Hukumu ya Babu Kumfanyia Akika Mju...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Babu Kumfanyia Akika Mjukuu Wake.

Question

Ni ipi hukumu ya babu kumfanyia Akika mjukuu wake pamoja kuwepo kwa baba wa mtoto huyo? Na je hukumu yake inatofautiana kwa kutofautiana mazingira ya baba ya kuwa na hali nzuri au hali ngumu? 

Answer

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Huwenda babu akamfanyia akika mjukuu wake pamoja kuwepo kwa baba wa mtoto huyo. Na babu anafanya akika pengine inakuwa hivyo kwa sababu ya kutoweza kifedha kwa baba wa mtoto huyo kufanyia akika ya mtoto wake, na pengine inakuwa hivyo kwa sababu babu huyo kupenda kumfanyia hivyo mjukuu wake.
Suala hili; wanazuoni wa Fiqhi walilizungumzia katika mlango wa akika na wengineo kama vile mlango wa Zaka walipouongelea utoaji Zaka kwa niaba ya mwenye Zaka bila ya idhini yake mwenyewe.
Na hukumu katika suala hili ni kwamba baba ndiye anaesemeshwa kiasili katika Akika. Ama kwa upande wa baba, kama atakuwa na hali ngumu kisha babu akaifanya Akika hiyo basi hakuna ubaya wowote, bali inapendeza kufanya hivyo.
Na kama babu ataifanya Akika hiyo kwa kuanza mwenyewe bila ya idhini ya baba, na baba huyo akaikubali basi hakuna ubaya wowote na itakuwa imejuzu, na kama sio hivyo basi atamlipa gharama zote za Akika hiyo akitaka. Na dalili ya kwamba anayetakiwa kufanya Akika ni baba ni kwamba huyo mtoto ni mwanaye aliyezaliwa, naye ndiye anayewajibika kwa matumizi yake kwa hiyo kila kinachohusika na matumizi ya mtoto ni pamoja na hiyo Akika na kwamba mtoto kisheria habebeshwi majukumu na kwa hivyo Akika haiwi wajibu kwa mali yake mtoto huyo.
Ama kujuzu kwa babu kumfanyia akika mjukuu wake, dalili yake imetajwa kutoka kwa Ibn Abbas R.A, "Kwamba Mtume S.A.W, aliwafanyia akika wajukuu wake; Hassan na Husein (kwa kuwachinjia) kondoo mmoja mmoja", Imetolewa na Abu Dawud na An-Nassaiy.
Na ikiwa ni kwa hali ngumu ya baba yake basi hilo liko wazi, na kama itakuwa kwa kutokuwepo ugumu wowote kwa baba yake, basi inaweza kuwa ni kwa idhini yake na hiyo itajuzu kama ilivyo kwa wenzake katika kutoa zaka kwa idhini ya mwenye mali, na kama itakuwa bila ya idhini yake basi itajuzu kwa kuwa yeye ni mzazi kwa ujumla; na pia kwa kuwa kuna kurithiana baina yao, na hata kama mzazi angelikuwa na hali ngumu basi matumizi yangewajibika kutoka kwa babu mwenye hali nzuri na kwa sababu babu ana haki ya kuitumia mali ya mtoto wake kwa ujumla, kwa hadithi ya Amru Bin Shoaib kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake Kwamba mtu mmoja alimwendea Mtume S.A.W, akamwambia: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika mimi nina mali na watoto, na mzazi wangu anahitaji mali yangu? Mtume S.A.W akamwambia: hakika wewe na mali yako ni mali ya baba yako, hakika watoto wenu ni katika chumo lenu lililo bora zaidi, basi kuleni katika chumo la watoto wenu". Imetolewa na Abu Dawud.
Abu Jaafar At Twahawiy anasema: "Wanazuoni wanaona kuwa chumo la mali alilolichuma mtott ni mali ya baba yake na wakatoa hoja ya kwamba kwa kutumia Hadithi hizi. Na wengine wakatofautiana nao katika hilo, wanasema: chochote atakachokichuma mtoto ni chake yeye tu na wala sio cha baba yake. Na wanasema: tamko la Mtume S.A.W, hii sio dalili ya kummilikisha mzazi mali ya mwanae bali hakika mambo yalivyo ni kuwa mtoto hapaswi kwenda kinyume na baba yake katika kitu chochote kwa hilo, na kuifanya amri yake ni ya kutekelezwa kama vile amri yake katika mali yake. Je hauoni anasema; " hakika wewe na mali yako ni mali ya baba yako". Basi mtoto hakuwa akimilikiwa na baba yake kwa nyongeza ya Mtume S.A.W, kwake na kwa hivyo hawezi kuwa mmiliki wa mali yake kwa nyongeza ya Mtume S.A.W, katika hilo.
Hakika Fahd ametuzungumzia na anasema: Mohammad Bin Saidi alituzungumzia na anasema: Abu Mu'awiyah alituzungumzia kutoka kwa Al A'mash, kutoka kwa Abi Swaleh kutoka kwa Abi Hurairah anasema: Mtume S.A.W. anasema: "Hakika mambo yalivyo, haijawahi kuninufaisha mimi mali kamwe haijaninufaisha mimi mali ya Abu Bakr", Basi Abu Bakr R.A. anasema: Hakika mimi na mali yangu ni yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu! Na Abubakar hakupokea hivyo kuwa mali yake ni mali ya Mtume S.A.W, kinyume na yeye mwenyewe lakini alichokikusudia ni kuwa amri yake inatekelezwa ndani ya mali hiyo na kwake. Na hivyo hivyo katika kauli yake: wewe na mali yako ni mali ya baba yako ni katika maana hiyo hiyo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi. Na inapokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kwamba ameharamisha mali za waislamu na damu zao na hakutofautisha baina mali ya baba au nyinginezo." [Sharhu Maani Al Athaar 158/4, Ch. Dar Al Kutub].
Kama baba atakuwa na mamlaka ya kuitumia mali ya mwana wake kwa kuchukua au kwa kupunguza basi yeye ana haki ya kuitumia kwa kutoa au kuongeza na kuweka akiba.
Na kama tulivyotaja, makundi miongoni mwa wanazuoni wanasema kwa kiujumla:
Shamsu Ed Diin Ar Ramliy anasema: "Na mfanyaji wa Akika ni yule mwenye jukumu la matumizi ya mtoto kwa kukadiria uwezo wake wa mali yake kinyume na mwana wake kwa sharti la kuwa mfanyaji wa Akika ana hali nzuri ya kifedha: kwa maana ya wepesi wa kimaumbile kuhusu kinachodhihirika kabla ya kupita muda wa yeye kuhitajika zaidi kuifanya Akika hiyo ya mwana wake, na muda huo haupiti kwa kuchelewa, na iwapo mtoto atabaleghe kabla hajafanyiwa Akika na baba yake, basi umri wa kufanyiwa Akika na mtu mwingine utakuwa umemalizika, na mtoto huyo atakuwa na hiari ya kujifanyia Akika yeye mwenyewe. Na Mtume S.A.W, alimfanyia Akika Hassani na nduguye Husein kwa kuwa wote wawili walikuwa chini yake kimatumizi kutokana na hali ngumu ya wazazi wao, au ilikuwa kwa idhini ya wazazi wao. Na mtoto wa zinaa anatunzwa na kulelewa na mama yake na imesuniwa kwa mama yake kumfanyia Akika, na wala haihitajiki katika kufanya hivyo kudhihirisha kwake kunakopelekea kuonekana kwa aibu ya uzinzi." [Nihayat Al Muhtaaj 138/8, Ch. Mustafa Al Halabiy]
Abu Abdullah Al Mwaq wa Madhehebu ya Maliki anasema: "Na imesuniwa kuchinja mnyama mmoja kunatosheleza kichinjo katika siku ya saba ya mtoto aliyezaliwa. Anasema Ibnu Arafah: Akika ni kichinjo kinachotumika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na huwa kwa kumchinja mbuzi mkomavu au uzawa wa pili wa aina zote za mifugo iliyosalimika na kasoro ya aina yoyote kuna shurutishwa kwa kuwa kwake katika mchana wa siku ya saba ya kuzaliwa kwa mwanadamu aliye hai. Na katika hukumu yake kuna maelezo aliyoyasikia Bin Kasim yanaingia moyoni mwangu kwamba hiyo ni sheria ya Kiislamu. Na Maziriy hakusimulia isipokuwa kwa kusema kuwa hiyo inapendeza zaidi. Na bin Habiib amepokea walikuwa wakichukizwa na kuiacha kwake. Anasema Albaajiy: sio kama uwajibu wa kuchinja. Na mwelekeo wa Imamu Malik: hiyo ni katika mali ya baba na sio katika mali ya mtoto. Na uwazi wa kauli yake atamfanyia Akika mtoto yatima kwa mali yake, kwamba hiyo haimlazimu ndugu yoyote isipokuwa wazazi". [At Taaj wa Al Eklil 289/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Ar Rahibaniy wa Kihanbali anasema: "(Na hawezi kufanya Akika asiyekuwa baba), isipokuwa pindi atakapokuwa ameshindwa kwa sababu ya umauti au kukataa. Amesema katika kitabu cha: [Sharhul-Iqnaai]: nikasema: na kwa maelezo yaliyotangulia kwamba Mtume S.A.W aliwafanyia Akika, Hassan na Husein ni kwa kuwa yeye Mtume ni mbora wa waumini wote kuliko nafsi zao. (Na mtoto hajifanyii mwenyewe Akika pale anapobaleghe (anapokuwa mkubwa) ameandika hivyo kwani hii inajuzu katika haki ya baba). Basi haifanyi mwingine yoyote kama vile yule asiyekuwa ndugu (kinyume na wote) miongoni mwao ni waandishi wa vitabu kama vile Al Mustauibu, Ar Raudhwah, Ar Riaayataani, Al Haawiyaani, na An Nadhmu na wengineo.. Na iwapo mtu asiyekuwa baba atafanya kwa maana ya kufanya Akika, au mtoto akajifanyia mwenyewe baada ya kubaleghe basi hilo halitachukiza kwa kutokuwa na dalili ya kuchukiza kwake. Imesemwa katika kitabu cha: Sharhul Iqnaai: Mimi nikasema: lakini hiyo haina hukumu ya Akika" [Matwaleb Uliy An Nuha Fi Sharhu Ghayat Al Muntaha 489/2, Ch. Al Maktab Al Islamiy]
Na ni bora zaidi kumwomba idhini yake; kwa kuwa ibada wanayokubaliana watu ni bora zaidi kuliko ibada wanayohitalifiana watu ndani yake, kwa maandiko ya baadhi ya wanazuoni wa Fiqhi walioweka sharti la kuomba idhini kwa yale yanalofanana na hilo.
Na Abu An Naja Al Hijawiy anasema: "Na ikiwa atamtolea mtu Zaka au Kafara kwa mali yake na kwa idhini yake itasihi na atakuwa na haki ya kubadilisha maamuzi yake kama atanuia kufanya hivyo, na ikiwa bila idhini yake haitasihi kama atakavyotoa kutoka katika mali ya anayetolewa bila ya idhini yake". [Al Iqnaa fi Fiqhi Al Imam Ahmad Bin Hanbal 286/1, Ch. Dar Al Maarifah]
Na Al Khatweeb As Sherbiniy anasema: " Na Asili ni yeye kutoa zaka kutoka katika mali yake tajiri kwa kuwa yeye hajitegemei katika kuimiliki kinyume na asiyepewa jukumu kama vile mtoto aliyeongoka na mtu baki (haijuzu kumtolea bila ya idhini yake)". [Al Iqnaa Fi Hal Alfaadh Ibiy Shujaa 229/1, Ch. Dar Al Fikr]
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia: Hakika mambo yalivyo, ni kuwa inajuzu kwa babu kufanya Akika ya mjukuu wake, hata kama mwanae ambaye ni baba wa mtoto aliyezaliwa yupo hai; awe na hali nzuri au ngumu, iwe ameifanya Akika hiyo kwa idhini yake au bila ya idhini yake, isipokuwa tu ni bora amwombe idhini baba wa mtoto kwa lengo la kuepusha ugomvi baina yao, kwa baadhi ya wanazuoni walioweka sharti la idhini ya baba mzazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas