Hukumu ya Kuhamisha Salio Kupitia ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuhamisha Salio Kupitia Huduma ya (Tafadhali Nikopeshe).

Question

 Ni ipi hukumu ya mtu kuhamisha salio kutoka katika kampuni ya mawasiliano ya simu mpaka kuweka pesa ndani ya simu yake kwa njia ya kadi; kwa maana ya kuongeza pesa zaidi ya pesa alizokopa, na huduma hii inajulikana kwa jina la (Tafadhali nikupeshe)?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Salio au vocha ni: Haki ya kifedha inayotolewa na kampuni ya mawasiliano kwa mteja mnunuzi; kwa ajili ya kuweza kutumia salio wakati autakao bila ya kuvuka mipaka ya pesa aliyopewa mteja kwa muda maalumu (unaojulikana kwa utaratibu wa kadi), mteja mnunuzi akitumiza wakati wake maalumu wa kadi kutokana na pesa zake basi huduma zitasimamishwa mpaka kutia salio jingine tena.
Na salio ni jambola ushirikiano maalumu baina ya kampuni na mteja mnunuzi kwa mujibu wa mkataba kuainisha kadiri ya pesa au salio la mnunuzi anaostahiki kutumia kwa huduma za kupiga simu zilizosawa na pesa alizolipa, kwani hii ni haki inayohusiana na pesa, na maana ya haki katika istilahi ni :kitu kimoja kilichokubaliwa na sheria kwa manufaa maalumu. Rejelea: [Al-Haq wa Mada Sultan Al-Dawlah fi Taqyideh kwa Daktari, Muhamad Fathi Ad-Deriny Uk. 260, Ch., Dar Al-Bashir].
Na uhusiano baina ya haki na manufaa ni kwamba manufaa ni masilahi maalumu, ama maana ya haki hapa ni njia ya kimaana kwa kupata masilahi , na vyombo vya kugusika ni: njia maalumu zilizojulikana zamani na sasa kwa kuzikopa, kuziazima, kuziweka rehani na njia nyingine miongoni mwa miamala.
Na kwa upande mwingine, kampuni za mawasiliano zimempa mteja mnunuzi nafasi ya kuomba kuongeza salio linapo kwisha kutoka na huduma ya (tafadhali nikopeshe) na kutokana na ombi hili kampuni inatoa salio kwa kuongeza kadiri ya thamani asili ya kadi, na shirika litakata pesa hizi baada tu, ya kuingiza salio.
Na kuingiza salio kwa wango kile kile cha fedha au kwa kuongeza kidogo na jambo hili ni kama kuuza manufaa.
Na mwanazuoni wa Madhehebu ya Shafiy Qalyuby anasema katika maelezo yake ya kitabu chake cha: [Al-Mohaly kwa Menhaj 2/152, Ch. Essa Al-Halaby) kuhusu dhana ya uuzaji wa kisheria ya kuwa ni: "Mkataba wa kuchukua pesa unafaidi umiliki kitu, au manufaa ya daima".
Na Imamu Ibn Mefleh Al-Hanbaliy alisema katika kitabu cha: [Sharh Al-Muqanee 4/4, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah –Bairut] katika dhana ya uuzaji wa kisheria: "Kumiliki mahala pa kimali au manufaa halali ya kudumu kwa mali halali sio riba au mkopo".
Na hakuna tofauti baina ya mfumo wa manufaa ya kimali na -mfumo wa kitu badala ya kitu kingine, au deni badala ya deni– katika kujuzu kwa uuzaji wake; katika jambo hilo Imamu Ibn Qatadah Al-Hanbaliy anasema katika kitabu cha [Al-Mughny 5\251, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: "Na manufaa ni kama mali; kwani yaweza kuimilikiwa katika hali ya maisha au baada ya mauti, na inaweza kuwa badala yake ni mali taslimu na deni na inahusika kwa jina kama ilivyo kwa baadhi ya mauzo mengine".
Na mwanafiqhi Ibn Hajar Al-Haytamiy wa kishafiy katika fatwa zake [3\93, Ch. Al-Maktabah Al-Islamiyah]: "Manufaa ni kama mali au deni; na thamani yake ni ya kitu, kimepatikana kweli au la".
Na asili ya Uhalali wa kuuziana ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba} [AL BAQARAH: 275], na Al-Imam Al-Qurtubiy alisema katika aya hii katika [Tafsiri yake, 3\356, Ch. Dar As-Shaab]: "Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba}. Jambo hili ni kutokana na Qur`ani kiujumla". na hukumu hii kwa uhalali wa uuzaji inaweza kuwa katika kila namna za mauzo,ila kinachoharamishwa na sharia na kuitoa katika hukumu ya kiasili, ni kama katika mauzo yanayoambatana na riba au mengine miongoni mwa mambo yaliyo haramu,na Al-imam Al-shawkani anasema katika [Tafsiri yake Fath Al-Qader 1/339, Ch. Dar Al-Qalim At-Twayyeb- Bairut]: Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba} yaani: Mwenyezi Mungu amehalalishia mauzo na ameharamisha namna moja miongoni mwa namna zake, ni mauzo yanayoambatana na riba". Na dalili ya uhalali katika mauzo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe} [AN NISAA, 29]. Imamu Shafiy R.A. alisema: katika kitabu chake cha: [Al-Um 3/3, Ch. Dar Al-Maarifah]: "Asili ya mauzo yote ni halali kama yatafanyika kwa ridha ya watu wanaouziana, isipokuwa yale aliyoyakataza Mtume S.A.W., nay ale yaliyo katika maana ile ile ya makatazo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na yote yaliyotofautiana na hayo tumeyahalalisha kwa jinsi tulivyoelezea uhalali wa kuuziana katika Qurani Tukufu".
Al-Imam At-Termiziy alisimulia katika kitabu chake: "Kutoka kwa Ismail Inb Ubaid Ibn Rifaah kutoka kwa baba yake na babu yake kwamba: Alitoka pamoja na Mtume S.A.W., kuelekea msikiti akawaona watu wanaofanya biashara,basi Mtume S.A.W., akasema: Enye wafanya biashara! Basi wakamuitikia Mtume S.A.W., na wakanyanyua vichwa vyao juu na kumuangalia Mtume S.A.W., akasema: Hakika wafanya biashara watafufuliwa siku ya kiama makafiri isipokuwa wanaomcha Mungu na wakweli kwa wengine".
Ama ikiwa uingizaji wa salio una nyongeza ya thamani yake kifedha ambayo imeingizwa basi hiyo ni katika kuuziana manufaa na ni sahihi, kwani ziada hii ni sahihi na ni malipo ya huduma ya shirika juu ya kazi ya kurusha salio, na inaweza kuzingatiwa jambo hili ni kama ajira kwa maana badala ya utumishi wa mtu anayerusha salio kwa mwengine, na inawezekana kuzingatia jambo hili ni miongoni mwa uuzaji wa faida maalumu kwa kuridhiana baina ya wanaouza, na jambo hili lina mfano katika fiqhi ya kiislamu,wanafiqhi walisema kuhusu jambo hili ni badala ya kazi ya watu na ni kama mshahara wao.
Na kadhalika ilikuja katika kitabu cha: [Al-Sharh Al-Saghir kwa Muhtasari Khalil kwa shekh Al-Darder -miongoni mwa vitabu vya Malikiyah, 3\197, 198 pamoja na maelezo ya Al-Sawy, Ch. Dar Al-Maaref]: Inaelezia juu ya ujira kwamba ujira ni mbele ya matumizi na jambo hili ni (kinyume cha mkopo; kwani ujira wa mkopo unakuwa juu ya anayechukuwa mkopo); kwani anayekopesha mkopo anafanya hisani kwa hivyo si lazima kulipa pesa juu ya hisani yake,na anayekupeshwa lazima kulipwa gharama ya mkopo".
Na miongoni mwa dalili za suala hili ni msingi usemao: "Malipo ni kwa kinacholipiwa", na maana yake ni kinacholipwa kutokana na huduma iliyotolewa. Na miongoni mwa yanayotajwa kuhusu utekelezaji wa msingi huu kwamba: malipo yanayotolewa wakati wa kuandikishiana mkataba wa kuuziana ni waraka wa kuhama kwa kinachomilikiwa na kumfikia mnunuzi kwa lengo la kunufaika. {Sharh Al-Qawaed Al-Fiqhiyah kwa shekhi Ahmad Al-Zarqa, Ku. 437-438, Ch Dar Al-Qalam, na Al-Qawaed Al-Fiqhiyah na matumizi yake katika madhehebu manne kwa Daktari Mohammad Al-Zuhely,1/543, Ch. Dar Al-Fikr- Demashq, na Durar Al-Hukkam katika Sharh Mujalat Al-Ahkam kwa Aly Hedar,1/90, 2/378, Ch. Dar Al-Jel].
Na ilikuja pia katika kitabu cha: [Al-Muntaha kwa Al-Bahuty Al-Hanbaliy 2/294, Ch. Aalam Al-Kutub] katika jambo hili kwa maana hii hii ya kulipa ujira mbele ya kazi.
Na manufaa hapa katika –kutuma salio– yanamrudia anayetumia salio yeye peke yake, na kwa hivyo basi lazima apewe matumizi yanayotokana na haya.
Na kurusha salio kutoka shirikani kwa njia ya kukata kiasi cha fedha mpakaa mteja atakapoamua kuingiza salio lake kwa kutumia njia ya kiingizia salio kwa maana ya nyongeza ya pesa zilizolipwa tofauti ya kile kiwango alichotumiwa, na hii pia ni katika mauziano ya manufaa, na nyongeza hapa ni malipo ya thamani kwa kuwepo muda maalumu.
Na kutokana na maelezo ya hapo juu mauziano baina ya mteja mnunuzi na shirika kwa mfumo wa malipo ya kidogo kidogo kwa wakati maalumu kwa ziada pesa kidogo yanakuwa sahihi kwa upande wa kisheria ,na dalili ya hayo kauli ya mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara} [AL BAQARAH 275]. Na Imam Al-Bukhariy ameshasimulia katika Sahihi yake: "Kutoka kwa mwana Aisha R.A., kwamba Mtume S.A.W., alinunulia chakula kutoka myahudi mmoja kwa wakati maalumu na alirehani ngao ya chuma".
Na Ibn Battal alisema katika maelezo ya [Sahihi Al-Bukhariy 6/208, Ch. Maktabat Al-Rushdi-Al-Reyadh]: "Wanazuoni wanaafikiana juu ya kuyajuzisha mauziano kwa mfumo wa malipo ya kidogo kidogo".
Na mwuzaji akizidishia katika thamani (pesa) ya bidhaa yake kwa ajili ya muda maalumu (kuchelewa), ni kujuzu pia kwa upande wa kisheria;kwani hii ni miongoni mwa faida,nah ii ni namna moja ya namna za mauzaji sahihi ya kisheria zinazoshurutia ziada katika bei kwa ajili ya kuchelewa malipo; kwani kuchelewa malipo kwa namna hii ni miongoni mwa faida ya manufaa baina yao,yaweza kuzidisha pesa katika bei;kwani namna hii ya biashara ni halali,na aghalabu ya watu wanahitaji mfumo wa biashara kama hii wakiwa wauzaji au wanunuzi. Na mfumo huu ni halali na sio riba;kwani ni biashara kwa mujibu wa kuitikia na kuikubali baina ya wawili wauzaji na wanunuzi na kuna bidhaa na bei yake,na hizi ni nguzo za biashara,na hii ni mwafaka wa kufuata kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara} [AL BAQARAH 275].
Na kama katika msingi wa kisheria yasemwa: bidhaa ikikuwa baina yao basi hakuna riba.
Na kauli yasema kwa kuijuzu ziada katika bei kwa ajili ya kuchelewainawafikiana na maoni ya jamhuri ya wanazuoni wa fiqhi wa Kihanafiy, Kimalikiy, Shafiyah na Wanazuoni wa Madhehebu ya Hanbali: Tazama: [Badaea Al-Sanaea kwa Al-Imam Al-Kasaeiy kutoka katika vitabu vya Wanazuoni wa madhehebu ya Hanbaliy 5/224, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, na As-Sharh Al-Kabir ala Mukhtasar Khalil kwa Shekhi Al-Dardir pamoja na maelezo ya Al-Desuoky katika Madhehebu ya Imamu Malik 3\58, Ch. Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiah, na Al-Muhazab kwa Imamu Al-Sheraziy katika Fiqhi Wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy 1\289, Ch. Dar Al-Fikr- Bairut, na Al-Mubdiu Sharhu Al-Muqniu cha mwanazuoni Ibn Mufleh kutoka katika vitabu vya Madhehebu Imamu Hanbali 4/103, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na maelezo haya yote yalinukuliwa na Tawuos Hakam, Hammad na Awzaiy wakiwa ni kati ya Wanazuoni wa Fiqhi waliotangulia, tazama: (Maalem Al-Sunan kwa Abi Sulaiman Al-Haby 3/123, Ch. Uchapishaji wa Kitaaluma katika mji wa Halab).
Imamu Shawkani katika kitabu cha: [Nail Al-Autwar Sharh Montaqaa Al-Akhbar 5/181, Ch. Dar Al-Hadeeth] anaizungumzia nyongeza kwa muda maalumu imeharamishwa: "Wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi, Imamu Hanbali, Imamu Zaid bin Ali, Muayid Billaahi na Jamhuri ya Wanazuoni wanasema: ziada inajuzu kwa muda maalumu kwa mujibu wa dalili za kiujumla na zilizo dhahiri…na tumezikusanya risala katika masuala haya na tukaiita Shifaaul Ilali Fii Ziaadati Thamani Limujaradil Ajal, na tukayafikia mafanikio ambayo hatujawahi kutanguliwa hapo kabla".
Na hivi ndivyo lilivyoamua Baraza la Fiqhi ya Kiislamu ambalo ni sehemu ya Jumuiya ya Kiislamu ya Jidah lililokuwa na kikao chake cha sita kilichofanyika kati ya 17 na 23 Shaaban 1410, sawa na 14 hadi 20 machi 1990; ambapo lilitoka na azimio namba (53/2/6) lililosema: "Ni inajuzu ziada ya thamani iliyocheleweshwa kwa thamani ya sasa, na pia inajuzu kutaja bei ya bidhaa ya inayouzwa kwa fedha taslimu na thamani yake kwa mfumo wa kulipa kidogo kidogo kwa muda unaojulikana, na kuuziana hakusihi isipokuwa watakapoafikiana wanaouziana na kuamua kufanya hivyo kwa fedha taslimu au kwa kulipa kidogo kidogo. Na kama mauziano yatatokea pamoja na kuwepo hali ya kusita sita kati ya kulipa fedha taslimu au kulipa kidogo kidogo, basi hayatakuwa yamepatikana makubaliano yaliyoamuliwa ya thamani moja maalumu, na kwa hiyo haitajuzu kisheria kuuziana huko".
Na haisemwi kwamba mfumo wa malipo ya awamu yaani kidogo kidogo sio maalumu au dhahiri; kwani mfumo wa malipo kwa njia ya kidogo kidogo huwa yanawekwa na mashirika ya simu, na anayerushiwa salio asiongeze salio lake katika wakati maalumu, na kwa hivyo basi shirika litachukuwa laini yake, na kadiri ya salio yake itakuwa kama deni juu yake mpaka atakapolilipa deni lake hilo kwa shirika husika, na shirika hilo linaweza kumchukulia hatua za kisheria ili haki zake zirejeshwe.
Ama uitwaji wa huduma hii kwa jina la (tafadhali nikopeshe) hauna athari yoyote katika makubaliano haya, lakini msingi wa mkataba una madhumuni ya makubaliano na sio kwa tamko lake hilo.
Al-Suyuty alisema katika kitabu cha: [Al-Ashbah wa Al-Nadhaer, Uk. 166, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah): "Msingi namba tano: Je, msingi wa makubaliano ni kwa mfumo wake au kwa maana yake? kuna maoni mawili tofauti. Maoni ya kwanza yanasema kwamba inajuzu kwa mfumo, na maoni ya pili yanasema kwamba inajuzu kwa maana yake".
Kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia tunaweza kusema kwamba kurusha vocha au salio kwa kupunguza pesa maalumu kwa huduma hii ni sahihi kwa upande wa kisheria, na hakuna tatizo lolote katika uitwaji huduma hii kwa jina la (tafadhali nikopeshe) kwani hii ni biashara na sio mkopo, na msingi wa hali hii ni maana ya mapatano na sio tamko lake.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas