Maelezo ya Kusudio la Kupanda kwa J...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maelezo ya Kusudio la Kupanda kwa Jua Kiasi cha Urefu wa Mkuki.

Question

Kumekuwa na misamiati mingi kwenye vitabu vya Fiqhi inayosema “kupanda kwa jua kiasi cha urefu wa mkuki”, ni nini makusudio ya msamiati huu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Imepokewa na Imamu Ahmad na An-Nisaaiy kutokana na Hadithi ya Abu Amama Al-Baahiliy, anasema: nimemsikia Amru Ibn Abasa anasema: “Nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je kuna muda ulio karibu zaidi kuliko muda mwingine wowote? Mtume akasema ndiyo, hakika muda ambao Mola Mtukufu Anakuwa karibu zaidi na mja ni wakati wa usiku wa manane, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wamtajao Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya muda huo, basi unaweza kuwa, kwani Swala ndani ya wakati huo inakuwa ni yenye kuhudhurishwa na kushuhudiwa mpaka machomozo ya jua, kwani lenyewe huchomoza kati ya pembe mbili za shetani, nao ni muda wa swala ya makafiri, basi acha kuswali mpaka jua lipande kidogo kiasi cha mkuki na kuchomoza miyale yake, kisha Swala inakuwa ni yenye kuhudhurishwa na kushuhudiwa mpaka pale jua linapokuwa lipo sawa sawa wa mshale kwa nusu ya mchana, kwani wenyewe ni muda ambao hufunguliwa milango ya jahanamu, hivyo acha kuswali mpaka jua linapopindukia, kisha Swala inakuwa ni yenye kuhudhurishwa na kushuhudiwa mpaka pale linapozama jua, kwani jua lenyewe huzama kati ya pembe mbili za shetani nao ni muda wa swala ya makafiri”.
Na katika vitabu sahihi vya Imamu Bukhariy na Muslim kutokana na Hadithi ya Abi Said Al-Khudriy R.A., amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anasema: “Hakuna Swala baada ya Swala ya Alfajiri mpaka lichomoze jua, na wala hakuna Swala baada ya Swala ya Al-Asiri mpaka lizame jua”.
Katika Hadithi hizi mbili zinafahamisha kuwa kuna wakati inakuwa kuswali ndani ya wakati huo ni jambo linalochukiza, na maana ya Swala kuchukiza ndani ya wakati huo kwa maana ya kuchukiza kwa kuswali Swala ya Sunna, nayo ni Swala ambayo haina wakati au sababu, na hiyo ni kama vile mtu kutaka kuswali rakaa mbili akimwabudu Mwenyezi Mungu kwa rakaa hizo, au mwenye kutaka kuswali Swala ya kumtaka ushauri Mwenyezi Mungu, basi anaweza kusukuma mbele muda wake, ama kwa mwenye kulipia kadha kwa Swala iliyompita kwenye wakati wake na mwenye kuswali rakaa mbili za udhu na Swala ya Haja, basi haingii kwenye katazo. Na miongoni mwa nyakati hizi ambazo kuswali ndani yake inachukiza ni pamoja na wakati wa kuchomoza kwa jua mpaka lipande kidogo kiasi cha urefu wa mkuki, na imepokelewa katika baadhi ya mapokezi kuwa ni: (kiasi cha urefu wa mikuki miwili).
Ni wakati ambao jua huwa limenyanyuka kutoka mawinguni kiasi cha urefu wa mkuki au mikuki miwili, hizo ni nyakati ambazo zimefungamanishwa na masuala mengi ya kisharia kama ni muda wa mwanzo wa wakati wa Swala ya Adhuha kwa baadhi ya wanachuoni wa Sharia au Fiqhi, lakini pia ni mwanzo wa wakati wa Swala za Idd mbili na Swala zengine.
Waarabu hapo zamani walikuwa wanapambanua na kutenganisha miaka kwa matukio, kwa mfano wanasema: mwaka wa tembo, walikuwa wanakadiria urefu wa muda kwa matukio yaliyotokea ndani ya kipindi kile, amenukuu Baihaqiy katika kitabu cha: [Al-Maarifa] kauli ya Imamu Shafiy: nimepata taarifa kutoka kwa baadhi waliopita kuwa mtu mmoja alitoa amri ya mtu kukaa mbele ya kaburi lake atakapokuwa ameshazikwa kiasi cha umbali wa urefu wa mzizi, hili sijaona watu wa zama hizi wakifanya hivyo. [Maarifat Sunan wa Al-Athar, 5/333, chapa ya Dar Qutaiba]. Kama vile walivyokuwa Waarabu wakitambua maeneo kutokana na maeneo yaliyo karibu nayo na mfano wa hivi. Mfumo wa Qur`ani umechunga umaalumu huu katika lugha ya Kiarabu Mwenyezi Mungu Akasema: {Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi} [ANAJM: 9] kwa maana ya Jibrir alimkaribia Mtume Muhammad S.A.W. pale alipoteremka kwenye sayari ya ardhi mpaka ikawa kati yake na Mtume Muhammad S.A.W. kiasi cha pinde mbili kwa maana ya kiasi cha pinde hizo. [Tafsiri ya Al-Baghwiy, 4/303, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Na yaliyopokewa kwenye Hadithi pamoja na kufungamanishwa na “kiwango cha urefu wa mkuki” au “mikuki miwili” hayo ni katika muundo huu wa Qur`ani, nayo ni katika alama ambazo wameziweka Waarabu za kupimia vitu, na kuna lugha karibu tano zikiwa na maana ya kiasi cha mshale kwa maana ya urefu wake, na makusudio ni kuchomoza kwa jua kiasi cha urefu wa mshale au urefu wa mishale miwli na kuwa linaonekana kwa mwenye kuangalia wakati wa kuchomoza kwake urefu wa mkuki au mikuki miwili, imenukuliwa kutoka kwa Ibn Rajab katika sherehe yake ya Hadithi ya katazo la Mtume S.A.W. kuswali baada ya Swala ya Alfajiri mpaka machomozo ya jua, na baada ya Swala Al-Asiri mpaka kuzama kwa jua, amesema: “Kisha akahusisha mpaka kuchomoza kwa jua kiasi cha urefu wa mkuki au mikuki miwili”, na akaseme Sufyan kutoka kwa Hisham pia kutoka kwa Ibn Syriyn: “Ni haramu kuswali muda wa kuchomoza kwa jua mpaka lifikie kiasi cha mtende” [4/55, chapa ya Maktabat Al-Gharb Al-Athariya – Madina Al-Nabawiya].
Ikiwa mtu ataangalia jua wakati wa kuchomoza kwake na kufikia kiwango hiki kwa mtazamo wake, basi kwake utakuwa umeondoka wakati wa kuchukiza kuswali, na unakuwa unaingia wakati wa Swala ya Adhuha kwa kauli ya baadhi ya wanachuoni wa Sharia au Fiqhi.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas