Ndoa ya Mwanamke Aliyeachwa Kabla ya Kutolewa Hukumu ya Mwisho Kuhusu Kumwacha.
Question
Hali ya mwanamke aliyeachika kwa mujibu wa hukumu ya mahakama ya Mwanzo wakati mume anapoomba kukata rufaa na kutolewa hukumu nyingine, na ombi lake la rufaa likakubaliwa basi hukumu ya kwanza ya kumpa talaka mke wake itaondolewa, na mke wake akawa ameitambua ile hukumu ya kwanza iliyotolewa na mahakama, kisha akaolewa na mwanaume mwengine, na kukutana naye kimwili. Je, ni nini hukumu ya ndoa hii ya pili? Na ni upi uhusiano kati yake na mumewe wa kwanza mpaka hukumu ya mwisho ilipolewa na Mahakama?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Inajulikana kuwa hukumu ya mwisho inaonesha usahihi wa hukumu ya kwanza au ubatili wake, hivyo hairuhusiwi kwa mke kuolewa na mtu mwengine kabla ya kutolewa kwa hukumu ya mwisho hata kama eda yake itakuwa imemalizika, lakini ni lazima kusubiri hukumu ya mwisho ya mahakama tu: kama hukumu ya kwanza itasisitizwa kwamba ilikuwa taarifa ya sahihi ya talaka. Na kama ikipingana nayo basi itakuwa ni kwa ajili ya kuonesha ubatili wa hukumu ya kwanza, kisha hapatakuwa na eda wakati huo; kwani itakuwa imejitokeza kwamba talaka iliyotolewa sio sahihi na athari zake hazikutekelezwa, na kwamba ndoa yake ni sahihi na hapakuwapo sababu yoyote inayoivunja.
Kama ikitolewa hukumu ya mwisho ya ubatili wa hukumu ya kwanza ambayo inahusu kumpa mke talaka, hii ina maana kwamba ndoa yake ya kwanza inaendelea kati yake na mumewe, kufuatana na asili, na kuendeleza kwa hali ile ile kama ilivyokuwa, na kwamba ndoa yake ya pili ni batili na ni kama vile haipo, na kukutana kimwili katika ndoa ya pili kunazingatiwa kuwa ni kule kunakoshukiwa tu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.