Kukopa Mkopo wa Salio Vocha na Sha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukopa Mkopo wa Salio Vocha na Sharti la Kuulipa kwa Malipo ya Ziada Zaidi.

Question

 Ni ipi hukumu ya kukopa salio na kwa sharti la kuulipa kwa malipo ya ziada?

Answer

 Al-Hamdu lillahi na sala na salamu ziwe juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na aali zake na masahaba wake na wanaomfuata. Ama baada ya utangulizi huu:
Kwa hakika kuwasiliana kwa njia ya simu ni huduma ya mfumo wa kisasa inayotolewa na mashirika yenye uhodari maalumu ambayo yanawapa wateja wake huduma hiyo kwa ajili ya kuwawezesha kuongea na kuwasiliana kwa njia ya sauti baina yao kwa umbali wowote ule bila ya kuhitaji kukaribiana kimwili baina yao, na huduma hii kwa upande wa Fiqhi ya Kiislamu ni miongoni mwa manufaa baina ya watu, lakini vifaa vingine halisia vya umeme ni miongoni mwa mali maalumu, na manufaa ni faida inayopatikana kwa kuvitumia vifaa hivyo maalumu, ni mfano wa faida anayoipata mtu katika nyumba kwa kuitumia kwake, na miongoni mwa mnyama kwa kumpanda kwake. [Durar Al-Hukkam Sharh Megalat Al-Ahkam 1\115, Mada 125, Ch. Dar Aj-Jeel].
Ama salio ni haki ya kifedha inayolipiwa kutoka kwenye shirika la mawasiliano kwa ajili ya kumnufaisha mteja kwa mawasiliano ya simu wakati wowote atakapo bila ya kupitisha mipaka ya wakati unaofuata utaratibu wa shirika, kwa pesa zilizolipwa mapema na mteja "Na hii inajulikana kwa mfumo wa kadi", na mteja akitumia wakati wake aliopangiwa na ukamalizika, huduma itasimama mpaka apate salio jingine jipya.
Salio ni mfumo wa thamani ya pesa za mteja ili azitumie kwa ajili ya huduma mbali mbali za simu, na hii ni miongoni mwa haki za mteja zinahusika na mali, na maana ya haki katika istilahi ya wanazuoni wa fiqhi ni: haki inayotambulika kisheria baina ya shirika na mteja mnunuzi kwa ajili ya kuitumia kwa manufaa maalumu. [Rejelea: Al-Haqi wa Mada Sultan Al-Dawlah fi Taqyeedeh, kwa Daktari Mohammad Fathiy Al-Dereniy Uk. 260, Ch. Dar Al-Bashir].
Na uhusiano baina ya haki na manufaa ni masilaha maalumu, ama haki ni njia ya kimaana kwa kuyapata masilaha, lakini vyombo vya kweli ni njia maalumu inayojulikana kama desturi kati ya zamani na sasa kwa kukopea mkopo, kukodisha na kuiweka rehani, na mengineyo katika muamala.
Na mashirika ya mawasiliana yanampa mteja uwezo unaojulikana kama "Kurusha salio" ili kuwarushia salio au baadhi yake wateja wengine, na sharti yakuwa ni namna moja kwa maana "vocha kwa vocha" na hii ni miongoni mwa aina za "Mikopo kwa ajili ya kunufaika nayo na kuwa na haki" na hali hii inajengeka kwa vitu vinavyolingana kwa pande zake zote, kwa sharti ya kuwa kwake bila ziada yoyote, na kwa kuwa kwake pia katika mlango wa uuzaji wa manufaa.
Basi namna ya kwanza ya kurusha vocha baina ya pande mbili ni kuulipia mkopo haki ya mteja kutoka katika shirika la mawasiliana na hilo shirika lazima litoe huduma au sehemu yake kwa mteja wa pili badala ya mteja wa kwanza kutokana na ombi lake, na wa pili anapokuwa na vocha ya kutosha anaweza pia kuliomba shirika kulirushia salio kwa mteja wa kwanza badala yake, na inakuwa ni sawa na kinachochukuliwa mwanzo na hali hii ipo katika mlango wa mkopo wa manufaa.
Na mkopo katika lugha ni: kumega. Na maana yake kisheria ni: Kumiliki kitu kwa sharti la kurejesha kitu kingine kama mbadala wake, na mkopo unaitwa kumega kwa kuwa mkopeshaji huwa anamega sehemu moja kutoka katika mali yake kwa ajili ya anayechukuwa mkopo huo. [Moghny Al-Mohtaj 3\29, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah).
Na imethibitika kwamba mkopo unajuzu kwa upande wa kisheria kutokana na Qur`ani na Sunna na Ijimaa ya Wanachuoni, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi} [AL BAQARAH 245). Na ujumla wa mkopo hapa upo katika haki ya Mwenyezi Mungu hata kama ni maana iliyoazimwa, na uhusiano hapa baina ya maana ya aya na maana ya mkopo ni ushirikiano wa maana mbili katika kuhakikisha na kuthibitisha kwamba mtu anayetoa mali yake kwa ajili ya kutaka thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kama kuupata mkopo wake, na maana iliyoazimwa katika sura ya mkopo kwa maana hii inaashiria kwa usheria wake na uzuri wa sheria juu yake; kwani haisihi kuifananisha maana nzuri kwa maana mbaya katika sheria.
Na Imam Abu-Bakr Al-Jassas anasema katika kitabu cha: [Ahkam Al-Qur`ani 3\616, Ch. Dar Al-Fikr): "Kauli ya Mwenyezi Mungu: {Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi} [AL BAQARAH 245) ni wito wa kutenda matendo mema na kuitoa mali katika njia ya kheri ya Mwenyezi Mungu kwa maneno laini na mazuri. Na mkopo umeitwa hivyo kwa lengo la kuisisitizia haki ya mkopeshaji katika thawabu; kwani kitu hakiwi mkopo isipokuwa kwa kuwepo mbadala wake kama haki ya mkopeshaji".
Na Imam Ar-Raziy anasema katika tafsiri yake kubwa [6\500, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy]: "Hekima ya kuizingatia katika Aya hii juu ya jambo lenye thawabu ya Mwenyezi Mungu, ni kuwa mkopo hauwezi kupotea bali ni lazima ulipwe, na vile vile thawabu za Mwenyezi Mungu haziwezi kupotea bali hurejeshwa kwa mtu".
Ama kwa upande wa Sunna ya Mtume S.A.W., ni kama ilivyosimuliwa na Muslim katika Sahihi yake kutoka katika Hadithi ya Abu Rafea R.A.: "kwamba Mtume S.A.W., alikopa ngamia mdogo kutoka kwa mtu mmoja, kisha akakuta kuna ngamia za sadaka zilizoletwa, Aba Rafea aliagiza kumlipa mtu huyo ngamia zake, akamrudishia Abu-Rafea kwa Mtume S.A.W., akasema: sijakuta ndani yake ila uchaguzi wa nne, alisema: mpe, kwani wema wa watu ni wazuri wa kulipa deni lao".
Kadhalika kuna Hadithi iliyotaja jambo la ukopeshaji kutokana thawabu, kama katika kauli ya Ibn Masuod R.A., kwamba Mtume S.A.W., alisema: "Kila mkopo ni sadaka" Al-Hafedh Al-Munzeriy amelizungumzia jambo hilo katika kitabu cha: [At-Targhib na Al-Tarhib 2\19, Ch., Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): [Ilisimuliwa na Al-Tabarany na Al-Baihaqiy kwa Isnadi Nzuri].
Na waislamu wote waliafikiani juu ya kuwa mkopo unajuzu (Al-Mughny Ch. Ibn Qudamah 4\207, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Araby).
Na asili ya lengo la mkopo ni sadaka nzuri katika haki ya mkopeshaji kwani jambo hili ni miongoni mwa njia za kukidhi haja ya anayehitaji na kumfariji haja yake. Imamu Muslimu amesimuliwa katika Sahihi yake kutoka kwa Abu-Hurairah R.A kwamba Mtume S.A.W., amesema: "Anayemrahisishia jambo mwenye shida, basi Mwenyezi Mungu atamrahisishia yeye jambo lake hapa duniani na kesho akhera". Na haikubaliki kuuchukuwa mkopo kama mapatano ya kibiashara ili iwe ni njia ya kiuchumi kwa ajili ya kupata pesa; kwani jambo hili ni namna moja ya riba ya zama za kijahili iliyotumia haja za wahitaji kwa lengo la kujipatia pesa na maulamaa wote waliharamisha sharti ya ziada wakati wa kurudisha mkopo ikiwa ziada hiyo inatokana na namna ya mkopo au la. Ibn Al-Mundhir anasema: Wanazuoni wote wameafikiana kuwa mkopeshaji akishurutisha alipwe ziada na anayechukuwa mkopo ni haramu. Na imesimuliwa na Ubay Ibn Kaab na Ibn Abbas na Ibn Masuod kwamba waliukataa mkopo unaoambatanishwa na manufaa; kwani mapatano ya aina hii ni ya namna ya sadaka na huruma, na kwa hivyo sharti yoyote ya ziada juu ya kiwango cha mkopo au kama mtu atatoa kitu kilichoharibika na kurudisha kilicho kizima, hii itakuwa ni moja ya aina za riba na hukumu yake ni haramu".
Na Al-Hafedh Ibn Abdulbar Al-Malikiy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Kafy katika fiqh Ahli Al-Madinah 2\728, Ch. Maktabet Al-Reyadh Al-Hadithah]: "Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kumkopesha mtu mwengine pesa kwa sharti ya kuuzidisha mkopo kwa kiasi kikubwa au kidogo cha fedha, na kila ziada katika mkopo au manufaa kwa mkopeshaji ni riba hata kama kiwango cha malipo ya ziada kitakuwa kidogo mno, na ni haramu".
Na anasema katika kitabu cha: [Al-Tamheed Lima fi Al-Muwataa Mina Al-Maany wa Al-Asaneed 4\68, Ch. Wezaret Umum Al-Awqaf wa Al-Shuun Al-Islamiyah Al-Maghreb]: "Waislamu wote wameafikiana kutokana na kauli ya Mtume S.A.W., kwamba sharti lolote la kuwepo ziada katika mkopo ni riba, hata kama kitakuwa kiwango kidogo cha nyongeza, kama Ibn Masuod alivyosema hata kama ni punje moja ya mbegu".
Ni wajibu katika mkopo kulipa kiasi kile kile kilichokopwa bila ya ziada ya aina yoyote, ila kama mkopaji hakuweza kulipa mithili ya mkopo, basi anaweza kulipa kadiri awezavyo hadi atakapokamilisha kiwango kile kile alichokopeshwa, na hii inaafikiana na kauli ya shekhe Al-Islam Zakaria Al-Ansariy katika kitabu chake [Fathu l-Wahab sharhu Manhaji Al-Tolab” 3\260-261, pamoja na maelezo ya Al-Jamal, Ch. Dar Al-Fikr]: "Anayechukuwa mkopo ni lazima aulipe mkopo huo bila ya ziada yoyote; kwani hii ni karibu na haki, na hatua hii ni inaafikiana na mafundisho ya Mtume S.A.W., alipokopa ngamia mdogo na alisema: kwa hakika ni mwema wenu anayelipa deni lake…(na unaharibika) yaani ukopeshaji (kwa uwepo wa sharti ya manufaa kwa mkopeshaji kwa kuulipa mkopo kwa nyongeza) kwa kadiri au sifa ya kurudisha kitu mbadala kama livyokopwa au kuazimwa badala ya kile kivunjika".
Na Al-Sanany alisema katika kitabu cha [Al-Taj Al-Modhahab 2\485, Ch. Maktabat Al-Yaman]: "(Ni wajibu) juu ya anayekopesha (kuurudi mithili yake kwa upande wa kiwango na jinsi kilivhokuwa) na namna yake (na sifa yake) sio zaidi au pungufu yake".
Na imetajwa katika matini ya kisheria yaani aya za Qurani zinazoashiria kuyazingatia manufaa kuwa ni mali kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kisa ya bwana wetu Musa A.S.: {Akasema: Mimi nataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi, khiari yako; lakini mimi sitaki kukutaabisha. Inshallah utanikuta miongoni mwa watu wema} [AL QASAS 27], basi Mtume Musa A.S., alimwoa binti ya Mtume Shoaib na ilhali anafanya kazi kama amejiajiri nafsi yake kwa baba yake Shoaib kwa muda wa miaka kumi,basi kuajiri nafsi yake kwa kazi badala ya kulipa pesa taslimu ni kama kufanya kazi kwa ajili ya manufaa,na msingi wa mahari yakuwa ni mali;kwa kauli ya Mwenyezi Mungu {Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini} [AN NISAA 24].
Kwa hiyo basi manufaa yanazingatiwa kuwa kama mali; kwani mwanachuoni wa Fiqhi ya Kiislamu ameyajaalia manufaa kuwa kama ni mahari. Al-Bahuty Al-Hanbaly alisema katika kitabu chake cha: [Kashaf Al-Qenaa 5\129-130, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): "Na kwa kuwa manufaa ya mungwana yaweza kuchukuliwa kama ujira badala ya mali, kwa hivyo inajuzu mahari kuwa inatokana na manufaa ya mtumwa, na anayesema sio mali ni makosa; kwani yaweza kuchukuwa badala yake na kama yasingekuwa mali yasingechukuliwa kuwa ni kama mali".
Na Al-Khateeb Al-Sherbeny anasema katika kitabu cha: [Mughny Al-Muhtag 4\367-368, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): "(Haisihi kuwa ni bidhaa) malipo mbadala au malipo ya bidhaa mbadala au deni au manufaa mengi au manufaa machache yasiyokwisha kwa uchache wake mpaka yakawa hayawezi kulipika kama mali (inasihi) kuwa (mahari)".
Na wanazuoni wa Kishafi walitaja kwamba kila kinachojuzu kuwa biashara ya malipo mbadala basi kinasihi kukikopesha isipokuwa mjakazi awe halali kwa anayemkopa. Na Al-Imam Al-Nawawy anasema katika kitabu cha: [Al-Rodhah 4\32, Ch. Dar Al-Maaref]: "Mali ni namna mbili, ya kwanza ni kila kitu kinachojuzu kaatika biashara ya mbadalishano, na inajuzu kumkopesha mnyama au kitu kingine chochote lakini kama mkopo huo utakuwa ni mjakazi basi ni lazima hali yake ithibitishwe kwanza, akiwa mtumwa huyo ni haramu kwa mkopeshaji kumoa, kwa upande wa nasabu au kitu kingine, katika hali hii yajuzu kuutimiza mkopo huo, lakini kwa upande mwengine akiwa ni halali kwa mkopeshaji kumwoa, katika hali hii haitajuzu kutimizia mkopo huo kutokana na maandiko ya kale na ya kisasa pia. Ya pili: ni ile siyojuzu mbadala ndani yake yajuzu kutimizia mkopo kwa sharti ya kuulipa mithili ya ulivyokuwa au kadiri yake, kwa hivyo haijuzu katika namna ya kwanza na inajuzu katika namna ya pili".
Na wametajwa pia juu ya kujuzu biashara ya malipo mbadala katika manufaa, na Al-Khatweeb Al-Sherbeniy anasema katika kitabu cha: [Mughny Al-Muhtag 3\25, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: "Biashara ya malipo mbadala inajuzu katika manufaa kama ilivyo katika kufundisha Qur`ani; kwani inathibitishia katika dhima ya wanaomiliki".
Na ujumla huu uliotajwa na Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafiy unaashiria kwamba misingi yao inahitaji kauli ya kusihi kwa mkopo wa manufaa mara moja, na pamoja ya hayo yakuwepo hitilafu miongoni mwa Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafiy ni kama wa madhehebu mengine ya kifiqhi katika jambo la kusihi kwa mkopo wa manufaa, baadhi yao walisema kuwa inajuzu na wengine wakatoa kauli ya kuzuiwa kwake, na wengine wakasema kuwa baadhi ya sura zake zinakatazwa.
Na kwa upande mwengine baadhi ya Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi walisema kuwa inajuzu na miongoni mwao ni Al-Metwaly, na Al-Atar aliikubali pia kauli hii ya kujuzu katika maelezo ya kitabu cha" [Sharh Al-Mhala Lijamu Al-Jawamea 2\368, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: "Ama mkopo katika manufaa unajuzu na rai hii ilinukuliwa na Ibn As-Sobkiy katika kitabu cha: [Tarshih Al-Tawsheh] kwamba Al-Mrtwaliy ambapo aliisema rai hii ya kujuzu". Na pia Ibn Taimiyah aliitoa rai hii pia ya kujuzu mkopo katika manufaa na rai hii ni kinyume cha rai ya Al- Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Hanbali hata kama maoni haya yasiyokuwa miongoni mwa yale yanayofanana, na alitaja kwamba kurejesha mfanowe katika hali hii lazima iwe kwa njia ya kuridhiana baina yao [Al-Insaf Lilmardawiy 5\125, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy], na alisema katika kitabu cha: [Al-Fatawa Al-Kubra 5\394, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: "Inajuzu kukopesha mkopo wa manufaa kama kwamba mtu anavuna naye siku moja na mwengine atavuna naye siku nyingine, au alimtayarishia makazi yake kwa kuwa mwengine atatayarishia makazi badala ya makazi ya kwanza, lakini aghalabu ya mambo ya manufaa ni kuwa miongoni mwa yenye kulingana nayo ili kurejeshia mfanowe kwa maridhiano".
Na imedhihirishwa kutokana na maoni ya Ibn Taimiyah kwamba kulipa deni kama lilivyo kwa kuridhiana baina yao ni miongoni mwa urahisishwaji; kwani msimamo wake ni kukaribisha kwa kiwango kisicho fanana nacho, na kwa hivyo, yanayoweza kufaa katika manufaa yanaweza kurejeshwa mithili yake kweli na ni wajibu kulipa kama asili yake ilivyo katika mlango wa mkopo.
Na kwa upande mwengine Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Hanbali na Al-Qadhi Hussein miongoni mwa Al-Shafieyyah walisema kwa kukatazwa kukopesha mkopo, na hii ni kwa mujibu wa madhehebu ya Hanafi na Maliki. Al-Rohaibaniy Al-Hanbaliy walifuata kauli ya kukatazwa, [3\240, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy]: (walisema kuwa mkopo wa manufaa hauswihi); kwani haijulikani, na rai hii ni kinyume cha rai ya sheikh Taqiy Ad-Diin, aliyesema kuwa inajuzu kukopesha,” ni kama mtu mmoja anavuna naye siku moja, na ilhali naye pia anavuna naye siku nyingine, au kuitayarishia nyumba kwake na mtu huyu pia kuitayarisha nyumba wakati mwengine” ni kama malipo mbadala baina ya nyumba hii na nyumba ile".
Na Al-Seyuty alitaja katika kitabu cha: [Al-Ashbah na Al-Nadhaer Uk. 523, Ch., Dar Al-Kutub Al-Elmiyah) kuwa katika mkopo wa manufaa, wanazuoni wa Kishafiy wana maoni mawili, lakini Al-Qadhi Hussein alisema kwa kukatazwa mkopo wa manufaa,na hii inadhihirisha kutoka kwa kauli yake: "Ni juzu mkopo wa malipo mbadala uitwaye (Al-Salam) katika mkopo wa manufaa, na hii ni pia kunakiliwa kutoka kwa kitabu cha Asili ya Al-Rodhah katika mlango wa Al-Salam kutoka kwa Al-ROYANY na aliikiri, na katika mkopo wake kuna maoni mawili, lakini kukatazwa ni ya kupendelea kwenye Al-Qadhi Hussein".
Na madhehebu ya wanazuoni wa Al-Hanafiyyah hawaruhusiwa mkopo wa kulipa manufaa kwa namna zake zote, na kwa hivyo hairuhusiwi kulipa mbadala ya vocha au salio ya simu ya mkono kwa mithili yake,na Al-Kasaiyy alisema katika kitabu cha: [Al-Badaea 7\31, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah]: "Haijuzu kulipa mkopo wa mbadala".
Na Al-Sarkhaseiy alisema katika kitabu cha: [Sharh Al-Sayr Al-Kaber 5\2120, Ch. Al-Sharekah Al-Sharqiyah Liliealanat]: "Na lau watu wawili kila mmoja wao alikuwa na farasi moja mkononi mfungwa juu ya sifa hii, na kila mtu alipa farasi yake kwa rafiki yake sharti anaitumia katika vita, na wakati ule ule anampa rafiki yake farasi yake mwenyewe, sharti hii ilikuwa ni sharti bovu (jambo hili halisihi; kwani sharti yao juu ya jambo hili ililifanya kuwa ni mbadala wa manufaa kwa manufaa,na mbadala wa manufaa kwa manufaa ni ijara mbovu)kama uuzaji wa makazi kwa makazi".
Kutokana na hayo ya hapo juu ,kwamba mbadala wa manufaa ya namna moja ni mbadala wa kukodisha au mbadala mbovu au mkopo mbovu haisihi,na kwa hivyo anayechukuwa kitu au manufaa ya namna moja lazima kuyarudishia kutoka namna yake au kuyarudishia mithili yake yawezesha kudhibiti kwa upande wa dhahiri na wa ndani.
Na alisema katika kitabu cha: [Al-Bahri Al-Raeq 6\133, 171, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: "Mkopo ni madhumuni kwa mithili yake an haijuzu katika ghairi ya mithili;kwani haiwezekani kuwa deni katika dhima,na anayekopesha kuumiliki kama ni mkopo sahihi, na mkopo huu wa mbovu lazima kuurudisha". Na alisema: "Kauli yake (sio katika mnyama) kwa maana haisihi katika mnyama kwani hawezekani kujua undani wake, na pia haiwezekani kukopeshwa kwani kopeshwa kwake ni mkopo mbovu lakini kadiri yake inadhaminiwa kwa bei yake, na uumiliki kwa pesa taslimu hata lau akiwa na mtumwa na akamwachia inajuzu kwani yeye ni mtumwa wake na ni milki yake".
Na katika kitabu cha: [Rad Al-Muhtar 6\62, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elimiyah]: "Na katika kitabu cha: Al Tatar khaniyah:ni juzu ikikubaliwa manufaa kutokana na namna yake katika dhahiri ya riwaya na ni yakuwa Fatwa juu yake".
Ama wanazuoni wa Maliki walisema kwamba inachojuzu salam inajuzu mkopo wake,na isiyojuzu salam haijuzu mkopo wake,na kwa upande mwengine hawaruhusiwi mkopo katika mjakazi anayehalalisha kwa mkopesha hata lau inajuzu katika salam.Na katika dhana ya salam waliepushia manufaa kwa baadhi ya mazuizi au mashuruti,na kwa hivyo Madhehebu ya Maliki hawaruhusu salam\ mbadala katika manufaa ,na kwa hivyo hairuhusu kumkopeshia mjakazi kutokana na msingi huu uliyotajwa hapo juu.Al-Sawi alisema katika maelezo yake juu ya kitabu cha: [Al-sharh Al-Saghir 3\292, Ch. Dar Al-Maaref]: "Al-Mosannef alisema kwamba: Kila inachosihi mbadala inajuzu kumkopeshia ila katika mjakazi anayehalalishia kwa mkopesha".
Na walichukuwa katika dhana ya mfumo wa salamu kwa anachosema Ibn Arafah anaposema: "Ni mkataba wa mbadala usiyo ni mbadala wa mithili". Walisema: Bsi kauli yake ni: (Pasipo na mbadala wa mithili) na kwa hivyo waliepusha bei ya kuchukuwa pesa baadaye, na kauli yake: (wala manufaa), [Sharh Al-Khorashiy juu ya Al-Mukhtasar 5\202, Ch. Dar Al-Fikr): "Na hukumu ya mkopo uliokatazwa ni kuurudisha ni kama bei mbovu, na anayechukuwa mkopo ni lazima kuirudishia thamani yake, na mithili ni katika mithili yake".
Na wafuasi wa zama hii ya Washafiyah walisema kwamba uhakiki katika madhehebu yao ulisimamisha juu ya tafsili,kwa hivyo walisema kwa kukatazwa katika baadhi ya sura zake na walisema kwa kujuzu katika baadhi nyingine,lakini walihitalifiana katika uwafiki kati ya maneno yaliyotumia katika kukatazwa na maneno yaliyojuzu yaliyotajwa na Imam Al-Nawawy katika kitabu cha: [Al-Rawdhah” baadhi yao walisema kwamba kukataza ni kuhusu kwa kopesha manufaa kitu pahala kitu kingine;kwani haijuzu mbadala \salam\katika namna yake,lakini katika manufaa yanayohusika dhima yanajuzu kopeshwa,na wengine walisema kwamba kukatazwa ni kuhusu mkopo wa manufaa ya nyumba,kwani haikuwa na mithili kwake,na walisema kwamba sababu zao hapa kwa kuwa haiwezikani au haiwezi kuirudishia mithili yake,na kwa hivyo Mashafi walisema kwa rai ya kujuzu kukopesha manufaa ya mikopo yanayoweza kudhibiti kwa wasifu na yaweza kuirudishwa mfano wake.
Na Abou Ishaq Al-Shirazy alisema katika kitabu cha: [Al-Mohadhab” 1\303, Ch. Issa Al-Halabiy]: "Inajuzu kila mali yaweza kumiliki kwa bei na kudhibiti kwa wasifu kwani yenyewe ni mkataba wa kumiliki kuuthibiti mbadala malipo ndani yake katika dhima na kwa hivyo inajuzu kuumiliki na kudhibiti kwa wasifu kama katika mfumo wa Salam yaani mbadala wa malipo)).
Na Al-Khatweeb Al-Sherbeny alisema katika “Moghny Al-Mohtaj” 3\32, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah): Alisema katika “Al-Rawdhah”: Haijuzu kukopesha manufaa; kwani malipo mbadala hayajuzu katika mfumo huu, na ilichukuliwa juu yake hapa kwamba mahala pake katika manufaa ya kitu maalumu kwa kitu maalumu,ama kilichokuwa katika dhima kinaweza kopesha kwani kinachojuzu katika malipo mbadala kinajuzu katika mkopo.Na haijuzu kukopesha maji ya mfereji kwa sababu ya kutofahamika undani wake (na yasiyosihi malipo mbadala ndani yake) kama mjakazi na mtoto wake na almasi na kadhalika(hayajuzu kukopesha kwake); kwani yasiyoweza kudhibiti au kuwepo kwake ni nadra au ngumu ya kurudishwa haijuzu kukopeshwa.Na rai ya pili: Ni kujuzu kama katika bei, lakini hitilafu zinasimama juu ya kwamba ni lazima katika mambo yanayokadiriwa. Na Al-Mawardiy alisema: Haijuzu kukopesha nyumba kwani haijuzu malipo mbadala katika nyumba, na Ibn Al-Refaah na Al-Sobkiy walisema kwa kauli kama hii".
Na Al-Shehab Al-Ramliy aliulizwa juu ya mkopo wa manufaa, ni inajuzu ama la? akajibu kwa kauli ya: "kwamba yanayo katika kitabu “Al-Rawdhah” ni katika mlango wa mkopo ni kukatazwa,na ndani yake kama asili yake katika mlango wa kukodisha ni kujuzu mkopo,na Al-Sobky na Al-Balqeny na wengine walisema kwa manufaa ya nyumba na kuzuia malipo mbadala ndani yake,na baadhi yao walisema kwa kujuzu katika dhima, na wengine walisema rai ya Al-Sobkiy na wengine ni karibu na usahihi [Fatawa Al-Ramliy 2\168, Ch. Al-Maktabah Al-Islamiyah].
Na matokeo ya hayo yaliyotangulia katika kitabu cha: [Al-Maslak] ya kwanza: kwamba ni miongoni mwa mlango wa mkopo juu ya hitilafu baina ya wanazuoni katika usahihi na kujuzu mkopo wa manufaa au la, tukichukuwa kwa madhehebu yaliyosema kwa kujuzu basi lazima kurudisha kama mithili;kwani ni msingi wa kuandika mkataba wa mkopo, kwani msingi wake ulisimamishwa juu ya rehema na kukupa na siyo kwa ajili ya kufaidika pesa au biashara,na tukichukuwa kwa madhehebu yaliyosema kwa kukatazwa mfumo wa kuendesha mkopo katika manufaa niwe katika yanayokamilisha sharti ya manufaa na kurudisha mfano wake iwezekanavyo au kuirudisha kadiri ya pesa zake,na hivyo pamoja na kumuweka katika dhambi ya kukatazwa.
Ama njia ya pili katika kutatua masuala ya malipo mbadala ya vocha kwa vocha nyingine zaidi, rai hii ilichukuwa suala hili kutoka mlango wa kukodi au bei manufaa kwa mengine kutoka namna yake ile ile, na kwa hivyo manufaa ya pesa hapa yanasimamisha juu ya kuridhiana miongoni mwao,na kwa hivyo malipo mbadala yanajuzu kutokana na kuwa hakuna riba katika manufaa.
Al-Nawawy alisema katika kitabu cha: [Rawdhat Al-Taleben 7\176, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy]: "inajuzu kuwa kukodisha ni kwa ajili ya manufaa, ikiwa ni kwa makubaliano ya jinsi ya kuikodisha nyumba kwa kupata manufaa ya nyumba hiyo, au kinyume chake kama kwamba anakodisha kwa ajili ya manufaa ya mtumwa, na kamwe hakuna riba katika manufaa, hata akikodisha nyumba kwa ajili ya kunufaika na nyumba mbili, au akakodisha dhahabu kwa dhahabu, basi itakuwa inajuzu, na hakuna sharti lolote la kupata pesa taslimu katika makabidhiano".
Na Ibn Hazm anasema katika kitabu cha: [Al-Mohala 7\23, Ch. Dar Al-Fikr): "ukodishaji kwa ajili ya kukodisha inajuzu na hii ni kama ukodishaji huo wa nyumba kwa ajili ya makazi au huduma ya mja kwa mja mwengine, au makazi kwa huduma ya mja au kwa ajili ya ushonaji, haya yote yanajuzu; kwani hakuna matini katika Qur`ani inayolikataza jambo hili, na hii ni kauli Imam Malik na Abou hanifa, wamesema: hayajuzu manufaa ya mambo ya kiraa nyumba kwa kiraa nyumba lakini inajuzu kwa huduma ya mtumwa)).
Na katika kitabu cha: [Al-Modawanah 3\517): "Mtu anakodisha nyumba kwa malipo ya kodi ya makazi ya nyumba yake, na mimi ikasema: je, unaonaje kama ningekukodishia nyumba ya kuishi kwa mwaka huu kwa kukaa katika nyumba yangu? Je jambo hili linajuzu katika kauli ya Imamu Malik? akasema: kwangu mimi inajuzu na ni sawa".
Na katika kitabu cha: [Kashaf Al-Qenaa”ni kati ya vitabu vya wanazuoni wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal 3\557, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: Je inajuzu kukodisha nyumba kwa ajili ya makazi, na nyingine kwa ajili ya kumhudumia mtumwa na kwa ajili ya kuolewa mwanamke kwa mujibu wa kisa cha Mtume SHUAYB A.S.; Kwani yeye aliifanya ndoa kuwa ni malipo mbadala ya kukodi, na kwa kuwa kila kinachojuzu kuwa bei katika biashara kinaweza kuwa kama malipo mbadala katika kukodi nyumba, na kwa hivyo basi kama kitu maalumu kinajuzu kuwa malipo mbadala, basi kinajuzu pia kunufaika nacho ikiwa ni kwa namna moja kama ya kwanza au kwa namna ya hitilafu kama katika rai ya pili, Al-Majdi amesema: katika maelezo yake: Ukimpeleka mtumwa wako kwa mshonaji ili amfundishe kazi hii kijana wake kwa mwaka mmoja inajujuzu katika Madhehebu ya Imamu Malik na kwetu pia".
Kwa mujibu wa njia hii iliyotangulia ni kuwa yanajuzu mabadilishano wa vocha ya simu ya mkono na mapigo ya simu kwa kinachokuwa kutoka namna yake pamoja na upendeleo;na kutokana na muamala hii kutoka mauzaji yaliyotimiza kumiliki manufaa kwa malipo mbadala kama ijara na kadhalika.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia, anayechukuwa mkopo wa salio la kupigia simu ni wajibu juu yake kulirejesha salio hilo kama salio alilolichukuwa kutoka kwa mkopeshaji,na ni kama ilichochukuliwa na salio yake ilirudia kwake tena,hata lau bei ya mapigo ya simu yanabadilika katika bei yake au katika sifa zake;kwani mahali ya mkopo ni salio na siyo ya kadiri ya mapigo ya simu yanayotumia kwa salio hii au sifa nzuri nyingine, lakini lau mkopeshaji anampa sharti ya kuzidishia pesa juu ya salio, itakuwa ni haramu kwa upande wa kisheria; kwani hii ni kutokana na riba na riba hii ni miongoni mwa madhambi makubwa yaliyoharamishiwa na sheria, na njia hii kwa mfumo huu ni mkopo haramu na ni wajibu kuulipa kama ulivyo bila ya nyongeza yoyote kwa kwa jinsi iwezikanavyo au kwa kadiri ya kiwango cha gharama zake, lakini kama sio kwa mfumo wa mkopo inakuwa ni sahihi hata kama kuna upendeleo baina yao na kuna sharti ya kuwepo ziada kutokana na muamala wa ujira wa kwamba kukodisha kwa ajili ya manufaa ni kwa manufaa yanayotokana na jinsi ulivyo.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas