Hukumu ya Mchinjaji Kuchukua Nywele Zake na Kucha Zake Baada ya Kuingia Mwezi wa Dhul-Hijjah
Question
Ni upeo gani wa Sunna au uzushi wa mchinjaji kutochukua chochote katika nywele zake na kucha zake baada ya kuingia mwezi wa Dhul-Hijjah?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kichinjo - kwa kutia dhwammah katika alifu ni lugha mashuhuri - wingi wake ni Vichinjo, nacho ni mbuzi au kondoo anayechinjwa siku ya kuchinja. Na tunaposema amemtoa mnyama maana yake amemchinja siku ya kuchinja. [Rejea mada ya: (Dhahu) katika kitabu cha: Al Muswbah Al Muneer kwa Al Fayumiy, Uk. 358, Ch. Al Maktabah Al Elmiyah, Bairut. Na Lesaan Al Arab kwa Ibn Mandhuor 476/14, Ch. Dar Swader, Bairut]
Na kichinjo ni kile kinachochinjwa katika wanyama wanaoliwa kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika yale masiku ya kuchinja. [Hashiyat Al Bijermiy Ala Sharhi Al Manhaj 294/4, Ch. Mustafa Al Halabiy]
Na kichinjo ni Sunna iliyotiliwa mkazo kwa mwenye uwezo, kwa yaliyopokewa na Muslim katika Sahihi yake, kutoka kwa Anas R.A. amesema: “Mtume S.A.W alichinja kondoo wawili wazuri wenye pembe walionona na aliwachinja kwa mikono yake akataja jina la Mwenyezi Mungu na akatoa takbira na akauweka mguu wake baina ya pande mbili za shingo”. Na pia kwa yaliyo kuja katika kitabu cha: [Sunnan Ibn Majah] kutoka kwa Abi Hurairah amesema: Hakika Mtume Wa Mwenyezi Mungu S.A.W., amesema: “Mwenye uwezo na akawa hakuchinja basi asiikurubie sehemu yetu ya kuswalia”. Al Baihaqiy amepokea kutoka kwa Hudhaifah Bin Usaid amesema: “Mimi niliwaona akina Abu Bakr na Omar R.A.wote wawili, hawachinji kwa ajili ya watu wao, kwa sababu ya kuchelea isije ikazoeleka kwa watu nao wakaifanya kuwa ni Sunna kwa watu wote”. Walichelea kwamba watu wasije wakaliona jambo hilo kuwa ni wajibu.
Na inasuniwa kwa mchinjaji anapotaka kuchinja, na kwa anayejua kwamba mtu mwingine anamchinjia, asiondoshe chochote katika nywele za kichwa chake au za mwilini mwake kwa kunyoa au kupunguza au kwa njia yoyote iwayo, wala asitoe kucha zake kwa kuzikata au kwa njia yoyote iwayo. Na hayo ni kutoka kuanza usiku wa kwanza wa mwezi wa Dhul-Hijjah hadi kumalizika kuchinja kichinjo.
Na dalili ya hayo ni iliyotolewa na Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Umm Salamah R.A. kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Zinapoingia siku kumi za kwanza za mwezi wa Dhul-Hijah, na mmoja wenu akataka kuchinja basi asiguse chochote katika nywele zake au mwili wake”. Na katika usimulizi mwingine katika kitabu cha: [Sahihu Muslim] pia: “Mtakapouona mwezi mwandamo wa Dhul-Hijah na mmoja wenu akataka kuchinja basi inachukiza kwake kukata nywele zake, (basi na ajizuie kukata nywele na kucha zake) au kukata kucha zake, wala haiwi haramu.
Basi inachukiza kwa mchinjaji kuondosha nywele zake au kukata kucha zake na haiharamishwi, kwa yaliyotolewa na Al Bukhariy katika Sahihi yake kutoka kwa Bibi Aisha R.A. Amesema: “Nilikuwa ninazisokota kamba za wanyama wa Mtume S.A.W., kisha yeye anawavisha hizo kamba na anawapeleka kunakohusika, na wala haharamishi chochote katika alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka siku ya kuchinja mnyama wake”.
Imamu An Nawawiy akanukulu katika kitabu cha: [Al Majmuo’] kutoka kwa Imamu Shafiy kauli yake: “Kutumwa kwa uongofu (kichinjo) ni bora zaidi ya utashi wa kuchinja, na maneno haya yakamaanisha kuwa hivyo si haramu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi”. [Al Majmuo’ Sharhu Al Muhazab 392/8, Ch. Dar Al Fikr]
Imamu An Nawawiy wa kishafiy akasema: “Madhehebu yetu ni kwamba kuondosha nywele au kucha katika kumi la ibada ya Hijjah kwa atakaye kuchinja kunachukiza chukizo la kuzuiliwa mpaka mtu achinje”. Na Malik na Abu Hazaifah wakasema: hayachukizi, Na Said Bin Al Musaib, Rabiah, Ahmad, Ishaq na Dawud wakasema Inaharamishwa. Na kutoka kwa Malik kwamba inachukiwa na Ad Daramiy akasimulia kutoka kwake kwamba ni haramu Katika (Hijjah ya) kujitolea na wala Haiwi haramu katika (Hijjah ya) wajibu.
Na lengo la kuzuia kunyoa na kukata kucha ni zuio la kuondosha kucha kwa kukata au kuvunja au kwa njia yoyote iwayo, na zuio la kunyoa nywele kwa kunyoa au kupunguza au kunyonfoa au kuzichoma au kwa maada ya kunyofolea au kwa njia yoyote iwayo, ziwe nywele hizo ni za utupuni, kwapani au masharubu na nyinginezo.
Wenzetu wakasema: “Hekima ya katazo hili ni kuwa mtu awe kamili ili aepushwe na moto, ba ikasemwa pia kuwa ni kujifafanisha na aliyehirimia”, Imemalizika kwa kutumia. [Al Majmuo’ Sharhu Al Muhazab 392/8, Kwa kutumia].
As Swawiy wa Kimalikiy akasema katika kitabu chake cha: [Hashiyat As Swawiy Ala Asharhi Aswagheer]: “Ni Sunna kuacha kunyoa nyewele za mwili mzima na kuacha kukata kucha pia ndani ya siku tisa za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hjjah kwa mwenye kutaka kuchinja hata kama ni kwa kumchinjia mtu mwingine badala yake”. [Hashiyat As Swawiy Ala Asharhi Aswagheer 141/1, Ch. Dar Al Maaref]
Imamu Ibn Qudamah wa Kihambaliy akafupisha hitilafu katika suala hilo basi akasema: “Na anayetaka kuchinja na akaingia katika kumi la ibada basi asitoe chochote katika nywele zake au ngozi yake. Al Qadhi na kundi miongoni mwa wenzetu wakasema: Hiyo inachukiza, sio haramu, na kwa rai hiyo akasema Imamu Malik na Shafiy, kwa ajili ya kauli ya Bibi Aisha R.A.,: “Nilikuwa ninazisokota kamba za wanyama wa Mtume S.A.W., kisha yeye anawavisha hizo kamba na anawapeleke kunakohusika, na wala haharamishi chochote katika alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka siku ya kuchinja mnyama wake”, Inawafikiana nayo. [Al Mughniy Al Matwbuo’ pamoja na Asharhu Al Kabeer 96/11, Ch. Al Kitaab Al Arabiy]
Na ya madhehebu kwa wanachuoni wa Kihambali uharamu wa kuchukua nywele na kucha kwa anayetaka kuchinja zikiingia siku kumi za kwanza katika mwezi wa Dhul-Hijja; Al Bahutiy anasema katika kitabu cha: [Sharhu Al Muntaha; Daqaiq Uliy An Nuha kwa Sharh Al Muntaha 614/1, Ch. Aalam Al Kutub]: “Na ikiingia Kumi la Ibada yaani siku kumi za kwanza mwezi wa Dul-Hijjah; “Imeharamishwa kwa anayechinja au kuchinjiwa kwa niaba yake, kutoa chochote katika nywele, kucha au ngozi yake hadi atakapochinja, yaani uchinjo wa kichinjo. Kwa mujibu wa Hadithi ya Ummu Salamah ambayo ni Mar-fuu)) Linapoingia kumi la ibada na akataka mmoja wenu kuchinja basi asichukue chochote katika nywele au kucha zake hadi atakapochinja. Na katika Mapokezi: wala kutoa kitu katika ngozi yake.
Na hayo yakajadiliwa katika yaliyotanguliza kutoka matamko ya Imamu An Nawawiy kutoka kwa Hadithi ya Bibi Aisha R.A.
Na kutokana na yaliyotangulia: Hakika mambo yalivyo inasuniwa kwa mwenye kutaka kuchinja asitoe chochote katika nywele au kucha zake unapoingia mwezi wa Dhul-Hijah mpaka atakapochinja, na wala haiwi haramu kwake kufanya hivyo, na kutochukua ni bora zaidi kwa ajili ya kutoka katika kwenda kinyume na Wafuasi wa Madhehebu ya Hambaliy.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.