Swala ya Ijumaa Kwenye Misikiti Mid...

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Ijumaa Kwenye Misikiti Midogo.

Question

Ni ipi hukumu ya kuswaliwa Swala ya Ijumaa kwenye Msikiti mdogo? 

Answer

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Sala na salamu ziwe kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, na watu wake, Masahaba wake na wale wote wanaomfuata.
Baada ya utangulizi huo.
Swala ya Ijumaa: ilifaradhishwa katika tukio la kwanza la kuhama Mtume S.A.W, Makka na kuhamia katika mji wa Madina, na imethibiti kufaradhishwa kwake kwa kauli yake Mola Mtukufu pale Aliposema: {Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, nawacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua} [AL-JUMA’,9].
Swala ya Ijumaa haina sharti la kuswaliwa msikitini, isipokuwa inafaa kuswaliwa sehemu ya wazi au kwenye majengo, na wala siyo sharti la kufaa kwake lazima iswaliwe msikitini, kwani inafaa Swala ya Ijumaa kuswaliwa kwenye Msikiti mdogo na sehemu zilizoandaliwa kuswalia.
Amesema Ibn Al-Qayim katika kitabu cha: [A’un Al-Maabud]: “baadhi wamesema sharti lazima iswaliwe msikitini kwa sababu yenyewe haijaswaliwa isipokuwa ndani ya msikiti, na akasema Abu Hanifa na Imamu Shafiy na wanachuoni mwengine kuwa: swala hii kuswaliwa msikitini si sharti, nayo ni kauli yenye nguvu kwani Mtume S.A.W. aliwahi kuswali katikati ya bonde la Ibn Saad na watu wa As-Sair, lau ingethibiti kutofaa kuiswali mahala hapo bado haijaonesha kuswaliwa msikitini ni katika sharti zake”. [kitabu cha U’un Al-Maabud, 3/281, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Na amesema As-Shaukaniy katika kitabu cha: [Nail Al-Autwar]: “Na amesema Hady kuwa ni sharti kuswaliwa msikitini, amesema: kwa sababu yenyewe haikuswaliwa isipokuwa ndani ya msikitini. Na akasema Abu Hanifa, Shafiy na Al-Muayid Bilah pamoja na wanachuoni mwengine kuwa: kuswaliwa msikitini siyo sharti, wakasema: ikiwa dalili yake haitatoa maelezo ya kina. Akasema katika kitabu cha Al-Bahr: nikasema: kutokuwa sharti la kuswaliwa msikitini ni kauli yenye nguvu ikiwa Mtume S.A.W Swala yake ilifaa kuswali kati kati ya bonde. Kwani imepokelewa kuwa Mtume S.A.W Swala yake ilifaa pale aliposwali kati kati ya bonde la Ibn Saad na watu wa As-Sair, na ikiwa itakuwa haikufaa Swala yake bado haijaonesha kuiswali msikitini kuwa ni katika masharti yake” [Kitabu cha Nail Al-Autar cha Shaukaniy, 3/278, chapa ya Dar Al-Hadith].
Amesema Imam An-Nawawiy: “wamesema watu wetu: na wala hakuna sharti la kuswaliwa msikitini, lakini inafaa kuswaliwa kwenye eneo la wazi kwa sharti eneo hilo liwe ndani ya kijiji au mji, lau wataenda kuiswali nje ya mji au kijijini swala yao haitokubalika bila ya kuwepo tofauti yoyote ile katika hilo, ni sawa sawa sehemu hiyo ya wazi ipo karibu na mji au mbali, na ni sawa sawa wameiswali kwenye nguzo (sehemu ya ndani) au sehemu ya wazi, na dalili yake ni kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Swalini kama mulivyoniona mimi nikiswali” na wala Mtume hakuswali hivi [Majmu’ Sharh Al-Muhadhab, 4/501, chapa ya Dar Al-Fikr].
Amesema Hafidh Zainuddin Abdulraheem Ibn Al-Hussein Al-Iraqiy: “Madhehebu yetu kwa maana ya madhehebu ya Imamu Shafiy tunasema kuwa: kuswaliwa Sala ya Ijumaa hakuusishi kuwa sharti kuswaliwa msikitini lakini huswaliwa kwenye maeneo tofauti” kitabu cha: [Tarh At-Tathrib katika sherhe At-Takrib, 3/190, chapa ya Dar Al-Fikr Al-Arabiy].
Lakini hata hivyo kuna masuala mengine yanayofungamana na swali, nayo ni kuwa Jopo la wanachuoni wamekubaliana kutofaa kuswaliwa swala nyingi za Ijumaa isipokuwa katika hali ya dharura, na dharura hukadiriwa kwa makadirio yake. Amekwenda kinyume nao Atwaa kama ilivyopokelewa na Abdulrazaq kutoka kwa Ibn Jarij amesema: nilimwuliza Ataa: Umeona watu wa Basra hauwatoshi msikiti mkubwa je, watafanyaje? Akasema: “Kila kundi la watu wanamsikiti wao wanakutana humo, kisha unawatosha”, amesema Ibn Jarij: watu wakapinga hilo la kukusanyika isipokuwa ndani ya msikiti mkubwa.
Amesema Ibn Qudama katika kitabu cha Al-Mughniy, 2/248, chapa ya Maktabat Al-Kahera: “Upambanuzi: ama kutokuwepo haja, basi wala haifai kuswaliwa Swala ya Ijumaa zaidi ya sehemu moja, ikiwa itatosheleza sehemu mbili, basi haifai kuswalia sehemu ya tatu, na vile vile zaidi ya sehemu hizo tatu, hatufahamu katika hili tofauti, isipokuwa Atwaa aliulizwa: watu wa Basra msikiti mkubwa hauwatoshi. Akasema: kila kundi la watu wanamsikiti wao wanaokusanyika ndani yake na kunawatosha hilo kukusanyika ndani ya msikiti mkubwa.
Na bora lililokubaliwa na Jopo la wanachuoni ni kuwa, ikiwa haijanukuliwa kutoka kwa Mtume S.A.W. – na Masahaba waliofuatia baada yake kuwa hawajawahi kukusanyika kwa zaidi ya Swala moja ya Ijumaa, ikiwa hakuna haja na umuhimu wa kufanya hivyo, hivyo haifai kuthibitisha hukumu kwa kuhukumu bila ya dalili”.
Na kutokana na maelezo hayo ni kuwa: Inafaa kuiswali Swala ya Ijumaa ndani ya Msikiti mdogo na wala hakuna ubaya wowote, lakini kilicho bora ni kutoiswali sehemu hiyo isipokuwa panapokuwa na dharura ya kufanya hivyo ili kuepukana na kwenda kinyume na Jamhuri ya wanachuoni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas