Mzinifu Kujinasibisha na Mtoto wa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mzinifu Kujinasibisha na Mtoto wa Zinaa.

Question

Mvulana mmoja alimdanganya msichana hadi akafanya naye uzinzi. Hatua hii ilisababisha ujauzito. Wote wawili walijutia yaliyowatokea, mvulana yule akanuia kumwoa msichana huyo ili dhambi yake isamehewe. Je! inaruhusiwa kwa mvulana huyo baada ya ndoa hii kujinasibisha na mtoto aliyetokana na mimba aliyoisababisha yeye mwenyewe au la?
Je, kuna hukumu gani ikiwa mvulana huyo alimlazimisha msichana huyo kufanya uzinzi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu...
Tatizo la watoto waliozaliwa nje ya ndoa ya kisheria ni msiba mkubwa, hasa katika siku hizi, ambako kuna sababu ambazo zimesababisha kuongezeka kwa tatizo hili. Yoyote sababu iwayo, ni wajibu wa wale wanaoshughulikia masomo ya kisheria na kijamii kutafuta sababu na kupata suluhisho. Semina na kozi za kupata ufumbuzi wa kisheria kwa tatizo hili kabla na baada ya tukio hilo, na labda kikao cha ishirini cha hivi karibuni cha baraza la Fiqh ya Kiislamu kilichofanyika Makkah tarehe 19 - 23 Muharram 1432 AH, sawa na 25 - 29 Desemba 2010.
Suala hili lina sehemu mbili, sehemu ya kwanza: suala la kumlazimisha na suala la kujipatia mtoto anayetokana na uzinzi, iwapo ni kumlazimisha au kwa ridhaa, na suala la kumlazimisha, anayelazimishwa hana dhambi wala adhabu, na hii inajulikana kwa umma, dalili zake ni nyingi na maarufu, ikiwa ni pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa} [AN NAHL 106], na kauli ya Mtume S.A.W. “Allaah Amewasamehe umma wangu kwa kukosea, kusahau, na yale wanayoyafanya kwa kulazimishwa kwa nguvu ambayo hawana khiyari nayo”. [Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas na ameisahihisha Ibn Hibban na Al-Hakim, na ina ushahidi]. Anayelazimishwa kufanya uzinzi, basi dhambi huondolewa kwake na adhabu pia.
Sehemu ya pili: ni inayohusiana na tatizo hili baada ya kutokea, na inavyoweza kutokea kwa ombi la mzinifu kujipatia mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi, katika hali hii yawezekana aliyeziniwa ameolewa au la, kama akiwa ameolewa au ni mjakazi anayelala na bwana wake, Wananvyuoni wote wameafikiana kwamba wito wa kujinasibisha kwa mzinifu haukubaliwi, lakini mtoto ananasibishwa na mwenye ndoa naye awe mtu huyo ni Mume au bwana kama hakukataa. Ibn Qudaamah anasema katika Al-Mughni: "Wao walikubaliana kwamba kama mtoto angezaliwa katika kitanda cha mtu mwingine, alisema kuwa mtoto huyo hanasibishwi, na wametofautiana ikiwa mtoto huyo alizaliwa nje ya kitanda." [6] / 226, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Wametoa dalili ya hilo kutokana na Hadithi iliyopokelewa katika Sahihi mbili kutokana na Hadithi ya Bi Aisha R.A. alisema: “Saad Ibn Abi Waqqas na Abdu Ibn Zamah waligombana kuhusu mtoto, Saad alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Utbah Ibn Abi Waqqas mwana wa ndugu yangu aliniambia kuwa mtoto huyo ni wake, uangalie anafanana naye. Abdu Ibn Zamah alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyo ni ndugu yangu, alizaliwa kitandani mwa baba yangu, Mtume S.A.W. akamwangalia akamwona anafanana na Utbah, akasema: Ewe Abdu Ibn Zamah mtoto huyo ni wako, mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa (yaani mume au bwana wa mjakazi), na mzinifu haki yake ni kupigwa mawe, ewe Sawadah binti Zamah ujifiche mbali naye. Basi Sawadah hakumwona kabisa".
Abu Omar Ibn Abdul-Bar alisema: “Katika Hadithi hii ina masuala ya Fiqh na Usuli, pamoja na Hukumu kwa mujibu wa yanayoonekana; kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W, amehukumu kuwa mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa, kwa mujibu wa yaliyoonekana na Sunna yake na hakujali mambo yenye shaka, vile vile katika hukumu ya suala la Liaan akahukumu kwa mujibu wa yaliyoonekana na hakujali mambo yaliyotajwa baada ya kauli yake kuwa: "Kama akija kwake basi yule ni kwa aliyemtupia". Vile vile kauli yake S.A.W.: "Ninahukumu kwake kwa mujibu wa ninavyosikia" Na katika Hadithi hii ni dalili kuhusu hali ya watu wa zama za jahilia walivyokuwa wanajinasibisha watoto waliozaliwa kutokana na uzinzi. Omar ibn Al-Khatwab R.A alikuwa akinasibisha watoto waliozaliwa katika zama za ujahili kwa wanaosema kuwa ni wao katika Uislamu ... Abu Omar alisema: hali hii kama hakuna kitanda, kwa sababu watu walikuwa katika zama za ujahili wanaoa, na ndoa zao kwa mujibu wa dini ya kiislamu haziruhusiwi, Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alizipitisha, lakini Uislamu ulipokuja Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alihukumu kwa ubatili wa uzinzi kwa mujibu wa marufuku ya Mwenyezi Mungu kwake kwa kusema: "Na mzinifu haki yake ni jiwe", akakanusha kunasibishwa kwa mtoto wa uzinzi katika Uislamu, na bila kupingwa Wanavyuoni wa umma wameafikiana hali hii kunukuliwa kutoka kwa Mtume S.A.W. Na Mtume S.A.W. amefanya kila mtoto aliyezaliwa juu ya kitanda cha mtu ananasibishwa kwake katika hali yoyote, ila akimkataa kwa hukumu ya Liana ... na bila kupingwa, Jamhuri ya wanavyuoni wameafikiana kwamba mwanamke aliye huru ni wa kulala naye kwa ndoa pamoja na kuwepo uwezekano wa kumwingilia na kumbebesha ujauzito, na kama ndoa inaambatana na uwezekano wa kukutana kimwili na kubeba ujauzito basi mtoto anayezaliwa ni wa mwenye kitanda (yaani mwenye ndoa) ambapo haki hii kwake haitoweki kamwe kwa madai ya mtu mwingine, wala kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa kiapo cha laana". [Al-Tamhiid limaa fil Muataa min Almaani Wal Asaniid 8/182, Wizara ya Awqaf na masuala ya Kiislamu -Morocco].
Al-Bajiy alisema: “Kuhusu kauli yake Mtume S.A.W: "Na mzinifu haki yake ni kupigwa mawe", maana yake ni kwamba kama mwanaume atakuwa ni mwenye ndoa atamdai mtoto kutoka kwa mjakazi au mwanamke asiye mjakazi, lakini kama hakumdai imetajwa na Muhammad Ibn Issa kuwa alimwuliza Ibn Kinanah kuhusu kundi la watu wamesilimu na baadhi yao wamedai mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi anaweza kunasibishwa kwake? Akasema: Ndiyo akiwa kutoka mjakazi au mwanamke asiye mjakazi , isipokuwa akidaiwa na bwana wa mjakazi huyo au mume wa mwanamke asiye mjakazi akawa ni mtoto wake, kwani Mtume S.A.W. alisema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa, na mzinifu haki yake ni jiwe" na Ibn Al-Qasim alisema rai hii pia”. [Al-Muntaqa Sharhul Mwataa 6/8, Matbatul Saadah].
Vile vile imepokelewa kutoka kwa Abu Daud kutoka kwa Amr Ibn Shuaib kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, amesema: "Mtu alisimama akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika yule mwanangu nimezini pamoja na mama yake katika zama za ujahili, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akasema: hakuna kudai katika Uislamu, jambo la ujahili lilipita, mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa, na mzinifu haki yake ni jiwe".
Na jiwe katika Hadithi hii maana yake ni kunyima, yaani mzinifu hana hadhi ya kupewa nasaba, kama kauli ya mtu aliyenyimwa kitu: huna isipokuwa udongo, na lililo mkononi mwako ni jiwe tu. Na imepokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. – kama ilivyotajwa katika Sunan Abi Daud na asili yake katika Sahihi mbili- kuwa ameikataza bei ya mbwa, maana mtu akija kuomba bei ya mbwa ujaze mikono yake udongo tu, na maana ya udongo ni usimpe chochote. [Rejea: Maalim Al-Sunan kwa Al-Khatabi 3/281, Al-Matbah Al-Ilmiyah].
Maana: kwamba kama mtu akiwa na mke au mjaka wake anaruhusiwa kulala naye akizaa mtoto, basi ananasibishwa kwa baba yake na ana haki ya kurithi na hukumu nyingine za kuzaliwa.
Lakini kama mwanamke mzinifu huyo si mke wala si mjakazi kwa bwana wake, basi wanavyuoni walitofautiana kuhusu nasaba ya mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi akitaka mwanamume mzinifu kumjinasibisha- kwa maoni mawili, maimamu wanne na wanavyuoni wa Al-Dhahiriyah wakasema kuwa: aliyezaliwa nje ya ndoa hakunasibishwa kwa yule mwanamume mwenye manii, au kwa mwingine ambaye anadai kuwa ni baba yake, lakini ananasibishwa kwa mama yake, na walieleza hali hiyo kuwa asili ya kuthibitisha nasaba ni kitanda na ndoa halali na sahihi, na chochote kingine hakithibitishi nasaba, yaani nasaba haikuthibitishwa kwa uzinzi. [Al-Mabsuot ya Srkhsi 17/154, Dar Al-Maarifah, Bada'a Al-Sana'a 6/242, Dar Al-Kuttab Al-Ilmiyah, na Sharhu Al-Kharashi, 6/101, Dar Al-Fikr, Rawdhat Al-Talebeen 6/44, Al-Maktab Al-Islami, Tohfatul Muhtaj 5/401, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi, na Al-Sharhul Kabiir ala Al-Muqnii kwa Ibn Abi Omar 7/36, Dar Al-Kitab Al-Arabi Lelnashr waltawzii].
Dalili yao ya kimsingi ni Hadithi ya Bi Aisha katika kisa cha kugombana kwa Saad na Abd Ibn Zamah, ambapo inasema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa (yaani mume au bwana wa mjakazi ), na mzinifu haki yake ni jiwe". Na dalili kutokana na Hadithi hii ni wazi.
Wao walitoa dalili ya Hadithi ya Ibn Abbas kama dalili kwamba Mtume S.A.W. aliema: "Hakuna uzinzi katika Uislamu, na aliyezini katika zama za ujahili atafuata nasaba yake, na mwenye kudai kuwa mtoto ni wake pasipo na ndoa sahihi, basi harithi wala harithiwi" [Imepokelewa kutoka kwa Abu Daawuud].
Ushahidi ni kwamba Mtume S.A.W. amebatilisha uzinzi katika Uislamu, na hakuambatanisha nasaba kwake, na akasamehe aliyezini katika zama za ujahili, na akaambatanisha nasaba kwa bwana wa mjakazi mzinzi, nayo inakusudiwa ni nasaba, hii inaonesha kuwa mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi hanasibishwi kwa mzinifu akimdai, katika hali hii hakuna tofauti kati ya kitanda (ndoa sahihi) na njia nyingine.
Miongoni mwa Hadithi walizoleta kama ushahidi ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Amr: kwamba Mtume, S.A.W. amehukumu kuwa kila mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi amenasibishwa baada ya kifo cha baba yake, na warithi walimdai, Mtume, S.A.W. amehukumu kuwa kila mtoto aliyezaliwa kutokana na mjakazi aliyemilikiwa na bwana wake siku ya kulala naye, basi mtoto huyo ananasibishwa kwa mwenye kumdai, na hana hadhi katika urithi uliogawanywa kabla yake, lakini ana hadhi katika mirathi isiyogawanywa, na hanasibishwi kwa baba yake kama baba yake alimkanusha, na kama mtoto huyo akizaliwa kutokana na mjakazi hakumilikiwa na bwana au kutokana na mwanamke asiye mjakazi aliyezini, basi mtoto huyo hanasibishwi kwa yule mwanamume aliyezini na mama yake, wala harithi, hata kama yule mwanamume akimdai mtoto huyo akizaliwa kutokana na mjakazi au mwanamke asiye mjakazi . [Imepokelewa kutoka kwa Ahmad, Abu Daud na Ibn Majah].
Na maana ya Hadithi hii ni kwamba mtoto aliyezaliwa kutokana na mjakazi aliyemilikiwa na baba yake mtoto siku ya kulala naye, basi mtoto huyo ananasibishwa kwa baba yake akimdai, atakuwa mrithi katika haki yake na kushiriki pamoja katika urithi, lakini hali hii inahusu urithi uliogawanywa baada ya kunasibishwa kwa mtoto, vile vile akiwa mwanamume yule hakumkanusha mtoto huyo katika uhai wake, lakini kama akimkanusha hanasibishwi kwake. Lakini kama mtoto aliyezaliwa kutokana na mjakazi asiyemilikiwa na baba yake mtoto siku ya kulala naye, yaani akazini pamoja naye, au kutokana na mwanamake asiye mjakazi na amezini naye, basi hairuhusiwi kunasibishwa kwake, hata kama akimdai katika uhai wake, kwani ni mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi. Hadithi hii inaonesha kwamba mzinifu kama akiomba nasaba ya mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi akizaliwa kutokana na mjakazi au mwanamke asiye mjakazi , basi hairuhusiwi kunasibishwa kwake na hathibitishwi nasaba kwake kabisa. [Rejea: Zaad Al-Ma'ad kwa Ibn Al-Qayyim 5/383, Mu’asasit Ar-Risalah].
Na miongoni mwa maana zilizoridhisha na zilizotajwa na wanavyuoni wa umma kwa mujibu wa maoni yao ni kwamba manii ya uzinzi
Yenye kupotea ovyo na hayana utakatifu, kwa hivyo hayana athari yoyote, kufuatana na rai iliyochaguliwa kwamba katazo hapa linaonesha ufisadi kama ikiwa jambo lenyewe linalokatazwa kama vile uzinzi na kufunga katika siku ya Eid Al-Adha, Ibn Al-Arabi anasema: “Mwenyezi Mungu ameneemisha waja wake kwa nasaba na ushemeji, Mwenyezi Mungu anasema: {Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji.} [AL-FURQAAN: 54], na hukumu zilitegemea mambo haya mawili (nasaba na ushemeji) kuhusu kuhalilisha na kuharamisha, na ubatili hauambatanishwi nayo, wala hauwi sawa nayo” [Rejea: Ahkam Al-Quran 3/447 Dar Al-Kitab Al-Ilmiyah], Pia kutothibitisha nasaba kwa mzinifu kunamzuia kufanya jambo lolote la haramu.
Sheikh Taqi Al-Din Ibn Taymiyah alisema: “Mwenyezi Mungu amrehemu aliuliza kuhusu: mwanamke aliyezini, akawa na mimba kutoka mzinifu huyo, na akazaa mtoto wa kike: je, mzinifu yule anaweza kumwoa msichana yule? Akasema: Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, hairuhusiwi kwa mujibu wa rai iliyochaguliwa na wanavyuoni wa umma, na hakuna hata mmoja wa masahaba amehalilisha jambo hili, wala mmoja wa wafuasi wao kwa wema, kwa hivyo, Imam Ahmad Ibn Hanbal na wanavyuoni wengine -ingawa wanasoma vitabu vingi- hawakuona upingaji katika suala hili, naye Imam Ahmad Ibn Hanbal alitoa fatwa kuwa kitendo hicho ni mauaji, akaambiwa kuwa: mtu mmoja amesema tofauti na Imam Malik akapinga rai ile, Imam Ahmad Ibn Hanbal akasema: mtu yule amesema uwongo, na akataja kwamba mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinizi ananasibishwa na mzinifu akiomba hivyo kwa mujibu wa rai ya kundi la wanavyuoni, na kwamba Omar Ibn Al-Khatwab amewanasibisha watoto katika zama za ujahili kwa baba zao, na Mtume, S.A.W. akasema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa (yaani mume au bwana wa mjakazi), na mzinifu haki yake ni kupigwa mawe". Hali hii ikiwa mwanamke huyu ana mume.” [Majmuu Al-Fatwa 32/38, Majmaa Al-Malik Fahd Litwibaatul Mushaf As-Shariif].
Wengi wa wanavyuoni wamempinga Ibn Taymiyah na Ibn Al-Qayyim, wakisema kuwa mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi ananasibishwa na mwanamume mzinifu akimwomba na kama mwanamke mzinifu hakuwa na mume au bwana, na rai hii imesimuliwa kutoka kwa Umar bin Al-Khatwab, Hasan Al-Basri, Ibn Sirin, Urwah Ibn Al-Zubayr, Suleiman Ibn Yasaar, An-Nakha'i, na Ibn Raahawayh , vile vile rai hii imepokelewa kutoka kwa Imam Abu Hanifa, aliposema: Sioni lolote baya kama mtu aliyezini pamoja na mwanawake, na akapata mimba, kumuoa na mimba yake na kumsitiri, na mtoto aliyezaliwa ni kwake. [Al-Mughni 9/123, Al-Sharhul Kabiir kwa Ibn Abi Omar 7/36, Majmuu Al-Fatawa 23/113, na Zad Al-Maad 5/384, na rejea Al-Hoja ala Ahlul Madinah kwa Mohammed Ibn Hassan 3/191, Alam Al-Kutub].
Lakini yamewekwa masharti yanayounganishwa ili kusahihisha nasaba hii, nayo ni toba ya mwanamume mzinifu na mwanamke mzinifu, na kuamua kutorudia tena dhambi hii mara nyingine, na kujuta juu ya matendo yake yaliyopita, na hivyo kwa ajili ya kuwahamasisha wale walio na nia ya kufanya dhambi wafanye ya wema na kutii, na inajulikana kwamba dini ya Kiislamu inapenda watu kutubia, na imembashiria mwenye kutubu baada ya toba yake, Mwenyezi Mungu anasema : {Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema.} [AL FURQAAN: 70], na miongoni mwa masharti hayo ni kwamba mwanamume mzinifu amwoe mwanamke mzinifu ili wafikie maana ya uhusiano wa tawi kwa asili yake, na kwa ajili ya kurekebisha kasoro iliyotokea kati yao. Maulamaa waliotangulia wamesema kwamba ndoa ya mwanamume mzinifu na mwanamke mzinfu ni bora zaidi, Abu Bakr R.A. aliulizwa kuhusu mwanamume aliyefanya uzinzi na mwanamke, kisha anataka kumuoa alisema: Hakuna toba bora kuliko kumwoa kwake, akaenda mbali na uzinzi kwa kuoa halali. [Kitabu cha Abdul Razzaq 7/204].
Vile vile katika Kitabu cha Abdul Razzaq [7/205], imepokelewa kutoka kwa Nafi' kwamba Ibn Umar alikuwa na mjakazi, na alikuwa na mvulana aliyelala naye, alimtukana , Ibn Umar akamwona mjakazi siku moja akamwuliza: umepata mimba? Akasema: Ndiyo. Akamwuliza: Kutoka kwa nani? Akasema: Kutoka kwa mtu fulani. Akasema: niliyemtukana? Akasema: Ndiyo. Ibn Umar alimuuliza mvulana yule, akakana, na alikuwa na kidole cha ziada. Ibn Umar akamwambia: "Je, unaonaje kama mzaliwa huyo akiwa na kidole cha ziada?" Akasema: Ni kutoka kwangu. Akasema: mjakazi alimzaa mtoto mwenye kidole cha ziada. Alisema: Ibn Umar alimwadhibu mjakazi, na akamwozesha mvulana yule, na akampa uhuru mtoto aliyezaliwa.
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Masud, Ibn Abbas, Jaber bin Abdullah, Alqamah, Taus, Al-Hassan, Qatada, na wengine kwama inaruhusiwa kumwoa mwanamke aliyezini.
Pia wamesema kuwa na sharti la kunasibisha, yaani kukiri kwa nasaba, na siyo sharti mwanamume kumwoa mama yake mtoto aliyenasibiwa kwa mwanamume yule.
Na miongoni mwa masharti ni kuwa mtoto awe kutokana na manii ya mzinifu tu, na kutokana na hivyo inathibitisha kwamba mwanamke mzinifu hakuwa na zaidi ya mwanamume mmoja tu.
Suala hili kwa upande wa kifiqhi linaonesha usahihi zaidi wa mtazamo wa mwisho wa wanavyuoni wa umma, lakini iliyokubaliwa ni kwamba uamuzi huondoa mgogoro, na fiqhi ya kisheria imechagua madhehebu ya wanavyuoni wa umma katika suala hili. [Rejea: Mausuatul fiqh walqadhaa fi Al-Ahwal Al-Shakhsiyah kwa Mshauri Muhammad Azmi Al-Bakri 3/521, Dar Mahmoud]; ilitajwa katika marekebisho ya Sheria ya familia nambari ya (100) kwa mwaka 1985 kwamba hukumu za kisheria zinazohusiana na familia zinahukumiwa kwa mujibu wa rai iliyochaguliwa na madhehebu ya Abu Hanifa, isipokuwa kwa kile kilichotengwa na hilo, na mtazamo ulio ni sahihi zaidi ni mtazamo wa wanavyuoni wa madhehebu wa Abu Hanifa ambao ni kutothibitishwa kwa nasaba.
Hata hivyo, inawezekana – katika hali ya swali hili – kuhibitisha nasaba pamoja na kutopinga kwa hukumu za mahakama. Hivyo, miongoni mwa masharti ya usahihi wa kukiri kwa nasaba kwa mujibu wa wanavyuoni wa umma ni kwamba mwanamume aliyekiri asiseme kuwa mtoto wake amezaliwa kutokana na uzinzi, kama hali hii, hivyo kukiri kwake kulikuwa sahihi na nasaba imethibitishwa na athari zake zimepitishwa, lakini tulichagua hukumu hii katika suala hili, kwa sababu masahaba wameiunga mkono hukumu hii kwa vitendo vyao, na hakuna upinzani na masharti yaliyowekwa na mwenye kusema kwa kuthibitishwa kwa nasababu kutokana na mzinifu, hasa baada ya toba yao na nia yao ya kuoana kwa ajili ya kusitiri. Aidha, tatizo hili linategemea maana kadhaa zinazoingiliana, miongoni mwao ni hifadhi ya nasaba, kutunza heshima na usafi wa moyo, na miongoni mwayo pia: kusitiri na kustahi, pamoja na: kuhamasisha watu watubu na kuwapendezesha toba, pamoja na: kumtunza mtoto aliyezaliwa kutokana na uzinzi kutokana na kupoteza maumivu katika uhai wake kwa sababu ya nasaba yake kwa mama yake, lakini inaonesha kwamba kuingiliana kwa maana hizi na utata wake katika hali kama hizo hufanya ushauri wa kuthibitishwa nasaba katika hali kama hizo kuwa bora zaidi, hali ambayo inahitaji Fatwa kwa kila kesi kwa mujibu wa hali yake ambayo humfanya Mufti awe na uweza wa kuirejea kanuni ya Istihsan kwa asili ya kawaida.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas