Usafi wa Majitaka Baada ya Kusafish...

Egypt's Dar Al-Ifta

Usafi wa Majitaka Baada ya Kusafishwa.

Question

Je kusafishwa kwa maji taka kunaweza kurudisha tena usafi wake, kwa namna ambayo inawezekana kuyatumia, kunufaika nayo na kuondoa uchafu na najisi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu na upanuzi wa viwanja vya kilimo hitajio la kutumia kiasi kikubwa cha maji limeongezeka, serikali imeamua kutumia njia zisizo za kawaida ili kuziba pengo kati ya kiasi cha maji kinachohitajika na maji yanayofaa hasa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Njia za kwaida zilitegemea matumizi ya maji yatokanayo na vyanzo kama vile mito na bahari, au maji ya chini ya ardhi baada ya madawa ya kusafishia maji, na kuyasafisha, kutokana na kuongezeka kwa hitajio la matumizi ya maji kwa kiasi kikubwa, na kwa sababu kuna matumizi kadhaa hayahitaji kiwango cha juu cha usafi, serikali imetafuta madawa ya kusafishia maji taka kwa namna inayofaa kwa ajili ya matumizi haya, hivyo kama kumwagilia mimea pambo, kumwagilia mashamba ya mifugo na kadhalika miongoni mwa yasiyohusiana na matumizi ya binadamu ya moja kwa moja au yasiyo moja kwa moja. Matatizo mengi ya kisheria na ya kijamii yameibuka, ikiwa ni pamoja na: Je, binadamu au wanyama, wanaweza kutumia maji haya kwa kunywa bila kujali kiwango cha usafi wake? Je! Ni kiwango gani cha usafi wa maji haya kinapatikana baada ya kusafishwa kwa madawa?
Kwa kuzingatia hisia za ujumla na za mbali na mambo yenye shaka hatupendekezi maji hayo yatumiwe na wanadamu au wanyama kwa kunywa baada ya kuyasafisha. Lakini kuhusu usafi wa maji kama hayo baada ya kuyasafisha, wanavyuoni wamekubaliana kwamba maji yaliyo machache na yale yaliyo mengi kama uchafu ukiangukia ndani yake na ukaibadilisha rangi au ladha au harufu ya maji hayo, basi maji hayo yatakuwa yamenajisika. Kiwango cha maji mengi ni takriban (191.25 Kjram) [Rejea: Al-Makayil wal Mawazin Al-Sharia uk 46, kwa Mufti Mkuu Prof.. Ali Jumaa, Al-Quds lilIilan wal Nashar- Cairo], na maji taka yanayokusanywa ni maji mengi ambayo yamebadilika sifa zake kuu tatu, na hakuna shaka kwamba maji hayo yamenajisiwa.
Maji yanayochanganywa na maji yaliyo chafuliwa yanasafishwa kwa njia tatu:
Njia ya kwanza: kuongezeka: kwa maana ya kumwagia maji safi juu ya maji yaliyochafuliwa mpaka kuzamisha na kutokomeza mabadiliko yaliyokuwemo ndani yake, yakaondolewa kwa sifa zake tatu za ladha, rangi na harufu [Rejea: Al-Manhaj Bisharhih Mughni Al-Muhtaj kwa Al-Khatib Al-Sherbini 1/126, Dar Al-Kuttab Al-Alamiyah, na Al-Mubdii kwa Ibn Muflih 1/207, Dar Al-Kuttab Al-Alamiyah], na asili yake ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhari kutoka kauli yake S.A.W. kwa Masahaba zake wakati bedui mmoja alipokojoa katika msikiti: "Mwacheni na mwagie ndoo ya maji. Akaimimina juu yake (sehemu iliyopatwa na mkojo".
Imam Al-Khatwabiy alisema: “Hadithi hii ina dalili kwamba maji kama yakimwagika kwa uwingi juu ya uchafu, maji haya yanasafisha” [Maalim Al-Sunan 1/116, Al-Matbatul Elmiyah].
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy wanagawa usafi kwa kuongezeka kwa matawi hayahusu suala la uwekaji madawa ya kusafishia maji taka, kwa upande wa nadharia, maji taka yanaweza kusafishwa kwa njia hii baada ya kuondolewa kwa uchafu kutokana na maji, Lakini kwa upande mwingine wa vitendo haiwezekani kufanya hivyo, kwa sababu ya uwingi wa maji yanayochafuliwa, ambayo yanahitaji kiwango kikubwa cha maji safi; kwa ajili ya kuyaondolea mabadiliko, na jambo hili halikutokea katika vituo vya madawa ya kusafishia maji, pengine ni kwa sababu ya gharama zake ambazo ni kubwa, na lengo ambalo madawa ya kusafishia maji hutafutwa kwa ajili yake halilingani na gharama hizi.
Njia ya pili: Usafishaji kupitia mifereji: Njia hii kwa wanavyuoni wasiofuata madhehebu wa Imam Shafiy wanaona kwamba huwa safi kwa maelezo juu yake [Rejea: Fathul Qadiir kwa Ibn Hammam 1/98, Dar Al Fikr. Na Kashaaf Al-Qinaa kwa Al-Bahwati 1/40, Dar Al Fikr. Al-Taji walIkliil Sharhu Mukhtasar Khalil kwa Al-Muaq 1/115, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Njia ya tatu: Usafishaji kupitia kubadilisha: Kubadilisha ni kugeuza kitu kutoka katika umbile na sifa fulani na kukipeleka kwenye tabia na sifa tofauti. Na mifano yake ni, pombe inapotengenezwa na kuwa siki, damu inapotengenezwa na kuwa miski, na chakula kinapogeuga kikawa matapishi, kwa hivyo basi kubadilisha maana yake ni kugeuza sifa ya kitu tu, njia hii ndiyo inayotumika katika madawa ya kusafishia maji taka kivitendo, ambapo njia hii inapita katika hatua nne za madawa ya kusafishia: kutenganisha uchafu, uingizaji hewa, kuua wadudu, na kuondolewa kwa bakteria kupitia klorini, na kwa kupitia hatua hizi sifa za maji huwa zinageuzwa kuwa karibu sana na maji ya mito, na katika hatua ya juu ya madawa kwa kutumia kile kinachoitwa: “Machujio ya mchanga, na kunyonya kaboni, oksaidi ya kemikali, na osmosis ya kinyume” kiwango cha usafi kinaongezeka ambapo baadhi ya elementi za maji kama vile mafuta na uchafu huwa vinaondolewa kabisa, maji yanageuzwa na kuwa karibu sana na maji safi ya kunywa yanayofaa kutumiwa na binadamu.
Wanavyuoni wametofautiana tangu zamani katika ukweli kwamba njia ya kubadilisha ni miongoni mwa njia za kusafisha, na mtazamo wao kuhusu pombe kama ikitengenezwa na binadamu kuwa siki unafaa na maneno yao hapa, na sababu ya kufaa huko ni kwamba maji taka yanashirikiana na pombe katika sifa ya unajisi, na njia inayotumika katika madawa ya kusafishia maji taka inafanana na ile inayotumika katika kutengeneza pombe ili iwe siki, katika njia hizi mbili kemikali inaongezwa kwa ajili ya kusafisha.
Kama kitu kimewekwa katika pombe na ikageuzwa siki, kwa wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy, na rai iliyochaguliwa ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad Ibn Hanbal ni kuwa pombe haiwezi kusafishwa kwa njia hiyo kama katika kitabu cha: [Tuhfatul Muhtaj kwa Ibn Hajar Al-Haytami 1/303, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy] na Kashaaf Al-Al-Qinaa kwa Al-Bahwati Al-Hanbali 1/187, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], lakini wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik na Abu Hanifah walipingana nao katika suala hili.
Al-Dardiir Al-Maliki anasema katika kitabu chake Al-Sharhul Kabiir: “(Na) miongoni mwa vitu safi ni (pombe iliyoganda) kwa ajili ya kuondolewa kwa ulevi wake, (au iliyotengenezwa siki)” [1/52 Dar Al-Fikr].
Katika maelezo ya Kharashi juu ya Al-Sharhul Kabiir: “Na pombe iliyoganda au iliyotengenezwa siki, ina maana kwamba pombe imegeuzwa kutoka sifa yake ya majimaji kwa sifa ya kuwa ganda au imegeuzwa kutoka sifa yake ya ulevi kwa kuwa siki, basi ni safi; kwa sababu uchafu ndani yake hauhusiani na sifa yake ya ulevi, sifa hii ikiondolewa, uchafu utaondolewa pia, uharimishaji na uchafu huunaungana na sababu kwa wakati wote. Lakini kama sifa ya ulevi ilibaki, basi pombe hii siyo safi. Na hakuna tofauti kati ya pombe iliyogeuka siki yenyewe au ile iliyotengenezwa na watu” [1/88, Dar Al-Fikr].
Katika kitabu cha [Al-Hidayah kwa Al-Margenyani]: “Kama pombe ikigeuzwa siki ni halali, ikiwa kugeuka yenyewe au kwa kutengenezwa siki na watu kupitia kuweka kitu chochote ndani yake, na haichukizi kugeuzwa siki” [4/398, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi].
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifah walisisitiza mtazamo wao kwa yafuatayo:
1) Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na anawahalalishia vizuri} [AL AARAAF: 157], na siki ni miongoni mwa vizuri.
2) Kauli yake Mtume S.A.W: "Siki bora ni siki ya pombe".
3) ikilinganishwa na kutengeneza kwa ngozi, kama kwamba ngozi za wafu ni chafu na zinasafishwa kwa kutengenezwa, hivyo pia pombe inasafishwa kwa kugeuzwa siki, na Hadithi zilizokuwa na katazo, basi katazo hili lina maana ya kusisitiza, kwa sababu Hadithi hizi zilikuwa mwanzoni, na kwani watu walikuwa wakizoea kunywa pombe na kila kitu kinachozoeleka na ambacho nafsi inakipenda, kwa hivyo Mtume S.A.W. aliogopa hila za shetani akawakataza Waislamu kugeuza pombe kuwa siki ili wasinywe siki, lakini baada ya muda mrefu wa kukataza Mtume S.A.W. hakuogopa hila hizi na akasisitiza akisema: “Mchuzi bora ni mchuzi wa siki” [Rejea: Mirqaatul Mafatiih 6/2385, Dar Al-Fikr], Katika baadhi ya mapokezi ya Abu Talhah ilipokelewa Hadithi inayoamuru kuvunja vyombo ambavyo pombe inawekwa ndani yake, na hali hii inasisitiza kuikataza pombe pia, ingawa kuvivunja vyombo hivi kunasababisha uharibifu wa fedha za watu wengine na inawezekana kuepukwa uharibifu huu kwa kumwaga pombe na kusafishwa kwa vyombo vyake tu.
Ibn Rushd ambaye ni mjukuu anasema kuwa: sababu ya tofauti kati ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifah na Shafiy ni kupinga kupima kwa Hadithi, yaani Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Talhah, basi mwenye kuelewa kuwa katazo liliotajwa katika Hadithi hii kwa ajili ya kuzuia visingizio tupu akafanya katazo lina maana ya kuchukiza, ili iwe juu ya chuki, na mwenye kuelewa kuwa katazo hili halina sababu akautaja uharamishaji, upimaji unaopinga ni kwamba imefahamika kutokana na umuhimu wa Sheria kwamba hukumu mbalimbali zinakuwa kwa ajili ya vitu tofauti, na pombe ni tofauti na siki, na siki ni halali. kwa pombe imegeuzwa na siki, siki lazima kuwa halali. [Bidayatul Mujtahid 3/28, Dar Al-Hadithi].
Imam Al-Qurtubiy katika tafsiri yake anasema kuwa: “Inawezekana katazo la kugeuza pombe na siki lilikuwa mwanzoni mwa Uislamu wakati wa kuteremshwa kwa katazo hili, ili watu wasiendelee kunywa, na kwa ajili ya kuzuia mila hiyo, na hali ikiwa hivyo, katika katazo la kubadilisha pombe kuwa siki, na amri ya kuimwaga, hakuna yaliyozuia kunywa kama ikiwa siki”” [6/290, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Kama ikithibitishwa uwezekano wa kufuta au kuzuia kugeuzwa pombe ili iwe siki, ilikuwa adhabu tu, basi suala hili kutokana na dalili zake yanachaguliwa maoni ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifah, kwamba nia ya kugeuzwa pombe ili iwe siki inaisafisha na inaruhusu kutumiwa, na kufuatana na suala hili lilipitishwa suala la madawa ya kusafisha maji taka kama ilivyoelezwa hapo juu. Na inawezekana kusema kwamba mchakato wa madawa ya kusafisha maji kwa hatua zake mbalimbali, pamoja na kuondolewa kwa uchafu na kupita kwa maji chujio zaidi ya moja na kuongeza baadhi ya vitu vinavyoondoa harufu mbaya, maji yanasafishwa kwa hatua hizi zote, lakini inawezekana kutumia maji hayo katika kilimo, kumwagilia wanyama, na mambo ya viwanda n.k, bila ya kunywa binadamu, hata maji haya yakifikia kiwango juu katika usafi wake, hivyo kwa ajili ya kuzingatia hisia za ujumla, na za mbali na mambo yenye shaka, na rai hii ilichukuliwa na Baraza la Fiqh la Kiislamu linalofuata Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu katika kikao chake cha kumi na moja, kilichofanyika katika Mji wa Makkah katika kipindi 19-26 Februari 1989, ambapo azimio lilitaja yafuatayo: “Kuhusu Swali linalohusiana na hukumu za maji taka baada ya kuyasafishwa: Je! Inaruhusiwa kuyatawadhia na kuogea kwa maji hayo? Je! Inaruhusiwa kuondosha kwa uchafu kwa kutumia maji hayo? Baada ya kupitia wataalamu wa madawa ya kusafisha maji taka kwa njia za kemikali na walioyaamua kwamba matibabu hutokea kwa kuondoa uchafu katika hatua nne: kutenganisha uchafu, uingizaji hewa safi, kuua wadudu, na kuondolewa kwa bakteria kupitia klorini, hivyo uchafu hautakuwa na athari yoyote katika ladha, rangi, na harufu mbaya, nao wataalamu hawa ni Waislamu waadilifu wanaosema kweli na waaminifu. Baraza hili limeamua yafuatayo: kwamba maji taka kama yakisafishwa kupitia njia zilizotajwa au zinazofanana nazo, na hakuna athari ya ladha wala rangi wala katika harufu mbaya maji yakawa safi na inawezekana kutumiwa katika kutia udhu na kuondoa uchafu; kulingana na msingi wa sheria unaoamua kwamba maji mengi ambayo uchafu ulianguka ndani yake yanasafishwa kwa kuondoa kwa uchafu huu ikiwa hakuna athari yoyote kwake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi. Na Mwenyezi Mungu ambariki Mtume wetu Muhammad, na familia yake na salamu nyingi ziwe juu yao, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote”. Kamati ya Fatwa katika Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kiislamu huko Kuwaiti yalichukua fatwa hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu: rai iliyochaguliwa katika suala hili ni kwamba: madawa ya kusafishia maji taka kupitia njia za kiteknolojia za kisasa yanageuza maji haya ili yawe safi na yaweze kutumiwa kutawadhiwa na kuondoa uchafu. Hivyo, inapendekezwa kutoyatumia maji haya kwa ajili ya kunywa, chakula na usafi ili tuepuke tofauti ya mwenye kusema kuwa maji hayo siyo safi, hata yakisafishwa vizuri sana. Na inaruhusiwa kuyatumia katika mambo mengine kama vile; kumwagilia mimea, kunyweshea mifugo, kusafishia barabara na kadhalika. Mambo ambayo hayahusiani moja kwa moja na binadamu na ibada yake inayohitaji usafi unaopatikana kwa maji safi tu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas