Kushirikiana Katika Mhanga (Udh-hiy...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushirikiana Katika Mhanga (Udh-hiyah)

Question

 Je, inajuzu kwa watu wengi wanashirikiana katika kuchinja ng’ombe mmoja, pamoja na tofauti ya nia zao katika uchinjo huo, ambapo mmoja kati yao ananuia Mhanga, na mwingine ananuia Akika, na mwingine ananuia kupata nyama? Na ikiwa hii ni sahihi, basi inajuzu kwa mtu mmoja kumchinja ng’ombe mmoja kwa nia mbali mbali?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Mara nyingi inatokea kuwa mtu anataka kushirikiana na mwingine katika mnyama mkubwa kama vile ng’ombe au ngamia ili kumchinja na kupata sehemu maalumu ya nyama yake, na lengo la kufanya hivi linahitilafiana, baadhi ya watu wanaona, kwa mfano, kuwa nyama ya ng’ombe ni tamu kuliko ya kondoo, au huenda ni rahisi, n.k.
Aina hii ya ushirika inaitwa: ushirika wa miliki, nao ni wa kisheria kama msingi wake.
Ibn Qudama anasema: “Ushirika ni kukutana katika kumiliki au kutenda. Nao umetajwa katika Qur`ani, Sunna, na Ijmaa; katika Qur`ani kauli ya Mwenyezi Mungu: {watashirikiana katika thuluthi (sehemu ya tatu)}. [AN NISAA: 12], na Mwenyezi Mungu alisema: {na bila shaka washiriki wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa wale walioamini na kutenda mema; na hao ni wachache}. [SWAD: 24]. Na katika Sunna, ilivyopokelewa kuwa: “Al-Baraa’ Ibn A’azib na Zaid Ibn Arqam walikuwa washiriki, wakanunua fedha kwa pesa na kwa kuchelewesha, na ilipofika habari kwa Mtume S.A.W, akawaamuru kuwa wapitishe ilivyokuwa kwa fedha, na warudishe ilivyokuwa kwa kuchelewesha”, na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa alisema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mimi ni mshiriki wa tatu kwa washiriki wawili, asipofanyia hiana mwenzake, akifanyiwa hiana mwenzake, Mimi natoka kati yao”. [ameipokea Abu Dawuud. Na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa alisema: “Mkono wa Allah juu ya washiriki wawili, wasipofanyiana hiana”.
Na Waislamu wamekubaliana pamoja kuwa ushirika unajuzu kwa jumla… na ushirika una aina mbili: ushirika wa miliki, na ushirika wa mikataba. [Al-Mughniy; 5/3, Ch. ya Maktabat Al-Qahira].
Na matini iko wazi katika suala hili, miongoni mwake: ilivyopokelewa na Jabir alisema: “Mtume S.A.W alituamuru kushirikiana katika ngamia na ng’ombe, kila watu saba kwa Badanah (ngamia au ng’ombe aliyenona)”. [Muttafaq].
Na katika mapokezi, alisema; “Tulishirikiana na Mtume S.A.W, katika Hija na Umra, kila saba kati yetu kwa Badanah, na mtu akamuuliza Jabir: je, ushirika wa ng’ombe ni ule ule wa ngamia, akasema; wote ni Badabah”. [Ameipokea Muslim].
Na kutoka kwa Abu Hudhaifa alisema: “Mtume S.A.W, katika Hija yake aliwashirikisha Waisalamu kila watu saba kwa ng’ombe mmoja”. [Ameipokea Ahmad].
Mwelekeo wa dalili ni kueleza suala na kuunda kushiriki katika mihanga na zawadi, na mapokezi ya Ahmad kwenye neno la (Waislamu) ambapo asili yake inaonesha ujumla, na kama kuonekana kuwa watu katika Hija ya Kuaga walikuwa aina mbali mbali; na miongoni mwao ni mwenye kustarehesha na mkusanyaji na mwenye kuchinja mhanga na mwenye kafara ya makatazo ya ibada, na inajulikana kuwa kuahirisha bayana baada ya wakati wake hakujuzu. Na kwa maoni haya walieleza baadhi ya wanazuoni.
Ibn Qudamah anasema: “(Ngamia anatosha kwa watu saba, na mfano wake ni ng’ombe) na hii ni kauli ya wengi wa wanazuoni. Na ile ilivyopokelewa na Ali, Ibn Umar, Ibn Masu’ud, Ibn Abbas, na Aisha, RA, na hivyo hivyo alisema; A’taa’, Tawuus, Salim, Al-Hassan, Amr Ibn Dinaar, Ath-Thawriy, Al-Awzai’iy, Shafiy, Abu Thawr, na wenye maoni.
Na kutoka kwa Umar alisema: Nafsi moja haitoshi kwa watu saba. Na hivyo hivyo alisema Imamu malik. Na Imamu Ahmad alisema: wanazuoni wote wanakubali hivi isipokuwa Ibn Umar. Na kutoka kwa Said Ibn Al-Musayab kuwa: ngamia anatosha kwa watu kumi, na ng’ombe kwa watu saba. Na hivyo alisema Is-haaq; kwa alivyopokea Raafi’ kuwa: “Mtume S.A.W, aligawanya, akasawazisha kondoo kumi kwa ngamia”. [muttafaq].
Na kutoka kwa Ibn Abbas alisema: “Tulikuwa na Mtume S.A.W katika safari, na siku ya Idi Kubwa ikaja, tukashirikiana katika ngamia watu kumi, na katika ng’ombe watu saba”. [Ameipokea Ibn Majah].
Na dalili yetu, alivyopokea Jabir alisema: “Tulichinja pamoja na Mtume S.A.W, tulikuwa Al-Hudaibiyah, ngamia kwa watu saba na ng’ombe kwa watu saba”. Na pia alisema: “tulikuwa tukistarehesha katika Hija pamoja na Mtume S.A.W., tukamchinja ng’ombe, tukashirikiana watu saba’. [Ameipokea Muslim].
Na mapokezi haya mawili ni sahihi sana kuliko mengine. Na kuhusu Hadithi ya Raafi’ inaonesha mgawanyo na siyo ya Kichinjo cha sadaka.
Kwa hiyo washiriki hawa wakiwa jamaa au sio watekelezaji wa faradhi au Sunna, na baadhi yao wanataka kupata nyama; hakika kila mtu kati yao anaambatana na nia yake, na hadhuriwi kwa nia ya mwingine”. [Al-Mughniy: 9/437].
Imamu An-Nawawiy anasema: “Inajuzu kuwa watu saba wanashirikiana katika ngamia au ng’ombe kwa ajili ya kutoa kichinjo cha sadaka, wakiwa wote ni jamaa au sio, au baadhi yao wanataka kupata nyama, na ikiwa Kichinjo ni cha nadhiri au cha kujitolea, na hii ni kwa madhehebu yetu, na pia ni kauli ya Maimamu Ahmad na Dawuud na wengi wa wanazuoni”.
Na akasema: “inajuzu kwa mtu kuchinja ngamia au ng’ombe badala ya kondoo saba ambao wanamlazimu kwa sababu mbali mbali, kama vile kujistarehesha, ukusanyaji, upoteaji, kuingiliana, makatazo ya Ihramu, nadhiri ya kutoa sadaka kwa kondoo anayochinjwa, na kutoa sadaka kwa kondoo”. [Al-Majmuu’ sharh Al-muhadhab: 8397, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: inabainika kuwa kujuzu kwa zaidi ya mtu mmoja kushirikiana katika kuchinja ng’ombe, kwa nia mbali mbali, kwa mujibu wa madhehebu ya wengi wa wanazuoni, vile vile inajuzu kwa mtu mmoja kuchinja ng’ombe mmoja kwa nia mbali mbali.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas