Hukumu ya Mume Kuyanyonya Maziwa y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Mume Kuyanyonya Maziwa ya Mke Wake

Question

 Ni ipi hukumu ya mume kuyanyonya maziwa ya mke wake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Asili ya kustareheshana mke na mume ni Uhalali, isipokuwa mambo yaliyokatazwa kwa kutajwa katika sheria, kama vile kumwingilia kimwili katika wakati wa hedhi au wakati wa nifasi au katika tupu ya nyuma, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watwahirike. Wakisha twahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojisafisha} [AL BAQARAH 222] Na Ahmad ameitoa katika Musnad yake, na Tirmidhiy katika kitabu chake cha Sunani, na akaipandisha iwe na hukumu ya Hasan, na Nasaaiy katika kitabu cha: [Al Fatawa Al-Kubra], kutoka kwa Ibn Abbas R.A., alisema: "Omar R.A, alikuja kwa Mtume S.A.W., na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nimeangamia, Mtume S.A.W, akasema: Ni kipi kilichokuangamiza? Omar R.A, akasema: Mimi nilimgeuza nyuma mke wangu wakati wa kumwingilia, akasema: na Mtume S.A.W, hakumjibia kitu chochote, akasema: Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Akampelekea Wahyi Mtume S.A.W, kwa Aya hii: {Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu.} [AL BAQARAH 223] Anasema: Nenda mbele, na nenda nyuma, lakini jiepusha na tupu ya nyuma na hedhi".
Imamu Ahmad na Abu Dawud wamepokea kutoka kwa Abu Hurairah R.A, kuwa Mtume S.A.W, anasema: "Amelaaniwa yoyote atakayemwingilia mke wake katika tupu ya nyuma".
Na Hadithi hiyo ni dalili ya kuharamisha kumwingilia mke wakati akiwa na hedhi au nifasi, na pia uharamishaji wa kumwingilia mke katika tupu yake ya nyuma.
Ama kuhusu yaliyotajwa katika swali kuhusu mume kuyatia mdomoni na kuyavuta vuta matiti ya mke wake, au kuyanyonya maziwa yake, ukweli ni kuwa asili yake ni kujuzu, kwa kutokuwepo katazo lolote kuhusu kunyonya huko, na kuingia kwake katika ujumla wa kujistarehesha halali kwa kiujumla; na kwa kuwa imehalalishwa kumwingilia mke, ambako ni kiwango cha juu mno cha kustarehe basi kingine kisichokuwa hicho kinajuzu zaidi.
Amesema Imamu Kassaniy Hanafiy katika kitabu cha: [Al Badai'I 331/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah] katika ufafanuzi wa hukumu za ndoa sahihi: "Na miongoni mwayo ni uhalali wa kutazama na kugusa, kuanzia kichwani mpaka miguuni katika hali ya kuwa kwake hai, kwani kumwingilia ni juu zaidi ya kutazama na kugusa na kwa hivyo basi kuhalalishwa kwake kunakuwa kuhalalishwa kugusa na kutazama kwa njia ya kuwa bora zaidi.
Na kadhalika kuyanyonya matiti; kwani kumwingilia ni juu zaidi kuliko kumnyonya matiti, na kwa hivyo basi kuhalalishwa kilicho chini ya kumwingilia kama vile kutazama na kugusa na kunyonya matiti na mfano wake, ni halali zaidi.
Na kama maziwa yatatoka katika matiti ya mke na mume akayameza basi inajuzu kufanya hivyo, na hakuna ubaya wowote katika hili. Kwani maziwa ni twahara na wala hayatii kinyaa kisheria au kiuhalisi.
Imekuja katika kitabu cha: [Al Majmou' Sharhu Al Mohazab kwa Imamu An Nawawiy 569/2, Ch. Dar Al Fikr] katika maelezo ya sehemu za maziwa, "(sehemu ya tatu) maziwa ya binadamu, nayo ni twahari kwa madhehebu yote, na hayo ndiyo yaliyoandikwa, na hivyo ndivyo walivyoona wanazuoni wetu isipokuwa mwenye kitabu cha:[Al Hawi] kwamba yeye alisimulia kutoka kwa Al Anmatwiy ambaye ni katika wanazuoni wetu, anaona kuwa maziwa ya binadamu ni najisi, lakini ni halali kwa mtoto kuyanywa kwa sababu ya dharura, ameitaja hukumu hii katika kitabu cha: [Al Biyuo'], na Ad Darmiy amesimulia mwisho wa kitabu cha: [As Silm], na pia As Shashiy na Ar Rwiyaniy wamesimulia hivyo, na hili siyo kitu chochote bali ni kosa la wazi, isipokuwa amesimulia mfano wa hayo kwa ajili ya kutahadharisha kuvutiwa zaidi nayo.
Na Sheikh Abu Hamed alinukulu makubalianao ya waislamu juu ya utwahara wa maziwa. Ar Ruyaniy anasema mwisho wa mlango wa kuuza kwa Al Gharar: Kama tukisema kwa Madhehebu haya kuwa mwanadamu hanajisiki kwa umauti kisha akafariki dunia akiwa na maziwa katika matiti yake basi maziwa hayo ni twahari na yanajuzu kuyanywa na kuyauza."
Na mume kuyameza maziwa ya mke wake hakuthibitishi uharamu wowote; kwani kunyonya maziwa baada ya miaka miwili hakuharamishi kitu chochote, na hii ni rai ya Jamhuri ya wanazuoni, kwa Hadithi iliyokuja kutoka kwa Umm Salamah R.A, anasema: Mtume S.A.W, amesema: "Haiwi haramu kwa kunyonya pamoja isipokuwa kwa kufika maziwa kwenye utumbo wa mtoto, na hali hii ikawa imetokea kabla ya mtoto kuwa mtambuzi". At Termiziy anasimulia katika kitabu chake cha Sunani, na akisema: Hadithi hii ina hukumu ya Hassan na ni sahihi. Na kwa kuifanyia kazi wengi wa wanazuoni miongoni mwa Maswahaba wa Mtume S.A.W, na wengineo ni kwamba unyonyeshaji hauharamishi isipokuwa mtoto aliyekuwa chini miaka miwili, na kinachotokea baada ya miaka miwili hakiharamishi kitu chochote.
Ibn Qudamah anasema katika kitabu cha: [Al Mughniy 177/8, Ch. Maktabat Al Qaherah]; "Hakika ni kuwa katika sharti la kuharamisha kwa kunyonya ni kutokea kwake ndani ya miaka miwili, na hii ni kauli ya wengi wa wanazuoni. yamepokelewa mfano wa hayo kutoka kwa Omar, Ali, Ibn Omar, Ibn Masuod, Ibn Abbas, Abu Huraira na wakeze Mtume S.A.W, isipokuwa Bibi Aisha, na hivyo ndivyo walivyoelekea As Shuabiy, Ibn Shabramah, Al Awzaiy, Shafiy, Is-Haq, Abu Yusuf, Muhammad, Abu Thaur na pia simulizi ya kutoka kwa Malik".
Na Sheikh Taqiy Ediin Ibn Taimiah aliulizwa hukumu ya – kama ilivyo katika kitabu cha: [Majmuu' Al Fatawa 55/34, Ch. Magma'u Al Malik Fahd, kampuni ya kuchapisha Misahafu – Al Madinah Al Munawarah] mwanamume anaempenda mke wake na akafanya naye mapenzi na akayanyonya maziwa yake, Je mke huo anakuwa haramu kwake?
Naye akajibu: "Kwamba kuyanyonya kwake maziwa ya mke wake hakuharamishi mke kwa mujibu wa madhehebu ya maimamu wanne".
Na kutokana na maelezo hayo, inaelezwa kwamba kunyonyesha maziwa ya mke hakuathiri chochote katika uharamishaji wa mke, na kwa hivyo hakika mume kuyanyonya matiti ya mke wake ni halali na ni katika njia za kujistarehesha kati ya mume na mke wake, na maziwa yakitoka katika matiti ya mke na mume akayameza basi hakuna ubaya wowote wa kisheria katika hilo, na haupatikani uharamu kwa kufanya hivyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


Share this:

Related Fatwas