Kusitisha Tawafu ya Kaaba kwa Ajili...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusitisha Tawafu ya Kaaba kwa Ajili ya Kusimamisha Swala ya Fardhi.

Question

 Swala inapokimiwa wakati mimi nikiwa bado ninalizunguka Kaaba, Je, inajuzu kwangu kuisitisha tawafu, au ninatakiwa kuikamilisha kisha nisimamishe Swala? Ikiwa hukumu ni kuikata, kisha Swala ikawa imekwishaswaliwa, Je, nitaanza Tawafu kuanzia pale nilipoishia, au nitaianza upya nusu ya kwanza ya Tawafu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Tawafu ni kuzunguka Nyumba Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Safaa na Marwa (Majabali Mawili yanayofanyiwa ibada ya Kusai Huko Makka) ni katika alama za kuadhimisha dini ya Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au kufanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili; na anayefanya wema (atalipwa) kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukurani na Mjuzi (wa kila jambo)}. [AL BAQARAH: 158].
Na Tawafu ama ni wajibu kama vile Tawafu ya Ifadha, au Sunna kama vile Tawafu ya Quduum, na inashurutishwa katika Tawafu iwe ya kudumu mfano wa Swala, kwa hiyo haikatwi isipokuwa kwa udhuru; na kwa sababu Mtume S.A.W, aliendelea naTawafu yake na hakuikata, na akasema: “Chukueni kwangu njia za ibada zenu”. [ameipokea Muslim], na ilivyopokelewa na An-Nasaii, kutoka kwa Tawuus alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Tawafu kuzunguka Nyumba ni Swala”.
Miongoni mwa nyudhuru hizo ambazo Tawafu inaweza kukatwa kwa ajili yake kusimamaisha Swala ya fardhi, kwa sababu kwa kuwa Tawafu ni wajibu, lakini Swala ni wajibu zaidi; na wakati mambo mawili ya wajibu yanapokutana basi lililo wajibu zaidi hutangulizwa.
Az-Zarkashiy anasema katika suala la: baadhi ya mambo ya wajibu ni wajibu zaidi kuliko mengine: “Al-Kadhi anasema: inajuzu kusemwa kuwa: baadhi ya mambo ya wajibu ni wajibu zaidi kuliko mengine, kama vile Sunna, baadhi yake zimesisitizwa kuliko zingine, kinyume na mwelekeo wa Al-Mu’tazilah; kwa sababu uwajibikaji kwa rai zao unaashiria Sifa ya Dhati, na Ibn Al-Qushairiy anasema: hii inajuzu kwetu, kwa sababu ya jinsi ilivyokemewa kwa ajili ya kuiacha, inakuwa wajibu zaidi, kwa mfano; Imani kwa Mwenyezi Mungu ni wajibu zaidi kuliko udhu”. [Al-Bahr Al-Muhiit; 1/244, Ch. Ya dar Al-Kutbiy].
Dalili ya kuwa Swala ni wajibu zaidi ni miongoni mwa Nguzo Tano za Uislamu, Imamu Bukhariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn Umar R.A, alisema kuwa: Mtume S.A.W, anasema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kushuhudia kuwa hakuna Mungu kwa haki isipokuwa Allah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, kusimamisha swala, kutoa zaka, Kuhiji Nyumba, na Kufunga Ramadhani”, na inavyosisitizwa umuhimu wa nyakati zake kauli ya Mwenyezi Mungu: {Kwa hakika Swala kwa Waislamu ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi}. [AN NISAA: 103].
Na ilivyopokelewa na Imamu Bukhariy na Muslim, kutoka kwa Abu Huraira, kutoka kwa Mtume S.A.W, alisema: “Inaposimamishwa Swala, basi hakuna kuswali ila Swala ya fardhi”, na hii ni dalili kuwa Swala ya fardhi ni muhimu sana kuliko Tawafu na ni wajibu kabisa.
Ikiamuliwa kisheria kukata Tawafu kwa ajili ya Swala ya faradhi, basi kuna mitizamio kadhaa:
Ama akianza mwanzo wa Tawafu, bila ya kuizingatia sehemu iliyotangulia, au akaizingatia sehemu iliyotangulia, na kama ataizingatia iliyotangulia, basi kuna mitizamo miwili:
Ama akatengua sehemu ya kwanza ambayo aliikata, basi akaswali kisha akarejea kwa ajili ya kukamilisha sehemu zote, au akaanza kutoka mahali alipopatoka, na mwelekeo wa hayo ni kuwa: Tawafu yote ni ibada moja, na haigawanywi, nayo kama Swala kwa pande zote, isipokuwa inajuzu kuzungumza ndani yake, kama alivyosema Mtume S.A.W, au Tawafuni ibada yenye sehemu mbali mbali, na sehemu hizi ni safari saba, na mpangilio na kudumu unaambatana na ibada yenye nguzo mbali mbali, lakini safari hizi saba hazina tofauti kati yake mfano wa twahara na Swala, na twahara inaambatana na viungo mbali mbali, na swala ina nguzo mbali mbali, lakini Tawafu na safari zake saba hazina tofauti hizi, kwa hiyo hazina mpangilio. Na hii ni kauli yenye nguvu zaidi, kwa alivyotoa dalili yake Ash-Shiraziy katika Al-Muhadhab kuwa: Ibn Umar R.A,: “Alikuwa akitufu kuzunguka Nyumba ,(Kaaba) na inaposimamishwa swala, huswali pamoja na Imamu, kisha huzingatia Tawafu iliyotangulia”.
Na wafuasi wa madhehebu ya Malik walisema: ni bora kukamilisha safari ya Tawafu kisha kwenda kuswali.
Imamu An-Nawawiy amesema: “Mtungaji na wanazuoni walisema: inaposimamishwa swala ya faradhi au mtu akapatwa na haja ya dharura, na yeye akitufu, basi atakata Tawafu, na atakapomaliza atazingatia kilichotangulia, ikiwa muda si mrefu, na hata ulikuwa mrefu, kwa rai ya madhehebu, kutokana na hitilafu iliyotangulia.
Al-Baghawiy na wengineo walisema: ikiwa Tawafu ni faradhi, basi haifai kuikata kwa ajili ya Swala ya Jeneza na Sunna ya Dhuha na Witri na Sunna nyinginezo za kudumu, kwa sababu Tawafu ni faradhi ya lazima na haikatwi kwa ajili yasiyotiliwa nguvu wala faradhi ya kutosheleza.
Walisema: hukumu ni ile ile ya Kusai, na Imamu Shafi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alieleza hayo yote katika kitabu chake cha: [Al-Umm], na Kadhi Abu-Twayib katika maelezo yake kwa Al-Umm alisema: Alisema katika kitabu cha: [Al-Umm]: Akiwa katika Tawafu ya Ifadha na Swala inasimamishwa, mimi napenda aswali pamoja na watu, kisha arudi katika Tawafu yake, na kuzingatia kwake yaliyopita, na akiogopa kuacha Witri au Sunna ya Dhuha au Swala ya Jeneza, mimi sipendi kuiacha Tawafu kwa ajili ya vitu hivi, asije kuacha faradhi kwa ajili ya isiyotiliwa nguvu au faradhi ya kutosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi”. [Al-Majmuu’ Sharh Al-Muhadhab: 8/67, Ch. Ya Al-Muniriyah].
Al-Bahutiy mfuasi wa madhehebu ya Hanbal alisema: “Akiikata Tawafu kwa muda mfupi, atazingatia kwenye Jiwe jeusi isije kuacha Sunna za kudumu, au Swala ya fardhi imesimamishwa, ataswali na kuzingatia yaliyopita, kwa Hadithi hii: “Inaposimamishwa Swala, basi hakuna Swala ila Swala ya faradhi”, na Tawafu ni Swala, kwa hiyo itaingia kwa jumla, na atazingatia kuanzia kwenye Jiwe Jeusi, hata ikiwa kuikata ni katikati ya safari; kwa sababu haizingatiwi baadhi ya safari, na hukumu ya Kusai ni ile ile ya Tawafu”. [Kashful Qinaa’ A’n Matn Al-Iqnaa’: 2/448, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Al-Kharshiy mfuasi wa madhehebu ya Malik anasema: “Kuikata Tawafu ya faradhi au Sunna ni wajibu kwa ajili ya kusimamisha Swala, na atazingatia yaliyopita, lakini ni bora kutoka kwake (katika Tawafu) awe amekamilisha safari mpaka kwenye jiwe Jeusi; na kama akitoka mahali pengine, Ibn Habiib anasema: ataingia mahali alipoachia, alisema hivyo katika kitabu chake cha At-Tawdhiih, nayo imetatajwa katika Al-Mudawanah na Al-Mawaziyah, na Ibn Habiib alipendelea kuanza safari hii, na wengine walisema: ni bora kuieleza kwa makubaliano, kama ilivyotajwa katika At-Tiraaz. [Mwisho].
Na atazingatia kabla hajaswali Sunna, kama ilivyosemwa na Ibn Al-Hajib katika Al-Mawaziyah; na kama akiswali Sunna kabla ya Tawafu yake, basi ataanza upya, na wengine walisema: Hivyo hivyo akikaa muda mrefu baada ya Swala kwa ajili ya dhikri, au mazungumzo, kwa sababu kuacha Sunna za kudumu”. [Sharh Al-Kharshiy A’la Mukhtasar Khalil: 2/316, Ch. Ya Dar Al-Fikr]
Kwa mujibu wa maelezo haya yaliyotangulia: Swala ya faradhi inaposimamishwa wakati mwenye kutufu anatufu fardhi au Sunna, inajuzu kwake kuikata Tawafu na kuswali kwanza, kisha kuzingatia yaliyo tangulia kwa safari za Tawafu zilizokatwa, na kuzikamilisha, na kama akiikata Tawafu katikati ya safari, ataanza upya safari hii aliyoikata, na safari zilizotangulia zitahesabika.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas