Kuswali Baina ya Nguzo.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuswali Baina ya Nguzo.

Question

Je, nini hukumu ya kuswali baina ya nguzo? Je, swala hii inakata safu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Baadhi ya maamuma wa swala ya jamaa huwa wanaswali baina ya nguzo, inaweza kuwa wanafanya hivyo pasipo na dharura, na wakati mwingine wanafanya hivyo kwa sababu ya idadi kubwa ya maamuma kama katika swala ya Ijumaa, na baadhi ya watu wanalipinga jambo hilo, wakisema kuwa swala baina ya nguzo inakata safu.
Na wanavyuoni walizungumzia swala baina ya nguzo katika kitabu cha swala; walipozungumzia swala ya jamaa, na waligusia hukumu yake zamani na wakati wa sasa.
Kwa hukumu ya suala hili, inachukiza kama hakuna dharura, kama vile msongamano wa maamuma na kadhalika. Na kuchukiza kunaondoka kwa kuwepo kwa dharura.
Dalili ya hivyo ni iliyopokelewa kutoka kwa Abdul Hamid Ibn Mahmoud, aliyesema: Tuliswali nyuma Mkuu wa wakuu, tulilazimishwa kuswali kati ya nguzo mbili tukaswali, Anas Ibn Malik alisema: tulikuwa tukijipusha na hali hii wakati wa Mtume, S.A.W. Na katika sehemu nyingine kutoka kwa Qarah Ibn Iyas Al-Mazni. Hadithi ya Anas ni Hasana, na kuna baadhi ya Wanavyuoni walichukizwa kuswali baina ya nguzo, na kwa rai hii Ahmed na Ishaaq wanasema, na kuna baadhi ya Wanavyuoni wengine wameruhusu hivyo.
Kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Harun Ibn Muslim kutoka kwa Qatada kutoka kwa Muawiya ibn Kara, kutoka kwa baba yake, alisema: tulikuwa tukikatazwa kuswali baina ya nguzo wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. na tulikuwa mbali sana na hilo.
Nilisema: Hadithi hizi mbili zilisahihishwa na Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan, Al-Hakim na wengine. Hekima ya ushahidi huo ni wazi; asili ya katazo haliwi zaidi ya kuwa ni karaha, na kuongeza katazo mpaka wakati wa Nabii, S.A.W yanafanya hukumu hii kuwa ni marfuu kama ilivyo kwa wengi wa madhehebu ya Wanavyuoni wa Usuul waliotangulia na wengi wa wanachuoni wa Hadithi . [Rejea: Al-Mustasfa kwa Al-Ghazali uk. 150, Dar Al-Kitab Al-Ilmiyyah, Al-Taqriib wal Tayseer kwa Al-Nawawi uk. Dar Al-Kitab Al-Arabiy].
Haikutajwa katika katazo inaonesha uharamu kama adhabu au kitu kingine, na sikujua yeyote miongoni mwa Wanavyuoni aliyeharimisha hivyo. Labda kwa ajili ya kufanya masahaba hivyo pamoja na ujuzi wao kwa uharamu wake. Kisha kuonya kwao kwamba hawakuwa wakifanya hivyo katika zama za Mtume, S.A.W. pamoja na kufanya hivyo katika wakati wa sasa, hali hii inaonesha kwamba katazo lina maana ya kuchukiza si haraamu, au hawajawahi kufanya hivyo kabisa.
Imetajwa Hadithi Marfuu lakini ina udhaifu katika Sanad yake, nayo ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Epukeni kusimama katika safu baina ya nguzo”. Al-Hafidh Al-Haythami alisema: Attabarani katika Al-Awasat na Al-Kabiir, ambapo Ismail Ibn Muslim Al-Makki nayo ni dhaifu. [Majma’ A l-Zawaid wa Manba’ Al-Fawaid 2/92, Maktabat Al-Qudsi].
Baadhi ya Wanavyuoni walitaja kama tulivyotaja:
Al-Mardaawi Al-Hanbali, alisema: “(Inachukiza kwa maamuma kusimama baina ya nguzo kama safu zao zimekatika).
Uzinduzi: Sehemu ya kutofautiana: Ikiwa hakuna dharura, basi kama ikiwepo dharura haichukizi kusimama baina ya nguzo. Faida: Kauli yake: “Kama safu zao zimekatika” kauli hii inarejea desturi, Ibn Manja alisema katika maelezo yake: Baadhi ya marafiki zetu waliweka masharti kuwa upana wa nguzo unafikia dhiraa tatu; kwani hiyo ni ile iliyokata safu, na Abu Al-Maali pia alisema hivyo [Al-Insaaf 2/299, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy]. Al-Kharashiy Al-Malikiy alisema: “Swala baina ya nguzo inachukiza kama hakuna dharura, na baadhi yao waliainisha Fatwa hii kwa swala ya jamaa, kwa ajili ya kukata safu na kauli hii ina maelezo kwa mujibu wa kauli ya Abu Al-Hassan: mahali pa nguzo si nafasi. Au kwa sababu ni mahali pa mkusanyiko wa viatu. Au kwani ni mahali pa shetani”. [Sharhu Mukhtasar Khalil kwa Kharashi 2/28, Dar Al-Fikr].
Vile vile baadhi ya wanavyuoni walisema kuwa hakuna kuchukiza kabisa. Imam Abu Bakr Ibn Al-Mundhir alisema: “Hakuna katika sehemu hii habari yoyote inayothibitisha kuwa Mtume, SAW, alikataza kuswali kati ya nguzo, na hakuna ila maneno ya Anas kuwa: Tulikuwa tukijiepusha hivyo. Kama yeyote akijiepusha hivyo, basi ni bora, wala hapati dhambi anayefanya hivyo”. [Al-Awsat fi Al-Sunan, & Al-Ijmaa wal Ikhtilaf 4/183, Dar Taiba, Al-Riyad].
Jibu ni kwamba: msimamo wa Ibn Al-Mundhir pasipo na dalili unahitaji kuangaliwa, baadhi ya mapokezi yaliyo wazi kwamba suala hili lilikuwa katika zama za Mtume, S.A.W, nalo linazingatiwa kuwa miongoni mwa Sunna alizozikiri Mtume S.A.W. kwa uchache. Lakini kutothibitika kwake si kwa upande wa Sanad yake tukatolea usahihisho wake kutoka kwa wanavyuoni wengi. Ndiyo baadhi ya wanavyuoni walizungumzia Sanad ya Hadithi ya pili, Al-Hafidh Ibn Rajab Al-Hanbali alisema: “Ibn Al-Madini alisema: Sanad ya Hadithi hii siyo safi. Abu Muslim alisema: Hadithi hii haijulikani. Na Abu Hatem alisema: Hadithi hii haijulikani.” [Fath Al-Bari kwa Ibn Rajab 4/59, Maktabat Al-Ghurabaa Al-Athariyah - mji wa Mtume]. Tunasema: kama tukiamini kuwa Hadithi hii ni dhaifu, basi ni ushahidi kwa Hadithi ya Anas ya kwanza, na inasamehewa katika ushahidi isiyosameheka katika asili. Aidha, inajulikana kwamba ibada iliyokubaliwa na Wanavyuoni ni bora kuliko isiyokubaliwa, na kutoka nje ya tofauti ni vizuri.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inajulikana kwamba inachukiza kuswali baima ya nguzo kwa maamuma katika swala ya jamaa kama hakuna dharura kama vile msongamano wa maamuma na ufinyu wa mahali pa kuswali.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas