Safari ya Hija ya Mwanamke Bila ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Safari ya Hija ya Mwanamke Bila ya Mume au Ndugu wa Karibu.

Question

 Mwanamke aliyeolewa anataka kuiteleleza Hija ya faradhi, lakini hayuko na mume wala ndugu wa karibu, Je, inajuzu kwake kuhiji pamoja na marafiki wa kike na wa kiume, anaowajua vizuri? Na kwa kujua kuwa mume wake hakatazi hivyo.

Answer

 Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote zake, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Aali zake na Masahaba wake na waliomfuata, na baada ya hayo…
Safari katika lugha ya Kiarabu ni: kwenda umbali mrefu, kinyume na umbali mfupi, ambapo hauzingatiwi safari. [Al-Misbah Al-Muniir: kidahizo cha: Sa Fa Ra, Uk. 278, Ch. ya Al-Maktabah Al-Ilmiyah].
Na katika istilahi ya Sharia, safari ni: Kutoka kwa nia ya kwenda umbali wa kupunguza Swala kisheria, au zaidi yake. [At-Ta’rifaat na Al-Jurjaaniy, uk. 52, Ch. ya Al-Matba’ah Al-Khairiyah; Al-Kuliyaat, na Abul-Baqaa’ Al-Kafawiy, uk. 511, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah; Jamii’ Al-U’luum Fi Istilahaat Al-Funuun, na AlKadhi Abdun-Nabii Ibn Abdir-Rasuul Al-Ahmananakriy: 2/123, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na kwa hivyo kutokana na tofauti kati ya wanazuoni kuhusu umbali wa kupunguza Swala kisheria; wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy wanaona kuwa: ni umbali wa kwenda muda wa siku tatu, namna ya kwenda kwa ngamia au kwa miguu; na wafuasi wa madhehebu ya Malik, Shafi, na Handbali wanaona kuwa ni: kwenda muda wa siku mbili bila nyusiku, au nyusiku mbili bila ya mchana, au siku moja na usiku mmoja tu.
Na maana ya ndugu wa karibu katika lugha ni: asiyejuzu kwake kumuoa mwanamke. Al-Azhariy anasema: ndugu wa karibu ni yule wa katika ukoo, ambaye haijuzu kwake kumuoa. [Al-Misbah Al-Muniir Fi Ghriib Ash-Sharh Al-Kabiir, na Al-Fayumiy, Kidahizo: Ha Ra Ma, Uk. 132].
Na katika istilahi ya Sharia (Ndugu wa karibu) ni yule anayejuzu kusafiri na kuwa naye peke yenu, na aliye haramu kwake kuoana naye, na uharamu wake ni wa kudumu na kwa sababu ya halali, na kauli yetu (kwa milele) kwa kuepusha dada ya mke, shangazi wake, na mama mdogo wake, na kauli yetu (kwa sababu iliyo mubaha) kwa kuepusha mama mkwe aliyeingiliwa kwa shubha, kwa sababu mama wa mke katika hali hii siye mharimiwa kutokana na tafsiri hii, na kwa sababu kuingilia kwa shubha hakuelezwi kuwa mubaha; na kauli yetu (uharamu wake) kwa kuepusha (Mulaa’anah) kwa sababu uharamu wake sio kwa uharamu mwenyewe, bali kwa ajili ya ubaya wake. [Mwisho kwa maelezo machache ya: Ihkaam Al-Ahkaam Sharh U’mdat Al-Ahkaam, na Ibn Daqiiq Ali’id: 2/57, Ch. ya Matba’at As-Sunnah Al-Muhammadiyah].
Na rai iliyochaguliwa kwa kutoa fatwa kuhusu kusafiri kwa mwanamke kwa ajili ya kuitekeleza Hija ya faradhi, bila ya kuwepo mume au ndugu wa karibu ni kuwa: inajuzu kwake kusafiri safari ya amani, pamoja na wanawake wenzake waaminifu.
Kuna dalili yake ilivyopokelewa na Imamu Bukhariy katika kitabu chake, kutoka kwa Adiyy bin Hatim alisema: nikiwa na Nabii SAW., mara mtu mmoja akamwendea, akalalamikia umaskini, kisha akaja mtu mwingine, akamlalamikia ujambazi, Mtume SAW, akasema: “Eew Adiyy, je , umeiona Hirah (ni mji ndani ya Iraqi) ? Nikajibu: sijaiona, lakini nimeambiwa. Mtume SAW, akasema: ungekuwa na umri mrefu, utaona mwanamke mwenye kusafiri akitokea Hirah, mpaka akaizunguka Kaabah, bila ya kuogopa kitu cho chote isipokuwa Mwenyezi Mungu…” Akasema Adiyy: niliishi mpaka nikamwona mwanamke anayesafiri akiondoka kutoka kwa Hirah hadi kuzunguka Kaabah bila ya kuogopa cho chote isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Na hii inaonesha kuwa: inaruhusiwa; kwa sababu kama isingelikuwa ruhusa, basi isingelisifiwa na Uislamu, Al Umraniy alisema hivyo katika kitabu cha Albayaan, Sharh Almuhadhab, katika Madhehebu ya Imam Shafiy: [3/35, Chapa ya Dar Alminhaj].
Hata hivyo, haisemwi kuwa Hadithi ya Adiyy haionyeshi kuwa mwanamke hasafiri bila ya ndugu wa karibu, kwa sababu Mtume S.A.W., katika Hadihi hii alituambia kuwa jambo kama hilo litatokea, halafu limekwisha tokea, na haiwajibishi kuwa inajuzu. Mfano wake ni kama alivyotuambia Mtume S.A.W., kuwa watakuwa matapeli na waongo duniani, lakini haya hayamaanishi kuruhusiwa.
Kwa sababu, Hadithi hiyo inaashiria kulaani matokeo mabaya, kinyume cha hayo, Hadithi ya Adiyy inaashiria kusifu, fadhila, na utukufu wa Uislamu na kunyanyua bendera yake. kwa hiyo, haiwezekani kuifahamu kimakosa .
Al-Hafidh Ibn Hajar anasema katika kitabu chak cha: [Fath Al-Bariy 4/76, Ch. ya Dar Al-Maarifah]: “Pana maelezo kuwa haya yanaashiria habari tu wala hayamaanishi ruhusa. Lakini kwa kujibiwa kwa maelezo haya ni kwamba habari hii imekuja katika muktadha wa kusifu, na kunyanyua bendera ya Uislamu mahala pote, na hayo kweli huashiria kuruhusiwa”. [Mwisho].
Pia kuna dalili ilivyopokelewa na Imamu Bukhariy katika kitabu chake kuwa Bwana wetu Umar Ibn Al-Khattab RA, amewaruhusu wake za Mtume S.A.W., kwenye Hija yake ya mwisho, akawatumia Uthman Ibn A’affan na Abdur-Rahman Ibn A’auf pamoja nao.
Na mwelekeo wa dalili yake, kama alivyosema Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu chake [Al-Fat-h: 4/76] ni “Makubaliano ya Umar, Uthman, Abdur-Rahman Ibn A’auf, na wake za Mtume S.A.W., kuhusu hivyo, pamoja na kutowakataza Masahaba wengine kuwa hivyo ni sahihi’. [Mwisho].
Imamu Al-mawardiy katika kitabu chake Al-Hawiy cha Fiqhi ya Imam Shafiy [4/364, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, 1414 H., 1994] anasema: “Imepokelewa na Omar Ibn Al-Khatwab R.A, akisema: pangeni Hija kwa vizazi hivi (anakusudia wanawake) na msile haki zao wala kupoteza masilahi yao, na hii ni amri kwa wanawake wahiji na kutokatazwa, na kutoshurutisha ndugu wa karibu pamoja nao”. [Mwisho].
Na haisemwi kuwa wake za Mtume S.A.W, ni mama wa waumini wote, na kwa hiyo inajuzu kwao wasafiri pamoja na ye yote kati yao, kwa sababu waumini wote ni ndugu wa karibu wa wakeze Mtume; kwa sababu hali ya kike ya wakeze Mtume hailingani na mama mzazi kuhusu hukumu zake zote; kwa mfano wakeze Mtume wanaamrishwa kuvaa hijabu mbele ya waumini wote, kinyume cha mama mzazi, na hakuna mirathi kati ya wakeze Mtume na waumini kwa ujumla, kwa mujibu wa hali hiyo ya kike, na kwa kuongeza kuwa hukumu muhimu zaidi kuhusu wakeze Mtume, ni kutojuzu waolewe na mtu ye yote kati ya waumini baada ya kufa kwa Mtume S.A.W.
Na miongoni mwa dalili ni kanuni ya Qiyasi ya safari ya mwanamke kutoka kwa nchi ambayo ndani yake hawezi kudhihirisha Uislamu wake, na kuhamia nje yake, katika hali hii haishurutishwi kuwepo ndugu wa karibu; kwa sababu uhusiano kati ya hali hizi mbili – Uhajiri na Hija – kuwa zote ni safari zinazowajibika.
Na rai tuliyoichagua ni Madhehebu ya wafuasi wa Imam Malik na Imamu Shafiy, kuhusu madhehebu ya Imamu Malik, Hija ya wajibu kwa mwanamke inashurutishwa kuwepo mume au ndugu wa karibu, na kama hakuwepo basi analazimika kutoka kwa marafiki waaminifu.
Sheikh Kharashiy katika Sharhu yake ya Mukhtasar Khalil [2/287, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Maana ya hayo kuwa marafiki waaminifu ni kutosha na ni mbadala ya ndugu wa karibu au mume katika Hija ya faradhi na yasiyo Sunna; yaani katika hali ya kutowepo mume na ndugu wa karibu, au kukataza kwao au kutoweza kwao”. [Mwisho]
Wafuasi wa madhehebu ya Imam Shafiy walifuata mwelekeo wa kuwa: inashurutishwa katika uwajibikaji wa Hija ya mwanamke, inashurutishwa kuwepo mume au ndugu wa karibu au marafiki waaminifu wa kike; na katika Al-Minhaaj, na Sharh yake na Sheikh Al-Khatib Ash-Shirbiniy [Mughniy Al-Muhtaj: 2/216, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]: “katika uwajibikaji wa Hija ya mwanamke inashurutishwa, zaidi ya ilivyotangulia, kuwepo mume au ndugu wa karibu wa ukoo au nyingineyo au wanawake waaminifu”. [Mwisho]
Na hii ni madhehebu ya Bi Aisha R.A., na pia ni kauli ya Ataa’, Said Ibn Jubair, Ibn Siriin, Al-Awzai’iy, Dawuud Adh-Dhahiriy na wafuasi wake, na pia ni chaguo la Sheikh Taqiy Ad-Diin Ibn Taimiyah; ambapo Al-mardawiy katika kitabu cha Al-Insaaf [3/311, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] ameinukuli naye, na Ibn Muflih katika kitabu cha Al-Furuu’ [3/236-237, Ch. ya A’alam Al-Kutub]: “Kila mwanamke mwenye hali ya usalama anahiji bila ya ndugu wa karibu, na akasema: hiyo ni ya kawaida katika kila safari yenye taa”. [Mwisho]
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy na Hanbal walielekea kushurutisha kuwepo ndugu wa karibu, na kuwa haijuzu safari ya mwanamke katika hali hii bila ya ndugu wa karibu. Hapa kuna tofauti kati ya pande mbili: wafuasi wa madhehebu ya Hanbal wanaona wafuate rai kukataza kwa uwazi, lakini Imamu Abu Hanifa anaona kuwa katazo linahusu hali ya safari ndefu na siyo fupi, na safari fupi ndiyo inayopungua na masafa maalum.
Na hii pia ni kauli ya Al-Hassan, An-Nakhi’iy, Ibn Al-Mundhir, na wenye maoni, na waliisema pia Ath-Thawriy, Al-Aa’mash, na Abu Thaur.
Walitoa dalili nyingi ambazo zinakataza kusafiri bila ya ndugu wa karibi, miongoni mwake ni:
Ilivyopokelewa katika vitabu viwili vya Sunna, kutoka kwa Abu Huraira R.A, alisema: Mtume S.A.W, alisema: “Siyo halali kwa mwanamke wa kuamini kwa Allah na Siku ya mwisho, asafiri safari ya muda wa siku moja na usiku mmoja, na hakuwa na ndugu wake wa karibu”.
Walisema: hii ni jambo la kawaida katika aina zote za safari, na Mtume S.A.W, hakutofautisha kati ya safari ya Hija na safari nyingine.
Hii inajadiliwa ama kuwa ni ya kawaida, basi inaambatana na dalili zilizotajwa hapo juu, au inakusudiwa kwa safari za biashara, ziara, Hija ya sunna, na aina nyingine za safari isipokuwa Hija ya Faradhi, au inakusudiwa kwa hali ya njia isiyo ya usalama.
Imam Nawawiy katika kitabu cha Al-Majmuu’ Sharh Al-Muhadhab [8/313, Ch. ya Al-Matbaa’ah Al-Muniriyah] anasema: “Jawabu kuhusu Hadithi walizozihojia ni kwa pande kadhaa: Kwanza: jawabu la Sheikh Abu Hamid na wengineo kuwa ni za kawaida, na zinazoambatana na tulivyotaja. Pili: inakusudiwa kuwa safari ya biashara, ziara, Hija ya sunna, na safari nyingine isipokuwa safari ya Hija ya faradhi. Tatu: ilivyotajwa na Kadhi At-Taiyb kuwa: inakusudiwa kwa hali ya njia isiyo ya usalama”. [Mwisho]
Walitoa dalili pia ilivyopokelewa katika vitabu viwili vya Sunna, kutoka kwa Ibn Abbas R.A, kuwa alimsikia Mtume SAW, akisema: “Mtu asikae na mwanamke faraghani isipokuwa pamoja na ndugu wa karibu, wala mwanamke asifunge safari isipokuwa pamoja na ndugu wa karibu, na mtu mmoja akamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimejiandika katika vita fulani, na mke wangu atakwenda Hija, akasema Mtume: Nenda kuhiji pamoja na mkeo”.
Al-Jassas mfuasi wa madhehebu ya hanafiy katika kitabu cha: [Ahkaam Al-Kuran; 2/38, Ch. ya dar Al-Fikr] kwa maelezo yake ya Hadithi hii anasema: “Hii inaonesha kuwa kauli yake: “mwanamke asifunge safari isipokuwa pamoja na ndugu wa karibu” inaambatana na mwanamke kwa pande tatu: Kwanza: mwenye swali amekwishafahamu hivyo kwake, kwa hiyo amemuulizia mkewe ambaye anataka kuhiji, na Mtume S.A.W, hakukataza hivyo kwake, basi hii inaonesha kuwa muradi wake S.A.W, ni wazi katika Hija na safari nyingineyo. Pili: kauli yake: “Nenda kuhiji pamoja na mkeo” ni habari kutoka kwake kuwa safari hii ni kwa ajili ya Hija, katika kauli yake: “asifunge safari isipokuwa pamoja na ndugu wa karibu”. [Mwisho] Tatu: Amri yake SA.W, kwa kuacha kwenda vita kwa ajili ya hukiji pamoja na mkewe, basi ingeliruhusiwi kwa mwanamke kuhiji bila ya ndugu wa karibu, asingelimuamuru mwanamume kuacha kwenda vita, kwani vita ni faradhi na siyo Sunna, na hii ni dalili pia kuwa Hija ya mwanamke huyu ilikuwa ni ya faradhi na siyo ya Sunna, kwa sababu ingelikuwa ya Sunna, asingelimuamuru kuacha kwenda vita iliyo ni ya faradhi kwa ajili ya Hija ya Sunna ya mwanamke; na kwa upande mwingine, Mtume S.A.W, hakumuulizia: je, Hija ya mwanamke ni ya faradhi au ya Sunna? na hii ni dalili kuwa hukumu ni moja ya hali hizi mbili, kwa upande wa kutojuzu kutoka kwake bila ya kuwepo ndugu wa karibu; na hii ni dalili kuwa kuwepo ndugu wa karibu ni sharti la kupata uwezo wa kuitekeleza Hija”. [Mwisho]
Na hayo yaliyotangulia ni mwelekeo wa dalili ya Hadithi.
Imam Ibn Hazm katika kitabu cha: [Al-Muhalla Bilathaar: 5/25, Ch. ya Dar Al-Fikr] alijadili maneno haya kuwa: kukataza kwa Mtume S.A.W., mwanamke asafiri bila ya kuwepo ndugu wa karibu, hayo ndiyo husemwa kwanza, kisha mwanamume alimuulizia mkewe ambaye alitoka kwa ajili ya kuitekeleza Hija bila ya ndugu wa karibu wala mume, na Mtume S.A.W, alimuamuru aende na kuhiji pamoja naye, na hakuamuru kumrudishe, wala kusema vibaya kuhusu safari yake kwenye Hija bila yake wala ndugu wa karibu. Na amri ya Mtume S.A.W, kuwa mwanamume aende na kuhiji pamoja na mkewe ni taarifa sahihi na kauli wazi kuwa hakuna shaka ya kuifahamu, kwa hiyo Mtume S.A.W, alikiri safari yake kama alivyoitoka, na kuithibitisha na hakuikataza; kwa mujibu wa hayo faradhi hapa ni ya mwanamume, na kama akihiji pamoja naye, basi atatekeleza wajibu wake wa urafiki, na asingefanya atakuwa mwenye maasi kwa mwenyezi Mungu, na mkewe aendelee kuitekeleza Hija yake, na atoke pamoja na mwanamume au bila yake, au pamoja na ndugu wa karibu au hata bila yake, kama alivyoikiri Mtume S.A.W, na hakuikataza.
Al-Badr Al-A’ainiy katika Sharh yake ya Sahih Al-Bukhariy [U’umdat Alqariy: 7/127, Ch. ya Idarat At-Tiba’ah Al-Muniriyah-Misri] alijibia maneno ya Ibn hazm akisema: “Hakika alisema hivyo kwa kuelekeza madhehebu yake kuwa: mwanamke anaweza kuhiji bila ya kuwepo mume wala ndugu wa karibu, na kama mwanamke ni mwenye mume basi amnalazimika kuhiji naye; na hii ni kinyume na alivyofahamu, kwa sababu Hadithi hii ni hoja dhidi yake, kwa sababu aliposema: nenda pamoja naye na kuamuru kutoka naye, hii ni dalili ya kutojuzu safari yake bila mume au ndugu wa karibu; wakati amemlazimisha kuacha nadhiri yake (ya kwenda vita), kwa sababu safari ya mke ndiyo inayoambatana naye. Na kama ukisema: udhahiri wa Hadithi huonesha kuwa mume au ndugu wa karibu akikataa kutoka pamoja naye katika Hija, atalazimishwa kufanya hivyo, wakati ninyi husema: kama mume au ndugu wa karibu akinyima, hatalazimishwi kufanya hivyo; nilisema: hata ikiwaa hivyo, haidhuru, lakini kusudi letu ni kuthibitisha sharti la kuwepo mume au ndugu wa karinu pamoja na mwanamke, wakati alipotaka kuitekeleza Hija, kuwa hili si jambo la lazima, lakini alitanabahisha kuwa mwanamke hasafiri bila ya mume wake’. [Mwisho]
Na rai hii pia inajadiliwa kuwa: siyo katika Hadithi inavyoonesha kwa yake nguvu kuwa: kuna uharamu wa mwanamke kuhiji bila ya ndugu wa karibu, lakini upeo wa kusudio lake ni kuwa: kuhiji kwa Sahaba huyu pamoja na mkewe ni bora zaidi na kitu kinachopewa kipaumbele kuliko Jihadi, kwa vyo vyote; na kwa sababu kukutana safarini kwa ajili ya kwenda vitani, na safari ya kwenda kuhiji pamoja na mkewe, inaishinda safari ya kuhiji naye; kwa sababu mtu anaweza kuishiriki jihadi nyingine badala ya hiyo, kinyume na Hija pamoja na mkewe.
Hadithi hii imepokelewa kwa matamshi mengine; katika Sunan Ad-daraqutniy, kutoka njia ya Amr Ibn Dinar, kutoka kwa Abu Maa’bad Maula Ibn Abbas, au Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas kuwa alisema: “Mtu mmoja alikuja Madinah, na Mtume SAW, akasema: Umefikia wapi? Akasema: kwa mwanamke fulani. akasema: amekufungia mlango wake? Hakika mwanamke hasafiri kwenda Hija isipokuwa pamoja na ndugu yake wa karibu”
Na Imepokelewa kwa matamshi yanayokaribiana na hayo na Abdur-Razaq katika kitabu chake, Isnadi ya Mursal, kutoka kwa Ibn U’yainah, kutoka kwa Amr Ibn Dinar, kutoka kwa Ikrimah.
Na hii imejadiliwa kuwa iliyohifadhiwa katika Hadithi hii kuwa ni Mursal, kutoka kwa Ikrimah, kama alivyosema hivyo Al-hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Al-Fat-h,] baada ya kutaja mapokezi haya, na vile vile alivyosema Ibn Hazm katika kitabu cha: [Al-Muhalla].
Na kuchukulia makubaliano ya Hadithi iwe ni Marfuu’ au kwa utendaji wa Mursal, hakika sababu ya kukataza katika Hadithi ni: hali ya hofu ya njia na kutopatikana usalama; na kama kupatikana usalama, basi sharti la kuwepo ndugu wa karibu ndilo limeeondolewa.
Wanachuoni walitoa dalili pia kuwa: mwanamke, katika hali hii, akitaka kusafiri ndani ya nyumba za kiislamu, basi haijuzu bila ya kuwepo ndugu wa karibu, mfano wa Hija ya Sunna.
Na hii inajadiliwa kuwa: ni Qiyasi ya Hija ya Sunna, ambayo si wajibu, kinyume na Hija ya faradhi, ambayo ni wajibu.
Kwa mujibu wa hayo: Inajuzu kwa mwanamke kusafiri kwa kuitekeleza Hija ya faradhi pamoja na wanawake wenzake waaminifu, wakati wa kutowepo mume au ndugu wa karibu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas