Matumizi ya nguvu kifamilia

Egypt's Dar Al-Ifta

Matumizi ya nguvu kifamilia

Question

Ipi hukumu ya matumizi ya nguvu kifamilia hasa dhidi ya mke?

Answer

Matumizi ya nguvu kifamilia ni jambo linalopingwa na lenye dhambi kwa upande wa Kisharia, na inakuwa haramu zaidi vitendo hivyo vinavyofanywa dhidi ya mke, kwani Sharia imejenga namna ya kuendana na mke katika msingi wa upendo na huruma, hivyo kumpiga mke au kumtesa ni haramu Kisharia, yaliyotajwa na Aya ndani ya Suratul-Nisaai miongoni mwa kupiga kwa hakika ni aina katika aina kumfunza adabu na nidhamu inayoendana na hali maalumu, nako kuna misingi yake ambayo watu wameisahau mpaka wamefikia katika utekelezaji wa kukiuka makusudio yake, hivyo hapo hakuna kizuizi cha kumzuia na kumtia hatiani sawa na mabadiliko ya mifumo ya sheria na ya kijamii, na kuzuiwa kwake kunakuwa sawa na kitendo alichofanya Mtume S.A.W na sawa na makusudio ya Sharia Tukufu na maadili yake.

Share this:

Related Fatwas