Kusoma Dua ya Qunuti katika Swala ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Dua ya Qunuti katika Swala ya Asubuhi.

Question

 Waislamu wanaoswali wametofautiana na Imamu kuhusu kusoma dua ya Qunuti katika Swala ya asubuhi. Imamu anaona kuwa dua ya Qunuti inaruhusiwa na ni Sunna, lakini Waislamu wanaoswali wanaona kuwa dua ya Qunuti hairuhusiwi, na kuisoma dua ya Qunuti katika kila siku ni uzushi. Tunaomba jibu lililokamili katika suala hili, ambalo labda linasababisha fitina katika msikiti, na kama dua ya Qunuti inapendekezwa, basi nafasi yake katika Swala ni wapi? Ni nini dua yake inayopendekezwa? Asante sana

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu.
Qunuti katika lugha ni: utii. Na asili yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {na watiifu wanaume na watiifu wanawake} [AL AHZAAB: 35] kisha kusimama katika swala kunaitwa Qunuti . [Rejea: Al-Sihah kwa Al-Jawhari 1/261, kidahizo cha: Qunuti , Dar Al-Elm lel Malayiin].
Al-Qadhi Abu Bakar Ibn Al-Arabi alisema katika maelezo ya Tirmidhi [Aridhatul Ahwadhi, 2/178, 179 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Nilifuatilia maana za Qunuti nimezikuta ni kumi: utii, ibada, utii mara kwa mara, Swala, kusimama, urefu wa kusimama, kuomba dua, unyenyekevu, kunyamaza kimya, kutogeuka, na maana hizo zote zinawezekana maana ya kwanza ni: kunyamaza kimya, unyenyekevu na kusimama. Imepokelewa katika Sahihi mbili na Sunan: "Swala iliyo bora ni swala pamoja urefu wa Qunuti" – maana yake ni kusimama katika swala za usiku ni bora zaidi kuliko kurukuu na kusujudu wakati wa siku”.
Kwa hiyo, wanavyuoni wa tafsiri wanaona kuwa Qunuti ni kutii kwa utulivu, au ni kuendelea kwa kutii, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama} [Rejea: Al-Jamii Liahkam Al-Qur'ani kwa Al-Qurtubi, 3/196, Al-Kutub Walwathaiq Al-Qawmiyah huko Kairo, Tafsir Ibn Katheer, 6/418, Ch. Dar Taybah kwa Kuchapisha na Usambazaji katika Riyadh].
Qunuuti katika istilahi: ni jina la dua katika swala, kwenye nafasi fulani ya kusimama. [Rejea: Al-Futuhaat Al-Rabaniyah Sharhu Al-Adhkaar Al-Nawawiyah kwa Ibn Allan Al-Sadiqi, 2/286, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Wanavyuoni wametofautiana kuhusu uhalali wa Qunuti, hukumu yake, wakati wake, sababu yake, na ikiwa inaruhusiwa au la? Basi, ikiwa ni halali, je, ni wajibu au inapendekeza au ni Sunna? Ni wakati gani inakuwa halali? Vile vile Wanavyuoni wametofautiana kuhusu nafasi yake, je, ni kabla ya kurukuu au baada yake?
Rai tuliyoichagua kwa fatwa ni kwamba dua ya qunuuti ni Sunna katika Swala ya asubuhi, kama ukiwepo msiba au la. Hivyo wingi wa wanavyuoni waliotangulia, masahaba na wafuasi, na wanavyuoni waliokuja baada yao walifuata mtazamo huo.
Dalili ya hili ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik, R.A: "Kuwa Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu yao – yaani juu ya wauaji wa wasomi wa Qur`ani - kisha akaacha dua hii, ama katika Swala ya asubuhi, hakuacha dua ya Qunuti hadi akafariki dunia".
Imamu Al-Nawawi alisema katika “Al-Majmuu” [3/484, Al Matbaah Al-Muniriyah]: “Ni Hadithi sahihi iliyopokelewa kutoka kwa kundi la wanavyuoni waliobobea katika Hadithi na walisema ni Hadithi sahihi. Pia Al-Hafiz Abu Abdullah Mohammed Ibn Ali Al-Balkhiy, Al-Hakim Abu Abdullah, na Baihaqiy, ilipokelewa kutoka kwa Ad-Daaraqutniy kwa mapokezi sahihi”.
Tulisema: Hadithi hii imepokelewa kupitia Abu Jaafar Al-Razi kutoka kwa Ar-Rabii Ibn Anas kutoka kwa Anas Ibn Malik, R.A: "Kuwa Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu yao – yaani juu ya wauaji wa masahaba walioihifadhi na wanaoisoma Qur`ani - kisha akaacha dua hii, ama katika Swala ya asubuhi, hakuacha dua ya Qunuti hadi akafariki dunia" .
Imepokelewa kutoka kwa Abdul Raziq katika kitabu cha [Al-Musannaf], na kupitia Ad-Daraqutwniy katika «Sunan», na Ahmad katika «Musnad», na Al-Hakim katika kitabu cha: [Al-Arobaini], na Al-Baihaqiy katika «Al-Sunan Al-Kubra» na ilipokelewa kutoka kwa Al-Hakim kuwa alisema: “Hadithi hii ina mapokezi sahihi, na wapokezi wake ni waaminifu”, na imepokelewa kutoka kwa Al-Tahhaawi Katika kitabu cha: [Sharhu Maani Al-Aathar 1/143, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], Nuruddin Al-Haythami katika kitabu cha: [Majma Al-Zawaa'id 2/331 Dar Al-Fikr] kuhusu mapokezi ya Hadithi hii kuwa: “Wapokezi wake ni waaminifu”.
Na Wanavyuoni walitofautiana pia kuhusu Abu Jaafar Al-Razi aitwaye Isa Ibn Mahan Al-Razi. Al-Hafez Ibn Hajar alisema katika kitabu cha: [Taqriib At-Tahdhiib ukurasa wa 629, Ch. Dar Al-Rasheed, Syria] kuwa Abu Jaafar Al-Razi: “Anasema kweli lakini uhifadhi wake ni mbaya”.
Kwa hiyo, Abu Jaafar Al-Razi ni miongoni mwa watu wanaokwepo katika nafasi ya tano kwa Ibn Hajar, na wanazingatiwa katika nafasi za udhaifu kwa ujumla, na wanashiriki watu wa nafasi ya nne katika hoja, na Hadithi inayopokelewa kutoka kwao ni Hasan kwa dhati yake. [Rejea: Al Faadh wa Ibaaraat Al-Jarhu wa Al-Taadil, na Dk / Ahmed Maabad Abdul Karim, uk. 181, Adhwaa Al-Salaf].
Kwa hiyo, tunaona kwamba Al-Hafidh Ibn Hajar amesema katika kitabu chake [Nataij Al-Afkaar Fi Takhriij Ahadith Al-Adhakaar] kuwa ni Hadithi sahihi [2/136, Ch. Dar Ibn Katheer, Dameski].
Hadithi hii ina ushahidi unaoongeza nguvu yake, katika Sahihi mbili kutoka kwa Asem alisema: niliuliza Anas Ibn Malik, R.A. kuhusu Qunuti katika swala, alisema: Ndiyo, nilimwuuliza: nafasi yake ni kabla ya kurukuu au baada yake. Akasema: ni kabla ya kurukuu. Nikasema: Ni kwamba kuna mtu fulani ameniambia kwamba umesema kuwa nafasi ya Qunuti ni baada ya kurukuu. Alisema: mtu huyo amesema uongo, lakini Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu kwa mwezi mmoja, kwani aliwatumwa baadhi ya Masahaba wanaoitwa wasomi nao ni wanaume sabini kwa watu wa makafiri waliokuwa na ahadi, Masahaba hawa wameuawa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akasoma dua ya Qunuti juu ya makafiri hawa kwa muda wa mwezi mmoja.
Hadithi hii haipokelewi kutoka kwa Asem pekee yake, lakini Abdul Aziz Ibn Sahib almfuata katika Hadithi hii, kama katika Sahih Al-Bukhariy, ambapo alisema katika Hadithi yake baada ya kutaja kisa cha wasomi: mtu aliwauliza watu kuhusu Qunuti , je ni baada ya kurukuu au baada ya kumaliza kusoma? Alisema: Hapana, lakini baada ya kumaliza kusoma.
Hamid alikubali rai hii kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A., alisema: Alipoulizwa kuhusu dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, alisema: Tulikuwa tukisoma dua ya Qunuti kabla ya kurukuu na baada yake pia. [Hadithi hii Imepokelwa kutoka kwa Ibn Majah katika Sunan yake].
Hii ina maana kwamba dua ya Qunuti ya kudumu ilikuwa kabla ya kurukuu. Kama ikiwepo msiba dua ya Qunuti ilikuwa baada ya kurukuu. Hii ni wazi pasipo na shida.
Al-Haafiz Ibn Hajar alisema katika kitabu cha: [Al-Fath”, (2/491). Ch. Dar Al Maarifa]: “Jumla zilizopokelewa kutoka kwa Anas kwamba, dua ya Qunuti kwa ajili ya shida Fulani huwa inakuwa baada ya kurukuu pasipo na tofauti kuhusu suala hilo, lakini kama isipokuwa na shida, basi dua ya Qunuti kufuatana na rai sahihi inakuwa kabla ya kurukuu. Kazi ya Masahaba ilikuwa tofauti katika suala hili, na inaonekana kwamba ni tofauti inayoruhusiwa.
Pia inavyothibitishwa hivyo kwa iliyopokelewa kutoka kwa Muslim katika sahihi yake kutoka kwa Al-Bara Ibn Azib R.A.: "Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa akisoma dua ya Qunuti katika swala ya Asubuhi na Magharibi".
Imam An-Nawawiy alisema katika kitabu cha: [Al-Majmuu 3/484]: “Hakuna madhara yoyote kama watu wakiacha kusoma dua ya Qunuti katika swala ya Maghribi, kwa sababu siyo wajibu au makubaliano ya wanavyuoni yamethibitisha kuwa dua ya Qunuti imefutwa katika swala ya Magharibi”.
Ibn Qutaiba ametaja katika kitabu cha: [Tawiil Mukhtalaf Al-Hadith Uk. 262, Ch. Dar Al-Jil - Beirut]: kwamba wanavyuoni hawatofautiana katika kutosoma dua ya Qunuti katika swala ya Magharibi.
Wale ambao walisema rai hii miongoni mwa Masahaba ni: Abu Bakr na Omar Ibn Al-Khatwab, Othman na Ali na Al-Baraa Ibn Azib R.A., na miongoni mwa wafuasi ni wingi, nayo ni madhehebu ya Ibn Abi Layla na Al-Hassan Ibn Saleh na Dawud.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika Sunan yake kutoka kwa Al-Awaam Ibn Hamza alisema: Niliuliza Abu Othman kuhusu kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi. Alisema: Baada ya kurukuu. Nikasema: Kutoka kwa nani? Akasema: Kutoka kwa Abu Bakr, Omar na Othman R.A. Na imepokelewa pia kutoka kwa Abu Rajaa amesema: “Ibn Abbas alisali swala ya asubuhi katika msikiti huu akasoma dua ya qunuuti na akasoma aya hii {na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuQunuti} [AL BAQARAH: 238]”, na pia: Kutoka kwa Obeid Ibn Al-Baraa kutoka kwa Al-Baraa: kuwa amesoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi.
Nayo ni madhehebu ya Imam Al-Shafi, katika kitabu cha [Al-Minhaj cha Al-Nawawi uk. 99, Dar Al-Minhaj, Jeddah]: “Ni Sunna kuQunuti baada ya rakaa ya pili ya Swala ya asubuhi”.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Ali Ibn Abu Hurairah kutoka katika madhehebu ya Imam Ashafiy: kuwa hasomi dua ya Qunuti katika Swala ya asubuhi, na Imam Al-Nawawiy akajibu kuhusu hili, akisema: “Hii ni ajabu na makosa”. [Rejea: Rawdhatul Twalibiin kwa Al-Nawawi, 1/254, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy].
Wafuwasi wa Madhehebu ya Imam Malik walisema kwamba inapendekezwa kusoma dua ya Qunuti katika Swala ya asubuhi. Vile vile katika kitabu cha [Al-Sharhul Kabiir kwa Sheikh Al-Dardir]: “(na) inapendekeza (kuqunuuti) yaan kusoma dua ya qunuuti (kwa siri katika swala ya asubuhi) (tu)”.
Sheikh Ad-Dusokiy alisema katika kitabu chake, akisema: “kauli yake: (inapendekezwa kusoma dua ya Qunuti) ni rai ile iliyotajwa na mtunzi kuwa inapendekezwa dua kuwa ni rai maarufu, Sahnoun alisema: Ni Sunna, pia Yahya Ibn Omar amesema: dua ya Qunuti hairuhusiwi, Ibn Ziyad alisema: aliyeacha kusoma dua ya Qunuti Swala yake huharibika, na kauli hii inaonesha kuwa kusoma dua ya Qunuti ni wajibu. Kauli yake: (yaani dua) hii inaonesha kuwa dua ya Qunuti hapa; kwani inamaanisha kwa mujibu wa lugha, mambo mengine, miongoni mwa mambo haya ni kutii na ibada” [Rejea: Al-Sharhul Kabiir kwa Sheikh Ad-Dardir Ala Mukhtasar Khalil -katika kitabu cha Al-Dusokiy - 1/248, 249, Ch. Dar Al-Fikr].
Inaeleweka kuwa yaliyo maarufu kutoka madhehebu ya Imam Malik ni kwamba inapendekezwa dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, Sahnoun alisema kwamba ni Sunna, na Ibn Ziyad miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Imam Malik alisema kwamba pasipo na dua ya Qunuti swala huharibika, inaeleweka kutoka maneno yake kuwa dua ya Qunuti ni wajibu.
Wafuasi wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa na Ahmad Ibn Hanbal walisema kwamba: hakuna dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, ambayo ni maoni ya Ibn Masoud na yamepokelewa pia kutoka kwa Ibn Omar, Ibn Abbas na Abu Ad-Dardaa kutoka kwa masahaba R.A., na Sufian Al-Thawriy pia alisema hivyo.
Kwa mujibu wa mtazamo wa wafuasi wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa kuwa hairuhusiwi kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, katika kitabu cha [Al-Kanz wa Sharhahu kwa Al-Zilai]: “(Hairuhusiwi kusoma dua ya Qunuti katika swala nyingine) yaani hairuhusiwi isipokuwa katika swala ya Witri tu.” [Rejea: Tabiin al-Haqaiq Sharhu Kanzul Daqaiq 1/170, 171, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Katika kitabu cha: [Al-Dur Al-Mukhtar] mtunzi wake alipotaja masharti ya swala, alitaja miongoni mwao: Ufuatiliaji wa Imamu maana katika masuala yaliyofanyiwa jitihada siyo katika masuala yaliyofutwa au yasiyoruhusiwa kufuatana na Sunna kama vile dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi. Ibn Abidin katika kitabu chake alisema: “kauli yake: (kama vile dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi), maana yake ni kwamba ama suala hili limefutwa kwa kulikadiria lilikuwa Sunna, au haliruhusiwi kwa mujibu wa Sunna kukadiria lilikuwa dua mbaya juu ya watu maalumu kwa muda wa mwezi mmoja tu, kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi ni mafano wa suala lililofutwa au lisiloruhusiwa” [Rejea: Radul Muhtar ala Al-Durr Al-Mukhtar, 1/471, 472, Ch. Dar Al Kutub Al-Elmiyah].
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad Ibn Hanbal wanaona kwamba inachukiza kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi; Katika Sharhul Muntaha kwa Al-Bahwatiy: “(Inachukiza kusoma dua ya Qunuti katika swala isipokuwa swala ya Witri tu) hata katika swala ya asubuhi, imepokelewa hivyo kutoka kwa Ibn Masuod, Ibn Abbas, Ibn Omar na Abu Al-Dardaa” [Daqaiq Uwli Nuha lisharhil Muntaha 1/242, Ch. Alam Al-Kutub].
Wamethibitisha hivyo kufuatana na yaliyotajwa katika sahihi mbili kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu ya watu miongoni mwa Waarabu kisha akaiacha.
Hii inajibiwa kuwa kinachoachwa na Mtume, S.A.W. katika Hadithi ni kuomba dua mbaya juu ya makafiri hawa tu, lakini hakuacha kusoma dua ya Qunuti kwa jumla wala hakuacha kusoma dua ya Qunuti katika swala nyingine isipokuwa swala ya asubuhi, na maana hii inazingatiwa, kwa sababu Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Anas katika kauli yake: bado akasoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi mpaka amefariki dunia, Hadithi hi ni sahihi na wazi, kwa hivyo, ni lazima kupatanisha kati ya Hadithi hizi mbili. Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy kwa mapokezi yake kutoka kwa Abd Al-Rahman Ibn Mahdi Al-Imam, alisema kuwa: Mtume S.A.W, ameacha kuwalaani makafiri tu, na alisema, maana hiyo inathibitishwa kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Hurairah kwamba, ambapo alisema: kisha Mtume S.A.W. akaacha kuomba dua kwa ajili yao, yaani kwa ajili ya walio wanyonge miongoni mwa Waumini na vile vile akaacha kuwaombea dua mbaya makafiri.
Kitabu cha: [Al-Badr Al-Aini Fi Sharh Sahihil Bukhariy kimefuata mtazamo ule [Omdatul Qari, 7/17, Idartul Twibatul Minbariyah] kikisema: “Ule mtazamo hauna dalili, kwa sababu kauli yake Mtume S.A.W. “Akaacha kuomba dua” maana yake ni kuacha kwa kuomba dua ya Qunuti kwa jumla katika swala zote. Na kuainisha kwa swala ya asubuhi bila ya ushahidi sio sahihi. Na kauli yake: “yaani akaacha kuomba dua tu” sio sahihi; kwani dua iliyotajwa ni dua ya Qunuti sio dua kwa jumla, hivyo ameacha dua ya Qunuti, na hali ya kuacha kitu baada ya kukifanya ina maana ya kufutwa kwa kitu hicho”.
Mtazamo ule una nguvu na unazingatiwa katika baadhi ya sehemu wake, na unathibitishwa kwa baadhi ya Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Sunan An-Nasai na Musnad Abi Yala kutoka kwa Anas R.A kuwa alisema: "Kisha akaiacha kuomba dua baada ya kurukuu)), Hadithi hii imesababisha tofauti. Ina maana kwamba kitu kilichoachwa ni dua ya Qunuti baada ya kurukuu, na hii siyo sababu ya kuifuta dua ya Qunuti, inavyodaiwa na wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa.
Kuhusu dua ya Qunuti ya kudumu, iliyo kabla ya kurukuu, ilibainishwa na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Asem iliyo katika Sahihi mbili. Nayo imefasiriwa, na inaeleweka katika Madhehbu ya Imam Abu Hanifa: kwamba Hadithi iliyofasiriwa inatangulia matini; kwa sababu ya nguvu wake, kwani Hadithi iliyofasiriwa haiwezekana kufasiriwa kwa maana nyingine, lakini matini inawezekana kufasiriwa.
Hitimisho ni kwamba aina za ushahidi wa maneno kulingana na masharti ni nne:
1- Maneno yaliyo wazi, nayo ni yale ambayo yako wazi kwa mwenye kuyasikia pamoja na uwezekano wa tafsiri na uainishaji.
2. Matini, nayo ni ile ambayo imeongezwa uwazi zaidi kuliko ile ya wazi, yaani kusikia maneno kutoka katika kauli iliyosmewa na anakusudia maana yake lakini inawezekana kufasiriwa kwa maana nyingine pia.
3 – Maneno yaliyofasiriwa, nayo ambayo yameongezwa uwazi wake zaidi kuliko matini kwa kadiri isiyokubali uwezekano wa uainishaji ikiwa ni ya jumla wala hayakubali tafsiri, ikiwa ni maalumu.
4 – Maneno yenye maana wazi, nayo ambayo hayakubali tafsiri wala uainishaji wala kufutwa. [Rejea: Sharhu Al-Qawaid Al-Fiqhiyah kwa Sheikh Ahmed Al-Zarqa, Uk. 146, Ch. Dar Al-Qalam, Dameskiy].
Waliopinga suala la kusoma dua ya Qunuti walithibitisha mtazamo wao kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi na Al-Nasai katika Al-Kubra, Ibn Majah, na Ahmad kutoka kwa Hadithi ya Abu Malik Al-Ashja'i Saad Ibn Tariq Ibn Ashim alisema: nilimwambia baba yangu: ewe baba yangu, umesali nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, Abu Bakr, Omar, Othman na Ali hapa katika Kufa, kwa muda karibu miaka hamsini na tano, je, walikuwa wakisoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi? Alisema: ewe mwanangu jambo hili ni uzushi.
Hiyo inajibiwa kwamba mapokezi haya ambayo yanathibitisha Qunuti ambapo ni ongezeko la maarifa ni lazima kutanguliwa. Na Tariq hakuhifadhi, na mwenye kuhifadhi ni hoja juu ya asiyehifadhi.
Pia walithibitisha mtazamo wao kwa kauli iliyopokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy kutoka kwa Abu Mahliz alisema: Nilisali pamoja na Ibn 'Omar swala ya asubuhi lakini hakusoma dua ya Qunuti, nikamwambia Ibn' Omar: Sikuoni unasoma dua ya Qunuti. Akasema: Sikuona yeyote miongoni mwa wenzetu anafanya hivyo.
Hiyo inajibiwa kuwa kusahau kwa baadhi ya Masahaba kwa baadhi ya Sunna hali hii haipotezi Hadithi ya mwenye kuthibitisha Sunna hii, kama Ibn Omar, R.A hakuihifadhi Hadithi hii au ameisahau, basi Anas, Al-Baraa Ibn Azib na wengine, wameihifadhi, kwa hivyo walioihifadhi wametanguliwa kama alivyosema Imam Al-Nawawiy katika kitabu chake: [Al-Majmuu' 3/485].
Pia walithibitisha mtazamo wao kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Daaraqutni katika Sunan yake na Al-Baihaqiy katika Al-Kubra kutoka kwa Ibn Abbas, R.A kwamba kusoam dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi ni uzushi.
Hiyo inajibiwa kuwa kauli hii ya Ibn Abbas ni dhaifu sana, na imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy kutoka kwa Abu Laila Al-Kofiy, na alisema katika kitabu cha: [Al-Sunan Al-Kubra 2/213, Ch. Maktabat Dar El-Baz - Mjini Makkah] kuwa: “Kauli hii si kweli, Abu Laila anaachwa, na imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba yeye akasoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi”.
Kwa mujibu wa kitabu cha [Al-Sunnah Al-Kubra kwa Al Baihaqiy] na Sharhu maani Al-Athar kwa Al-Tahawi [1/252] kutoka kwa Abu Rajaa alisema kuwa: Ibn Abbas alisali swala ya asubuhi pamoja sisi akasoma dua ya Qunuti kabla ya kurukuu, na wakati alipoondoka, alisema swala hii ni swala ya kati ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuQunuti} [AL BAQARAH 238].
Katika taarifa hii kwamba Ibn Abbas R.A. alikuwa akisoma dua ya Qunuti kabla ya kurukuu, na anazingatia hivyo ni Qunuti ya kawaida, lakini Hadithi zile nyingine zilizopokelewa kutoka kwake zinazingatiwa kuwa zinahusu swala ya kupata haja au ya msiba, nafasi ya dua ya Qunuti baada ya kuinua kutoka kurukuu, na hizi ni jumla ya Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A., kuhusu suala hili.
Imam An-Nawawy ametaja katika kitabu cha [Al-Majmuu 484-485/ 3] dalili mbili kwa wanaozuia kusoma dua ya Qunuti, kisha akajibu:
Moja: Ni Hadithi iliyotajwa katika kitabu cha Al-Sunna Al-Kubra kwa Al-Baihaqiy kutoka kwa Ibn Masuod R.A., alisema kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akusoma dua ya Qunuti katika swala yake kabisa.
Hiyo inajibiwa kuwa Hadithi hiyo imepokelewa kutoka kwa Mohammad Ibn Jaber As-Suhaimi, na baadhi ya wanavyuoni wamedhoofisha Hadithi yake na wameiacha, na tukidhani kuwa ni sahihi, basi ni inathibitisha dua ya Qunuti na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Anas inaikataa, na uthibitisho unatanguliwa juu ya kukataa, kwa sababu uthibitisho unaongeza elimu.
Na Hadithi nyingine: ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ad-Daraqutniy, Al-Twabaraaniy katika kitabu cha Al-Kabiir na Al-Awsat na Al-Baihaqiy katika kitabu cha Al-Kubra kutoka kwa Umm Salamah, kutoka kwa Mtume, S.A.W.: kuwa amekataza kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi.
Hii inajibiwa kuwa Hadithi hiyo ni dhaifu; kwa sababu imepokelewa kutoka kwa Mohammad Ibn Yala kutoka kwa Anbash Ibn Abdul Rahman kutoka kwa Abdullah Ibn Nafi kutoka kwa baba yake kutoka kwa Umm Salamah. Al-Daaraqutni alisema katika Sunan yake [2/38 Ch. Dar Al-Maarifa, Beirut] kuwa: “Watu hawa watatu ni dhaifu, na hairuhusiwi kwa Nafi kusikia Hadithi kutoka kwa Umm Salamah”.
Ibn Hajar amesema kutoka kwa Anbasah Ibn Abdul Rahman kuwa: “Hadithi hii imeachwa na Abu Hatem”. [Rejea: Taqriib Al-Tahdhiib, 433, na Al-Jarhu wal Taadiil kwa Abu Hatim Al-Raziy 6/402, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy].
Tukidhani kuwa Hadithi hii ni sahihi, basi inajibiwa kama ilivyojibiwa Hadithi iliyopita.
Waliozuia dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi walisema – wakiwa waliosema kuwa dua ya Qunuti imefutwa au waliosema kuwa dua hii ilikuwa kwa ajili ya misiba tu – kuhusu Hadithi ya Anas R.A: "Mtume S.A.W. bado anasema dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi mpaka alifariki dunia": kwamba ina mitazamo mengi, na kuna uwezekano: kwamba alitaka kwa Qunuti: urefu wa kusimama, hali hii inaitwa Qunuti pia. [Rejea: Sharhu Al-Muntaha kwa Al-Bahwati Al-Hanbali 1/242].
Hii maana inajibiwa kwa maana ya Hadithi ambayo inaonesha kwamba maana ya Qunuti ni dua: (Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu yao – yaani juu ya wauaji wa wasomi Qur`ani - kisha akaacha dua hii, ama katika swala ya asubuhi, hakuacha dua ya Qunuti hadi akafariki dunia)).
Sheikh Taqi Al-Din Ibn Taimiyah na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayim waliona kuwa kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi kila siku ni kinyume na Sunna, lakini mwenye kufanya hivyo hakatazwi, na wakajadiliana kwa muda mrefu na matokeo ya majadiliano hayo ni:
Mtume alisoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja, kisha akaacha dua hii na siyo miongoni mwa Sunna yake kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi siku zote, lakini hii haimaanishi kuwa inachukiza kusoma dua ya Qunuti, lakini kufuata Sunna zake ni bora zaidi.
Inathibitisha hivyo ni kwamba kama Mtume S.A.W. akisoma dua maalumu ya Qunuti siku zote, Waislamu walikuwa watafikisha taarifa hiyo kutoka kwa Mtume S.A.W, kwani jambo hili ni miongoni mwa mambo yanayofikishwa kwa hamu. Na namna gani kuwa Mtume S.A.W. anasoma dua maalumu ya Qunuti siku zote katika swala ya asubuhi, na Waislamu hawakufikisha taarifa hiyo katika Hadithi sahihi wala katika Hadithi dhaifu? [Rejea maneno yao kwa ukamilifu katika: Al-Fataawa Al-Kubra kwa Ibn Taimiyah 2/245: 252, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah, na Zad Al-Miaad kwa Ibn Al-Qayim 1 / 271-285, Muasasat A-Resalah].
Mtazamo huu unajadiliwa kwa kusema kuwa: kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi siku zote siyo miongoni mwa Sunna ya Mtume S.A.W., na hii haimaanishi kuwa dua hii inachukiza wala ni uzushi, lakini suala hili lina utata sana; kwa sababu suala hili pengine ni halali na halina karaha. Au ni haramu na kinyume na Sunna, basi inapaswa kuwa suala hili linachukiza.
Kuhusu kufikisha taarifa hiyo, inajibiwa kwa kusema kuwa: hali ya kufikisha habari tayari imeshatokea, imepokelewa kutoka kwa Anas kwamba Mtume S.A.W. bado akasoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi mpaka akafariki dunia. Vile vile dua ya Qunuti imepokelewa kutoka kwa masahaba wengine R.A kama ilivyobainishwa hapo juu.
Ibn Taimiyah na Ibn Al-Qayim walisema kuwa Mtume, S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa sababu fulani, kisha akaiacha wakati wa hakuna sababu, hivyo dua ya Qunuti inaruhusiwa katika wakati wa msiba tu, na rai hii imechaguliwa na Wanavyuoni wa Hadithi.
Kisha walisema kuwa katika Hadithi ya Anas kuna Abu Jaafar Ar-Raziy naye ni dhaifu imedhoofishwa na zaidi ya mmoja miongoni mwa wenye kuhifadhi, na tukidhani kuwa kauli hii ni sahihi, basi hakuna dalili inayothibitisha dua hii maalumu ya Qunuti kabisa, na hakuna dalili inayothibitisha kuwa dua hii ni ya Qunuti. Kwani urefu wa kusimama katika swala unaitwa Qunuti, pia ibada iliyodumu, dua, tasbihi, na utulivu vitu hivi vyote vinaitwa Qunuti, na Anas R.A. mwenyewe hakusema kuwa: bado Mtume S.A.W. anasoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu akipanda sauti yake kwa kusema kuwa: “Ewe Mola! Niongoze niwe miongoni mwa wale uliowaongoza ... nk” na waliosali nyuma yake wanasema “Amin”. Na hakuna shaka kuwa kauli yake: Ewe Mola wetu mlezi himdi zote ni zako wewe... nk. ni Qunuti pia, na kurefusha kwa nguzo hii ni Qunuti pia, na kurefusha kwa kusoma Qur`ani katika swala ni Qunuti pia, na dua hii ni Qunuti .. Basi namna gani mmefahamu kuwa Anas R.A alikusudia kuwa Qunuti ni dua hii tu?!
Haiwezi kusema kuwa kuainisha dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi tu ni dalili ya kuwa ni dua maalumu, kwani vitu vilivyotajwa hapo juu kama ibada na dua ni miongoni mwa Qunuti, na Anas R.A hakuainisha dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi tu.
Haiwezi kusema kuwa: Ni kuomba dua mbaya juu ya makafiri, wala ni dua kwa ajili ya waumini waliodhulumiwa, kwa sababu Anas R.A aliambiwa kwamba Mtume S.A.W. alikuwa akisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja, kisha akaiacha, basi inafahamika kuwa dua hii ambayo Mtume aliiomba ni dua ya Qunuti inayojulikana. Vile vile Abu Bakr, Omar, Othman, Ali, Al-Bara Ibn Azib, Abu Hurairah, Abdullah Ibn Abbas, Abu Musa Al-Ash'ari, Anas Ibn Malik na wengine walisoma dua ya Qunuti.
Jibu lao lilikuwa, kama ilivyoelezwa awali, na kama ifuatavyo:
Kwanza, Anas R.A. alisema kwamba Mtume S.A.W alikuwa akisoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi na swala ya magharibi kama ilivyotajwa na Al-Bukhari, basi hakuainisha dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi tu, na hivyo vilivyotajwa na Al-Bara Ibn Azib. Kwa nini dua ya Qunuti imeainishwa katika swala ya asubuhi tu?
Kama mkisema kuwa: dua ya Qunuti katika swala ya magharibi imefutwa, waliopinga miongoni mwa watu wa Kufa watasema: vivyo hivyo dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, na kama mtaleta dalili ya kufutwa kwa dua ya Qunuti katika swala ya magharibi itakuwa dalili pia ya kufutwa kwake katika swala ya asubuhi, na kamwe hamtaweza kuthibitisha kufutwa kwa dua ya Qunuti katika swala ya magharibi na kuiainisha katika swala ya asubuhi tu.
Linajadiliwa hili: kwamba kuacha dua ya Qunuti katika swala ya magharibi haina madhara, kama alivyosema Al-Nawawi, na kwamba Wanavyuoni hawatofuatiani kuhusu kuiacha dua ya Qunuti katika swala ya magharibi, kama iliyopitishwa na Ibn Qutaibah. Na kwamba dalili inayothibitishia kufutwa kwa dua ya Qunuti katika swala ya magharibi si sahihi peke yake kwa kufutwa dua hii katika swala ya asubuhi, kwa sababu kuna Hadithi nyingine zilizopokelewa zinathibitisha kudumu kwa kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, basi hali hizi ni sawa.
Kisha wakasema: kama mkisema kuwa: dua ya Qunuti katika swala ya magharibi ilikuwa dua kwa ajili ya msiba tu, waliopinga miongoni mwa wanavyuoni wa Hadithi watasema kuwa: ndiyo hata swala ya asubuhi pia, ni nini tofauti baina swala hizi mbili? Wakasema: inaonesha kuwa dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi ilikuwa dua kwa ajili ya msiba tu na siyo dua ya kawaida, ni kwamba Anas mwenyewe aliambia hivyo, na mmetegemea Hadithi iliyopokelewa na Anas, na Anas R.A mwenyewe aliambia kwamba ilikuwa dua kwa ajili ya msiba tu kisha Mtume S.A.W. aliiacha. Katika Sahihi mbili imepokelewa kutoka kwa Anas R.A. alisema kuwa: "Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu ya watu miongoni mwa Waarabu kisha akaiacha".
Hili inajadiliwa kuwa: hatukusema hivyo kabisa, lakini tulisema hapo juu maneno ya Ibn Qutaibah kuwa: Wanavyuoni hawatofautiana kuhusu kuiacha dua ya Qunuti katika swala ya magharibi, kisha hiyo Qunuti iliyoachwa na Mtume, S.A.W. ni dua iliyokuwa baada ya kurukuu, lakini hiyo iliyo kabla ya kurukuu Mtume S.A.W. hakuiacha kabisa. Hii inathibitishwa kwa Hadithi nyingine katika sahihi mbili -na imetangulia hapo juu – inaonesha makusudi ya Hadithi mliyoitegemea, kwamba Asem alimwuliza Anas Ibn Malik, R.A. kuhusu dua ya Qunuti katika swala, ilikuwa kabla ya kurukuu au baada yake? Akasema: ilikuwa kabla ya kurukuu. Asem akasema: mtu fulani ameniambia kuwa umesema baada ya kurukuu. Akasema: alisema uongo, bali Mtume S.A.W. alikuwa akisoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja tu. Imefahamika kuwa dua ya Qunuti ilikuwa baada ya kurukuu kwa ajili ya misiba tu, lakini siyo kabla yake.
Jibu la pili: imepokelewa kutoka kwa Shababah kutoka kwa Qais Ibn Al-Rabii kutoka kwa Asem Ibn Suleiman alisema: tulimwambia Anas Ibn Malik: kwamba baadhi ya watu wanadai kuwa Mtume, S.A.W. alikuwa anaendelea kuisoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, akasema: walisema uongo, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja akiwaombea dua mbaya juu ya watu maalumu miongoni mwa waarabu, na Qais Ibn Al-Rabii amedhoofisha na Yahya Ibn Maain lakini wengine wamemthibitisha siyo pasipo na Abu Jaafar Ar-Raziy namna gani Abu Jaafar ni hoja katika kauli yake: Mtume S.A.W bado akasoma dua ya Qunuti mpaka akafariki dunia, na Qais si hoja katika Hadithi hiyo, naye amethibitishwa zaidi kuliko Abu Jaafar au kama yeye, na waliomdhoofisha Abu Jaafar ni zaidi ya wale waliomdhoofisha Qais, kwa maana udhaifu wa Qais umepokelewa kutoka kwa Yahya, na akataja sababu ya udhaifu wake, akasema Ahmed Ibn Said Ibn Mariyam nilimwuliza Yahya kuhusu Qais Ibn Al-Rabii, akasema: ni dhaifu kwani haandiki Hadithi yake, alikuwa akisema Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Obeida, ingawa Hadithi hii hii ilikuwa imepokelewa kutoka kwa Mansour, kosa kama hili halilazimishi kuiacha Hadithi ya mpokezi, kwa sababu upeo wa hali hii unasababisha kosa katika kutaja jina la Obeida badala ya Mansour, na pengine wengi wa wapokezi wanakosa kama hivyo?
Hii pia inajadiliwa kwa Hadithi ya Asem iliyotangulia katika sahihi mbili, ambapo Asma alisema: Nilimwuliza Anas Ibn Malik, R.A. kuhusu dua ya Qunuti katika swala, akasema: Ndiyo, nikamwuliza: ilikuwa kabla ya kurukuu au baada yake. Akasema: ilikuwa kabla ya kurukuu. Nikasema: Basi mtu fulani ameniambia kwamba umesema kuwa dua ya Qunuti ilikuwa baada ya kurukuu. Akasema: alisema uongo, bali Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa akisoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja tu, kwani aliwatuma masahaba walioitwa wasomaji walioihifadhi Qurani nao ni wanaume sabini kwa watu miongoni mwa makafiri, nao walikuwa na ahadi pamoja na Mtume wa Allah, makafiri hawa waliwauwa masahaba wale, kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. akaendelea kusoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja juu ya makafiri hawa.
Kwa ajili ya kupatanisha katika ya Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Asem na ile iliyopokelewa kutoka kwa Qais, na kuondoa kwa utata uliodhahiri kati yao, tunaweza kusema kwamba Qais angalau alikuwa alituhumiwa kuwa ni dhaifu - lakini Hadithi yake kuhusu dua ya Qunuti, iliyosomwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. kwa muda wa mwezi mmoja tu akiomba dua mbaya juu ya baadhi ya makafiri miongoni mwa Waarabu, na hiyo ilikuwa baada ya kurukuu. Lakini Hadithi ya Asem, ilikuwa kuhusu dua ya Qunuti ya kudumu, na ikawa kabla ya kurukuu.
Jibu la tatu: imeambiwa kwamba watu hawakuwa wakisoma dua ya Qunuti, na kuanza kwa dua ya Qunuti ilikuwa wakati Mtume, S.A.W. alipoomba dua mbaya juu ya makabila ya Ral na Dhakwaan. Imepokelewa katika Sahih ya Al-Bukhari kutoka kwa Hadithi ya Abdl Aziz ibn Suhaib kutoka kwa Anas alisema: Mtume, S.A.W. aliwatuma wanaume sabini kwa ajili ya haja, wanaume hawa wanaitwa wasomaji walioihifadhi Qur'ani, Hayyan wa Bani Sulaim Ral na Dhakwaan aliwashambulia kwenye kisima kinachoitwa kisima cha Maunah, Masahaba wakasema: tunaapa kwa Mwenyezi Mungu hatukutaka kukudhuru, lakini tutapita tu kwa ajili ya haja ya Mtume S.A.W. tu. Makafiri wakawauwa masahaba hawa, Mtume S.A.W. akaomba dua mbaya juu yao kwa muda wa mwezi mmoja katika swala ya Asubuhi, na hivyo ndivyo ni mwanzo wa Qunuti na hatukuwa tukisoma dua ya Qunuti kabla ya wakati huu.
Hii inaonesha kwamba siyo kutoka Sunna yake Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kusoma dua ya Qunuti wakati wote, na kauli ya Anas: hivyo ndivyo ni mwanzo wa Qunuti, pamoja na kauli yake: akaomba dua mbaya juu yao kwa muda wa mwezi mmoja kisha akaiacha – ni dalili ya kwamba anachotaka kukithibitisha ni Qunuti ya misiba nayo aliyowekea muda wake mwezi mmoja, na hii pia kama alivyoQunuti katika swala iliyoko katika wakati wa giza kwa muda wa mwezi mmoja kama ilivyopokelewa katika sahihi mbili kutoka kwa Yahya Ibn Abi Kathiir kutoka kwa Abu Salamah kwamba Abu Hurairah R.A aliwaambia kwamba Mtume S.A.W.: akasoma dua ya Qunuti baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja katika swala kama akisema: Mwenyezi Mungu anasikia anayemsifu, akasema katika dua yake ya Qunuti: "Ewe Mola wangu, mwokoe Al-Walid Ibn Al-Walid, ewe Mola wangu, mwokoe Salamah Ibn Hisham, ewe Mola wangu, mwokoe Aiaash Ibn Abi Rabiah, ewe Mola wangu, waokoe waliodhulumiwa miongoni mwa Waumini, ewe Mola wangu! Wadhikishe kwa (kabila la) Madhar na uajaalie miaka (ya shida) kama miaka ya Yusuf.". Abu Hurairah akasema: Kisha nikaona Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. akaiacha dua hii nikasema: Naona Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa kaiacha dua kwao. Akasema: aliambiwa kuwa unawaona wamekufa?
Dua yake katika swala ya asubuhi ilikuwa kwa ajili ya msiba, na kwa hivyo Anas aliainisha muda wa dua hii ilikuwa kwa mwezi mmoja tu.
Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ikrimah ilitangulia hapo juu kutoka Ibn Abbas: "Mtume S.A.W. alisoma dua ya Qunuti kwa muda wa mwezi mmoja katika swala zote Adhuhuri, Al-Asiri, Magharibi, Isha, na Asubuhi", Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Abu Dawuud na wengine, nayo ni Hadithi sahihi.
Al-Twabaraniy alitaja katika kitabu cha: [Al-Awsat], kwa Ad-Daraqutniy, na Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Al-Kubra” kutoka kwa Muhammad Ibn Anas: Tuliambiwa na Mutrif ibn Tarif kutoka kwa Abu Al-Jahm kutoka kwa Al-Baraa Ibn Azib kwamba Mtume S.A.W. alikuwa hakusali sala ya faradhi ila akasoma dua ya Qunuti.
Hii inajadiliwa kuwa mwanzo wa dua ya Qunuti ulikusudiwa Qunuti ya msiba na ilikuwa baada ya kurukuu, lakini Qunuti ya kudumu ilikuwa kabla ya kurukuu, kama ilivyobainishwa kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Asem iliyotangulia katika Sahihi mbili.
Lakini kufahamu kuwa dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi ina maana ya Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Abbas na Al-Bara Ibn Azib kwamba Mtume S.A.W alikuwa hakusali swala ya faradhi ila akasoma dua ya Qunuti, basi maana hii si kweli; kwa sababu hakuna upweke kwa swala ya asubuhi kama katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Anas.
Hatuwezi kusahau kusema kwamba Ibn Al-Qayim alisema kuhusu Hadithi hii iliyopokelewa kutoka kwa Al-Baraa kuwa: haina hoja.
Jibu la nne: Hadithi zote zilizopokelewa kutoka kwa Anas ni sahihi na zinaonyesha makusudi, baadhi ya Hadithi hizi zinathibitisha nyingine na pasipo na kupinga. Katika Sahihi mbili kutoka Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Asem Al-Ahwal alisema: Nilimwuliza Anas Ibn Malik kuhusu dua ya Qunuti katika swala? Akasema: Ilikuwa qunuuti. Nikasema: Ilikuwa kabla ya kurukuu au baada yake? Akasema: Kabla yake? Nikasema: Mtu fulani aliniambia kwamba wewe ulisema: Qunuti ilikuwa baada ya kurukuu, akasema: Mu huyu alisema uongo lakini nikisema kuwa Mtume wa Allah S.A.W. baada ya kurukuu kwa muda wa mwezi mmoja.
Basi Qunuti aliyoitaja kabla ya kurukuu ina maana ya urefu wa kusimama kabla ya kurukuu, kama kulikuwa na dua ya ziada au la, na ile Qunuti aliyoitaja baada ya kurukuu ni urefu wa kusimama katika dua. Mtume S.A.W. akafanya hivyo kwa muda wa mwezi mmoja akiomba dua mbaya juu ya watu na kuomba dua kwa ajili ya watu wengine, kisha akaendelea kurefusha nguzo hii kwa ajili ya kuomba dua na kusifu mpaka akafariki dunia. Kama ilivyopokelewa katika Sahihi mbili, kutoka kwa Anas R.A., alisema: sifupishi katika swala kama nilivyomwona Mtume, S.A.W anaswali pamoja nasi. Thabit alisema: Anas alikuwa akifanya kitu sikukuona mnafanya kama yeye, alikuwa kama akiinua kichwa chake kutoka kurukuu, akasema, hata inasemwa amesahau, na kati ya sijida mbili hata inasemwa amesahau.
Inajulikana kuwa hakuwa kimya aliposimama muda mrefu, lakini alikuwa akimsifu Mola wake na kumtukuza na kumombea dua, na dua hii ni tofauti na Qunuti iliyohusishwa kwa muda wa mwezi mmoja, hiyo ilikuwa ni kuomba dua mbaya juu ya makabila ya Ral, Dhakwaan, Asiyah, na Bani Lihayan, vile vile alikuwa akiomba dua kwa ajili ya wale walioonewa katika Makkah. Hivyo neno la qunuuti haina maana ya dua.
Hii inajadiliwa kwamba Qunuti ina maana kadhaa katika lugha. Na katika istilahi ya wanavyuoni maana yake ni kuomba dua mahususi. Na kama hivyo ndivyo, nini iliyobadilisha maana ya qunuuti hapa ili iwe kurefusha kusimama pasipo na sababu, na iliyofahamika ni dua ya Qunuti yenyewe, na hali ya kufahamu ni dalili nguvu, basi ni lazima dalili au sababu ipatikane ili kubadilisha maana ya Qunuti ili iwe kurefusha kusimama.
Vile vile tunasema: Nini inazuia kupata hali hizi mbili pamoja, nazo ni kurefusha kwa kusimama na kuomba dua, hakuna shaka kuwa Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Anas zinaonyesha kuwa maana ya Qunuti ni kuomba dua tu. Kisha tunauliza: Je faida ya kutaja Qunuti kwa maana ya kurefusha kusimama kwa aliyeulizia Qunuti kwa maana ya dua, imepokelewa katika Sahihi mbili kutoka kwa Asem alisema: nilimwuliza Anas Ibn Malik, R.A. kuhusu Qunuti katika swala mpaka mwisho wa Hadithi, na qunuuti katika swali na katika jibu la Anas kwa maana ya dua siyo kwa maana ya kurefusha kusimama katika swala.
Walisema pia kwamba Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Masahaba ni aina mbili:
Moja yao ni: Qunuti wakati wa msiba kama Qunuti ya Abu Bakr Al-Swddiq R.A. katika mapambano dhidi ya Musaylimah, na katika mapambano dhidi ya watu wa kitabu, na pia Qunuti ya Omar na Ali wakati wa mapambano dhidi Muawiyah na watu wa Sham.
Ya pili: ni maana ya ujumla, nayo ina maana ya kurefusha nguzo ya kusimama kwa ajili ya dua na kumsifu Allah.
Inajadiliwa hii kwamba hatutambui Hadithi hizi zilizopokelewa kutoka kwa Masahaba kuhusu Qunuti katika swala ya asubuhi kufuatana na maana hizi mbili tu.
Ni lazima tahadhari kwamba Masheikh wawili Ibn Taymiyah na Ibn Al-Qayim walitaja katika muktadha wa maneno yao kuwa ingawa haikuwa kutoka Sunna yake Mtume S.A.W. kuisoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi, hii haimaanishi kuwa inachukiza hali nyingine au ni uzushi, na kwamba anayeamini kuwa inaruhusiwa kuendelea kusoma dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi akifanya bidii katika dalili na maana zake anaweza kufanya hivyo, kama katika mambo yote yaliyoruhusiwa kufanyiwa jitihada kwake. Kwa hivyo ni lazima kwa maamuma afuate imamu katika jambo linaloruhusiwa kujitahidiwa, kama Imamu akiQunuti maamuma anaQunuti pamoja naye, na kama Imamu akiacha Qunuti, maamuma anamfuata.
Wanavyuoni walioruhu Qunuti katika swala ya asubuhi walitofautiana katika nafasi yake; Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik kufuatana na rai maarufu kwao wanaona kwamba Qunuti inakuwa kabla ya rakaa ya pili bila ya takbira kabla yake, kwani hali hii ina upole kwa maamuma aliyetanguliwa na kutojitenga kati ya nguzo mbili za swala zake, na rai ambayo ni maarufu kwao pia ni kuisoma dua ya Qunuti kwa siri. [Rejea: Sharhu Mukhtasar Khalil kwa Al-Kharashi 1/282, Dar Al-Fikr, Kifayat Al-Talib Ar-Rabani kwa Ali Ibn Khalaf, 1, 273, na Mawahib Al-Jaliil kwa Al-Hattab / Dar Al-Fikr, 1/539, Dar Al-Fikr].
Wanavyuoni wa Madhehebu ya Imam Al-Shafi -kama katika kitabu cha [Al-Majmuu kwa An-Nawawiy 3 / 475.481] - kwamba Qunuti ni baada ya kurukuu rakaa ya pili, kama imam akiqunuti kabla ya kurukuu, basi rai ambayo ni maarufu kwao ni hairuhusiwi, na iliyo sahihi zaidi ni kuisoma dua ya Qunuti kwa sauti.
Tulisema: Hadithi sahihi zimepokelewa kufuatana na hali mbili kama ilivyotangulia, hakuna utata, kwani tofauti hii ni halali pia kama ilivyotangulia kutoka kwa maneno ya Ibn Hajar.
Wanavyuoni wametofautiana kuhusu maneno ya dua ya Qunuti pia, Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik wamesema kuwa dua ya Qunuti ni: “Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakuamini na tunakutegemea, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anayekukufuru. Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe tu ndie tunaekuabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia. Kama akiomba dua nyingine kama vile: “Ewe Mwenyezi Mungu niongoze ... mpaka mwisho wake akatekeleza moja iliyoruhusiwa na hakutekeleza nyingine. [Rejea: Minah Al-Jalil kwa Sheikh Aliishi 1/260, Ch. Dar Al-Fikr, na Sharhu Khalil kwa Al-Kharashi 1/283, 284].
Kwa mujibu wa Sunna kwa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Al-Shafi -kama katika kitabu cha [Al-Majmuu kwa An-Nawawiy 3 / 475.476] – dua ya Qunuti ni kusema kuwa: “Ewe Mwenyezi Mungu niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afaya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya wapenzi na nibariki katika ulichonipa na nikinge na shari ya ulilolihukumu kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi.
Hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi. Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka”, na hakuna vibaya kama ukiongeza kuwa: “wala hatukuki uliemfanya adui” kabla ya kusema: “Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka”, na baada ya hivyo: “sifa njema ni zako kwa ajili ya ulilolihukumu, naomba msamaha wako, na narejea kwako (kwa kutubia). Kama akiwa imam hakuomba dua kwa ajili yake mwenyewe tu, bali anaomba dua kwa ajili ya Waislamu wote kama vile; Ewe Mwenyezi Mungu tuongoze pamoja na uliowaongoza, na kadhalika.
Imamu An-Nawawiy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Majmuu 3 / 475.476] kuwa: “Rai iliyochaguliwa ni kwamba siyo sharti kuomba dua kwa maneno haya. Kama mtu akisoma dua ya Qunuti iliyopokelewa kutoka kwa bwana wetu Omar R.A. basi ni sawa, na inapendekezwa kuchanganya kati ya dua ya Qunuti iliyopokelewa kutoka kwa bwana wetu Omar R.A. na dua iliyotangulia hapo juu. Kama akichanganya kati yao, basi iliyo sahihi zaidi ni kuchelewesha dua ya Omar, na kufuatana na mtazamo mwengine inapendekeza kuitanguliwa dua ya Omar. Na kama akifupisha dua, basi inatosha kuomba dua ya kwanza tu, lakini inapendekeza kuchanganya kati ya dua hizi mbili kama mtu akiswali pekee yake au akiswali Imamu pamoja na watu wanaokubali kurefusha swala, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi”.
Inaonekana kutokana na yaliyotangulia kuwa tofauti hii ni miongoni mwa tofauti inayoruhusiwa, na asili ya jambo katika tofauti hii linategemea upanuzi, kama akisoma dua yoyote miongoni mwa dua zilizopokelewa inamtosha kwa mujibu wa alivyosema Imam Al-Mawardi katika kitabu cha [Al-Hawi 2/153, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah].
Kwa mujibu wa yaliyotangulia hapo juu, tunasema kwamba wanavyuoni wametofautiana katika hukumu ya dua ya Qunuti katika Swala ya asubuhi, baadhi yao walisema: Ni Sunna, na baadhi yao walisema kwamba imefutwa, na baadhi yao walisema: Ni wakati wa msiba tu, na rai iliyochaguliwa ni Sunna katika swala ya asubuhi, na si uzushi unaokatazwa, na kwamba Qunuti sio katika wakati wa msiba tu, baada yaliyoelezwa kuwa dua ya Qunuti ilipokelewa kutoka kwa Makhalifa katika wakati ambapo hakuna msiba, na dua ya Qunuti kama alivyosema Ibn Hazm katika kitabu cha: [Al-Muhala 2/57 Dar Al-Fikr] kuwa: “Dua ya Qunuti ni kwa ajili ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, basi hali ya kusoma dua ya Qunuti ni nzuri na hali ya kuiacha inaruhusiwa”.
Hata hivyo, hukumu ya dua ya Qunuti katika swala ya asubuhi ni miongoni mwa masuala yenye utata ambapo hakuna kukanusha katika kuisoma au kuiacha, msingi unasema: “Halikanushwi Suala ambalo wanazuoni wametofautiana juu yake bali linalokanushwa ni lile ambalo wanazuoni wote wamekubaliana juu yake”. [Rejea: Al-Ashbah wal Nadhair kwa Al-Soyuti uk. 158 Ch. Dar Al-Kutub Al- Elmiyah]. Hivyo inapaswa Waislamu wasifanye masuala yenye tata sababu ya kueneza fitna na kutawanika kati yao, vile vile ni lazima kutoitwa neno la uzushi kwa jambo ambalo ni Sunna iliyofuatiwa na iliyopokelewa na umma kwa kukubalika; lakini uzushi uliokatazwa kama alivyosema Imam Al-Ghazaliy katika kitabu cha: [Al-Ihyaa 2/3, Ch. Dar Al-Marifa- Beirut] kuwa: “Uzushi ni ule unaopinga Sunna iliyothibitishwa, na unaoondoa jambo kutoka Sheria pamoja na kubaki sababu yake”, Allah amefanya dini ni nyepesi, na hataitilia mikazo dini hii Mtu yeyote ila itamshinda, Mwenyezi Mungu anasema: {Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito} [AL BAQARAH 185]. Vile vile Mwenyezi Mungu akasema: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} [AL HIJJ 78]. Na katika kitabu cha: [Al-Sunan Al-Kubra kwa Al-Baihaqiy] kutoka kwa Jabir Ibn Abdallah R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema kuwa: “Hakika dini hii ni nguvu, basi uitekeleze kwa upole, na usichukishe ibada ya Mwenyezi Mungu kwa mwenyewe, basi msafiri anayeendelea katika safari yake muda mrefu pasipo na kupata raha hataweza kufika, lakini atamtaabisha ngamia wake tu)).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


Share this:

Related Fatwas