Fitina ya Kutoswali Nyuma ya Mtu An...

Egypt's Dar Al-Ifta

Fitina ya Kutoswali Nyuma ya Mtu Anayefikiriwa Kuwa ni Mzushi.

Question

Tunaingia msikitini ili tuswali swala ya jamaa, wakati mwingine huwa tunaona baadhi ya watu ambao hawaswali nyuma ya Imamu wa msikiti, na wao huwa wanasubiri mpaka Imamu huyo amalize swala yake, basi wao huwa wanasimamisha swala nyingine ya jamaa kwa kisingizio kwamba Imamu aliyeswalisha kabla yao ni mzushi, je tendo hilo linaruhusiwa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Swala ni mojawapo ya nguzo za Uislamu, ililazimishwa na Mwenyezi Mungu juu ya Waislamu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, alibainisha jinsi ya kuswali, Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Malik Ibn Al-Huwayrith kwamba Mtume, S.A.W, alisema: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali”, na kuswali pamoja na jamaa ni bora zaidi kuliko kuswali pekee, Imepokelewa kutoka kwa sahihi mbili [Al-Bukhari na Muslim] kutoka kwa Ibn Umar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Kuswala pamoja na jamaa ni bora zaidi kuliko kuswali pekee mara ishirini na saba”, na kuswali pamoja na jamaa kunahitaji Imamu ili afuatwe, na uimamu ni: kuunganisha swala ya aswaliye na aswaliye mwingine, kwa masharti yaliyooneshwa na Sharia, wanavyuoni wameweka masharti lazima yapatikane kwa watu wanao waswalisha watu katika Swala, masharti hayo yanafahamika katika vitabu vya Fiqhi, na kama mashati hayo yakipatikana, basi watu hawa wanaruhusiwa kuwaswalisha watu.
Inajulikana kwamba Imamu kama hakuacha sharti lolote au nguzo yoyote miongoni mwa nguzo za swala, basi swala yake ni sahihi na uimamu wake ni sahihi pia. Kama Imamu akiwa mzushi, kama uzushi wake ulisababisha ukafiri, kama aliyesingizia uwongo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hairuhusiwi kuswali nyuma ya Imamu yule kwa mujibu wa makubaliano ya Wanavyuoni wote. Kwani amekuwa kafiri na hairuhusiwi kuwaongoza Waislamu. Lakini kama uzushi wake hausababishi ukafiri, Wanavyuoni wametofautiana katika swala nyuma yake, baadhi yao wakasema hairuhusiwi kuswali nyuma yake, na baadhi yao walisema, inaruhusiwa kuswali nyuma yake, na kila kundi la Wanavyuoni lina hoja na dalili zake.
Sasa hivi imebaki kubainisha hukumu hii katika siku hizi ambapo watu walisingizia uwongo watu wengine kuwa wao ni wenye uzushi katika masuala ambapo Wanavyuoni wametofautiana, kama suala la kutonyoa ndevu na kufupisha nguo na kadhalika. Inatupasa katika hali hii kubainisha baadhi ya dhana muhimu ya kimsingi, yaani: kuainisha maana ya uzushi, na taarifa ya kwamba hakuna tofauti kati ya Waislamu katika masuala yasiyopingwa.
Jambo la kwanza: Maelezo ya maana ya uzushi:
Uzushi katika lugha: ni kila jipya, Abu Adnan alisema: mwenye uzushi ambaye hufanya kitu kipya [Taji Al-Arus kwa Al-Zubaidi 20/307, Wizara ya Taarifa - Kuwaiti].
Na uzushi katika Sharia: Kuna njia mbili za Wanavyuoni katika kufafanua uzushi katika Sharia:
Njia ya kwanza: ni njia ya Ezz Ibn Abdel Salam, ambako amezingatia kwamba yale ambayo Mtume S.A.W. hakuyafanya ni uzushi, na ameugawa uzushi huu katika sehemu ambako alisema: “Kufanya mambo yasiyokuwa katika enzi ya Mtume S.A.W., yamegawanywa katika: uzushi wajibu, uzushi ulioharimishwa, uzushi uliopendekezwa, uzushi uliochukiza, na uzushi ulioruhusiwa, na njia ya kujua hali hii, ni kutoa uzushi kwa misingi ya Sharia: kama uzushi ukiingia misingi ya wajibu, basi ni wajibu, kama ukiingia katika misingi ya marufuku, basi ni marufuku, kama ukiingia katika misngi iliyopendekezwa, basi ulipendekezwa, kama ukiingia katika misingi ya machukizo, basi ni chukizo. Na kama ukiingia katika misingi iliyoruhusiwa, basi uliruhusiwa.” [Qawaid Al-Ahkaam fi Masalih Al-Anaam kwa Al-Iz Ibn Abdeal-Salam 2/337, Dar Al-Qalam].
Njia ya pili: Imefanya dhana ya uzushi katika Uislamu ni maalumu zaidi kuliko katika lugha, imeufanya uzushi ni mbaya tu, na haikugawa uzushi katika uzushi wajibu, uzushi uliopendekezwa, uzushi uliochukiza, na uzushi ulioruhusiwa, lakini kwake alibainisha dhana ya uzushi ulioharamishwa, na miongoni mwa waliokubali hali hii ni Ibn Rajab Al-Hanbali R.A. anaeleza maana hii akisema: “Maana ya uzushi: ni jambo jipya ambalo halina msingi katika Sharia unaolithibitisha, lakini jambo ambalo lina msingi katika Sharia unaolithibitisha sio uzushi, ingawa jambo hili ni uzushi katika lugha”. [Jamii’ Al-Ulum Wal Hikam kwa Ibn Rajab 2/127, Muasasat Ar-Risalah].
Kwa kweli, njia hizi mbili zilikubaliana kuwa uzushi ambao ni mbaya katika Sharia – aliyeufanya anapata dhambi – ni ambao hauna msingi katika Sharia unaouthibitisha, nao uliokusudiwa katika Hadithi ya Mtume S.A.W. iliyopokelewa kutoka kwa Muslim kuwa: “kila uzushi ni upotofu”. Maimamu wa Wanavyuoni wa umma walifuata ufahamu huu wazi na wa moja kwa moja.
Jambo la pili ambalo tunapaswa kusisitiza:
Ni kwamba hakuna tofauti kati ya Waislamu katika masuala yasiyopingwa. Kwani masuala haya yanawakilisha utambulisho wa Uislamu usiopingwa na yeyote, nayo ni mambo ya dini yanayofahamika vizuri, lakini mambo mengine yanayohitajia jitihada inaruhusiwa kwa Muislamu kufuata madhehebu yoyote madamu wenye madhehebu haya ni Wanavyuoni, wana haki ya kujitahidi na kuzingatia dalili, na haikuzingatiwa jitihada ya yeyote asiyekuwa na masharti ya jitihada, hii ina maana kwamba hairuhusiwi kwa yeyote kumtuhumu anayempinga kuhusu jambo lisilokubaliwa na Wanavyuoni kuwa ni mwenye uzushi, na upotofu, katika masuala yaliyokubaliwa na wanavyuoni katika kila wakati, na hakuna yeyote anayethubutu kuwapotosha Wanavyuoni hawa wakuu, lakini anaweza kufuata madhehebu maalumu pasi na mwingine, na hali hii haitawanyishi umma, lakini msisitizo wa mmoja wao kuwa madhehebu yake tu ni sahihi, na ya wengine ni ya uongo, msisitizo huu unasababisha tofauti na ugomvi.
Mwenyezi Mungu anasema: {Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri} [AL-ANFAAL: 46].
Ibn Qudaamah alisema: “Mwenyezi Mungu ameumba Wanavyuoni miongoni mwa watu waliotangulia katika umma huu, Wanavyuoni hawa walitengeneza misingi ya Uislamu, walieleza matatizo ya hukumu, na makubaliano yao ni hoja isiyopingwa na tofauti zao ni rehema kubwa”. [Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 1/2, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Hivyo, Wanavyuoni walielewa msingi wa tofauti na maana yake, na hakuna yeyote aliyemtuhuma mwingine kuwa ni mwenye upotofu au mwenye uzushi kwa sababu amejitahidi tu, hata kama alifanya makosa katika jitihada hizi, Al-Hafidh Al-Dhahabiy alisema: “Kama Imamu yeyote akifanya kosa linalowezekana kusamehewa katika jitihada zake katika suala lolote, kama tukimtuhumu kuwa ni mwenye uzushi na tukimhama, basi hakuna atakaye salimika, sio Ibn Nasr (Muhammad Ibn Nasr Ibn Al-Hajaj Al-Marwazi Abu Abdullah), wala Ibn Mundah (Abu Abdullah Muhammad Ibn Yahya Al-Abdiy), wala wanachuoni wakubwa zaidi kuliko wao, Na Mwenyezi Mungu anawaongoza watu kwenye haki, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote, Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na matamanio na uovu”. [Sair Alaam Al-Nubalaa 14/40, Muasasatu Risalah].
Baada ya kueleza dhana hizi za kimsingi, tunasema kwamba: Hakika mtu huyu amemtuhumu Imamu kuwa ni mwenye uzushi katika mambo ambapo Wanavyuoni wametofautiana kati ya kuwa ni wajibu na Sunna kama suala la kutonyoa ndevu, au kati ya uharamu na kuchukiza kwa kusikiliza muziki, au masuala mengine, si hivyo tu, lakini amefanya madhehebu yake tu ni sahihi pasina mengine, bali amelipa nguvu zaidi akilifanya suala hili ni sawa na masuala yasiyopingwa, kama uwajibikaji wa kuswali na kufunga, na lile suala la kunyoa ndevu na kutofupisha mavazi na masuala mengine ni miongoni mwa masuala ya utata katika Fiqhi ya Kiislamu, ambayo Muislamu anaweza kufuata maoni yoyote ya Wanavyuoni. Na hairuhusiwi kuwaainisha watu na kuwatuhumu kwa uovu na uzushi, kwa sababu walifuata maoni kinyume na maoni yaliyopitishwa na wao, na kuwatuhumu watu kwa upotofu na uzushi, kwa njia hii husababisha ugomvi kati ya Waislamu, nalo ni kosa kubwa tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutoka kosa hili.
Hivyo, katika hali ya swali hili: hairuhusiwi kuwasingizia watu uwongo katika masuala ya kudhani, wala hairuhusiwi kuacha swala nyuma na aliyefanya chochote katika masuala haya kwa kisingizio kwamba mambo haya ni uzushi, lakini masuala haya ni ya utata wala hairuhusiwi kuwagongananisha watu wa umma kwa sababu ya tofauti katika masuala haya, wala watu hawaruhusiwi kuvutiwa na masuala haya, na Mwenyezi Mungu alituamuru kuwa kikundi kimoja, na tulikatazwa kuwa vikundi vingi, Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziunganishe nyoyo za Waislamu wote na neno lao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas