Utafiti Kukusu Zinaa ya Ndugu za Ka...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utafiti Kukusu Zinaa ya Ndugu za Karibu

Question

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu

Answer

Ufafanuzi:

Maana ya zinaa kilugha ni: Kumwingilia mwanamke bila ya kufunga ndoa kisheria. Taz. Al-Mu’jam Al-Wasiit: Kidahizo: (ZA NA YA).

Na Maana yake ya kisheria ni: kuingiza dhakari kwenye tupu iliyoharamishwa kwa makusudi, bila ya shubha, na tupu yenye kufaa kuingiliwa, na kazi hiyo inaleta adhabu. [Taz. Mughniy Al-Muhtaaj, Sharh Manhaj At-Taalibiin: 4/43, Ch. ya Dar Al-Fikr].

Na walioharamishwa miongoni mwa wanawake na wanaume ni:  Wale ambao ndoa yao ni haramu kutokana na undugu wao wa karibu au ujmaa. [Taz. Al-Misbaah Al-Muniir: Al-Mu’jam Al-Wasiit: Kidahizo: (Ra Ha Ma).

Mjadala hapa unahusu wale waliokatazwa kuwaoa kwa kudumu, na kuna sababu tatu za hilo, nazo ni:

A – Undugu: nao ni: Mama na wajuu yake, binti na wadogo zake, dada, shangazi wa baba, shangazi wa mama, mpwa wa kaka, na mpwa wa dada.

b – Mkwe: ambao ni: Mama wa mke na binti wa kambo ikiwa ataingia mama, mama wa kambo na mkwe.

C - Kunyonyesha, hivyo ni haramu ya kunyonyesha kile kilichoharamishwa kutokana na nasaba. [Taz. Al-Iqnaa’ Fii Hall Alfaadh Abi Shujaa’: 2/416, Dar Al Fikr, Beirut].

Zina ya ndugu za karibu ni uhusiano kamili wa kingono kati ya watu wawili ambao wana uhusiano unaozuia mahusiano ya kingono kati yao kwa mujibu wa Sharia ya Mwenyezi Mungu.

Ukubwa wa kosa la zinaa, na kueleza kuwa ni ya daraja, na kwamba kuifanya na ndugu wa karibu ni moja ya uhalifu mbaya zaidi:

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha zinaa, na hajawahi kuiruhusu katika  Sharia zote, na akaielezea kuwa uchafu, na akasema Mwenyezi: {Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua?}. [AL AA'RAAF: 28]. 

Hapana shaka kwamba zinaa inawadhuru wengine, na kwa sababu hii kiwango cha kosa lake kinatofautiana, na inajulikana kuwa kumdhuru jirani au ndugu wa karibu ni kosa kubwa zaidi kuliko kumdhuru mtu wa mbali, na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasisitiza kutendewa majirani na ndugu wa karibu.

Kwa hiyo, zinaa ya ndugu za karibu ni mbaya zaidi, na kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameikemea ndoa na mama wa kambo zaidi kuliko alivyoikemea zinaa, na ameiwekea adhabu kali ambayo haitofautishi baina ya aliyefunga ndoa na wengine, kulingana na zinaa. Yote haya yanaashiria ubaya wa “zinaa ya ndgugu za karibu”, kwa hiyo ni kitendo kibaya kabisa katika jamii {ila mnyama wa ardhi anaye kula mizizi yake}.

Ibn Hajar Al-Haytami amesema: (Dhambi kubwa ya hamsini na nane baada ya mia tatu: Zinaa, Mungu atuepushe nayo na kwa nyingine kwa fadhila na ukarimu wake) Mola Mtukufu amesema: {Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya}. [AL ISRAA; 32], na pia amesema: {Na ambao wanafanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, washuhudizieni watu wane katika nyinyi. Watakapo shuhudia, basi wazuieni majumbani mpaka wafishwe na mauti au Mwenyezi Mungu awatolee njia nyingine}. [An Nisaa: 15], na pia amesema: {Na wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu. [AN NISAA: 16], na pia amesema: {Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya}. [AN NNISAA: 22]. 

Mwenyezi Mungu alielezea nikaha, ambayo ni zinaa, katika Aya ya mwisho yenye maelezo matatu, na zinaa katika Aya ya kwanza yenye maelezo mawili tu. kwa sababu ya pili ni chafu na mbaya zaidi; Kwa sababu mke wa baba anafanana na mama, hivyo kumwingilia ni miongoni mwa machafu makubwa zaidi, kwa sababu kuingiliana na mama ni miongoni mwa mambo machafu hata mbele ya wajinga wa Ujahili.

Na uchafu ni dhambi mbaya zaidi, na uchukizo unaambatana na dharau, na ni maalumu  zaidi kuliko uasherati, na huu kwa upande wa Mwenyezi Mungu juu ya haki ya mja wake unaashiria upeo wa udhalili na upotevu.

Bali ikasemwa hivyo pamoja na kauli yake: {Na ni njia mbaya}. [An Nisaa: 22], Kwa sababu hayo kabla ya kuharamishwa yalikuwa ni ya kulaumiwa katika nyoyo zao na ni chukizo kwao, Na walikuwa wakiita mwana wa mtu aliyezaliwa na mke wa baba yake awe (Mchukizwa), na kulikuwa mazoea ya baadhi ya makabila ya Waarabu kuwa mtu anamuoa mke wa baba yake, na sera hii ilikuwa ni lazima kati ya Al-Ansaar yaani watu wa Madinah, na ilikuwa halali kwa makubaliano kati ya Makureshi.

Na fahamu kwamba viwango vya ubaya ni vitatu: kiakili, kisharia, na kikawaida, basi (uchafu) ni Ishara ya kwanza, na (uchukizo) ni ishara ya pili, na (njia mbaya) ni ishara ya tatu, na aliyekusanya sifa hizi zote basi amefikia upeo wa ubaya...

Na walikubaliana pamoja kwamba kinachomaanishwa na uchafu hapa ni zinaa, kama ilivyosemwa. Inapingana na yale yanayopokelewa na Abu Muslim, isipokuwa inasemekana kuwa haihesabiwi, na kuitwa uchafu kwa sababu kuongeza ubaya zaidi kuliko mabaya mengi.

Haisemwi kuwa ukafiri ni mbaya zaidi kuliko hilo na pia uuaji, na wala haziitwi moja katika mawili hayo ni uchafu. Kwa sababu tunasema kuwa haifai kuita kila moja katika hayo ni uchafu, lakini ni sahihi kusema kwamba hayakuitwa hivyo.

Na jawabu yake wakati huo ni kwamba kafiri haoni kuwa ukafiri ni kosa ndani ya nafsi yake, wala haoni kuwa ni ubaya, bali ni sawa, na hali kadhalika uuaji ambapo muuaji anajivunia kuufanya, na kufikiria kuwa ni ujasiri.

Ama zinaa kila mwenye kuifanya anaiona kuwa ni uchafu, ni ubaya na ni fedheha hadi mwisho.

Pia, nguvu zinazodhibiti uwezo wa mwanadamu ni tatu: Za kutamka, za hasira, na za matamanio. Ya kwanza imeharibika kwa ukafiri na uzushi na mfano wa hayo, na ya pili ni kwa mauaji na mfano wa hayo. Na mbaya zaidi kati ya hizi tatu ni matamanio, ambayo ufisadi wake umelikuwa ni upotovu mbaya zaidi. Na kwa sababu hii, kitendo hiki kilitajwa kwa jina la uchafu. [Az-Zawajir: 2/212-214, Dar Al-Fikr].

Ar-Ruhaibaniy amesema: (Na) ilijulikana kwamba zinaa (inatofauti) na dhambi yake na uhalifu wake kutokana na vyanzo vyake; na imebainishwa kwa kauli yake (zinaa na mwanamke mwenye mume au maharimu) wake mwenye uhusiano wa damu au kunyonyesha (ni kubwa kuliko zinaa ya asiye na mume au mwanamke wa mbali).

Kwa kuwa kuna kuhusisha kupoteza heshima ya mume, kuharibu kitanda chake, kuunganisha nasaba kwake ambayo haikutoka kwake, na aina nyingine za madhara, ni dhambi kubwa na uhalifu kuliko zinaa ya asiye na mume na mwanamke wa mbali, na (kama mumewe ni jirani, basi ujirani mbaya huongezeka), na kumdhuru jirani ni ubaya wa hali ya juu kabisa, na hilo ni miongoni mwa makosa makubwa, au ikiwa jirani ni ndugu (au jamaa) zake, basi (kukata uhusiano na ndugu na jamaa huongezeka), kwa hiyo dhambi inaongezeka maradufu.

Na imethibiti kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema: “Mtu asiyeepusha mabaya yake na jirani yake hataingia peponi” na hakuna dhambi kubwa kuliko kuzini na mke wa jirani.

Ikiwa jirani hayupo na kutokuwepo kwake ni kwa ajili ya  kumtii Mwenyezi Mungu, kama vile ibada, kutafuta elimu na jihadi, dhambi hiyo inaongezeka maradufu, hata yule aliyezini na mwanamke wa mume aliye vitani katika njia ya Mwenyezi Mungu atasimamishwa mbele ya mume Siku ya Kiyama, na ataambiwa mume: Chukua utakavyo miongoni mwa mema yake. Mtume S.A.W, akasema: (Mnaonaje)?” Maana yake: Je, mnadhani ataachiwa nini baadhi ya matendo yake mema? Amehukumu kuwa anachukua chochote anachotaka kulingana na ukubwa wa haja ya tendo moja la heri, ambapo baba hamwachii mwanawe, wala rafiki hamwachii rafiki yake haki iliyo wajibu juu yake, Iwapo itatokea kwamba mwanamke huyo ana uhusiano naye, basi kukata uhusiano wake wa undugu kunaongezwa kwenye hilo, na ikitokea kwamba mzinzi ameolewa, basi dhambi ni kubwa zaidi.

Akiwa ni mzee, hiyo itakuwa ni dhambi na adhabu kubwa zaidi, naye ni miongoni mwa watatu ambao Mwenyezi Mungu hatasema nao Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, na wataadhibiwa kwa ajili ya hilo.

Likifanyika jambo hilo ndani ya Mwezi Mtukufu au Mji mtukufu au Wakati bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu, kama wakati wa ibada ya Swala na wakati wa kujibiwa dua, basi dhambi itaongezeka. Kwa hiyo,  matokeo ya dhambi na viwango vyake vya kuzidi katika suala la dhambi na adhabu huzingatiwa.

Na kwa kuwa maana ya zinaa iko katika kulawiti, kutokana na ukweli kwamba ni kupenya dhakari katika sehemu iliyokatazwa, n.k., bali ni yenye ubaya zaidi, kwa sababu ni uharamu mkubwa  zaidi kutokana na Sharia na akili. [Mataalibu Ulii An Nuhaa; 6/173-174, Al-Maktab Al-Islaamiy, Damascus, 1961].

Na kutokana na hatari hii na uhalifu wa kutisha, Sharia imemuadhibu vikali yule aliyeolewa na Maharimu yake, na kubainisha wazi kuwa kuzini na Maharimu ni kosa kubwa zaidi.

Kutoka kwa Al-Baraa amesema: “Kaka wa mama yangu Abu Burdah Ibn Niyaar alipita karibu yangu na alikuwa na bendera, nikasema: Unakwenda wapi? Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amenituma kwa mtu aliyemwoa mke wa baba yake ili nimletee kichwa chake”. [Ameipokea At-Tirmidhiy: 1362] akasema: Katika mlango, kutoka kwa: Qurrah Al-Muzaniy: Hadithi ya Baraa ni Hassan Gharib.

Kutoka kwa Ibn Abbas, kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema: “Atakayefanya tendo la kumuingilia Maharimu yake, muueni”. Hadithi hii hatuijui ila kwa njia hii, na Ibrahim Ibn Ismail ameidhoofisha Hadithi hii.

Imepokewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kutoka katika njia nyingi, ambapo  Imepokewa na Al-Baraa Ibn Aazib, na Qurrah Ibin Iyas Al-Muzaniy, Kwamba mtu alioa mke wa baba yake, na Mtume S.A.W, akaamrisha auliwe, na hili likatekelezwa na maulamaa wenzetu, ambao walisema: Yeyote aliyemwingilia maharimu wake, na hali ya kujua, basi lazima auawe. Na Imamu Ahmad alisema: “Yeyote aliyemwingilia mama yake atauliwa”, na Is-haaq alisema: “Yeyote aliyemwingilia maharimu wake atauliwa’. [Ameipokea At-Tirmidhiy: 1462].

Taarifa ya kauli za Wanachuoni kuhusu kutoridhishwa kwa kuangalia mambo yaliyojaramishwa, na wale ambao ni wakali juu ya yale yanayoruhusiwa kwa kuogopa fitina:

Ifahamike kwamba Sharia inaruhusu maafikiano katika uhusiano kati ya Maharimu wa kiume na wa kike kwa msingi wa akili ya kawaida, na inawaondolea shaka wale wanaokalifishwa. Lakini yote haya yanahusiana na kuwepo kwa hisia hii ya hali ya juu miongoni mwa maharimu, kwa hivyo ikitoka katika muktadha huu, inaondoka kutoka kwenye duara la halali, kama hukumu nyinginezo za kisharia katika sehemu hii, bali hii ndiyo inafaa zaidi.

Sharia tukufu imetanabahisha kwa namna yake ya kawaida, ambayo huhifadhi chupa na haikwaruzi, na inaashiria asili ya suala na haifichui.

Kutoka kwa Ibn Amr, kutoka kwa Mtume S.A.W: “Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na umri wa miaka saba, na wapigeni kwa kutoswali wakiwa na umri wa miaka kumi, Na watengeni katika vitanda vyao”. [Ameipokea Abu Dawuud na wengineo]. Na Al-Munawiy alisema: (Na watengeni vitandani mwao), yaani, watengeni watoto wenu katika vitanda vyao walalavyo wakifika umri wa miaka kumi, kwa kuogopa vishawishi vya matamanio, hata wakiwa ni dada zake.

Na At-Taybiy alisema: Aliiunganisha amri ya kuali na kuwatenganisha katika vitanda vyao katika utoto kwa ajili ya adabu na kuhifadhi amri yote ya Mwenyezi Mungu na kuwaelimisha na kuishi pamoja baina ya watu na kwamba wasisimame kwenye tuhuma na kuepuka mambo ya haramu. [Faidhul Qadiir: 5/521, Al-Mktabah At-Tijaariyyah Al-Kubraa, Misri].

Ili kudumisha uhusiano huu wenye nguvu, baadhi ya wasomi walisisitiza umuhimu wa hali ya kuwatazama maharimu. Ibn Qudamah alisema: Inajuzu kwa mwanamume kuwatazama jamaa zake wa kike kwenye kile kinachoonekana, kama vile shingo, kichwa, viganja, sehemu za chini za miguu, na hana haki ya kutazama yale ambayo huwa yanafichwa kama kifua, mgongo, na kadhalika.

Na Al-Athram alisema: Nilimuuliza Abu Abdullah kuhusu mtu anayetazama nywele za mke wa baba yake au mke wa mwanawe. Akasema: Haya yamo katika Qur`ani: {wala wasionyeshe uzuri wao}. [AN NUUR: 31] isipokuwa kwa kadhaa wa kadhaa. Nikasema: Akautazama mguu wa mke wa baba yake na kifua chake, akasema: Hapana, sipendi hayo yote. Kisha akasema: Nachukia kuwa yeye kutazama mama yake na dada yake kitu kama hiki, na kila kitu kwa tamaa... Abu Bakr alisema: Kuchukia kwa Ahmed kuutazama mguu na kifua cha mama yake ni kwa ajili ya kujilinda; Kwa sababu hiyo inaleta tamaa, ina maana kwamba inachukiwa na haikatazwi.

Al-Hassan, Ash-Shaabiy, na Adh-Dahhak wamekataza kutazama nywele za wanawake maharimu. Imepokewa kutoka kwa Hind bint Al-Muhallab, alisema: Nikamwambia Al-Hassan: Je, mwanamume anatazama herini ya dada yake au shingoni mwake? Akasema: Hapana, si vyema!

Adh-Dhahhak akasema: Ningeeingia kwa mama yangu, ningesema: Ewe mzee, funika nywele zako... Na Ahmed akaacha kutazama nywele za mama wa mkewe na bintiye; Kwa sababu hawakutajwa katika Aya. [Al-Mughniy: 7/98, Maktabat Al-Qaahirah].

Na baadhi ya wanachuoni wameeleza katika suala la kutazama kuwa hukumu hubadilika kwenye kuogopa fitina, kutoka katika duara la kuruhusiwa kwenda  duara la kuchukia au kukataza, kwa kutegemea hali ilivyo, na hili linaonekana wazi katika kuzungumzia hijabu ya mjakazi.

Ibn Qudamah amesema: Huu ni ushahidi kwamba kuzuia wajakazi hijabu kulijulikana sana miongoni mwao, na kwamba kutozuia hijabu ya wanawake wengine kulikuwa kunajulikana.

Wafuasi wa Imamu Shafi walisema: Inajuzu kutazama kisichokuwa siri, ambacho kiko juu ya kitovu na chini ya goti, Na baadhi ya wenzetu walilingania baina ya mwanamke aliye huru na mtumwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema: {Wala wasioneshe uzuri wao}. [An-Nuur: 31]; Na kwa sababu ya kuharamisha kutazama ni kuogopa fitina, na fitina inayoogopewa ni sawa juu ya mwanamke huru na mjakazi, na uhuru ni hukumu ambayo haiathiri mambo ya asili, na tumetaja kile kinachoashiria uainishaji, na tofauti inatakiwa baina yao, na ikiwa hawafarakani katika yale waliyoyataja, basi walifarakana kwa ajili ya uharamisho na ugumu wa kuficha.

Lakini ikiwa mjakazi ni mzuri na kuna hofu ya fitina, ni haramu kumtazama, kama ilivyo haramu kumtazama mvulana hali ya kuogopa fitina kutokana na kumtazama.

Imamu Ahmad alisema kuhusu mjakazi, ikiwa ni mzuri: anapaswa kusitiriwa, na kijakazi asiangaliwe, hebu! ni sura gani zinazoweka ndani ya moyo misukosuko. [Al-Mughniy: 7/103].

Taarifa ya kwamba kinachoruhusiwa miongoni mwa mambo ya haramu hugeuka kuwa haramu kwa baadhi ya watu:

Na haya tuliyoyataja  kuhusu mjakazi ni mfano tu unaofahamika makusudio ya Wanafiqhi katika maneno yao, na yapo maneno yaliyo wazi katika yale tunayoyahusu, yanayoonesha kuwa kugusana maharimu wenyewe kwa wenyewe kunaweza kuwa haramu panapokuwepo matamanio. na hili lau watu wangelilijua na kulifanyia, mmea wa uovu ungeng'olewa kutoka kwenye nyoyo kabla haujaota mizizi.

Al-Qarafiy amesema: Wamenifahamisha baadhi ya wanachuoni kwamba walijiepusha kuwabusu watoto wao mdomoni na kuwabusu shingoni na vichwa vyao, wakibishana kwamba Mwenyezi Mungu amekataza kufanywa matamanio kwa ndugu na jamaa, matamanio ni yale anayoyapata raha katika busu, basi mwenye kustarehesha hilo litazuiliwa katika hali yake, na kwenye shavu, kinywa, kichwa, shingo, na mwili wote kwake ni sawa, na anafanya hivyo kwa ajili ya mapenzi na upole, basi hilo linajuzu. Na kunyume na hivyo, hapana.

Nikasema: Haya ni maneno ya kweli, na hakuna shaka juu yake, na nimeona baadhi ya watu wakipata raha kwa kumbusu mtoto wao shavuni au mdomoni kama ilivyo kwa watu wengi mtu akimbusu mkewe, na wakiamini kwamba hii ilikuwa ni heshima kwa mwanawe, lakini sivyo hivyo, bali ni kutimiza masilahi na radhi yake, na anachangamka kwa ajili ya hayo, na moyo wake unafurahi, na anapata raha nyingi.

Ni kosa kwa mtu kuwa na dada yake mzuri au binti yake ambaye anataka kuwa na mke wa kufanana naye, akambusu shavuni au kinywani, na akapenda hayo, na anaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha kuwabusu wengine.

Sivyo hivyo, lakini kukutana na maharimu wa kike ni haramu zaidi, kama kuzini nao ni mbaya zaidi kuliko zinaa na wanawake wasio maharimu. Na hakuna mwenye umbile safi, na akaona uzuri usio wa kawaida usioelekea umbile lake, na huenda akili yake na sheria yake zikamtenga, niliona watu wana uzembe mkubwa katika hilo.

Na kauli ya Malik, Mwenyezi Mungu amrehemu kuwa: “Anabusu shavu la binti yake” inaeleweka kuwa hili au lile ni sawa kwake.

Inapotokea tofauti katika nafsi, inakuwa ni starehe iliyoharamishwa, na mtu hutazama moyo wake na kuufanya hakimu katika hilo. [Al-Furuuq: 4/254].

Utajo wa waliosema kuwa miongoni mwa maharimu ni yule ambaye haruhusiwi kuwa naye peke yake kwa ajili ya sababu maalumu:

Ibn Qudamah amesema: Kafiri si maharimu kwa mwanamke Muislamu, hata kama ni binti yake. Imamu Ahmad alisema kuhusu Myahudi au Mkristo ambaye binti yake alisilimu: Asimuoze, wala asisafiri naye, kwa sababu siye maharimu kwa ajili yake.

Abu Hanifa na Shafi wamesema: Ni maharimu kwake, kwa sababu ameharamishwa kwake milele. Na maoni yetu: Uthibitisho wa kuwa na uharimu unalazimu kuwa peke yake naye, kwa hivyo hauthibitishwi kwa kafiri juu ya mwanamke Muislamu, kama vile kulea mtoto, na kwa sababu hatamhifadhi, atamtia fitina katika dini yake kama mtoto.

Na hayo waliyoyataja yanabatilisha suala la mama ya aliyezini naye, na bintiye, na mwanamke aliyeharamishwa kwa sababu ya Liaan, na Majusi na bintiye.

Na ifahamike kuwa hakuna hitilafu kuhusu Majusi; kwa sababu haaminiwi na bintiye, na hali ya kuwa anaamini ni halali kwake. Na Imamu Ahmed aliitaja hivyo katika sehemu kadhaa. [Al-Mughniy: 3/231, Maktabat Al-Qaahirah].

Na hii ya Imamu Ahmad ndiyo Fiqhi yenyewe, kwa hivyo Majusi anaamini kuwa dada yake ni halali kwake, basi vipi awe naye peke yake, pamoja na kwamba mwenye kuamini kuwa kitu kinaruhusiwa si lazima kwake kukifanya, Kadhalika, maharimu ambaye ana yakini ya kuzini na maharimu wake si nje ya hukumu hiyo, ikiwa yeye hastahiki zaidi kuliko yeye.

Taarifa kwamba mwanamke hujiepusha na yule aliyemtaka kuhusu nafsi yake, na huitumia kwa kukimbia, kusukuma, au kupiga kelele, nk. Vinginevyo, ana haki ya kumuua:

Yote yaliyotajwa ni utangulizi wa asili ya utafiti, jambo ambalo mwanamke anapaswa kufanya ikiwa atatamaniwa na baadhi ya maharimu wake.

Inajulikana kuwa mchokozi huzuiwa kidogo kidogo, hivyo anaweza kuanza kwa kumtishia, au kumjulisha anayemtisha, au kumrekodi na kumtishia kwa kashfa mbele ya watu au mbele ya polisi, au kutafuta msaada wa mtu anayemshuhudia hata kama alikuwa atajificha, na kadhalika.

Hii ni mifano ya mapokezi yanayoonesha kile mwanamke anachofanya ili kujitetea. Na tunaanza kwa kutaja yale aliyoyafanya Ummu Hakim R.A, ambapo mtumwa wake pale alipomtaka kuhusu nafsi yake. Ili hadithi ihusiane na nukta iliyotangulia; Kwa sababu wapo Wanachuoni waliosema kuwa mtumwa ni maharimu kwa bibi yake wa kike. Hata hivyo, mtumwa alimtamani; kuthibitisha tuliyoyataja, kuwa baadhi ya wanaume hunyanyasa maharimu wake, ili Mufti na Hakimu wachukue hadhari.

