Hukumu ya Kuthibiti Uharamu kwa Kuteremsha Maziwa ya Kunyonywa kwa Njia ya Madawa au kwa Vifaa Vilivyotengenezwa.
Question
Je uharamu unathibiti kwa kunyonya maziwa kama utokaji wa maziwa hayo ya mama umesababishwa na madawa au mfano wake, na wala sio kwa sababu ya uzazi? Na je, Hukumu yake inakuwa sawa hata kama mwenye maziwa sio mke, kama vile Bikira au mwanamke aliyeachwa?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Uharamu wa ndoa kwa kunyonya ni kama vile uharamu unaotokana na nasaba, na hiyo ni kwa ajili ya Hadithi iliyopokelewa na Maimamu wawili kutoa kwa Ibn Abbas R.A, kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Yanayoharamika kwa kunyonya ni sawa na Yanayoharamika kwa nasaba". Na vile vile kwa kuwa kunyonya kunasababisha kujuzu kukaa peke yao (mtoto wa kike na wa kiume) na kutazama bila ya kuingia hukumu nyingine ya nasaba kama vile kurithi, gharama za matumizi, uwalii juu ya nafsi na mali, na yote ambayo hayathibiti kwa kunyonya.
Sheikh wa Uislamu Zakarita Al Answariy anasema katika kitabu cha: [Asniy Al Matwalib 415/3, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]; "Na athari yake (yaani kunyonya) ni uharamishaji wa ndoa kuanzia mwanzo na kudumu, na kujuzu kumwangalia na kuwa naye faragha na kutoutengua udhu kwa kumgusa, na kuwajibisha fidia na kuodoshwa kwa mahari, bila ya uwepo wa hukumu zingine za nasaba, na gharama za matumizi na kumwachia huru mtumwa na kutoweka kwa kisasi na kuurudi ushahidi.
Na hakuna hitilafu baina ya wanazuoni kwamba wanakuwa haramu watoto wa kike kwa mtoto wa kiume aliyenyonya nao kama wanavyokuwa haramu kwa nasaba. Na wanawake hao ni saba waliotajwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu} [AN NISAA 23].
Mnyonyeshaji anakuwa haramu kwa mtoto aliyemnyonyesha kwani huyo ni mama yake, na baba zake na mama zake kwa nasaba au kwa kunyonya pamoja au kwa kunyonya mababu na mabibi zake, na watoto wake kwa kunyonya kama vile watoto wake kwa nasaba, kwani watoto hao ni ndugu zake wa kiume na wa kike; Wawe ni katika wenye maziwa –aliye ni mume wa mwanamke anayenyonyesha ambaye mume huyo alikuwa sababu ya kutoka maziwa– au mwingine na hiyo, iwe ni yule aliyetangulia kuzaliwa kwake au kuzaliwa kwake kulitokea baadaye kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na dada zenu kwa kunyonya} [AN NISAA 23].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akauthibitishia uharamu na undugu baina ya binti wote wa mnyonyeshaji na baina ya aliyenyonya siku zote, bila ya kutenga baina ya dada ua kaka, na binti wa binti zake au binti wa mtoto wake wa kiume hata wakishuka chini. Na dada zake na kaka zake, kutoka nasaba au kunyonya kwa shangazi zake au khalati zake, na baba wa mwenye maziwa; babu wa aliyenyonya, na kaka yake; amu yake, na kadhalika waliobakia miongoni mwa ndugu wa mwenye maziwa kwa kupima huko; basi mama yake ni nyanya yake, na watoto wa dada zake na kaka zake ni amu zake na shangazi zake, kwa yalitangulia kwamba uharamu unaendelea kwa asili za (babu zake) mwenye maziwa na vizazi wake.
Na inashurutishwa ili uharamu upatikane kwa kunyonya ni kuwa mtoto awe hajafikia miaka miwili, na iwapo atafikia miaka miwili basi kunyonya kwake hakutaathiri na kusababisha uharamu. Na hiyo kwa ajili kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wa wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha} [AL BAQARAH 233]. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajaalia hiyo miaka miwili ni utimizi wa kunyonya, na hakuna kitu baada ya kutimizia unyonyeshaj. [Badai' As Swanai' 6/4, Ch. Al Maktabah Al Elmiyah].
Na kwa iliyopokelewa na Al Bukhariy na Muslim kutoka kwa Aisha Mama wa wanaamini R.A., kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Hakika mambo yaliyo ni kwamba kunyonya kunatokana na njaa". Na kwa iliyopokelewa na At Termiziy na akasema kuwa Hadithi hiyo ni Hassan sahihi, kutoka kwa Umm Salama R.A., kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Haiwi haramu kwa kunyonya pamoja isipokuwa kwa kufika maziwa yaliyoingia kwenye utumbo katika maziwa na hali hii ikawa imetokea kabla ya mtoto kuwa mtambuzi".
Na hayo ni madhehebu ya jamhuri ya wanazuoni, Imamu At Termiziy baada ya kupokelea Hadithi iliyotanguliza, [450/3, Ch. Al Halabiy]. "Na kuifuata hiyo kwa wengi wa wanazuoni miongoni mwa maswahaba wa Mtume S.A.W., na wengineo, kwamba kunyonya hakuharimishi isipokuwa iliyokuwa kabla ya kutimiza miaka miwili, na iliyokuwa baada ya miaka miwili kamili haiharmishi kitu chochote.
Imamu An Nawawiy amesema katika sherehe yake kwa kitabu cha: [Sahihi ya Muslim 30/10, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy]: Na wengi wa wanazuoni miongoni mwa maswahaba na wafuasi na wanazuoni wa miji walisema hata sasa; hauthibiti isipokuwa kwa kunyoya aliyekuwa chini ya miaka miwili. Isipokuwa Abu Hanifa akasema: miaka miwili na nusu, na Zaffar akasema: miaka mitatu, kutoka kwa usimulizi wa Malik akasema: miaka miwili na siku kadhaa.
Na inashurutishwa pia ili kupatikana uharamu: ni kuwa idadi ya kunyonya ni mara tano zilizo tofauti au zaidi, na idadi iliyo chini ya mara tano haiathiri chochote katika uharamishaji, kwa yaliyopokelewa na Muslim Kutoka na Aisha R.A. akasema: Ilikuwa miongoni mwa zilizoshuka kutokana na Qur'ani "(Kunyonya mara kumi zinazoeleweka kunaharamisha), kisha hukumu hii ikafutwa na kuwa (mara tano zinazojulikana), Basi Mtume S.A.W. alifarika dunia na Nazo katika yanayosomwa kutoka katika Qur'ani.
Na Sheikh wa Uislamu Zakariya Al Nswariy wa Kishafiy akasema katika kitabu cha: [Asni Al Matwalib Sharhu Rawdh At Twalib 417/3]; "Na hakuna athari kwa aliye chini ya unyonyeshaji wa tano, Muslim akapokelea kutoka kwa Aisha R.A. akasema: (Ilikuwa miongoni mwa iliyoshuka kutoka Qur'ani "(Kunyonya mara kumi zinazoeleweka kunaharamisha), kisha hukumu hii ikafutwa na kuwa (mara tano zinazojulikana), Basi Mtume S.A.W. alifarika dunia na Nazo katika yanayosomwa kutoka katika Qur'ani. Kwa maana kuwa hukumu zake mnasomewa au wanazosoma wale ambao hawajafikiwa na kufutwa kwake kwa kuwa karibu nayo, na tegemeo katika idadi ni mazoea yanayojulikana.
Na Imamu Ar Ramliy amesema katika kitabu cha: [Nihayat Al Muhtaaj 176/7, Ch. Mustafa Al Halabiy]; "Na sharti ya unyonyeshaji unaoharamisha ni kunyosha mara tano au vyakula kama mfano mikate au unga laini au baadhi ya hivyo, kwa Hadithi ya Muslim kutokana na Aisha R.A., katika hiyo. Na usomaji huu wa nadra unatumiwa kama hoja katika hukumu mbali mbali kama Hadithi moja katika hoja inayotegemewa, na hekima ya mara tano: ni kuwa viungo vya hisia ambavyo ndivyo sababu ya kutambua pia, na kuvidhibiti kwa njia ya mazoea, kwani haikuwahi kupokelewa kwake uthibiti kwa upande wa lugha au upande wa sharia.
Na mwanachuo mkuu Al Khatweb As Sherbiniy akasema katika kitabu cha: [Mughniy Al Muhtaaj 149/5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]; "Na ni wajibu katika ushahidi wa kunyonya pamoja kuukumbuka muda ambao kunyonya huko kulitokea, nao ni kabla ya mtoto kufikia miaka miwili katika kunyonya huko, na kukumbuka pia idadi ya kunyonya, ambayo ni mara tano, na lazima aseme: mara tano hizo zilikuwa tofauti; kwani watu wengi – kama asemavyo Al Adhraiyu – hawajui kuwa kutoka kwenye ziwa na kwenda kwenye lingine au mtoto kusita kunyonya kwa ajili ya kucheza au kupumua na mfano wa hayo na kisha kurejea tena na kuendelea kunyonya huhesabika kuwa ni mara moja".
Na uharamu unatokea kwa maziwa bila ya sharti la ndoa kwani sababu hapo katika kuharamisha ni usehemu wake, kwa maana kuwa sehemu ya mama mnyonyeshaji imekuwa sehemu ya mtoto aliyenyonya.
Asarkhasiy akasema katika kitabu cha: [Al Mabsuotw 132/5, Ch. Dar Al Maarifah]; 'Tuliambiwa kutoka kwa Mtume S.A.W., kwamba akasema: Yanayoharamika kwa kunyonya ni sawa na yanayoharamika kwa nasaba. [Ilipokelewa na Al Bukhariy na Muslim kutoka Hadithi ya Ibn Abbas, na Urwah akataja kutoka kwa Bibi Aisha R.A, Hadithi hiyo basi akasema: Yanayoharamika kwa kunyonya ni sawa na yanayoharamika kwa uzawa, [Inapokelewa na Muslim].
Na hiyo ndani yake kuna dalili ya kuwa kunyonya pamoja ni katika sababu za kuharamisha, na kwamba kuko kama nasaba katika kuthibiti kwa uharamu, kwani kuthibiti kwa uharamu ni kwa ukweli wa kuwa sehemu au kufanana kwake na sehemu, na katika kunyonya pamoja kuna mfanano wa kuwa sehemu kwa yale yanayotokana na maziwa ambayo ni sehemu ya binadamu katika kuotesha nyama za mwili na kukuza mifupa.
Na Mtume S.A.W, akaashiria kwa hayo, basi akasema; 'Unyonyeshaji ni ulioiotesha nyama za mwili na kukuza mifupa", imetolewa na Ibn Abdulbar katika kitabu cha: [At Tamheed] kutoka Hadithi ya Abdullahai Bin Masoud, na katika Hadithi hiyo kwamba uharamu kwa njia ya kunyonya pamoja kama unavyothibiti kwa upande wa akina mama unathibiti pia kwa upande wa akina baba, na baba ni mume aliyesababisha kutoka kwa maziwa ya mama kwa kukutana naye kimwili. Basi Mtume S.A.W, anamfananisha na nasaba katika uharamu, na uharamu huo wa nasaba unathibiti katika pande zote mbili na vile vile kwa kunyonya.
Na hayo kwa Hadithi ya Omrah kutoka kwa Bibi Aisha R.A, amesema: Mtume S.A.W., alikuwa nyumbani kwangu, basi nilisikia sauti ya mwanamume anaomba idhini kwa Hafswah R.A., basi nikasema: huyo ni mwanamume anaomba idhini katika nyumba yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Basi Mtume S.A.W. akasema: simuoni isipokuwa ni Fulani – ni ami wa Hafswa kwa kunyonya, nikasema: kama Fulani angekuwa ami yangu kwa kunyonya pamoja, na yuko hai, je angeingia katika hili? Mtume akasema: Ndio, kwa kunyonya kinaharamika kila kilichoharamika kwa uzawa". [Ilipokelewa na Al Bukhariy]
Na katika Hadithi nyingine kutoka kwa Bibi Aisha R.A., akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika kuwa Aflah Bin Abi Qai'ees anaingia na mimi nina nguo hafifu, basi Mtume S.A.W. akasema: Ataingia kwako kwani yeye ni ami yako kwa kunyonya pamoja na hawezi kuwa isipokuwa kwa kuyazingatia maziwa ni ya baba, na maana iliyomo ni kuwa sababu ya maziwa haya ni kitendo cha kukutana kimwili, na uharamu uliojitokeza unathibitika kwa pande zote mbili kama uzazi (uzawa).
Mwanachuoni mkubwa Al Qarafiy akasema katika kitabu cha: [Al Frouq 121/3, Ch. Alam Al Kutub]; Na kunyonya kumewekwa kwa sababu ya kuharamisha ni kuwa sehemu ya mama mnyonyeshaji ambaye ni maziwa, na yamekuwa sehemu ya mtoto aliyenyonya kwa kumlisha maziwa hayo, na kuwa kwake katika viungo vyake, na hali hii ikafanana na maji ya mbengu na mwili wake kwa kumbebesha mimba mama katika nasaba, kwa kuwa wawili hawa ni sehemu ya pande mbili.
Na mhakikishi Ibn Hajar Al Haiytamiy amesema katika kitabu cha: [Tuhfatu Al Muhtaaj 284/8, Ch. Dar Ihyaa At Turaath Al Arabiy]; "Na sababu ya kuharamishwa ndoa kwa kunyonya pamoja ni kwa kuwa maziwa ni sehemu ya mama mnyonyeshaji, na yamekuwa sehemu ya mtoto aliyenyonyeshwa na kwa hivyo inafananishwa na mbegu yake ya uzazi katika nasaba, na kwa kuishia kwake katika hilo haikuthibiti kwake hukumu zozote isipokuwa uharamu huo, bila ya kuelekea katika urithi na uachiaji huru mtumwa na kuondoka kwa hukumu ya Kisasi na kuondoka kwa hukumu ya ushahidi".
Na katika hili, kinachotazamwa kisheria ni hali maalumu ya kunyonyesha bila kushurutisha sababu maalumu, iwe sababu hiyo ni uzazi au dawa, au chombo au homoni, kwa kuwa tu kuthibitika na utokaji wa maziwa umetuka. Na kwa hukumu hiyo, Jamhuri ya Wanazuoni pamoja na kuwepo tofauti baina yao katika hali ya mwanamke kuwa miaka tisa au chini ya hapo, basi wao hawashurutishi kwa kuthibiti uharamu wa maziwa ya mwanamke ni kutanguliwa na ujauzito, na kwa hiyo maziwa ya bikira ambaye hajakutana kimwili na mwanaume na wala hajawahi kubeba ujauzito yanakuwa haramu, na kwa ujumilisho wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mama zenu walio kunyonyesheni} [AN NISAA 23]. Na kwani ni maziwa ya mwanamke basi uharamu uliyahangaikia.
Ibn Abdeen akasema katika kitabu cha: [Rad Al Muhtaar 408/2, Ch. Ihyaa At Turaath]; "Na maziwa ya Mwenye Bikira binti wa miaka tisa yanaharamisha lakini chini ya miaka tisa hayaharamishi".
Ibn Roshd akasema katika kitabu cha: [Al Muqademat]: "Uharamu unatuka kwa maziwa ya bikira ambaye hajazaa, na hata kama bila ya kuingiliwa ikiwa ni maziwa au maji maji ya njano". [Kwa njia ya Hashiyat Ad Dosouqiy ala Asharhi Al Kabeer 502/2, Ch. Dar Al Fikr]
Sheikh Taqiy Adeen Al Haswaniy Ashafiy akasema katika kitabu cha: [Kefayatu Al Akhbaar 85/2, Ch. Muswtafa Al Halabiy]; Sharti la tatu: kuwa kwake na uwezekano wa kutoka kwa uzazi, na kama itaonekana maziwa kwa mtoto aliye chini ya miaka tisa basi si haramu, na kama akiwa binti wa miaka tisa yanaharamisha, hata kama hakuhukumiwa kuwa ni mwenye kubaleghe, kwani uwezekano wa kubaleghe upo, na kunyonya pamoja ni kama nasaba basi inatosha ndani yake kuwa na uwezekano huo, na hakuna tofauti baina ya mnyonyeshaji kama mke au hapana, au kuwa kwake bikira au hapana, na imesemwa pia kuwa haiwi haramu kunyonya maziwa ya bikira, lakini ya sahihi ni yanaharamisha na Shafiy ameyataja".
Na iwapo atamwoa binti huyo baada ya kunyonya, basi mke wake anakuwa mke wa mama wa mnyonyeshwaji na wala sio baba yake kwa kuwa yeye hakusababisha chochote katika maziwa na wala haisihi maziwa hayo yakawa ni ya baba, na kwa hivyo huyo sio baba kwa mtoto aliyenyonyeshwa.
Na hukumu ya kunywa dawa au chochote kwa ajili ya kutoa maziwa hiyo kiasili ni halali kama hakusabishi matatizo yoyote, na kama kuna madhara basi ni haramu. Na msingi wa kifiqhi unaopitisha hukumu hii unasema: Kwamba madhara yanaondoshwa. Na asili yake ni iliyopokelewa na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas R.A., wote wawili, kuwa Mtume S.A.W., akasema: "Hakuna madhara na wala kudhuru".
Na kutokana na maelezo hayo yaliayotangulia: Kwa hakika uharamu utathibiti kwa njia ya kunyonya pamoja hutokea kwa kunyonya maziwa yatokayo kwa mama, hata kama sababu ya kutoka kwa maziwa hayo ni dawa au mfano wake na wala haikuwa sababu ya kutoka kwake ni uzazi.
Na mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.