Najisi ya Damu ya Mwanadamu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Najisi ya Damu ya Mwanadamu.

Question

Je, damu ya mwanadamu ni twahara au ni najisi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Wanazuoni wa fiqhi waliafikina juu ya kuwa damu ya Hedhi na Nifasi ni damu najisi, na dalili yao juu ya hivyo kwa Hadithi ya Bibi Aisha R.A. kwamba Fatima bint abi Hubayshi alikuja kwa Mtume S.A.W. Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Mimi ni mwanamke huwa nakuwa na Hedhi daima siwi twahara, Je, Niache Swala? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.: “La, Hakika huo ni mshipa wala siyo hedhi. Zinapofika siku za hedhi basi wacha Swala na ikimalizika kadiri ya muda wake (ile hedhi) osha ile damu na uswali”. (wamekubaliana Bukhari na Muslimu), na kadhalika kwa Hadithi ya Asmaa bint abi Bakar R.A.: Mwanamke alikuja kwa Mtume S.A.W. Akasema: Unaonaje mmoja kati yetu ikipata nguo yake damu ya hedhi afanyaje?Akasema Mtume S.A.W.: “Ikiingia damu ya hedhi nguo ya mmoja kati yenu basi aikwangue ile damu kisha aikoshe nguo yake kisha aiswalie”. [wamekubaliana Bukhari na Muslimu] kwa maana ya kuisafisha damu kwa ncha za vidole chake na makucha pamoja na kuyaweka maji juu yake mpaka kuiondoa athari zake halafu akaiosha.
Ama yasiyo Hedhi na Nifasi kuna hitilafu miongoni mwa wanazuoni, juu ya rai mbili:
Jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi ya madhehebu manne wanaona kuwa damu ya wanadamu wote ni najisi isipokuwa damu ya hedhi na nifasi,na kila mmoja wao ana misingi yake hasa,lakini wanashirikiana katika kauli ya unajisi isipokuwa damu chache na wanahitalifiana juu ya kiasi cha uchache wake . Wanazuoni wa Kimaliki na Kihanafi wanaona kwamba damu chache ni kama kadiri ya derham au upungufu yake. Na kauli sahihi nao ni upana wa derham siyo uzito wake, lakini wafuasi wa Madhehebu ya Hanafiy wanasema ni kama upana wa kiganja kimoja, mtu anachukuwa maji kwa kiganja chake na ananyoosha kiganja kinachobaki (katika maji) kinakuwa ni kadiri ya kiganja, na Malikiya pia ni sawa mafano huo. [Rejelea: Fadhe Al-Kadiir 1\200, Ch, Dar Al-Fekr, Warad Al-Mehtar 1\317,318, Ch, Dar Al-Fekr, na Hashiyat Al-Swawiy 1\75, Ch, Dar Al-Maaref].
Na Shafiy na Al-Hambaliyah wanaona kwamba kiasi cha damu kinarejea kwa Urfu. [Rejelea: Hashiat Al-Bejouriy Ali Ibn Al-Qasem 1\103, na Al-Inswaf 1\198, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]. Na katika kiasi ya uchache kuna kauli zingine.
zimenakiliwa kutoka kwa jamhuri ya wanazuoni kwamba damu ya mwanadamu nyingi ni najisi, AHMAD alipoulizwa :Je, damu ya usaha ni sawa unayo?alisema:Hakuna hitilafu baina ya watu juu ya unajisi wa damu,lakini kuna hitilafu juu ya usaha. [Sharhu Al-Omdah Libn Taimiah 1\105,Ch. Maktabat Al-Ebikan].
Ibn Hazm alisema katika kitabu chake cha: [Marateb Al-Ijmaa Uk. 19, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Waliafikiana juu ya damu nyingi zozote za viumbe ni najisi ,isipokuwa damu ya samaki”.
An-Nawawiy alisema: “Dalili za unajisi wa damu ni dhahiri,na sikujua hitilafu yoyote kati ya waislamu juu ya hayo,isipokuwa ilisimuliwa na Swaheb Al-Hawiy kutoka kwa baadhi ya wanachuoni wa elimu ya maneno Al-Mutakalimeen. walisema ni twahara lakini Al-Mutakalimeen hawachukuliwa na maneno yao katika Ijimaa,lakini hitilafu juu ya madhehebu sahihi ya jamhuri ya wanachuoni wa elimu ya Usuul kutoka kwa wanazuoni wenzetu na wengine hususan katika masuala ya kifiqhi”. [Al-Majmuu 2\557, Ch. Maktabat Al-Irshad].
Al-Qurtubiy alisema katika tafsiri yake: “Wanazuoni waliafikiana juu ya damu ni haramu na najisi”. [2\221, Ch. Dar Al-Kutub Al-Masriyah].
Na Ibn Hajar alisema katika kitabu chake cha: [Fath Al-Bariy 1\352, Ch. Dar Al-Maarefah]: “Kuna itifaki miongoni mwa wanazuoni: Damu ni najisi”.
Na kwa upande mwingine wanazuoni wa Kishafiy wanaona kwa mujibu wa msingi wa Al-Urfu katika uchache na wingi wa damu kwamba-damu nyingi ya mwanadamu ikiwa ilitoka kwa hijama si haramu sharti ya kuwa kutoka kwa mtu yule yule na sio kutoka kwa mwingine ,na bila ya kuchanganya na damu mtu mwingine [Rejelea: Al-Iqnaa Be Hashiyat Al-Bejermiy 1\447, Ch. Dar Al-Fekr, na Hashiyat Al-Bejuriy 1\107]. Na Jamhuri ya wanazuoni wana hoja yao juu ya kauli yao kwa unajisi wa damu ya mwanadamu kutoka kwa Hadithi ya bibi Aisha R.A. tuliyoitaja hapo juu, hata walau ililetwa katika Hedhi ila hakuna tofauti baina ya damu ya Hedhi na damu nyingine.
Na pia wana hoja kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu} [AL-ANAM: 145].
Atwabariy anasema katika tafsiri yake: [9\633, Ch. Muasasat Al-Resalah]: “Katika sharti lake Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu damu anapowaambia waja wake uharamu wa damu ya kumwagika tu ni dalili wazi juu ya kuwa damu nyingine ni halali na sio najisi].
Na Ar-Raziy anasema katika tafsiri yake [11\21, Ch. Dar Ihyaa At-Tutath Al-Arabiy]: “Shafiy R.A aliharimisha damu zote zikiwa ni za kumwagika kinyume na zingine, na Abu Hanifa alisema: Damu ya samaki si haramu. Ama Shafi alisisitiza kwa dhahiri ya aya hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu amekuharimisheni nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe}. Na hii ni damu basi ni wajibu kuiharamisha, na Abu Hanifa alisisitiza kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika}. Kwa hivyo alisema kwa hakika sikukuta kitu chochote kilicho haramishwa isipokuwa mambo haya tu, kwa maana damu isiyo mwagika si haramu kwa mujibu wa Aya hii, na maana hiyo, Aya hii imeteremka kwa jambo maalumu. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeharimishwa nyamafu, na damu}, ni hukumu kwa ujumla na hukumu maalumu inatangulia juu ya hukumu ya kiujumla. Shafiy R.A. Alijibu kwa kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa} Aya hii haina dalili juu ya uhalali isipokuwa juu ya vitu hivi vilivyotajwa katika Aya hii, bali ni dalili juu ya kuviharimisha vitu hivi, na hivi havikanusha kubaini baadaye uharamisho wa vitu vingine, na labda Aya ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Mmeharamishwa nyamafu} iliteremka baadaye, basi ilikuwa ni kama tangazo ama ubainifu kwa uharamisho wa damu ikiwa ni damu ya kumwagika au siyo ya kuwa ya mwagika, ikithibitisha jambo hili linawajibika kwa uharamu kwa damu zote na unajisi wake, na kwa hivyo ni lazima kuziondosha damu hizi kutoka kwenye nyama kadiri iwezekanavyo, na kadhalika katika samaki, na damu yoyote iliyoangukia majini au nguoni zinanajisi kilichoangukiwa juu yake].
Na Malik alisimulia katika Al-Muwata’ kutoka kwa Nafie kwamba Abdullahi Ibn Omar alikuwa akitokwa na damu puani akiondoka na kwenda kutawadha, kisha alirejea tena kujenga na hakusema. Al-Bajiy anasema katika maneno yake kuhusu maudhui ya uchache ama uwinyingi wa damu ya kutiririka puani: (Tawi\sehemu) na nyingi ni kutiririka au kudondoka kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Au damu ya kumwagika} [AL-ANAAM:145], na ikiwa haikutiririka au kudondoka, mtu anaweza kuifuta damu tu kwa vidole vyake, ikiwa ni zaidi ya vidole vinne vya juu na haikuzidi, hiyo ni damu chache, basi hawezi kutoka ndani ya swala na hii ni kauli ya Ibn Nafee katika [Al-Majmuah] na kadhalika katika kitabu cha: [Al-Mawaz] maneno kama haya. Na maana ya kuondoka hapa ni kukata Swala yake na anaweza kuiendelea baada ya kuziosha damu kutoka unajisi wake kwani Swala yake ni batili. (Al-Montaqiy 1\85, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy, Kairo).
Na kwa upande mwigine baadhi ya wanazuoni wanaona kwamba damu ya mwanadamu ni twahara hata japo kuwa ni nyingi, na hawa ni baadhi ya wanachuoni waliokuja baadaye kama As-Shawkaniy (Rejelea: Al-Darariy Al-Madeyah 1\32, Ch. Dar AlL-Kutub Al-Elmiyah]. Na dalili zao juu ya hayo ni kusisitiza kwa asili kwani asili ya vitu ni twahara mpaka ipatikane sababu ya unajisi, na hatukujua kuwa Mtume S.A.W. aliamrisha kwa kuziosha damu ila damu za Hedhi.
Kadhalika wana dalili zao juu ya kuwa waislamu wakiendelea kuswali kwa majeraha yao katika vita [Imepokewa na Al-Bukhariy kwa maelezo] na Ibn Hajar alisema katika maelezo: Aliyotajwa na Ibn Abi Shaybah kutoka kwa Hashem kutoka kwa Yunus kutoka kwa Al-Hassan], na damu zikitiririka nyingi,kama za Shahidi huzikwa kwa damu yake na haoshwi; kwa mujibu wa amri ya Mtume S.A.W. kuwazika Mashahidi wa Uhud kwa damu zao na hakuwaswalia juu yao na hakuwaosha [Imepokewa na Al-Bukhariy kutoka Hadithi ya Jabir Ibn Abdallah], na lau damu ikiwa ni najisi,basi ilikuwa ni wajibu kuwaosha miongoni mwa mashahidi.
Na kujibiwa juu ya maoni hayo hapo juu: Ni Kwamba kukanusha kwa kujua kitu hakukanushi kuwepo kitu,basi kutokujua kwamba Mtume S.A.W.alimrishia kuosha damu ya Hedhi si maana yake hakuamrisha kuiosha damu nyingine, na kwa hakika unajisi wa damu sio kwa amri ya Mtume S.A.W. tu bali ni kutokana na dalili za Jamhuri ya wanazuoni zilizotangulia.
Ama kauli yao kwamba Waislamu wanaendelea mpaka sasa wanaswali kwa majeraha yao, na Shahidi anazikwa kwa damu yake bila ya kuoshwa ni dalili kwa Jamhuri si dhidi yao; kwani miongoni mwa misingi iliyowekwa na wanazuoni wa kishafiy kwa utwahara wa damu nyingi ikiwa ni damu kutoka kwa mtu yule yule kutoka katika mwili wake siyo kunakiliwa kutoka mtu mwingine, na hali mbili zilizotangulia zinaingia chini ya msingi huu.
Kutokana na yaliyotangulia linadhahiri afikiano la wanazuoni wa fiqhi juu ya unajisi wa damu za Hedhi na Nifasi bila ya hitilafu.Kadhalika waliafikiana juu ya uchache wa damu japokuwa imesemwa juu ya unajisi wake isipokuwa pia imeruhusiwa, ama damu nyingi ,wanazuoni wa fiqhi walisema kwa unajisi wake -na hii ni rai ya kuchaguliwa- Na baadhi ya wanazuoni walisema kwa kuruhusu kwa damu nyingi sharti la kuwa kutoka kwa mtu yule yule sio kutoka kwa mtu mwingine,na ni kama katika hali ya kuzikwa kwa Shahidi kwa damu yake bila ya kumwosha, na Swala ya Waislamu wanaopigana jihadi kuswali na majeraha yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas