Matumizi ya Binti Ambaye Bado Haja...

Egypt's Dar Al-Ifta

Matumizi ya Binti Ambaye Bado Hajaolewa

Question

 Je! Baba anawajibu wa matumizi kwa binti yake asiye olewa hata ikiwa binti ana kipato kinachomtosha?

Answer

 Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Wanavyuoni wamekubaliana kuwa ni wajibu wa baba kutoa matumizi kutoka kwenye mali yake kwa watoto wake ambao ni maskini wasio na mali, wala hawana chumo linalowatosha, wakiwa wanaume au wanakike, kwa mujibu wa Qur`ani na Sunna na makubaliano ya wanavyuoni; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada} [AL BAQARAH: 233].
Mwenyezi Mungu amemlazimisha baba kuleta chakula kwa mke kwa ajili ya watoto, gharama ya watoto ni wajibu juu ya baba yao pia, na Mwenyezi Mungu anasema: {Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao} [AT TALAQ: 6], uwajibu wa malipo ya kuwanyonyesha watoto unapelekea uwajibu wa kuwaletea chakula. [Mughni Al-Muhtaj 3/446, Dar Al-Fikr], imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy na Muslim "kutoka kwa Aisha R.A: kwamba Hind Binti Utbah alisema: Ewe Mtume wa Allah! Hakika Abu Sufyan ni mtu mchoyo, hanipi pesa zinazonitosha na mtoto wangu, isipokuwa nilizochukua kutoka kwake, pasipo kufahamu kwake, Mtume S.A.W. alisema: Chukua pesa zinazokutosha wewe na mtoto wako kwa wema".
Ibn Qudaamah alisema [Al-Mughni 9/256, Al-Kitab Al-Arabi]: “Kuhusu makubaliano, wanavyuoni walikubaliana kuwa ni wajibu kwa kila mwanamume kutumia kutoka kwenye mali yake kwa watoto ambao hawana mali, na kwa sababu mtoto ni sehemu ya baba yake, na kama ni lazima kutumia kutoka kwenye mali yake kwa nafsi yake na familia yake vile vile ni lazima kutumia kutoka kwenye mali yake kwa mtoto wake.”
Kama binti akiwa mkwasi kwa chumo au pesa, basi si wajibu juu ya baba yake matumizi ya binti yake , hata kama baba akiwa tajiri; kwa sababu ni wajibu kwa faraja tu, na mkwasi hana haja ya faraja [Encyclopedia ya Kifiqhi 41/79, Wizara ya Mambo ya Wakfu ya Kuwait].
Al-Marghinaniy Al-Hanafiy [Al-Hidayah Sharhu Bidayatul Mubtadi 4/414, Dar Al-Fikr] alisema: “Matumizi ya mtoto ni wajibu juu ya baba yake hata akimpinga katika dini yake; kwa sababu ni malipo yake. Vile vile Matumizi ya mtoto ni wajibu juu ya baba yake kama mtoto hana pesa, lakini kama mtoto ana pesa basi msingi ni kwamba matumizi ya mtu yeyote ni wajibu juu ya nafsi yake akiwa ni mtoto au mtu mzima.”
Ad-Dasouqiy Al-Malikiy alisema [Hashitu Ad-Dasouqiy Ala Al-Sharhul Kabiir 2/524, Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: “Matumizi ya mwanamke ambaye ni huru, hana pesa, na hana kazi ni juu ya baba yake ambaye ni muungwana, mpaka kuolewa.”
As-Shiraziy alisema katika kitabu cha: [Al-Muhadhab 2/166, Issa Al-Halabiy]: “Mtu hana haki ya matumizi juu ya jamaa zake pasipo na haja, kama ni mkwasi hana haki ya matumizi, kwa sababu ni lazima kwa faraja na mkwasi hana haja ya faraja, lakini kama ni maskini, hawezi kupata chumo kwa sababu hajabaleghe bado au uzee au uwazimu au ugonjwa, katika hali hii mtu anastahili matumizi juu ya jamaa zake, kwani anahitaji, hana fedha na hana mapato, kama akiwa na uwezo wa kupata chumo kwa afya na nguvu, kama akiwa miongoni mwa wazazi basi kuna maoni mawili: ya kwanza ni: anastahili matumizi kwa sababu anahitaji matumizi haya kutoka kwa jamaa zake. Maoni ya pili ni: hastahili, kwa sababu ya nguvu ni kama ukwasi, kwa hivyo Mtume S.A.W. amesawazisha kati yao katika uharimisho wa kutoa zaka akisema: "Sadaka hairuhusiwi kwa mkwasi wala kwa mwenye nguvu". Na kama akiwa miongoni mwa wazaliwa basi kuna njia mbili: miongoni mwa wanavyuoni waliosema: Suala hili lina mitazamo miwili kama katika suala la wazazi, na wengine walisema mtu huyo hastahili; kwa sababu ana utukufu mkubwa kwa hivyo anastahili matumizi ingawa ana nguvu, lakini utakatifu wa mtoto ni dhaifu kwa hivyo hastahili matumizi ingawa ana nguvu pia”.
Ni lazima baba ana mali anazoweza kuzitumia kwa binti yake. Kama akiwa maskini basi si wajubu juu yake jambo hilo. Mtu asiye na chochote basi hana chochote. Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim katika Swahihi yake kutoka kwa Jaber R.A alisema: Mtu alimwacha huru mtumwa wake baada ya kufa kwake, Mtume S.A.W., akasema: “Nani atamnunua huyu kwangu mimi?” Nua’im bin Abdullah akamnunua. Akachukua thamani yake akampelekea mwenyewe, kisha Mtume S.A.W., akasema: “Anza kujitolea mwenyewe. Kikizidi kitu watolee watu wako wa nyumbani ‎‎(anza na mke, kwanza, kisha watoto). Kikizidi kitu, watolee ndugu na jamaa ‎zako (anza na ndugu na jamaa wa karibu, kisha wa mbali). Kikizidi basi ‎watolee wa huku na huko, na kule na hapa (walio karibu zaidi nawe na ‎ambao si watu wa ukoo wako, kama majirani wa karibu”.
Ibn Qudaamah Al-Hambaliy alisema katika kitabu chake cha; [Al-Mughniy 9/256]: “Alisema: na mtu analazimishwa matumizi ya wazazi wake, na mtoto wake, wa kiume na wa kike, kama ni maskini, na ana mali alizoweza kuzitumia kwao, na msingi wa uwajibu wa matumizi ya wazazi kwa watoto ni yaliyotajwa katika Qur`ani na Sunna na makubaliano ya wanavyuoni; Kuhusu Qur`ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao} [AT-TALAQ: 6].
Mwenyezi Mungu amemlazimisha baba kulipa malipo ya kumnyonyesha mtoto. Vile vile Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada} [AL BAQARAH: 233], na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema} [AL ISRAA: 23], na miongoni mwa kutende wema ni matumizi kwa wazazi kama wanahitaji. Katika Sunna: kauli yake Mtume S.A.W., kwa Hind: “Chukua pesa zinazokutosha wewe na mtoto wako kwa wema”, pia imepokelewa kutoka kwa Aisha R.A. kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Chakula kilicho bora ni kile ambacho mtu amekula kutokana na mapato yake, na hakika mwanawe anatokana na mapato yake pia". Imepokelewa kutoka kwa Abu Daawuud. Kuhusu makubaliano ya wanavyuoni, Ibn Al-Mundhir alisema: “Wanavyuoni wamekubaliana kwamba wazazi ambao ni maskini, hawana mapato, wala hawana mali, matumizi yao ni wajibu juu ya mtoto. Vile vile Wanavyuoni wamekubaliana kwamba watoto wasio na mali, matumizi yao ni wajibu juu ya baba yao na kwa sababu mtoto ni sehemu ya baba yake, na kama ni lazima kutumia kutoka kwenye mali yake kwa nafsi yake na familia yake vile vile ni lazima kutumia kutoka kwenye mali yake kwa mtoto wake”.
Ar-Ramliy alisema katika [Sharhih ala Al-Manhaj 7/218, 219, Dar Al-Fikr]: “Matumizi ya watoto ni wajibu juu ya mzazi akiwa mtoto huyo ni wa kiume au wa kike, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na juu ya baba yake} na maana ya {Na juu ya mrithi mfano wa hivyo}, Aya hii ambayo Abu Hanifa R.A. Aliichukulia ni wajibu wa matumizi kwa maharimu: yaani katika hali ya kutokuwa na madhara kama alivyosema Ibn Abbas, R.A., na anajua Qur'ani zaidi kuliko wengine ... lakini ni lazima kwa sharti la ukwasi wa anayetumia; kwani ni faraja kwa yanayobakia kutoka kwenye mali yake, familia yake, mke wake na mtumishi wake, mama na mwanawe kama alivyosema Al-Awza’i, kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imam Muslim: “Anza kujitolea mwenyewe. Kikizidi kitu wape watu wako wa nyumbani. Kikizidi kitu, wape ndugu na jamaa ‎zako” Na ni lazima kuleta chakula kwa watoto, lakini si lazima kwa watoto ambao wana mali zinazowatosha.
Kwa hivyo, si lazima kwa baba kumpa fedha za matumizi binti yake ambaye ni tajiri au ana kazi, na kama si hivyo, basi matumizi ya Mtoto wake huyo ni wajibu wake Baba mzazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

Share this:

Related Fatwas