Ibn Asaakir ametaja: Ilipofika siku ya kufungua Makkah, Ummu Hakim, bint Al-Harith Ibn Hisham, mke wa Ikrimah Ibin Abi Jahl, alisilimu, Kisha Ummu Hakim akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Ikrimah alikimbia kwenda Yemen na aliogopa kwamba wewe utamwua, basi mpe amani. Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amesema: Yuko salama. Basi akatoka kwenda kumtafuta, pamoja naye mtumwa wake Mrumi, ambaye akamtaka kuhusu nafsi yake, basi akatumia hila, mpaka akampeleka kwenye kitongoji kutoka kwa watu wake, akawaomba msaada wao dhidi ya mtumwa huyu, wakamkamata na kumfunga.

Ummu Hakim akafikia mahali pa Ikrimah, ambapo akafika katika moja ya mipaka ya Tihama, akapanda baharini, Basi rubani wa meli akamwambia: Maliza! Akasema: Niseme nini?! akasema: Sema hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu. Ikrimah akasema: Mimi niliepukana na hili tu! Basi Ummu Hakim akalifikia jambo hili, na akaanza kumsisitiza na kusema: Ewe binamu, mimi nilikujia kutoka kwa mtu wa karibu zaidi, mtu mwema zaidi, na mbora wa watu, usijiangamize! Akasimama karibu naye mpaka akamshika, akasema: Nilipata amani ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, kwa ajili yako. Akasema: Je kweli umefanya! Akasema: Ndiyo, nilizungumza naye, na akakuwekea salama. Basi akarudi naye, kisha akamhadithia kisa cha mtumwa wake Mrumi, basi Ikrima akamuua, na alikuwa hajasilimu bado siku hiyo. [Tariikh Dimashq: 41/63, Dar Al-Fikr Li Attiba’ah Wan Nashr Wat Tawzii’].

Kutoka kwa Anas: Siku ya Hunayn, Ummu Sulaym alichukua jambia/upanga, na alikuwa  nayo, Abu Talha alimuona na akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu Ummu Sulaym alikuwa na jambia, na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, akamwambia:  Ni yanini jambia hii? Akasema: Nimeichukua, atakaponijia mmoja wa washirikina, nitamkata tumboni mwake, akacheka Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. Akasema Ummu Sulaym: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, waue hao walio huru baada yetu, je wameshindwa na wewe? Na Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, amesema: “Ewe Ummu Sulaym, Mwenyezi Mungu ametosha na bora zaidi”. [Ameipokea Muslim].

Na dalili katika Hadithi hii ilielekezwa kwa ridhaa ya Mtume S.A.W, kwa Sahaba wa kike kumzuia kafiri na nafsi yake, na hii inajumuisha damu na tupu, na kwa sababu kama kafiri atamkamata angekuwa mjakazi; kwa hiyo Ilikuwa ni wajibu kumzuia, hata kama kwa kuua.

Kutoka kwa Khawlah bint Tha’labah, amesema: Kuhusu mimi, Wallahi, na kuhusu Aws Ibn Samit kwamba Mwenyezi Mungu, aliteremsha mwanzo wa Suratul  Mujadalah.

Akasema: Nilikuwa naye, hali alikuwa ni mzee mwenye tabia mbaya na hana subira, Akasema: Kisha akanijia siku moja, nikamuuliza kitu, akakasirika, kasema: Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu, Akasema: Kisha akatoka na akakaa katika baraza la watu wake kwa muda, kisha akanijia, basi kama akinitaka kuhusu nafsi yangu, nikasema: Hapana, na kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hutanifikia, baada ya kusema uliyoyasema mpaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake atuhukumu kwa hukumu yake, Akasema: Alinikaripia, nami nikamkatalia, basi nikamshinda kama mwanamke anavyomshinda mzee dhaifu, nikamtupilia mbali, Akasema: Kisha nikatoka kwenda kwa baadhi ya majirani zangu wa kike na nikaazima nguo zake, kisha nikatoka mpaka nilipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, nikakaa mbele yake na nikataja yale niliyoyapata kutoka kwake, nikaanza kumlalamikia mbele yake S.A.W, kuhusu niliyoyapata miongoni mwa tabia yake mbaya. [Ameipokea Ahmad katika Al-Musnad: 45/300, Ch. ya Ar-Risalah].

Ushahidi wa hayo kuwa Sahaba huyu wa kike hakumuwezesha mumewe nafsi yake baada ya kutamka maneno ya Dhihaar, na alidhania kuwa ni talaka, lakini hakumsukuma kwa kumuua kwa sababu alikuwa na msukumo wa kitu kidogo kuliko hicho, na hayo hutofautiana kulingana na mwanaume na mwanamke.

Na kutoka kwa Maamar, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Al-Qasim Ibn Muhammad, amesema: Nadhani ilikuwa kutoka kwa Ubaid bin Umair alisema: Mtu mmoja alikaribisha watu wa kabila la Hudhail, basi wakamtuma kijakazi ili kutema kuni, mgeni akapendezwa naye, hivyo akamfuata, na akamtaka kuhusu nafsi yake, lakini akakataa, akapigana naye kwa muda, kisha akamtoroka, akampiga kwa jiwe, akalichana ini lake, akafa, kisha akaja kwa jamaa yake na kuwaambia, basi jamaa yake wakaenda kwa Umar, wakamwambia, hapo Umar akatuma na kutafuta athari zake, na Umar akasema: “Aliyeuliwa ni kutokana na uhalifu wa kisharia, kamwe hakuwa na fidia”. [Ameipokea Abdur Rqazzaq katika Musannaf yake: 9/434, Al-Maktab Al-Islamiy, Beirut; Ibn Abi Shaibah: 5/439, Maktabat Ar-Rushd]. Na Tamko ni la mpokezi wa kwanza.

Na kutoka kwa Al-Qasim Ibn Muhammad kuwa: “Abus Sayarah alimpenda sana mke wa Abu Jundub, na akamtaka kuhusu nafsi yake, na mwanamke akasema: “Usifanye hivyo, kwa sababu Abu Jundub akijua hivyo atakuua, lakini alikataa kuachana naye, basi akazungumza na kaka yake Abu Jundub, naye akazungumza naye, lakini akakataa kuachana naye. Basi mwanamke akamfahamisha Abu Jundub kuhusu hilo, akasema natawaambia watu kwamba mimi naenda kwenye ngamia, na giza litakapoingia nakuja na kuingia nyumbani, na akikujia mlete kwangu. Na Abu Jundub akawaaga watu na kuwaambia kuwa anakwenda kwenye ngamia, lakini usiku ulipoingia alikuja na kuvizia na kuingia ndani ya nyumba.

Na Abus Sayarah alimjia kumuomba ombi lake na mwanamke akisaga, na kumtaka kuhusu nafsi yake, na akasema: Ole wako! umeliona jambo hili unaloniitia, je nililiomba hata kidogo, akasema: Hapana, lakini sitakuwa na subira juu yako. Akasema: Ingia nyumbani mpaka nijiandae kwa ajili yako. Alipoingia nyumbani, Abu Jundub akafunga mlango, akamchukua, akamgonga kuanzia shingoni mpaka mfupa wa mwisho. Kisha yule mwanamke akaenda kwa ndugu yake Abu Jundub na kusema: Msaidie yule mtu kwa sababu Abu Jundub atamuua. Basi ndugu yake akamuomba kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hivyo akamwacha, na Abu Jundub akamchukua mpaka kwenye zizi la ngamia na akamtupa pale.

Basi kila mtu alipopitia akamwambia: Una nini? Akasema: Nilianguka kutoka katika ngamia, basi akanivunja, kwa hiyo akawa na nundu. Kisha akaenda Umar Ibn Al-Khattab RA, akamwambia, basi Umar akatuma mjumbe kwa Abu Jundub na akamjulisha jambo hilo moja kwa moja, hivyo akawaita watu wa majini, ambao walimuamini, basi Umar akampiga Abus Sayarah viboko mia moja, na kufuta dia yake”. [Ameipokea Al-Kharaaitiy katika I’tilaal Al-Quluub: 1/98, Ch. ya Nizaar Mustafa Al-Baaz, Makkah Al-Mukaramah. Riyadh].

Ushahidi kutoka katika hadithi hizo mbili ni idhini ya Umar RA, kwa mwanamke katika kutetea heshima yake, hata kama kwa kuua, na sawa na hiyo katika hadithi ifuatayo kutoka kwa idhini ya kiongozi Adh-Dahhak, ambaye ni miongoni mwa Masahaba wadogo, kama katika: An Nubalaa: 3/241, Ch. ya Ar-Risaalah.

Imepokewa na Suleiman Ibn Yasaar kuwa: “Mwanamke mmoja wa Sham alimjia Adh-Dahhak Ibin Qais na kumwambia kwamba mtu amemfungulia mlango wake, akilia kuomba msaada, lakini hakuna aliyemsaidia, na ilikuwa wakati wa baridi, basi akamfungulia mlango, akatwaa jiwe la kusagia, akamtupia akamuua, kisha akamtuma mjumbe pamoja naye kutazama, kumbe!  ni mwizi na alikuwa na mizigo, hapo Adh-Dhahhak alibatilisha hukumu yake”. [Ameipokea Ibn Abi Shaibah: 5/439, Maktabat Ar Rushd, Riyadh; Al-Khilaal Fi As-Sunnah1/166, Dar Ar-Rayah, Riyadh].

Na Musa’ab Ibn Abdullah Az-Zubairiy amesema: Abdullah Ibn Mutii’ alishindwa siku ya Al-Harrah, akapita mwanamke aliyejifunika nikabu huko Madina, na mwanamke akampigia kelele akimbie, na huyu ni Abdullah Ibn Mutii’ umeanzisha vita kwa watu?! Abdullah akasema wewe hujui kuwa ni yeye. Akasema: Abdullah Ibn Mutii’ aliingia ndani ya nyumba ya mwanamke, akajificha kwenye rafu, kisha akaja mtu mmoja wa Sham kumtaka mwanamke kuhusu nafsi yake, na mwanamke aliomba msaada wa mtu aliyepo kwenye rafu, akateremka kwake na kumuua, na mwanamke akamuuliza: Naapa kwa baba na mama yangu, wewe ni nani? Akasema: Lau si rafu, ningekuambia! [Tahdhiib Al-Kamaal: 16/154].

Ushahidi wa hadithi ni kwamba mwanamke huyo aliomba msaada kwa mtu ambaye angemsaidia, na Abdullah bin Mutii’ akamuua mtu wa Sham, na huyu Ibn Mutii’ alikuwa mtawala wa watu wa Madina, miongoni mwa  Makureshi na wengineo katika vita vya Al-Harrah. Baba yake alimleta kwa Mtume S.A.W, akampa tende, na alimuita Abdullah, alimuombea dua ya baraka. [Isnad yake ni nzuri, kama ilivyotajwa katika Al-Isaabah, na Ibn Hajar: 5/21, Dar Al-kutub Al-Ilmiyyah, Beirut].

Kama tulivyotaja, baadhi ya Wanachuoni walisema:

Al-Khallal amesema: Ali Ibn Al-Hassan Ibn Suleiman aliniambia, Hanbal alituambia: Nilimuuliza Abu Abdillahi, nikasema: Mwanamke anayetakiwa kuhusu nafsi yake na mwanamume, akakataa, kisha akapata nafasi na akamuua kwa ajili ya kujitetea, je anahatia kwa hilo? Akasema: “Ikiwa amejua hahitaji kingine isipokuwa anamtaka yeye tu na akamuua kwa ajili ya  kujitetea na akafa, basi yeye hana kitu juu yake, lakini akitaka vitu na nguo tu, nafikiri kwamba ampe hivyo, wala asimaliza nafsi yake, kwa sababu nguo na vitu vina mbadala, na nafsi haina mbadala”. [As-Sunnah: 1/163, Dar Ar-Raayah, Riyadh].

Ibn Qudamah amesema: Ahmad amesema kuhusu mwanamke aliyetakiwa na mwanamume kuhusu nafsi yake, na akamuua kwa ajili ya kujilinda, akasema; ikiwa mwanamke akijua kuwa mwanamume hataki kitu isipokuwa nafsi yake, akamuua kwa ajili ya kujitetea, basi hakuna kitu juu yake.

Na akataja Hadithi iliyopokelewa na Az-Zuhriy, kutoka kwa Al-Qasim Ibn Muhammad, kutoka kwa Ubaid bin Umair, kwamba mtu mmoja alikuwa mwenyeji wa watu wa kabila la Hudhail, na mtu huyu akamtaka mwanamke kuhusu nafsi yake, na mwanamke akampiga mawe na kumuua, na Umar akasema: Wallahi hatakuwa na fidia hata kidogo.

Na kwa sababu ikiwa inajuzu kutetea mali zake, ambazo inajuzu kuzitumia na kuzitoa, basi mwanamke kujilinda nafsi yake na kujiepusha kutokana na uchafu, ambao haujuzu kwa vyo vyote, ni lazima zaidi.

Hili likithibitishwa, basi lazima kujitetea mwenyewe iwezekanavyo; Kwa sababu kukubali ni haramu, na kutotetea ni aina ya kukubali. [Al-Mughniy; 9/183].

Al-Mawardiy amesema: “Iwapo mtu anajihofia nafsi yake kwa  mtu anayetaka kumuua, au mnyang`anyi, au mwenye kujeruhi mwili wake, au anamhofia mwanawe au mke wake, basi ana haki ya kujitetea kulingana na tutakayoeleza, hata kama kumsukuma kutapelekea kumuua, ni sawa mtu huyo ni mwenye kukalifishwa, ambaye ni mtu mzima mwenye akili timamu, au kama ni mtoto na mwendawazimu, au ni mnyama mkali na  ngamia mkali, kwa sababu ameamrishwa kujilinda nafsi yake, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Wala msijiuwe}. [An Nisaa: 29], na kauli yake Mtume S.A.W: “Mwenyezi Mungu amemharamishia Muislamu (kuharibu)mali yake na damu yake(kuua nafsi yake)”.

Na kwa imepokelewa kuwa: Kijakazi alitoka mjini kwenda kutema kuni, na mtu mmoja akamfuata, akamtaka kuhusu nafsi yake, na kijakazi akampiga jiwe na kumuua. Hayo yamefika kwa Umar R.A, na Umar akasema: Huyu ni muuaji wa Mwenyezi Mungu, Wallahi hatakuwa na fidia hata kidogo, na maana ya (muuaji wa Mwenyezi Mungu) kuwa Mwenyezi Mungu amehalalisha kuuawa. 

Na kauli yake (Wallahi hatakuwa na fidia hata kidogo) kuna maana mbili: mojawapo kuwa ni: Kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba halipwi damu yake” na ya pili: Kwamba imefahamika kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba aliye halali kuuawa   halipwi damu yake, na kwa sababu ombi hilo ni kosa na adhabu kwa  mhalifu ni halali.

(Sura) Ikithibitika kuwa inajuzu kujitetea kwa kumuua, jambo lililokubalika kwa pamoja, basi nafsi yake haina makosa ikiwa ni mwenye kukalifishwa au la... Na ushahidi wetu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu}. [AT TAWBAH: 91], na huyu kwa mujibu wa kujitetea ni mfanya wema, hivyo ni lazima asiwe na gharama.

Na Mwenyezi Mungu amesema: {Na wanao jitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu}. [ASH SHURAA: 41].

Ikisemwa: Hainasibishwi dhulma kwa mtu asiyekalifishwa. Ikasemwa: Dhulma ni kukiweka kitu mahali pasipostahili, basi mteteaji anakuwa amedhulumiwa, na ikiwa haijanasibishwa dhulma kwa mchokozi, kutokana na kutokalifishwa.

Na imepokewa kutoka kwa Mtume S.A.W, akisema: “Haijuzu kuchukua mali ya Muislamu isipokuwa kwa ridhaa yake”. Hivyo dhahiri yake kuwa kutochukuliwa gharama kutoka kwake isipokuwa kwa ridhaa yake tu. Na kuzingatia kuwa: Ni maangamizo yenye malipo yanayoruhusiwa, kwa hivyo dhamana lazima iondolewe kwa mlinganisho wa kumuua mtu mzima, mwenye akili timamu, na kukalifishwa.

Ikisemwa: Kinachokusudiwa kuwa mtu aliyekalifishwa ni kuwa ameruhusu kujiua kwa ombi, na haisihi kwa asiyekalifishwa kujiua kwa ombi; Maana hakuna hukumu kwa kusudio lake..... Na hukumu ya pili: kuhusu yule ambaye inajuzu kumuepusha naye, ikiwa mchokozi anataka yeye mwenyewe, mwanawe, au mkewe, kwa ajili ya kuua, uasherati, ubaya, au anataka mali yake, wake zake, au alilostahiki zaidi kuliko yeye.

Kwa hivyo hukumu ya kumuepusha kwa niaba ya familia na watoto wengine ni kama hukumu ya kumuepusha na yeye mwenyewe, na hukumu ya kumuepusha na mali na wake zake ni kama hukumu ya kuepusha na  nafsi; Kwa mujibu wa pokezi la Said bin Zaid, kwamba Mtume S.A.W, amesema: “Yeyote anayeuliwa kutokana na mali yake, basi ni shahidi”. Na shahidi ndiyo ni yule aliyepigana.

Na akasema S.A.W: “Hakika damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni haramu kwenu, kama vile uharamu wa siku yenu hii, nchi yenu hii, na Mwezi wenu huu” Kwa hiyo aliunganisha damu, mali, na heshima, akionesha ushiriki wao katika hukumu ya kujitetea. [Al-Hawiy; 13/451-454, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, Beirut].

Ibn Hazm amesema: Na ambaye mke wake ana yakini kuwa mume amemtaliki mara tatu, au mwisho wa tatu, au chini ya tatu, na hakushuhudia kwamba alimrudisha mpaka alipotimia eda yake, kisha akamshika kiuchokozi. Ni lazima juu yake kumkimbia - ikiwa hana uthibitisho – na kama akimlazimisha basi ana haki ya kumuua kwa ajili ya kujilinda.

Vinginevyo, anazini naye, ikiwa atamwezesha kufanya naye ngono, kwani si halali kwake – ni kama msafiri, na hukumu yake juu ya kila kitu ni hukumu ya mtu wa mbali. [Al-Muhalla: 9/486, Dar Al-Fikr, Beirut].

Maneno zaidi ya wanachuoni yatakuja katika nukta ifuatayo.

Hukumu ya kulipiza kisasi dhidi ya muuaji katika kesi hii:

Kanuni ya msingi katika kuzuia mchokozi kuwa anaepushwa kwa njia ya kidogo kidogo, kama inavyojulikana, ikiwa inawezekana kufanywa hivyo, Lakini ikiwa hatazuiliwa isipokuwa kwa kuuwa basi atauliwa, na hakuna pesa ya damu kwa muuaji wake kwa mujibu wa kauli ya wanachuoni wengi, na kwa sababu mwanamke hapa lazima asijiwezeshe, na lisiloweza kutimia wajibu bila yake, basi ni wajibu. Na mwenye Sheria alihesabu yeyote anayeuliwa kutokana na heshima yake anakuwa ni shahidi, kwa hivyo hii inaashiria uhalali wa kupigana kwa jumla.

Al-Khatib Ash-Shirbiniy amesema: (Siyaal) na (Musawalah) katika lugha ya kiarabu ni: ushambuliaji na kupigana, na (Swaail) mchokozi ni dhalimu... Na asili ya mlango huu ni kauli yake Mwenyezi Mungu: {Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni}.

na akaifungua katika kitabu cha Al-Muharrar kwa habari ya Imamu Bukhariy, kauli yake Mtume S.A.W: “Mnusuru ndugu yako akiwa amedhulumu au amedhulumiwa” na mshambuliaji ni dhalimu, hivyo anazuiliwa na dhulma yake; Huo ndio ushindi wake (wake) yaani mwenye kushambuliwa  (kumzuia kila mwenye kushambulia), awe Muislamu au kafiri, mwenye akili timamu au mwendawazimu, mtu mzima au kijana, jamaa au mtu wa mbali, binadamu au mwingine (juu ya) mwenye kuheshimiwa (nafsi au kiungo) au faida (au tupu au pesa) kwa habari ya "Anayeuliwa kutokana na damu yake ni shahidi, na anayeuliwa kutokana na mali yake ni shahidi, na anayeuliwa kutokana na jamaa zake ni shahidi”. Ameipokea Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, na akaisahihisha.

Ushahidi wa hayo kuwa alipomfanya shahidi, hii iliashiria kuwa alikuwa na haki ya kuua na kupigana, kama vile yeyote aliyeuliwa na watu wa vita alikuwa na haki ya kuua na kupigana.

Tanbihi: Katika maana ya tupu, ishara kwa aliyekusudia kutamani familia yake mbali na tupu, kama vile busu, na Ar-Ruyaaniy aliwaambatanisha dada na binti kwa mke. [Mughniy Al-Muhtaj Sharh Minhaaj At-Talibiin: 4/194, Ch. ya Dar Al-Fikr.

Al-Baijuriy amesema: Kama tendo la ndoa ni utangulizi wake, kama ulivyojua kutokana na yale yaliyopita, na “jamaa zake” ni pamoja na mkewe, wanawe na karibu, na ukajua kwamba nyongeza katika hizo tatu si kizuizi.

kwa hivyo ni lazima awatetee maharimu wa mtu mwingine, hata wakiwa makafiri, na hata kama mshambuliaji ni Muislamu.

(Kauli yake: akapigania hivyo) yaani kuepusha mshambuliaji, lakini kumuepusha kidodo kidogo iwezekanavyo, kuanza kwa kumfukuza, kumkemea, kuomba msaada, kumpiga kwa mkono, kumpiga kwa mjeledi, kumpiga kwa fimbo,  kumkata kiungo, kisha kuua; Kwa sababu hilo linajuzu kwa dharura, na hakuna dharura pamoja na kuwepo lililo jepesi zaidi.

Hata hivyo, lazima ya mpangilio kati ya kukemea na kuomba msaada ikiwa madhara yatokanayo na kuomba msaada ni makubwa kuliko madhara yanayotokana na kukemewa, Kana kwamba ni kushikilia mtawala dhalimu, vinginevyo hakuna mpangilio kati yake.

Na anapokiuka mpangilio huu kwa kuwa sawa na utaratibu wa baadae pamoja na uwezekano wa lililo kabla yake, akiwa ni mwenye kudhamini, na ikiwa lile jepesi lisingewezekana, kana kwamba mapigano baina yao yanahusika na jambo likawa kubwa na haiwezekani kulidhibiti, mazingatio ya mpangilio huondoka.

Na ikiwa mshambuliwa hakupata chochote ila upanga, basi anaweza kumpiga, hata kama mshambulizi alikuwa akirudisha nyuma kwa mjeledi na fimbo; Kwa sababu wakati huo hawezi tu kujitetea isipokuwa kwa ule upanga, na haichukuliwi kuwa ni mzembe katika kuacha ushirika wa mjeledi na fimbo, na sio lazima kupangilia ikiwa mshambuliaji hana heshima, kama vile kafiri na aliyeritadi, hapo ana haki ya kumuua moja kwa moja, kwa sababu hana heshima.

Na ni wajibu kupangilia katika mambo machafu kwa mujibu wa rai ya kukubalika. Na Sheikh wa Uislamu amesema: Si wajibu kupangilia humo; Kwa sababu kila wakati kuna tofauti ambayo haivumiliki. Na rai hii ni nzuri.

(Kauli yake: yaani kuhusu yeye mwenyewe, pesa zake, au maharimu wake) ni tafsiri ya usemi wake “kuhusu hilo” kwa hivyo kiashiria kinahusisha moja kati ya hizo tatu. (Kauli yake: Na mshambulizi aliuliwa kwa ajili ya hayo) yaani juu yake mwenyewe, mali yake, au maharimu wake. (Na kauli yake: kuepusha ushambuliaji wake) yaani ikiwa hakuzuiliwa isipokuwa kwa kuua, kwa sababu ya ulazima wa utaratibu, kama ilivyojulikana kutokana na hayo yaliyotangulia. (Kauli yake: Hapana dhamana juu yake) yaani hakuna dhambi juu yake pia; Kwa habari ya “Mwenye kuuliwa kutokana na dini yake ni shahidi, na mwenye kuuliwa kutokana na damu yake ni shahidi, na mwenye kuuliwa kutokana na  mali yake ni shahidi, na mwenye kuuliwa kutokana na familia yake ni shahidi”. Ameipokea Abuu Dawud, na At-Tirmidhiy na akaisahihisha.

Na naana ya “kutokana na “ ni “kwa ajili ya” katika hayo yaliyotangulia, kwa hiyo maana ya “kutokana na dini yake” ni “kwa ajili ya dini yake”, yaani ili kutetea dini yake, na kadhalika.

Ushahidi hapa kuwa: alipomfanya shahidi, ilionesha kuwa alikuwa na haki ya kupigana na kuua, bali aliamrishwa kufanya hivyo, jambo ambalo liliashiria kuwa hakuna dhamana kwake. Kwa sababu kuna mgongano kati ya amri ya kupigana,  kuua, na dhamana.

Na sawa na hayo ni yule aliyepigana na watu wa vita, na lau wangemuua angekuwa shahidi, na hii inaashiria kuwa anayo haki ya kupigana na kuua, bali ni kuwa ameamrishwa kufanya hivyo, kwa hivyo hii inaonesha kuwa hakuna dhamana juu yake. Hasiyat Al-Baijuriy Alaa Sharh Ibn Qasim Al-Ghazziy: 2/249, Ch. ya Issa Al-Halabiy.

Al-Bahuutiy amesema: (Na anayeshambulia nafsi ya mwingine) akiwa mnyama au binadamu (au) anashambulia (wanawake wake) kama mama yake, binti yake, dada yake, mke wake na kadhalika. Wao ni (au) juu ya (mtoto wake au mali yake) hata ikiwa ni kidogo) yaani mali (mnyama au mwanadamu, hata akiwa) anayetakwa ni nafsi yake au heshima yake au mtoto wake au mali yake, (sio sawa) na anayetaka (au) mshambuliaji alikuwa (mvulana au mwendawazimu) kama mnyama, na kama alishambulia (nyumbani mwake au popote pengine, hata kama) alikuwa (akitaka kuiba) yaani akitafuta kuiba (na hakuogopa) yaani mshambuliwa, kwa sababu kama angezuiwa kufanya hivyo, ingempelekea kuangamia, kumdhuru nafsi yake, heshima yake na mali yake, na kwa sababu kama hilo lisingeruhusiwa, watu wangejichukulia maamuzi wenyewe kwa wenyewe, na ingepelekea fujo.

(Na ikiwa alimzuia kwa maneno, basi hana haki ya kumpiga) kwa kitu (Na ikiwa hatazuiliwa kwa maneno, basi anaweza), yaani mshambuliwa (kumpiga kwa cho chote kile anachofikiri kinaweza kumzuia, akidhani kuwa anaweza kumzuia kwa kumpiga fimbo, hana haki ya kumpiga kwa chuma), kwa sababu ni chombo cha kuua (na hata kama alikuwa akikimbia, hana haki ya kumuua, wala asimfuate) kama wapiganaji, (na akimpiga na kumzuia, hana haki ya kuzidisha) kwa sababu inatosha kuacha uovu wake. Kashful Qinaa’: 6/154, Ch. ya Dar Al-Fikr.

Sheikh Ad-Dardiir amesema: (Inajuzu kumzuia mchokozi)  juu ya nafsi, mali, au wanawake, na maana ya inajuzu ni ruhusa, kwa hivyo inasadikika kuwa ni wajibu (baada ya onyo) inayotakiwa kama katika hali ya mpiganiaji (kwa anayefahamu) yaani mwenye akili timamu, kwa kumwambia: Nakusihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu niachilie, na mfano wa hayo, yaani ikiwezekana kama ilivyotajwa hapo juu kuhusu mpiganaji, na kama hatazuiliwa au hakuweza, basi inajuzu kumzuia kwa kuua na mengineyo. Ash-Sharh Al-Kabiir pamoja na Hashiyat Ad-Disuuqiy: 4/357, Ch. ya Dar Al-Fikr.

Na uuaji huu mfanyaji wake hana dhambi, bali analipwa thawabu kwa kutimiza wajibu, na wala si lazima kulipiza kisasi iwapo ataleta ushahidi, lakini asipoleta ushahidi, basi hana uhusiano wowote na dini, siyo mahakamani.

Lakini iwapo dalili zinazomdhamini muuaji, basi hakimu anaweza kuzitegemea, lakini baadhi yao walikwenda mbele zaidi ya hayo. Ibn Taymiyyah amesema: “Yeyote anayekabiliwa kwa ujeuri, analazimika kumzuia mshambulizi, na ikiwa hataweza kuzuiwa isipokuwa kwa kuua, basi ni haki yake kwa mujibu wa makubaliano ya Mafaqihi.

Ikiwa muuaji atadai kuwa amemshambulia, na jamaa wa aliyeuliwa wanakanusha, basi ikiwa muuaji alijulikana kwa wema, na akamuua mahali pasipo na wasiwasi, basi kauli ya muuaji haikubaliwi.

Na ikiwa anajulikana kwa ujeuri, na muuaji anajulikana kwa wema, basi inakubaliwa kauli ya muuaji, pamoja na kiapo chake, hasa ikiwa kuna uhusiano kati yao kabla ya hapo. Al-Ikhtiyaraat Al-Fiqhiyyah: Uk.595, Dar Al-Maa’rifah, Beirut.

Tanbihi: Uuaji huu hauchukuliwi kuwa ni kitendo cha adhabu, na kauli kama hii ndiyo inakatazwa, ili kutopinga uamuzi wa hakimu, lakini ni aina ya kumzuia mshambulizi.

Hatua za unyanyasaji:

1- Tamaa na kidokezo: Je, ni aina moja au inajumuisha aina kadhaa:

Tamaa kati ya mwanamume na mwanamke ni tamaa ya asili na hulka, lakini tabia njema huepuka kuanzisha uhusiano wa jinsia na ndugu za karibu , hata kwa njia ya ndoa.

Na kinachoimarisha maumbile haya ni sheria ya kidini inayozuia hili, na kufanya kukata tamaa kuwa kizuizi kati ya maharimu; na ikiwa mtu atakua na imani ya kuwa hana njia ya kufikia aina fulani hata kidogo, hii humfanya kikawaida aondoe mawazo yake kutoka kwao hadi kile anachoweza, kama alivyosema mshairi:

Ikiwa huwezi kufanya kitu, basi kiache

na uende mbele ya kile unachoweza.

Iwapo silika imeharibika, mtu huyo alimili kwa yale ambayo hayaruhusiwi kufikiwa kutoka kwa baadhi ya maharimu, na hii inaweza kufikia kwenye kupendezwa na tamaa, na akajificha ndani yake hisia ya kidini, haya, woga, au kwa sababu ya kitu kingine.

Na hapo jambo hili si kitu isipokuwa tamaa tu, na halifikii hatua ya kudokeza. Bali jambo hili ni kama jambo lingine, liwe la kupendeza kwa  mtu wa jinsia nyingine, isipokuwa mhusika wake haoneshi hivyo, na anajaribu kuzuia tamaa hii ili isiwe na nguvu zaidi; Kwa sababu jambo hili ni sawa na mmea mchanga, lakini ukiachwa ungekua na kuota mizizi ardhini, itakuwa vigumu kung'oa, na kama ung’olewa tangu mwanzo, itakuwa rahisi na nyepesi zaidi.

Ama dokezo ni kwa kufikisha yaliyomo ndani ya nafsi kwa upande mwingine, kufariji anachohisi kutokana na maumivu ya mapenzi, au kumsisimua kubadilishana anachokikuta ndani yake, na hilo lina namna nyingi.

Inaweza kurefusha mtazamo kwa makusudi ili mhusika mwingine aelewe kilicho ndani yake, na ikiwa mwanzilishi ni mwanamke, basi ana mtindo wake wa kawaida katika hali kama hiyo ya mapambo na kuzidisha kubainisha uzuri au kumwita amguse, kwa njia yoyote, kwa sababu mwanaume ameathiriwa na mengi kama haya.

2- Je, kauli wazi ni kauli tu, au inaleta unyanyasaji:

Ama kutangaza ombi la uchafu au kuutamani, huku hata kama sio kunyanyasa kwa kitendo, ni kuudhi kwa maneno, kwani mwanamke hajisikii salama kwa mtu huyu wa karibu, anaweza kumdanganya usingizini au kumtia ganzi ili amfanyie chochote anachotaka.

Na mtu kama huyo hajazingatiwa bado awe karibu katika masharti ya upweke, kutazama, hijabu, na kadhalika; Kwa sababu mambo haya yameruhusiwa kwa ajili ya usalama wa fitna, basi pasipoletwa usalama wa fitna, hapo mtu huyo ni kama mtu wa mbali au mbaya zaidi.

3- Unyanyasaji:

Ama unyanyasaji halisi, ni shambulio, kugusa, kukumbatia, na kadhalika, na hii inachukuliwa ni zinaa, hata kama adhabu yake si adhabu ya Hadd, bali ni adhabu ya Taa’ziir yaani adhabu ya kutiwa adabu, kwa maneno ya Mtume S.A.W: “Zinaa ya macho ni kutazama, zinaa ya masikio ni kusikia, zinaa ya ulimi ni kunena, zinaa ya mkono ni kupiga, na zinaa ya mguu ni kukanyaga, na moyo unapenda na kutamani”. [Muttafaq].

Ash-Shiraziy amesema: Na anayeharamishwa kumwingilia katika tupu ni kama zinaa au kulawiti ni haramu kumgusa mahali pasipo hapo kwa matamanio, na dalili ya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na ambao wanazilinda tupu zao! Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa}. [Al Muminun: 5-6], na kwa kuwa Mtume SAW, amesema: “Ye yote kati yenu asiwe peke yeke na mwanamke ambaye si Mahram wake, kwani shetani ni wa tatu wao”.

Ikiwa upweke naye ni haramu, basi kumwingilia ni haramu zaidi, kwa sababu linakaribisha haramu. Akifanya hivyo basi adhabu ya Hadd haitakiwi kwake, kwa ilivyopokelewa na Ibn Masoud RA, kuwa: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W, na akasema: Nilimchukua mwanamke kwenye bustani na nikapata kila kitu kutoka kwake, isipokuwa kwamba sikumwingilia, basi nifanyie chochote unachotaka, hapo Mtume akamsomea: {Na shika Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu}. [HUUD: 114], na hutiwa adabu kwa sababu ni dhambi ambayo haina adhabu ya Hadd wala kafara, basi inaamuliwa kuadibishwa kisheria. Al-Muhadhab: 3/339, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah].

4- Tendo:

Ama tendo kamili ni uchafu, na adhabu yake ni adhabu ya Hadd ya zinaa ya ndugu za karibu, ambayo ni kuua akiwa ameoa au hakuoa, na dalili yake ni kuwa aliipotosha tabia yake na akaiacha, hivyo basi yeye anastahiki adhabu maalumu, ambayo imetajwa katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Baraa amesema: “Kaka wa mama yangu Abu Burdah Ibn Niyaar alipita karibu yangu na alikuwa na bendera, nikasema: Unakwenda wapi? Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amenituma kwa mtu aliyemwoa mke wa baba yake ili nimletee kichwa chake”.

Katika Mlango huu, kutoka kwa Qurrah Al-Muzaniy, Hadithi hii ya Al-Baraa ni Hassan Ghariib. Na Muhammad Ibn Is-haaq amepokea Hadithi hii kutoka kwa Adyi Ibn Taabit, kutoka kwa Abdillahi Ibn Yaziid, kutoka kwa Al-Baraa. Na hadithi hii imepokewa kutoka kwa Asha’ath , kutoka kwa Adyi , kutoka kwa Yaziid Ibn Al-Baraa, kutoka kwa kaka wa mama yake, kutoka kwa Mtume S.A.W. Na ameipokea At-Tirmidhiy na akasema: ni Hassan Ghariib.

Kutokea hatua yoyote, kwa makubaliano au bila ya makubaliano:

Iwapo jambo linakwenda nje ya fikra tu kwa hatua zifuatazo zilizotajwa, basi mwanamke achukue hadhari ili asimzidishie matamanio, bali amtishie, asipokataa basi analalamika kwa mtu anayeweza kumzuia.

Kuhusu mwanamume, jambo hilo ni rahisi zaidi kutoshindwa kwa nguvu, lakini linaweza kuwa ni kwa kutongoza, na hapa inambidi aepuke na upweke kwa tishio la kufichua jambo hilo pia; Kwa sababu anaweza asijimiliki baada ya muda.

Na mwenye kuzuiliwa, hata kwa kuua - kwa mujibu wa daraja tulilolitaja - yuko katika hatua ya tendo na unyanyasaji. Ama tendo hilo liko wazi, na kuhusu unyanyasaji, maana kugusa na mfano wa hayo pia imekatazwa, kama hapo awali, lazima azuiwe mfano wa mchokozi.

Ama kauli wazi, kanuni yake ni kwamba haipelekei kuzuiwa kwa kuua, isipokuwa mawaidha, vitisho, kuogopesha, na kuwafahamisha wanaoweza kumzuia havikufanya kazi.

Lakini ikiwa mhusika anaogopa fitna juu ya nafsi yake kutokana na msisitizo huo, au anajua kwamba mchokozi anamsumbua usingizini au atamtia dawa kwa kitendo hicho cha dhambi, basi hapa anayo haki ya kumzuia mfano wa mchokozi pia.

Lakini ikiwa uhalifu ulifanywa kwa ridhaa ya pande zote mbili, hivyo basi hakuna suala la "kuzuia mchokozi", lakini adhabu ya Hadd au kutiwa adabu inatumika kwa pande zote mbili.

Sura za Suala hili:

Sura nyingi zimechukuliwa kutoka hapo juu, kwa mfano: baba na binti yake, mtoto na mama yake, mtoto na dada ya baba yake, mtoto na dada ya mama yake, mtoto na mke wa baba yake, mtoto na dada yake, mtoto na bibi yake, binti na kaka ya baba yake, binti na kaka ya mama yake, au babu, na kadhalika.

Imewahi kutajwa taarifa ya Maharimu, kwa hivyo uhusiano wa kihesabu unaweza kupatikana kati yao inapohitajika.

Ofisi ya kutoa Fatwa imewahi kutoa Fatwa juu ya jambo kama hilo?

Na jambo hili si siri tena, bali limeenea, na kwa hivyo maswali juu ya suala hili yamefika Ofisi ya kutoa Fatwa, na kwa kuwa mada hiyo ni ya kulaumiwa na aibu juu yake, sehemu kubwa zaidi ilikuwa ya maswali yasiyo ya moja kwa moja, kama:

E-mail, simu iliyosajiliwa, simu ya moja kwa moja, kisha kuombwa Fatwa ya mdomo.

Inaweza kuwa swali ni la moja kwa moja au lisilo wazi, na muulizaji mara nyingi anadai kwamba swali si lake, bali ni la rafiki au mtu wa karibu yake.

Atahri za kisaikolojia na kijamii:

Msukosuko wa hisia kati ya upendo na chuki ya Maharimu, ambayo husababisha hali ya nafsi yenye shida.

Kuibuka kwa hisia hasi zinazoharibu uhusiano wote wa kifamilia, kama vile wivu, migogoro, chuki, dharau na hasira.

Kuibuka kwa alama za huzuni, kuteleza, na uchokozi kwa wengine, na hata kuelekea kwake mwenyewe.

Kuibuka kwa majaribio ya kujiua, kujaribu dawa za kulevya, au ukahaba wa umma.

Ugumu wa kuanzisha mahusiano mema ya kihisia au ngono wakati wa ndoa, pamoja na kuhisia mashaka kwa upande mwingine.

Kuenea kwa ukatili na kutokuwa na huruma, kama matokeo ya ukosefu wa maadili, na kama matokeo ya kuua watoto wa zinaa au kuwatupa mitaani.

Kuenea kwa upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume, na ubaridi kwa wanawake.

Kuibuka kwa magonjwa ya akili katika wanafamilia.

Kutokuwa na imani katika mambo ya kidini na ya kifamilia.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas