na Al-Baydhawiy alisema katika tafsiri yake [Anwar At-Tanziil wa Asrar At-Twawiil 1\126, Ca, Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy]: “Na ndani yake dalili juu ya kuwa Itikafu inakuwa katika msikiti wowote, na siyo katika msikiti maalumu bila ya msikiti mwingine”.
Na kwa mujibu wa tulivyotaja hapo juu, kundi moja la wanazuoni walisema:
Imam Malik alisema: “Tunaafikiana kwetu sisi kwamba hakuna tofauti kuwa si karaha itikafu katika kila msikiti yaweza kusimamisha swala ya Ijumaa, na pia sikuona ukaraha kufanyaka itikafu katika misikiti isiyo swaliwa Swala ya Ijumaa, ila karaha ni kwa mwenye kufanya Itikafu kutoka nje ya msikiti wake anaofanya Itikafu na kwenda kuswali Ijumaa msikiti mwingine ikiwa msikiti hauswaliwi Swala ya Ijumaa ,basi sioni tatizo la kufanya Itikafu katika msikiti kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {na hali mnakaa Itikafu msikitini}. [AL- BAQARAH: 187]. kutokana na maana ya Aya hii kwamba Mwenyezi Mungu ametaja misikiti kwa ujumla na hakuhusisha msikiti msikiti wowote)). Malik alisema: “Kutokana na maana hiyo mtu yeyote anaweza kufanya Itikafu katika misikiti isiyoswaliwa swala ya Ijumaa akiwa halazimiki kutoka kwake kwenda msikiti unaoswaliwa swala ya Ijumaa”. (Al-Muwata’ 1\313, Cha, Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy).
Na Al-Bukhariy alisema katika sahihi yake (2\711, Ch. Dar Ibn Kathiir-Bairut): “Mlango wa Itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani katika misikiti yote kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha} [AL-BAQARAH: 187].
Na Abu Al-Hassan Aly Ibn Muhamad Al-Menofiy Al-Masriy Al-Malikiy alisema katika kitabu cha: [Sharhu Al-Resalah]: “(wala haikuwa) Al-itikafu (ila katika misikiti) kwa maana haisihi katika nyumba wala maduka na kadhalika (kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:{na hali mnakaa Itikafu msikitini} [AL- BAQARAh: 187]. Basi Itikafu inasihi katika msikiti wowote katika nchi yoyote, hata ikiwa si misikiti mitatu mitakatifu” [Kifayat Al-Twaleb Ar-Rabaniy 465, Dar Al-Fekr-Bairut].
Na Ibn Najm Al-Hanafiy alisema katika kitabu cha: [Sharhu Al-Kanzu]: Na Kadhi Khan alisahihishia katika Fatwa zake kwamba Itikafu inakuwa sahihi katika kila msikiti wenye adhana na iqamah, na alichagua katika kitabu cha: [Al-Hidayah ya kwamba Itikafu haisihi ila katika msikiti wa kuswaliwa swala ya jamaa, na kutoka kwa Abu Yusuf alihusisha ulazima wa Itikafu ya Ramadhni katika msikiti wa swala ya jamaa, ama katika Sunna inajuzu katika msikiti usio na swala ya jamaa. Alitaja rai hii katika kitabu cha: [Al-Hidayah] na alisahihishia katika kitabu cha: [Fathu Al-Qadiir} kutoka kwa baadhi ya wanazuoni iliposimuliwa na Abu-Hanifah ya kuwa Itikafu inakuwa sahihi katika kila msikiti una Imamu na muadhini maalumu na kuswaliwa swala tano za jamaa, na katika kitabu cha: [Al-Kafiy] Abu-Hanifah alitaka katika msikiti wowote,na alitaka Itikafu katika msikiti mkubwa hata ikiwa hakuswaliwi swala ya jamaa ndani yake, na hayo yote kwa kubainisha usahihi wa itikafu, ama kwa upande wa ubora wa mahala pa Itikafu ni katika Msikiti Mtakatifu wa Makka kisha katika Msikiti wa Mtume S.A.W., katika Madinah na kisha katika Msikiti wa Baytu Al-Maqdisi kisha msikiti wa swala ya jamaa kisha katika misikiti mikubwa yanayojaa watu wengi…..kadhalika katika vitabu vya: [Al-Badaea na Sharhu Al-Twahawiy]”. [Al-Bahr Al-Raeq 2\324, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]. Na Ibn Hazm Al-Dhahiriy alisema kwamba: “Masuala: Na Itikafu inajuzu katika kila msikiti wa kuswaliwa swala ya Ijumaa ndani yake au hakuswaliwi Ijumaa ndani yake, ukiwa una sakafu au uko wazi, na msikiti huu ukiwa hauswaliwi swala ya jamaa ndani yake wala hauna Imamu, basi ni wajibu juu ya mtu huyu kutoka kwenda msikiti wa kuswaliwa swala ya jamaa ila ukiwa mbali na itakuwa ni uzito kwake basi si lazima kwake, ama kwa mwanamke asiyelazimika swala ya jamaa basi anaweza kuifanya Itikafu yake katika msikiti huu mdogo. Na wala haijuzu kwa mwanamke au mwanaume kufanya Itikafu pamoja au mmoja wao peke yake katika msikiti wa nyumba yake? Na dalili ya hayo kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hali mnakaa Itikafu msikitini.} [AL- BAQARA: 187]. Mwenyezi Mungu amesema kwa ujumla juu ya msikiti bila ya kuhusisha msikiti maalumu” [Al-Muhala 3\428, Ch. Dar AL-Fikr –Bairut].
Ama kauli ya kuhusisha Itikafu kwa Misikiti mitatu Mitakatifu ni kutokana na kauli ya Hudhaifah Ibn Al-Yamaniy R.A. na kauli hii ni haikuchuliwa na imekanushwa na jamhuri ya wanazuoni, kwani Hudhaifah alisisitiza juu ya simulizi moja iliyosemwa kuwa Itikafu ni lazima katika misikiti mitatu mitakatifu.
Na uchaguaji katika jambo hili ni kufanya kinyume cha Hadithi ya Hudhaifah kwa sababu zifuatazo:
Ya kwanza: Kuna hitilafu kati ya wanazuoni juu ya Hadithi ya Hudhaifah kwa Rafuuhu (kuinuliwa) kwake au waqfuhu (kusimamishwa) kwake,na haikusemwa kwamba kuinuliwa kwake (Hadithi) ni ziada katika uaminifu wake na ni kitu kinachokubalika kwa ujumla; kwani wahakiki wa suala hili hawasemwi kwa ujumla katika jambo hili, bali walisema kwamba kila Hadithi ina shani yake maalumu. Shekhi Salah Ad-Diin Al-Alaey alisema kwamba: “Inayoonekana kutokana na maneno ya wanazuoni waliotangulia kama Yahya Ibn Saeed Al-Qatwan na Abdulrahman Ibn Mahdiy na kadhalika baadhi ya waliokuja baada ya hawa wawili kama Ahmad Ibn Hanbal na Aly Ibn Al-Madeniy na Yahya Ibn Maayan na tabaka hili na waliokuja baada yao kama Al-Bukhariy, Abi Zaraah, Abi Hatem Ar-Raziin, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaiy na mifano yao na Ad-Dar Qatweniy na Al-Khaliliy, wanazuoni hawa wana maono yao kila mmoja ana rai yake katika suala hili lakini wote hawahukumu katika suala hili kwa sura ya ujumla kwa mujibu wa Hadithi zote kwani kila Hadithi ina ufahamu wake na mnasaba wake, na hukumu hii ni haki”. [Al-Nukat Ala Muqademat Ibn As-Swalah 2\157, Ch. Adhwaa As-Salaf Ar-Reyaadh].
Na Ibn Rajab Al-Hanbaliy alisema: “Hakuna tofauti katika ziyada baina ya Isnadi na Matini kama tulivyotaja katika Hadithi ya “Ndoa bila wali”, na imekaririwa katika kitabu hiki utajo wa tofauti katika waslu (kiunganishi) na irsaali (upelekaji), na waqfu (kusimamishwa) na rafuu (kuinuliwa),na maneno ya Ahmad na wengine waliohifadhi wanaelekea juu ya kuizingatia ni kauli yenye uaminifu na aliyehifadhi zaidi pia. Na Ahmad alisema katika Hadithi moja ya Hammad Ibn Salamah: kitu chochote kinafaa anaweza kukipeleka,na Al-Hakem alitaja kwamba maimamu wa Hadithi kwa mfumo wa wengi ni kama kwamba wengi wa maimamu hawa walipeleka Hadithi na hii ni dalili ya nguvu.Na hii ni kinyume cha kilichotajwa katika Al-Mustadrak” (Sarhu Ilal At-Tirmidhiy, 2\637, Maktabat Al-Mana, Az-Zarqaa, Al-Urdun).
Na kwa upande wa tafsiri ya hapo juu ya Al-Bukhariy pengine kuna ishara kwa upungufu mmoja katika Hadithi (marfuu), na jambo hili linafahamika na anayekuwa na elimu ya njia ya Al-Bukhariy katika tafsiri yake.
Ya pili: Inaweza kuchukuliwa Hadithi ya Hudhaifah juu ya hali ya ukamilifu kama katika Hadithi nyingine zilizofanana nazo, mfano wake Hadithi: “Hakuna swala kikiletwa chakula,wala kwa mwenye kubanwa na haja kubwa na ndogo”, jambo hili linachukuwa maana yake juu ya ukamilifu wa swala, kama alivyotajwa na Al-Menyawiy katika kitabu cha: [Faidhi Al-Qadiir 3\835, Ch. Dar Al-Fikr, Bairut].
Ya tatu: Ni wasiwasi uliokuja wa Ibn Masoud kwa jambo hilo,haiwezekani kuichukua dalili hii kama hoja kwa msemo wa sahaba kwa kuwepo kutofautiana kati ya sahaba; kwa sababu ya sharti la kutotofautiana kwa mwenye hoja, amesema Ibn Qudamah: “Asili ya pili kwa wenye kutofautiana ndani yake: “msemo wa sahaba ikiwa hakudhihiri mwenye kutofautiana naye” na kadhalika inasimuliwa kwamba: Rai hii ni hoja inatangulizwa juu ya kiasi, na inahusisha ujumla na hii ni rai ya Imam Malik, na Shafiy ya zamani, na baadhi ya wafuasi wa Al-Hanafiyah (Rawdhat An-Nadiir 1\466, Ch. Mu’assaset Ar-Rayaan kwa uchapishaji na kueneza).
Ya nne: Inawezekana Hudhaifah ameichukuwa rai hii kutoka katika Hadithi ya “Wala isifunge safari ila kwenda misikiti mitatu:Msikiti wa Makka, Msikiti wangu,na Msikti wa Al-Aqasa)), maana ya maneno yake yanachukuliwa kutokana na ufahamu wake kutoka Hadithi nyingine na siyo ufahamu wake wenyewe, kwa hivyo haichukuliwi kama ni hoja au dalili katika matini yaliyotajwa; na baadhi ya wanazuoni wanaafikiana na hayo, kati yao ni :Al-Fakher Ar-Raziy na Ibn Rudhed Al-Hafid.
AL-Fakher Ar-Raziy alisema: “Wanazuoni waliafiki kwamba sharti ya Itikafu siyo kukaa msikitini; kwani msikiti ulijengwa kwa ajili ya kutekeleza matendo ya utiifu ndani yake, halafu walitofautiana katika amri hii, alinukuliwa na bwana wetu Ali Ibn Abu Twalib R.A. alisema kwamba: Haijuzu Itikafu ila katika Msikiti wa Makka,na hoja yake hapa ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu:{Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu}[AL-BAQARA:125]. Maana ya hayo ni kwamba nyumba ya Mwenyezi Mungu ni kwa wanaojitenga wote kwa ajili ya Itikafu, na lau yajuzu kufanya Itikafu katika msikiti mwingine, yasingekuwa sahihi ile ya ujumla katika maana ya Aya hapo juu, na Atwaa alisema: Haijuzu Itikafu ila katika Msikiti wa Makka na Msikiti wa Madinah kutokana na usimulizi wa Abdullah Ibn Al-Zubeer kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Swala katika msikiti wangu huu ni bora mara elfu kwa thawabu kuliko katika msikiti mwingine isipo kuwa Msikiti wa Makah, na swala katika Msikiti wa Makka ni bora kuliko swala mara mia katika Msikiti wangu huu)). Na Hudhaifah alisema: inajuzu kufanya Itikafu katika Misikiti hii miwili na katika Msikiti wa Baytul Maqdis kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Wala isifunge safari ila kwenda misikiti mitatu:Masjid-Makka, Msikiti wangu ,na Msikiti wa Al-Aqasa”, na Az-Zuheriy alisema: “Haisihi Itikafu ila katika msikiti unaoswaliwa Ijumaa, na Hudhaifah alisema: Haisihi Itikafu ila katika msikiti wenye Imamu na Muadhini, na Ashafiy R.A., Alisema: Itikafu inakuwa katika misikiti yote ila kwamba Itikafu ni bora zaidi katika msikiti unaoswaliwa Ijumaa hata mtu anayefanya Itikafu hahitaji kutoka msikitini kwenda kuswali Ijumaa, na Ashafiy R.A., aanatoa hoja kwa Aya ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini}. [AL- BAQARAH: 187],
Kwani kauli ya Mwenyezi Mungu hapa ni kwa ujumla inachukuwa misikiti yote” [Mafateh Al-Ghaibu au At-Tafsiir Al-Kabiir 5\276, Ch. Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy, Bairut].
Na Ibn Rushd Al-Hafedh alisema: “Ama sababu ya kutofautiana kwao katika kuihusisha baadhi ya misikiti au wanaosema misikiti yote yaweza kufanyika Itikafu, walichukuwa kutokana na dhahiri ya Aya, na wanaosema kwa kuihusisha baadhi ya misikiti ni kwa mujibu wa kiasi, walishurutisha msikiti unaoswaliwa swala ya Ijumaa ili asikate Itikafu yake ili kutoka kwenda kuswali swala ya Ijumaa, au anaweza kufanya Itikafu katika msikiti kama Msikiti wa Mtume S.A.W., Aliyefanyia Itikafu yake S.A.W., na asichukuwe kiasi hiki juu ya misikiti mingine kwani yote haiku sawa na Misikiti mitatu mitakatifu katika heshima au utukufu wao”. [Bidayat Al-Mujtahed 2\77, Ch. Dar Al-Hadith, Bairrut].
Ya tano: Maimamu wa madhehebu yanayofuatwa hawakuchukua uwazi wa ya Hadithi ya Hudhaifah, na watu walichukua kinyume chake.
Ibn Rajab Al-Hanbaliy alisema: “Hadithi gharibu yoyote ni dhidi ya Hadithi mashuhuri, na wanazuoni waliotangulia waliisifia Hadithi mashuhuri kati za Hadithi zote, na Hadithi gharibu walizishutumu kwa ujumla, na kati ya kauli hii ni kauli ya Ibn Al-Mubarak: elimu inakujia kutoka hapa na hapo, yaani kutoka katika Hadithi mashuhuri. iliyopokewa na Al-Baihaqiy kutoka kwa At-Termidhiy kutoka kwa Ahmad Ibn Abdha, kutoka kwa Abi Wahb kutoka kwake, imepokewa pia kutoka kwa Az-Zaheriy kutoka kwa Ali Ibn Hussein, alisema: si katika elimu lile lisilojulikana, bali elimu ni linalojulikana kati ya wanazuoni, na katika suala hili Imam Malik alisema: shari ya elimu ni (Hadithi) gharibu, na kheri ya elimu ni (Hadithi) dhahiri iliyosimuliwa na watu. Na Muhamad Ibn Jaber alisimulia kutoka kwa Al-Aamash kutoka kwa Ibrahim alisema: Walichukizwa na Hadithi gharibu, na kauli gharibu. Na kutoka kwa Abi Yusuf alisema: Anayetaka Hadithi za gharibu ni mwongo….na Ali Ibn Uthman Al-Nufailiy alinakili kutoka kwa Ahmad alisema: Shari za Hadithi gharibu ni zile zisizofanyiwa kazi wala hazitegemewi. Na Al-Maruziy alisema: Nilisikia Ahmad anasema: Waliacha Hadithi maarufu na walichukuwa Hadithi gharibu na hii ni dalili juu ya upungufu wa Fiqhi kati yao…. Abu Bakr Al-Khatweb alisema: Wengi wa wanaotaka kusema katika zama hizi , wengi wao wanategemea vitabu vya (Hadithi) gharibu badala ya vitabu vya (Hadithi) mashuhuri, na wanasikia kauli ya kukanushwa badala ya kauli kweli,na wanashughulika sana kwa kauli zenye upungufu na makosa kutokana na wasimulizi waliotiwa kasoro na wasimulizi wenye udhaifu mpaka imekuwa kwao jambo sahihi wanaona ni geni na wanaliepusha, na hilo ni kwa sababu ya upungufu wa elimu yao ya kutenganisha na kwa sababu ya kutokujua hali za wasimulizi na mahala pao, na umbali wao na elimu hii. Na hii iliyotajwa na Al-Khatweb ni kweli kwani wengi wa wanazuoni wa kisasa hawavipi umuhimu vitabu vya Asili ya usahihi kama vitabu sita na kadhalika, na wanazipa umuhimu sehemu za Hadithi gharibu zaidi na vitabu vya kanusha kama: Musand Al-Bazar, Maajim At-Twabaraniy, Afrad Ad-Darqatweniy, na vitabu hivi vyote ni gharibu katika maoni yake. Na kati ya ugharibu wa (Hadithi) zake kuna Hadithi Munkari na Shadha nazo ziko namna mbili: Inayokuwa gharibu kwa upande wa Isnadi yake, na At-Termidhiy atataja baadhi ya mifano yake baadaye, na ya pili ni gharibu kwa matini yake ni kama Hadithi zilizokuwa kuna Hadithi nyingine sahihi badala ya Hadithi hizi na wanazuoni waliafikiana na ugharibu wa Hadithi hizi na usahihi wa Hadithi nyingine zilizochukuliwa”. [Sharhu Ilal At-Termidhiy 2\621-625]
Na At-Twhawiy Al-Hanafiy alisema “Mlango wa bayana ya matatizo yaliyosimuliwa na Hudhaifah Al-Yamaniy R.A kutoka kwa Mtume S.A.W., katika misikiti isiyojuzu kufanyia Itikafu ndani yake: Muhamad Ibn Senan As-Shezeriy alisema: alituhadithia Hisham Ibn Ammar alisema: Alituhadithia Sofiyan Ibn Ayinah kutoka kwa Jamea Ibn Abi Rashed kutoka kwa Abi Wael alisema: Huzayfah alisema kwa Abdullah: Hakuna badiliko katika Itikafu baina ya nyumba yako na nyumba ya Abu Musa, na nilijua kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Haisihi Itikafu ila katika Misikiti mitatu:Msikiti wa Makkah, Msikiti wa Mtume S.A.W., na Msikiti wa Baytul Maqdisi”. Abdullahi alisema: Labda wewe ulisahau na wao walihifadhi, na ulifanya makosa na wao walifanya usahihi. Abu Jaafar alisema: Tulizingatia Hadithi hii tulimkuta Hudhaifah alimwambia Ibn Masoud ya kuwa alikwishajua kwa lililotajwa na Mtume S.A.W., na Ibn Masuod aliacha kukanusha kwake katika jambo hili, na jawabu yake juu ya hayo kutoka kwa kauli yake: “Labda walihifadhi” alichukuwa nakala kutoka kwa lililotajwa, na walifanya usahihi lililofanyiwa, na dhahiri ya Qur`ani ina dalili juu ya hayo kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini}. [AL- BAQARA: 187], kauli ya Mwenyezi Mungu inamaana ya ujumla na kuweza kufanya Itikafu misikiti yote. Na Waislamu walikuwa wakifanya Itikafu katika misikiti ya nchi zao, hasa katika misikiti inayoswaliwa swala ya jamaa na Ijumaa na yenye maimamu na waadhini kutokana na kauli ya wanazuoni katika jambo hili, na tunamuomba Mwenyezi Mungu mafanikio” [Sharhu Mushkel Al-Athar 7\201, Ch. Muasaset Al-Resalah].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, inabainika kuwa inajuzu kufanya Itikafu katika misikiti mingine isiyo kuwa Misikiti Mitatu Mitakatifu: (Msikiti wa Makka, Msikiti wa Mtume na Baitulmaqdis), kadhalika ni wazi kwamba kazi zote zilizotangulia zinahusisha Hadithi ya Hudhaifah iliyotajwa kuhusu jambo hili la Itikafu na amejibiwa kwa sehemu nyingi hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas