Kuuza Cheki.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuza Cheki.

Question

Ni ipi Hukumu ya kuuza cheki kwa bei chini ya thamani yake kabla ya wakati wa kustahiki kwake hata ikija miadi ya kustahiki mwuzaji anaichukua cheki bila ya upungufu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Baadhi ya watu wanamwuzia cheki mtu mwingine au benki nyingine kabla miadi ya kustahiki kwake, na aghalabu ya uuzaji huu unakuwa kwa bei ya chini ya thamani yake, na nia ya watu katika muamala huu inatofautina, baadhi yao wanaiuza kwa sababu ya uhitaji wake kwa pesa taslimu, au anakuwa hawezi kuchukua pesa za cheki kwa sababu ya safari yake nje ya nchi au kwa sababu ya hofu yake inayotokana na kuchelewa kuipata cheki hiyo.
Cheki: Ni hati maalumu ya benki inayotumiwa kuidhinisha malipo ya fedha kwa aliyetajwa kwenye hati hiyo kutoka kwenye fedha za aliyeiandika hati hiyo, na inaambatana na amri ya malipo ya moja kwa moja bila ya sharti lolote, licha ya kufuata sheria, na huwa inatolewa na mtu maalumu anaetambulika kama "Mtoa cheki" kwa benki, "na haya ni malipo yanayofanyika kwa cheki" na cheki inatakiwa ilipwe moja kwa moja baada ya kuliona jina la anayefaidika au kwa idhini ya mbebaji wa cheki kwa "pesa taslimu maalumu". Rejelea: [Mawsoat Al-Mustalahat Al-Iqtisadiyah wa Al-Ihsaiyah kwa Abdulaziz Hekal Uk. 123, cha, Dar Al-Nahdhah Al-Arabiyah-Bayrut]. Na hii inathibitishwa kwa hukumu ya Naqdhi katika hukumu zake za siku hizi kwa mujibu wa sheria namba 17 kwa mwaka 1999.
Na hukumu katika jambo hili ni kujuzu kwa mujibu wa kwamba ikiwa cheki ina baki ya pesa katika benki, na inakamilisha sharti zote za wanazuoni wa fiqhi katika uuzaji.
Na dalili ya uuzaji huu ni kuiuza katika hali ya ujumla wake kwa hivyo kunaipatia hoja kwa ujumla wa matini ya kisheria ambayo inahalalisha uuzaji huo, na matini hizi ni nyingi na zijulikana, na tutazitaja hapa kwa kifupi. Ama kuhusu ya kuwa moja ya mbadala wa wawili ni deni basi haidhuru; kwani wanazuoni wa fiqhi waliafikiana juu ya sharti la kuitaja thamani ya bei katika mkataba, na ipasa kuwa ni mali ya mnunuaji, na yawezekana kulipa pesa taslimu, na kujua kiasi na sifa zake. [Al-Mawsuaah Al-Kuwaytiyyah,15/28 cha,Wizara ya Mambo ya Waqfu na mambo ya Kiislamu-Kuwet], ikizitekeleza sifa hizi katika cheki, basi hukumu ya uuzaji wa cheki ni sahihi, na Abdulrazik alisimulia kuwa: bin Jariri alisema kwamba: bin Alzuber aliniambia kwamba alimsikia Jabir bin Abdallah aliulizwa kuwa mtu ana deni, je, anaweza kumwuzia mja? alisema: "Haidhuru, anaweza". Na Hadithi ina hukumu ya “Mawqouf”, na usahihi wake ni “mawqouf” juu ya sharti la Muslim.
Ikisemwa: Hii ni kutoka katika mlango wa ((weka na kufanya haraka)) na hii haijuzu.
Basi jawabu la jambo hili ni kwamba: Jambo hili haliwezi kuwa katika sura zote isipokuwa sura ya kuuza cheki kwa mtu anayekuwa na deni la cheki na haujafika wakati wa kustahiki kulipwa kwa cheki hiyo. Na mbali ya hivyo, wanazuoni wanahitalifiana katika swala hili, na Abdulrazek alisema; Maamar alituambia kutoka kwa Ibn Tawoos, kutoka kwa Baba yake, kutoka kwa bin Abbas, aliulizwa kuhusu swala la deni: “Kama mtu ana deni juu ya mtu mwingine kwa wakati maalumu na akamwambia nilipe deni langu sasa hivi na mimi nipunguze kidogo, alisema: "Haidhuru, na jambo hili ni sawa”na kauli hii ni sahihi juu ya sharti la mashekhe wawili.
Ikisemwa:kwamba baadhi ya wanazuoni hawakuona kujuzu kwa jambo hili; kwani huku ni kuuza mali kwa mali kwa njia ya riba bila ya kushika vitu viwili vya mbadala, na jambo hili linakatazwa katika Hadithi sahihi za Mtume S.A.W., na miongoni mwa Hadithi hizi zimesimuliwa na Bukhary na Muslim kutoka kwa Ubadah Ibn Alsamet, alisema: "Mtume S.A.W., alisema: Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, na ngano kwa ngano, na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, yaani kitu kwa mfano wake, na vitu hivi vikihitalifiana mnaweza kuviuza mnavyotaka". Na Hadithi ya Abi Said Al-Khudariy katika Sahihi mbili: "Msiuze dhahabu kwa dhahabu wala karatasi kwa karatasi ila mithili kwa mithili".
Basi jawabu ni kwamba: Upingani huu wenyewe ni sahihi, lakini suala hili haliendani na hali hii; kwani linalosemwa na wanazuoni wa fiqhi linahusu dhahabu na fedha ama sarafu zingine ziliitwa zamani kwa jina la "pesa" haziingii katika hukumu hii; kwani pesa hizi hazitengenezwi na madini ya dhahabu au fedha, kwa hivyo pesa za dhahabu na fedha tu zinaingia katika hukumu hii.
Al-Soyuty alisema kwamba: "Hakuna Riba katika pesa za kawaida hata kama zitaenea kama pesa zilizotengenezwa kwa dhahabu au fedha". [Al-Ashbah na Al-Nadhaer uku 370].
Kwa upande mwingine, yapasa kujua kwamba miongoni mwa masharti ya kujuzu uuzaji huu ni kukabidhiana mkono kwa mkono baina ya mwenye cheki na mnunuzi wake, kwa hivyo Al-Bahuty alisema katika kitabu cha [Kashaaf Al-Qenaa, 3/307, cha, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: "ni sharti" kwa usahihi wa uuzaji wa deni thabiti katika dhima ya anayedaiwa (achukue pesa zake hapo alipo kama atakuwa amemuuzia kisichouzika).
Na Ibn Qudamah alisema katika kitabu cha: [Al-Mughny 4\37, cha, Maktabet Al-Qaherah]: "Ibn Al-Munzer alisema: Wanazuoni waliafikiana juu ya kwamba kuuza deni haijuzu. Na Ahmad alisema: Ni Ijmaa. Na Abuobaida alisema katika kitabu cha Al-Ghareb kwamba "Mtume S.A.W., hakuruhusu uuzaji Al-kali kwa Al-kali" Na alifasiri kauli ya Mtume S.A.W., kwa deni kwa deni].
Na kwa ufupi: Asili ya masuala haya ni kujuzu, lakini kwa kutimiza sharti la cheki tulizozitaja hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi
 

Share this:

Related Fatwas