Kumnyonyesha Mtoto Anayelelewa Baad...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumnyonyesha Mtoto Anayelelewa Baada ya Kupita Miaka Miwili.

Question

 Ikiwa Mtoto wa kiume au wa kike anaelelewa, ana umri wa zaidi ya miaka miwili, je atanyonyeshwa ili kuthibitisha uharamu wa anaonyonya nao au hapana? Na ni ipi njia ya kunyonyesha ambayo inaharamisha kwa kunyonya pamoja katika hali kama hiyo?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Madhehebu yote yaliyopo katika umma na yanayofuatwa, yanakiri kuwa unyonyeshaji ambao unaharamisha, lazima uwe baina ya miaka miwili. Kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha} [AL BAQARAH 233]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili} [LUQMAN 14]. Na kwa Hadithi ya Mama wa Waumini, Bibi Aisha R.A, katika vitabu viwili vya Sahihi; "Hakika kunyonyesha kunasababishwa na janga la njaa" [Inaafikiana nayo]. Na kuna Hadithi nyinginezo nyingi zinazoyaashiria hayo.
Na wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki wameruhusu kuongeza kiasi cha mwezi mmoja au miezi miwili baada ya kupita miaka miwili. Na Imamu Abu Hanifa ameufanya muda wa kunyonya kuwa ni miaka miwili na nusu, ampabo alifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kuchukua kwake mimba hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} [AL AHQAAF 15]. Kwamba muda wote uliotajwa ni muda kwa kila upande peke yake na siyo wa jumla ya mida miwili. Na mwenzanke Imamu Zafar akaukadiria muda huo kuwa ni miaka mitatu. [Al Mabsuotw 136/5, Ch. Dar Al Maarifah]
Na iwapo mtoto atauvuka muda uliotajwa na wanazuoni kama ndio wakati wa kunyonya – nao ni miaka mitatu – basi kumnyonyesha mtoto katika muda huo hakutambuliki kisheria, na wala hakupelekei uharamu wa kuoana mtoto huyo na atakaonyonya nao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas