Kutofunga kwa Ajili ya Upasuaji ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutofunga kwa Ajili ya Upasuaji Usio wa Haraka.

Question

Mimi huwa ninapata baadhi ya maumivu yanayosababishwa na ugonjwa nilionao na unaohitaji upasuaji, na daktari anayenitibu aliniambia kwamba upasuaji huo sio wa kuharakishwa, na kuna uwezekano wa kucheleweshwa hadi baada ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani, na sasa sihisi maumivu yoyote yasababishwayo na ugonjwa huu, lakini ninafikiria kuufanya upasuaji siku chache zijazo badala ya kuchelewesha, na jambo hili linahitaji mgonjwa ale chakula baadhi ya siku za Ramadhani. Je, katika hali kama hii, inakubalika mimi kula chakula na kutofunga au hapana?  

Answer

Alhamdulillahi sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na jamaa zake na Maswahaba wake na wanaofuata njia na dini yake. Ama baada ya utangulizi huu:
Kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kitabu chake: {Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru} [AL-BAQARAH 185].
Maana ya aya hii ni kwamba; Mwenyezi Mungu S.W. amemfaridhishia kila muislamu aliyebaleghe na mwenye afya, Saumu ya Ramadhani, na amewaruhusu kufuturu kwa msafiri na mgonjwa mpaka kumaliza hali yao na sababu ya ruhusa,watakidhi siku zao wasizofunga Ramadhani;na jambo hilo lipo katika asili ya sharia ili kuondoa tabu na mashaka juu ya waislamu, Mwenyezi Mungu amesema katika Qur`ani:{Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini } [AL- HAJJ 78]. Na Mwenyezi Mungu amesema katika aya nyingine: {Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.} [Al -MAIDAH, 6].
Ahmad alisimulia katika kitabu chake kutoka kwa Abu Hurairah R.A. Alisema: Mtume S.A.W. amesema: “Lau anayekunywa maji angelijua alichonacho tumboni na hali ya kuwa amesimama, basi angetapita”.
Hadithi hii inatoa dalili juu ya kwamba kukitoa chakula nje ya tumbo ni namna ya dawa au ponyo linaloondosha adha na maumivu, na sababu za maradhi ya mwili wa binadamu. Na inasemwa kwamba kunywa ukiwa umesimama hali hiyo huharakisha mchanganyiko tumboni na kukitoa chakula nje iwe ni dawa yake [Fat-h Al-Bariy Li Ibn Hajar 10\83, Ch. Dar Al-Maarifah], lakini mtu anayefunga akifanya hivyo kwa lengo la kupona, wakati huu hakuna dhambi juu yake bali lazima ailipe siku badala ya siku hii.
Wanazuoni wote waliafikiana juu ya kwamba ugonjwa ni udhuru unaopelekea ruhusa ya kula kwa mgonjwa [Al-Mughniy kwa Ibn Qudamah 3\41, Ch Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy], na wakati ule ule si kila ugonjwa unapelekea uwepo wa ruhusa ya kula, madhehebu ya jamhuri ya wanazuoni yalikiri kwamba ni ruhusa kula kwa kuwa na maradhi yanayosababisha uzito mkubwa kwa mgonjwa hadi ukawa hauvumiliki, kama mtu hawezi kuhimili kufunga Ramadhani, au anahofia maradhi yake yataongezeka kama akifunga, au anahofia kuchelewa kupona; kwani maradhi yanatofautiana, kuna baadhi yake hayana athari yoyote ya saumu kwake kama maumivu ya meno, na upasuaji wa kidole na kidonda kidogo na kadhalika.
Na pia kuna maradhi ambayo saumu huwa inasaidia kupona kwake na haijuzu kwa mtu kula anapokuwa na maradhi kama haya, kwani saumu kwake haimdhuru wala haimsababishii uzito wa aina yoyote, bali ina faida kubwa kwake. Ama kwa upande wa ruhusa ya kula kwa mtu aliye mgonjwa ni kwa ajili ya kuepusha maumivu na uzito juu yake.
Na kwa upande mwingine wanazuoni wanatofautiana katika maradhi yanayopelekea mtu kuruhusiwa kula. Baadhi yao kama Al-Hassan na Ibn Siriin walisema kwamba kila mgonjwa anaruhusiwa kula, ni sawa awe mtu huyo ana uzito au hana. Lakini Al-Asam alisema kwamba hairuhusiwi kula kwa mgonjwa asiyekuwa na uzito wowote wa kufunga kwa maana hawezi kuimaliza saumu yake – na hii ni kwa maana kamili ya maradhi. Na wanazuoni wengi wa Fiqhi walisema kwamba maradhi yanayopelekea ruhusi ya kula ni maradhi yanayomsababishia mtu madhara au yanayomsababishia ongezeko la ugonjwa wake, kwani hakuna tofauti kati ya kitendo kinacholeta hofu kwa adha yake au kile kinachosababisha madhara kama vile mtu mwenye homa anapohofia kama angefunga angezidisha homa yake, pia anayehisi maumivu makali ya jicho, akifunga atazidisha maumivu ya jicho lake, kwa hivyo walisema: vipi inasememwa kwamba kila ugonjwa unaleta ruhusa na hali ya kuwa tunajua kuwa kuna baadhi ya maradhi ambayo huwa yanapona kwa saumu, yaani saumu katika hali hii ina faida kwa mgonjwa, yaani kila mgonjwa ana hali yake ya kipekee, kutokana na hali ya ugonjwa wake na rai ya daktari. [At-Tafsiir Al-Kabiir Lil Imam Ar-Raziy: 5\243, Ch. Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Na Alau Edeen Al-Kasaniy Al-Hanafiy anasema katika kitabu cha [AL-BADAEA: 2\94, C., Dar Al-Kutub AL-Ilmiyah]: :Na kadhalika ugonjwa kwa ujumla sio kwa sababu ya ruhusa; kwani ruhusa hupatikana kwa sababu ya ugonjwa na safari kwa maana ya uzito wa mtu kuwa na saumu, kwa ajili ya kuwarahisishia kwa kuwaepushia uzito wa ugonjwa na saumu kwa mujibu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu:{Mwenyezi Mungu anakutakieni wepesi wala kutakieni ugumu}. Na kati ya magonjwa yanayopona kutokana na saumu na saumu hiyo huwa inamsaidia mtu kupona, na saumu katika hali hii inakuwa rahisi zaidi kuliko kula kwa mgonjwa, bali chakula kinamdhuru mtu, na ruhusa ni katika ibada ambazo lengo lake ni kumrahisishia mgonjwa kwa kuifuata ruhusa hii ya Mwenyezi Mungu)).
Na Ibn Jiziy Al-Malikiy anataja hukumu ya saumu katika hali mbali mbali za mgonjwa anaposema katika kitabu cha [Al-Qwaneen Al-Fiqhiyah: Uk,107, Ch. Dar Al-Fikr]: “Basi mgonjwa ana hali mbali mbali: Ya kwanza: Mgonjwa hawezi kufunga au anahofia mauti kwa sababu ya maradhi au udhaifu iwapo ataamua kufunga, kwa hivyo kula kwake ni wajibu katika hali kama hii. Na hali ya pili: Ni kwamba anaweza kufunga lakini kwa uzito mkubwa, basi inajuzu kwake kula. Na Ibn Al-Arabiy alisema: ni mwenye kuipendelea zaidi hali hii ya pili. Na hali ya tatu: Ni kwamba mtu anaweza kufunga kwa uzito mkubwa wa saumu na akawa anahofia maradhi kuongezeka, na katika hali kama hii kuna rai mbili juu ya uwajibu wa kula kwake.
Na hali ya nne: Ni kutokuwepo uzito wowote kwa mgonjwa wala kuhofia kuwa ugonjwa utazidi, katika hali hii, jamhuri ya wanazuoni wanaafikiana kutojuzu kula, lakini IBN SIRIN alisema kinyume na kauli ya jamhuri ya wanazuoni)).
Na Al-Imam Al-Nawawaiy amesema katika kitabu cha: [Al-Majmuo’: 6\261-262, Cha ll - Matebara AL-Muniriyah]: “Mgonjwa asiyeweza kufunga kwa sababu ya kuwa na maradhi yanayotarajiwa kupona, mtu huyu halazimiki kufunga wakati huu wa maradhi, na atalazimika kulipa siku alizofungua, hapo baadaye; kutokana na kinachotajwa na Al-Muswanaf, hususan akipatwa adha au uzito wowote kutokana na kufunga saumu, na haishurutishwi kuimaliza hali hii na hali ya kuwa hawezi kufunga, bali wanazuoni wetu walisema kwamba: Sharti ya kuruhusiwa kula ni pale mtu anapopatwa adha au uzito usiyohimilika kwa kufunga kwake saumu, walisema: Na hii ni kwa tafsili iliyotajwa hapo juu katika mlango wa Tayamamu. Wanazuoni wetu walisema: Ama maradhi madogo yasiyosababisha adha ya wazi kwa mtu basi hayo hayahitaji ruhusa ya kula bila tofauti kwetu, na hii ni kinyume na rai ya watu wanaofuata Madheheby ya Dhahiri)).
Na Ibn Qudamah Al-Hanbaliy alisema katika kitabu cha [Al-Mughniy: 3\41-42, Ch. Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabiy]: “Maradhi yanayosababisha uwepo wa ruhusa ya kula ni yale maradhi makali yanayoongezeka kwa kufunga saumu au yanayosababisha hofu ya kuchelewa kupona kwa mgonjwa. Inasemwa na Ahmad: Je Mgonjwa ataweza kula wakati gani? Alisema: Asipoweza kufunga. pakaulizwa: Ni kama anapokuwa na homa? Akasema: Na maradhi yoyote makali zaidi kuliko homa. Na imesimuliwa na baadhi ya waliotangulia kwamba wanaoruhusiwa kula wanaruhusiwa kwa kuwa na maradhi yoyote, hata kwa kuwa na maumivu ya kidole na jino; kwa mujibu wa maana jumla ya aya ya Qur`ani inayohusika na jambo hili, na hilo ni sawa sawa na hali ya msafiri hata asiohitaji kula lakini anaruhusiwa kula kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile mgonjwa. Na tuna sisi anaye udiriki mwezi mwezi wa Ramadhani, haimuudhi saumu, basi akalazimika kufunga kama mtu mwenye afya njema, na Aya ya Qur`ani ni kuhusu msafiri na mgonjwa tu, na dalili ya hayo ni kwamba msafiri safari ndogo haruhusiwi kula, na tofauti kati ya msafiri na mgonjwa ni kwamba safari ina dhana ya safari ndefu, na hekima iliyopo katika hayo ni kwamba uzito mdogo hauruhusu (kula), na uzito mkubwa hauna udhibiti wowote katika nafsi yake; kwa hivyo hekima hapa inachukuliwa kwa dhana ya safari ndefu sio safari fupi, na hii ni kwa ajili ya kuwarahisishia watu. Na kwa upande wa maradhi, hakuna misingi maalumu, kwa kuwa maradhi yana tofautiana, kuna saumu inayomdhuru mtu anayefunga, na kuna nyingine isiyomdhuru mtu anayefunga kama vile maumivu ya jino na upasuaji wa kidole, kidonda na kadhalika, kwa hivyo, maradhi hayakuwa sahihi ni kama misingi, na yanaweza kuchukuliwa hekima kama msingi wa kitu hiki, na hasa kwa kinachohofiwa kuwa ni madhara juu ya mtu”.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia, kwa mujibu wa swali la kwanza la upasuaji: Ni kwamba kwa kuwa upasuaji unaotaka kuufanya hauna haraka yoyote kwa ushahidi wa daktari, na hakuna hofu yoyote ya kutokea madhara ya kuchelewesha au mashaka yanayoweza kupatikana wakati wa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kabla ya kuufanya upasuaji huo, basi unaweza kula katika hali hii kwa mujibu wa rai hii iliyopendelewa na Jamhuri ya wanazuoni wa fiqhi kama tulivyotaja hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 


 

Share this:

Related Fatwas