Mtu Mwingine Kusema Bismillahi Bad...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtu Mwingine Kusema Bismillahi Badala ya Mchinjaji.

Question

Je, kusema Bismilahi kwa asiye mchinjaji, usemaji huo utatosha katika uchinjaji wa kichinjo hicho? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuhalalishia wanyama na akatuwajibisha tuwachinje kwa ajili ya kuifanya nyama yao iwe nzuri na kwa ajili ya kutimiza neema yake, na akatuharamishia mnyama aliyekufa bila ya kuchinjwa kisharia na uchinjaji wake sio kwa njia yoyote ile, lakini kwa njia maalumu ambayo sharia tukufu imetuainishia.
Na wanazuoni wamekubaliana kiwango maalumu cha uchinjaji wa kisharia ambao ni umwagaji wa damu ya mnyama katika sehemu ya kuchinjwa, na wakatofautiana: ni ipi hiyo sehemu ya kuchinjwa? Je ni katika koo au katika mshipa wa shingo na moja ya mshipa wa fahamu au ni koo pamoja na mshipa wa shingo? Na wala haishurutishwi umio.
Na wametofautiana katika kusema Bismillahi, je ni wajibu au ni Sunna, na aliyesema kuwa hiyo ni wajibu alisema: kichinjo hakisihi kwa kuachwa kwa makusudi, na ikiwa kitaachwa kwa usahaulifu basi kitasihi kichinjo hicho, na wakakifaradhisha kwa mchinjaji tu na wala si kwa mwingine kama tutakavyoona, na iwapo atasema hivyo asiye mchinjaji basi haitoshi katika uchinjaji huo wa mnyama.
Ama ambaye anasema kuwa kusema Bismillahi ni Sunna, basi amesema: “Kichinjo kitakuwa halali kwa kuachwa Bismillahi kwa makusudi, au kuachwa kwa usahaulifu”. Na kinachochaguliwa katika Fatwa ni rai ya Jamhuri ya wanazuoni katika uwajibu unaofungamana na kukumbuka bila kusahau na iwapo Bismillahi itaachwa kwa kusahau basi mnyama atakuwa halali, na ikiwa atasema Bismillahi asiye mchinjaji basi usemaji huo hautoshi katika uchinjaji wa kichinjo hicho, na inajuzu katika hali kama hii tukifuata kauli ya Imamu Shafi ya kuwa Bismillahi ni Sunna.
Na yafuatayo ni maelezo kwa ufafanuzi katika pointi mbili:
Ya Kwanza: Kueleza uhakika wa uchinjaji wa kisheria pamoja na hukumu ya kusema Bismilahi.
Ya Pili: Hukumu ya kusema Bismillahi kwa asiye mchinjaji.
Ya Kwanza: Maana ya Uchinjaji (Utambuzi) katika lugha;
Utimilifu kama alivyosema Ibn Mandhuur katika kitabu cha: [Al Lisaan] ambapo amesema: “Na asili ya utambuzi kilugha ni kukamilisha kitu kwa ujumla, na miongoni mwa hayo kuna kukamilika kiumri na kiakili, nako ni kukamilika Umri, amesema: na Khaliil amesema: utambuzi wa umri ni mtu kumjuwa mnyama wake kwa maana ya farasi wake mwaka mmoja, na huu ni ukamilishaji wa kukamilika kwa uwezo (nguvu) yake”. [Lisaan Al Arab, Mada ya Zaka 288/14, Ch. Dar Al Maaref, na Az Zaaher Fi Ghareeb Alfaadh Ashafiy kwa Abi Mandhuor Al Azhariy, Uk. 263, Ch. Dar At Twalae’].
Na kuchinja kisharia ni kumchinja mnyama anayeliwa na wa nchi kavu au kumchinjia kwa kukata koo na mshipa mkuu, au kujeruhi kunakozuiliwa. [Ar Raudh Al Muraba’ kwa Al Bahutiy, Uk. 689, Ch. Dar Al Muayad na Muasasat Ar Resalah]
Na Imamu Mkuu wa Al Azhar; sheikh Jad Al Haq Ali Jad Al Haq na Mufti wa Misri aliyepita alitoa maelezo kuchinja kisharia katika Fatwa aliyoitoa kwake tarehe 12, Mfunguo Mosi 1401 Hijra, sawa na tarehe 13 /8/1981 kwamba: kuchinja ni kwa kitu kikali kwa namna ambayo damu itatoka na kukata mishipa ya fahamu na mishipa ya damu iliyopo kati ya kichwa na kifua.
Kwa hiyo, basi uchinjaji wa kisharia ambao mnyama wa nchi kavu anahalalishwa nao ni kuwa anachinjwa au Anamchinja kwa kitu kikali katika vinavyopelekea damu kumwagika na kuikata mishipa, kwa maana ya kuibubujisha damu ya kichinjo na kuikata mishipa yake ya shingoni kati ya kichwa na kifua na mnyama kufa kwa kitendo hicho, na ukamilifu wa uchinjaji ni kulikata koo na mshipa mkuu wa hewa (nayo ni mapito ya chakula maji na hewa) na kukata pamoja na viwili hivyo, mishipa miwili mikubwa iliyo kandokando ya koo pamoja na mshipa mkuu wa hewa.
Na wanavyuoni wa Fiqhi wakatofautiana katika hukumu ya kusema Bismillahi katika uchinjaji, basi madhehebu ya Hanafi wanaonaona kuwa kusema Bismilaahi ni wajibu, na ikiachwa kwa makusudi basi kichinjo au kiwindo hakiwi halali. Na kama ikiachwa kwa usahaulifu basi kichinjo kitakuwa ni halali kuliwa. [Ad Daar Al Mukhtaar na Hashiyatahu 299/6, Ch. Dar Al Fikr]
Na katika madhehebu ya Kishafiy ni kwamba kusema Bismillahi wakati wa kuchinja au kuwinda siyo wajibu lakini ni Sunna, na kama ikaachwa kwa makusudi au kwa usahaulifu basi itakuwa halali kuliwa, na wajibu ni kutokutaja isipokuwa Jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu. [Mughniy Al Muhtaaj 105/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na wanavyuoni wa Madhehebu ya Maliki wana kauli mbili: Ya kwanza ni ile inayotegemewa ni uwajibu wa kutaja jina na kutohalalika kile kilichochinjwa bila kutaja jina kwa makusudi, na kuhalalika kilichosahaulika kutajwa jina. Na kauli ya pili kama Madhehebu ya Imamu Shafi kuwa kuacha kutaja jina kwa makusudi au kwa kusahau hakuharamishi kichinjo na mnyama aliyewindwa. [Balghat As Saalik La Aqrab Al Matwalib 171/2, Ch. Dar Al Maaref]
Na adhehebu ya Kiambali; ni uwajibu wa kusema Bismllahi, na kutohalalika kichinjo ambacho kimeachwa kusemwa Bismillahi juu yake kwa makusudi au kwa kutofahamu, lakini ikiachwa kwa usahaulifu basi ni halali kuliwa. [Kashaaf Al Qinaai’ 208/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Ya Pili: Hukumu ya kusema Bismillahi kutoka kwa asiye Mchinjaji:
Haitoshelezi kusema Bismillahi kwa asiyekuwa mchinjaji katika uchinjaji wa mnyama; kwani usemaji huo lazima ufanywe moja kwa moja na mchinjaji yeye mwenyewe. Na dalili za hayo ni kama yafuatayo:
Dalili ya Kwanza; Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu niMwepesi wa kuhisabu}. [AL MAIDAH 4}
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu}. Amri iliyomo ndani yake ni kwa uwajibu na kiwakilishi jina katika neno "juu yake" kinarejea kwa kinachochinjwa, na wala hataji ila mchinjaji kama ambavyo hataji wakati wa kutawadha isipokuwa mwenye kutawadha. Kwa hiyo Mtume S.A.W. akasema katika uwindaji: “Ukimtumia mbwa wako na ukisomee jina la Mwenyezi Mungu juu yake”, basi neno la (ukimtumia), na (ukisomee), yana maana yake ni kwamba wewe mwenyewe ndiye unayesema Bismillahi.
Dalili ya Pili; ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mnakheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu}, [AL HAJI 36]. Na amri ndani yake ni kwa uwajibu.
Na hizo ni baadhi ya kauli za wanavyuoni ambazo zinaunga mkono maoni hayo:
Al Haswkafiy amesema katika kitabu cha: [Ad Durr Al Mukhtaar]: “Na inashurutishwa kusema Bismillahi katika uchinjaji (wakati wa uchinjaji) au kutupa ili kuwinda au wakati wa kuanza kurusha mkuki.
Na Ibn Abdeen akafafanua maneno hayo basi akasema: “Na Kauli yake: (kutoka kwa mchinjaji) amekusudia kwa neno mchinjaji kwa maana ya muhalalishaji wa mnyama aliyechinjwa: na kwa hivyo ikakusanya mtupa mkuki na mshale na mweka chuma, na akakusudia kwa namna ambayo kama wangelikuwa wachinjaji ni wawili kama mmoja wao alitaja jina na mwenzake akaacha kwa makusudi basi mnyama huyo atakuwa haramu kuliwa”. [Hashiyat Ibn Abdeen Ala Ad Dar Al Mukhtaar 302/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na katika kitabu cha: [Al Fatawa Al Hindiyah 352/5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: “Na katika masharti ya kusema Bismillahi ni kuwa kusema huko kufanywe na mchinjaji hata kama mtu mwingine atafanya hivyo na mchinjaji akawa kimya hali ya kuwa anakumbuka bila ya kusahau basi haitahalalika”.
An Nafrawiy anasema katika kitabu cha: [Sharhu An Nafrawiy Ala Ar Resalah 382/1, Ch. Dar Al Fikr]; “(Na aseme mchinjaji) au mwenye kuchinja kwa upande wa uwajibu pale anapotaka kuchinja (Bismillahi Allahu Akbar) amesema Khaliil: (Na nia yake imekuwa wajibu na kutaja Bismillahi iwapo atakumbuka au ataweza)”.
Al Mardawiy akasema katika kitabu chake cha: [Shuruti Ad Dhaabeh 399/10, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]; “Sharti la nne ni kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa uchinjaji”.
Na katika kitabu cha: [Matwaleb Uliy An Noha kwa Ar Ruhaibaniy 421/3, Ch. Alam Al Kutub], “Sharti la nne: ni kusema Bismillahi pale anapounyanyua mkono wake kwa ajili ya kuchinja; kwa maana kuwa kwenda kinyume ni haramu (mchinjaji) nafasi yake haichukuliwi na mtu mwingine yeyote. Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msile katika wale wasio somewa jina laMwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu}. [AL ANAAM 121] Na upotofu ni haramu”.
Ibn Qudamah akasema katika kitabu cha: [Shuruti Ad Dhaabeh 293/9, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]: “(Na kutamka jina kunazingatiwa wakati wa kuanza kurusha mkuki kwani kitendo kilichopo ni kutoka kwa aliyerusha, kwa hiyo usemaji wa Bismillahi unazingatiwa kutoka kwake, kama ambavyo uchinjaji unazingatiwa kwa mchinjaji, na wakati wa urushaji wa mkuki kutoka kwa mrushaji (Ahmad amelizungumzia jambo hili)”.
As Shaukaniy akasema katika kitabu cha: {As Saili Aj Jarar Fi Sharh Hadaiq Al Azhaar 65/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: “Uhalisi kwamba kutaja jina la Mwenyezi Mungu ni faradhi juu ya mchinjaji”.
Na kutokana na maelezo hayo: Ni kwamba kusema Bismillahi kwa asiyekuwa mchinjaji hakutoshelezi wakati wa kuchinja mnyama, kwa mujibu wa madhehebu ya aliyesema kuwa kusema Bismillahi ni wajibu, iwapo mchinjaji hakusema Bismillahi kwa makusudi basi hakika yeye atakuwa anaifuata kauli ya anayesema kuwa kufanya hivyo ni Sunna, na kwa hivyo hakika mambo yalivyo kichinjo hicho ni halali na wala hakuna ubaya wowote kukila.
Na Mweneyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas